MAWASILIANO YA BAGAMOYO NA DAR YAKATIKA DARAJA LAKATIKA MAPINGA

April 12, 2014

Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.
Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe. Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati ya mto kuwa na mwinuko. Mvua nyingi maji yamepita pembeni na hata kwenda nje ya daraja.

JK AONGOZA WATANZANIA KUMBUKUMBU YA MIAKA 30 YA KIFO CHA SOKOINE

April 12, 2014
 Rais Jakaya Kikwete leo ameongozi taifa katika maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine katika maadhimisho yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Monduli Juu.
Pichani ni juu Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kifo chake.
 Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akiweka shada la maua

*MATUKIO YA MAFURIKO JIJINI DAR, MWENGE, ITV NI HATARI TUPU FOLENI YA KUFA MTU

April 12, 2014


 Sehemu ya maduka yaliyopo eneo la Kituo cha daladala cha ITV yakiwa yamezingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Kutokana na mvua hizo na maji kujaa kumesababisha msongamano mkubwa wa mago kuanzia jana jioni na leo.
 Barabara ya kuelekea Goba....

JKT RUVU WAIPIGISHA KWATA COASTAL UNION,WAICHAPA KIMOJA TU

April 12, 2014


NA SAFARI CHUWA,TANGA.
Bao la Gido Chawala lililofungwa dakika ya 17 lilitosha kuwapa ushindi Jkt Ruvu kwenye mechi yao ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani hii leo.



Bao hilo lilitokana na penati iliyotolewa na mwamuzi wa mchezo huo Adrew Sahmba kutoka mkoani Pwani kuamuru ipigwe kutokana na mshambuliaji wa Coastal Union,Selemani Kassim Selembe kuunawa mpira eneo la hatari.