BENKI YA CRDB YAENDESHA SEMINA KWA WATEJA WAKE WA MKOA WA TANGA

November 15, 2022

 

 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika ufunguzi rasmi wa Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
Afisa Mkuu wa Biasra wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati akitoa mada ya biashara  na uwekezaji katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Chiku Issa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.
 
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba (kulia) asalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati alipowasili kwa lengo la ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na wa pili kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kirambata.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwasalimia baadhi ya viongozi waandamizi wa Benki ya CRDB, wakati alipowasili kwa lengo la ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.









Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, muda mfupi baada ya ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.


DKT MPANGO KUFUNGUA MASHINDANO YA SHIMUTA TANGA NOVEMBA 21,2022

November 15, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza na waandishi wa habari

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya CCM Mkwakwani Jijini Tanga ambacho pia kitatumika katika mashindano ya Shimuta

Mwenyekiti wa SHIMUTA Taifa Roselyne Massam akizungumza kuhusu maandalizi ya mashindano hayo yanayoanza leo Jijini Tanga

Mratibu Mkuu wa Shirikisho hilo Maswet Masinde alieleza namna walivyojipanga kuhakikisha hakuna mamluki atakayechezeshwa kwenye timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwani wamejipanga kusimamia sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza katika michezo yote.




Na Oscar Assenga,TANGA.

MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ya Mashirika ya Umma,Makampuni na Taasisi Binafasi nchini (Shimuta) Novemba 21 mwaka huu kwenye viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.


Hayo yalibainishwa leo na Mwenyekiti wa SHIMUTA Taifa Roselyne Massam wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu mashndano hayo ambapo alisema kwa mara ya kwanza tokea yalipoanza mwaka huu 2022 yameweka rekodi mpya.


Alisema rekodi hiyo inatokana na kuongezeka kwa idadi ya timu na sasa kufikia 52 zitakazochukua kuwasaka mabingwa kupitia michezo watakayoshindaniwa ambayo itatimua vumbi leo Novemba 15 katika viwanja mbalimbali Jijini hapa


Mwenyekiti huyo alisema amesema tangu wameshika hatamu ya kuliongoza shirikisho hilo haijawahi kutokea kushirikisha timu nyingi zaidi kama mwaka huu jambo ambalo linaonyesha mwitikio umekuwa ni mkubwa na michezo hiyo kuonekana kuleta tija kwa washiriki mashirika, makampuni na taasisi zenyewe wanazotoka.

Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Shirikisho hilo Maswet Masinde alieleza namna walivyojipanga kuhakikisha hakuna mamluki atakayechezeshwa kwenye timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwani wamejipanga kusimamia sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza katika michezo yote.

Mashinde alisema kwamba msimu huu wamekuwa wakali zaidi kuhakikisha wanadhibiti mamluko hivyo wamekwisha kufanya uhakiki kuondoa mamluki kwa kutumia taasisi za umma ikiwemo NHIF, WCF, PSSF kuhakiki washiriki lengo likiwa ni michezo hii iwe ni kwaajili ya watumishi wale ambao wanatambulika kisheria na ili uwe mshiriki unapewa leseni maalumu na lazima uwe umehakikiwa kwenye mifuko hiyo.

Mratibu huyo alisema kwamba mpaka sasa wanamichezo 2183 ambao tayari wameshafika hapa jiji la Tanga na ni namba kubwa ya wanamichezo wanaoshiriki lakini tuna kanuni ambazo zinaongoza katika mashindan pia watatumia kanuni za michezo husika pale inapobidi huku akisisitiza umuhimu wa waamuzi wasimamie sheria taratibu na miongozo inayoongoza michezo husika ili kusiwepo na manung'uniko ya hapa na pale

Akieleza namna mkoa huo ulivyojipanga kuelekea Mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema kwamba mkoa upo salama na kuwahakikishia ulinzi na usalama muda wowote watakapokuwepo kwenye mashindano hayo.

Mkuu huyo wa Mkoa alitumia nafasi hiyo pia kuwataka wakazi wa Tanga wakiwemo wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo kuchangamkia fursa za uwepo wa mashindano hayo kujiongezea kipato.

"Mashindano haya ni zaidi ya michezo yana faida ya kipato lakini yanainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuongeza pato la taifa, nitoe wito kwa wafanyabiashara wote wachangamikie fursa na kujitokeza kwa wingi katika michezo hii " alisema Mgumba.


"Suala la hali ya ulinzi na usalama liko vizuri tumeendelea kuimarisha doria kwa sababu tumepata ujio wa watu wengi hivyo hali ya usalama iko vizuri tumeendelea kujiimarisha zaidi doria za mchana na usiku kuwahakikishia wanamichezo na wageni wetu wote wanakuwa salama wakati na hata baada ya kumaliza michezo" aliongeza

Michezo itakayochezwa wakati wa mashindano hayo ni michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa Pete , Wavu, Kikapu, Dats, Pool table, Vishale , Draft kukimbia kwa magunia, Riadha kuvuta kamba Bao na mingineyo kedekede, lengo kuu hasa ikiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya taasisi, mashirika na makampuni kuimarisha afya kupitia michezo ikiwa pia ni kuondokana na magonjwa yasiyoambukiza.

Michezo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka ni kwa mara ya pili mfululizo kufanyika ndani ya mkoa wa Tanga mwaka huu yakija na kauli mbiu ya 'SHIMUTA familia moja'.

ELIMU YA USALAMA,ULINZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA YATOLEWA NA TASAC MOROGORO

November 15, 2022



 



AFISA Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin akimuonyesha mmoja wa watumiaji wa vyombo vya majini namna ya kuvaa jaketi okozi













 



Na Mwandishi Wetu,Morogoro

 

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetoa elimu ya Usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.

Ukaguzi huo ni sehemu mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango. 

Zoezi hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini  wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika wilaya ya Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzuzungatia wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.


Zoezi hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 ifakara katika maeneo ya Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea katika mikoa ya  iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.


Zoezi hilo liliendeshwa pia kwa ushirkiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko ambapo waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo safarini.