NAIBU WAZIRI MPINA AZITAKA RADIO ZA JAMII KUHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
(katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa
katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia)
ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
Aliyeinama
katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi
wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
Bw.
Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi
akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi wa soko la mji wa Masasi kwa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
(kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira mjini Masasi.
(PICHA NA EVELYN MKOKOI)
……………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka
Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri
Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa,
mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akitolea Mfano wa Radio Pride FM
ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara,
ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake
kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo
kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.
Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea
Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la
kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa
kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya
kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea
mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.
Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa
Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri
Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za
mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani
humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi
ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.
“Nimeona kuwa uchomaji moto
misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia
nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa
uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari
kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa
alisisitiza.”
Ziara ya Naibu Waziri Mpina
Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda
na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa
Masasi.
Radio Maria waiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii
Mwashamu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za
kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu
April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki
la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria
Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio
Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es
Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John
Maendeleo.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea
kuanzishwa kwa Redio hiyo
Mkurugenzi
wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais
wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na
marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius
Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya
Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda
akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika
kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe
za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius
Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ).
Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Rais wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira
ameiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii ili
ziweze kuwa na vituo vingi vya kurushia matangazo yake.
Hayo yamesemwa leo na Rais huyo wakati
alipokuwa akisoma risala kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya
miaka 20 ya redio hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre,
Jijini Dar es Salaam.
Kira amefafanua kuwa redio za kijamii hasa
zilizojikita katika nyanja za kiimani zinasaidia kufundisha maadili na
kufanya wananchi wakomae kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za
aina hiyo zinapewa leseni za kurusha matangazo yake nchi nzima.
“Ndugu mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu
(coverage areas) ambapo tatizo hili linatokana na sheria ya leseni za
redio ambayo hairuhusu redio za aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi
nchini nzima, tunaomba serikali itusaidie kuiboresha sheria hii ili
tuongeze vituo vya matangazo ya dini”, alisema Kira.
Rais huyo ameongeza kuwa majimbo yote
yanahitaji kufikiwa na huduma za maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji
wote kuendelea kuisikiliza redio hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu
za mkononi kwani hivi sasa huduma hiyo inapatika nchi nzima.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai
kwa uongozi wa redio hiyo kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi
visivyokuwa vya dini ili iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa
familia.
“Tunasema kuwa redio Maria ni sauti ya
kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema ni sauti ya Mungu ndani ya
familia kwa kuwa inafanya kazi ya kuunganisha familia, vyombo vingine
vya habari vinafanya kazi kubwa ya kuigawa familia lakini Redio Maria ni
tofauti”, alisema Pengo.
Askofu Pengo amewashukuru wananchi wote
waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni njia
moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima Mama Bikira Maria.
Nchini Tanzania, Redio Maria ilianzishwa
Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea ikiwa na lengo
la kumsaidia Mama Bikira Maria katika kazi yake ya kumtangaza Yesu
Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo 10 Tanzania Bara na viwili
Zanzibar.
BOHARI LATEKETEA KWA MOTO SINZA LEGO JIJINI DAR JIONI HII
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua
Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
Rais Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)