WAKATI UFOO SARO AKIWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI HIVI NDIO HALI ILIVYO NYUMBANI KWAO KWAZIZIMA

October 14, 2013
  DSC 0108 5ec3cNi msiba wenye kuhuzunisha na kushtua.
Watu wakitafakari jambo nyumbani kwa kina Ufoo Saro, baada ya jana kupigwa risasi yeye pamoja na mama yake. Katika tukio hilo, mama yake Anastazia Saro alifariki Dunia, wakati aliyedaiwa kufanya tukio hilo naye alijipiga risasi na kufa papo hapo kwa tukio hilo linalotafsiriwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

chanzo:handenikwetu.blogspot.com

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA LEO

October 14, 2013
Release No. 174
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 14, 2013

KAMATI YA RUFANI YA MAADILI YAFANYA MAPITIO
Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana (Oktoba 13 mwaka huu) kusikiliza maombi ya mapitio (revision) na mwongozo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili.

Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati hiyo ya juu kabisa ya masuala ya maadili kutokana na ugumu wa utekelezaji wa uamuzi wa Kamati ya Maadili juu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake.

Kamati ya Rufani ya Maadili itaendelea na kikao chake kesho (Oktoba 15 mwaka huu), na baadaye itakutana na waandishi wa habari (saa 10 jioni) kwa ajili ya kutangaza uamuzi wake juu ya mwongozo ulioombwa na Sekretarieti ya TFF.

KIONGOZI WA MWENGE AFUNGUA KITUO CHA IDYDCC
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ali Amir amefungua kituo cha kwanza cha Football for Hope kilicho mkoani Iringa kwa kuwataka wananchi kukituia vizuri ili wanufaike na huruma za kijamii zinazotolewa na taasisi ya IDYDC pamoja na kuendeleza mpira wa miguu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jana (Oktoba 13 mwaka huu), kiongozi huyo amesema taasisi ya IDYDC (Iringa Development of Youth, Disabled and Child Care) wamefanya vizuri kuamua kutumia mpira wa miguu kusaidia jamii kwa kuelimisha juu ya mambo mbalimbali kama ugonjwa wa ukimwi, kusaidia walemavu, haki za watoto na afya ya jamii.

Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Patrick Onyango amesema amefurahishwa na kukamilika kwa kituo ambacho kitasaidia jamii.
Amesema idadi kubwa ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo inadhihirisha ni kiasi gani kituo hicho kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii.

Onyango alisema hicho ni kituo cha 14 kukamilika kati ya 20 vinavyojengwa barani Afrika ikiwa ni mpango wa FIFA kurudisha kwa jamii mafanikio iliyopata kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia barani Afrika.

Kituo hicho kina uwanja mdogo wa mita 20 kwa 40 uliowekwa nyasi bandia, jengo lenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya semina, chumba cha kupimia ukimwi, chumba cha ushauri nasaha, maktaba na ofisi.

Zaidi ya dola 270,000 za Marekani zimetumika kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kilicho eneo la Mtwivila, Iringa mjini.

KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Mtanzania Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya Botswana na Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Botswana kati ya Oktoba 25 na 27 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba tisa.

Waamuzi hao wataongozwa na Pamela Majo atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Rudo Nhananga, namba mbili ni Stellah Ruvinga na mezani atakuwepo Tambudzi Tavengwa.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MATUKIO YA PICHA KATIKA UCHAGUZI WA TRBA MKOA WA TANGA.

October 14, 2013
VIONGOZI WAPYA WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,TRBA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUCHAGULIWA LEO.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA KIKAPU MKOA WA TANGA HAMISI JAFFARY AKIWASHUKURU WAJUMBE KWA KUMCHAGUA KATIKA UCHAGUZI HUO

WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,WAKIMSILIKIZA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO HAMISI JAFFARY KUSHOTO NI FRANK MASUMBA,KATIKATI NI HASSANI SAKALA NA SAA MAMY MOHAMED

MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA TANGA,AHMED RAJABU "BABLA' KATIKA AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA MWENYEKITI WAO HAMISI JAFFARY WAKATI AKISHUKURU KWA KUMUWEZESHA KUKIONGOZA KWA AWAMU NYENGINE CHAMA HICHO.



HAMISI JAFFARY MWENYEKITI MPYA KIKAPU TANGA

October 14, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Tanga (TRBA),Hamisi Jaffary amefanikiwa kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika jana,katika ukumbi wa Bandari mkoani hapa.

Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga Peter Semfuko ulikuwa na upinzani mkubwa kwa baadhi ya nafasi ambazo zilikuwa zikigombewa na wagombea zaidi ya wawili.

Akitangaza matokeo hayo,Semfuko alimtangaza Jaffary kushika nafasi hiyo baada ya kupata kura 23 za ndio kati ya 24 ambazo zilipigwa na wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi kwenye wadhifa ambao alikuwa akigombea peke yake.

Katika uchaguzi huo nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Rajab Ahmed “Babla”kwa kupata kura 23 huku kura I ikisema hapana ambapo pia hakuwa na mpinzani.

Nafasi ya Katibu Mkuu ilichukuliwa na Calistus Zakaria kwa kumbwaga mpinzani wake Patric Semindu kwa kupata kura 15 kati 6 alizipata mgombea mwenzake.

Kwenye uchaguzi huo nafasi ya Katibu Msaidizi ilichukuliwa na Gilo Mwanakatwe aliyepata kura 19 kati 2 alizopata mpinzani wake Said Ramadhani huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na Twahiru Mdimu aliyepata kura 19.

Nafasi nyengine ni wajumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Ally Senkole,Hassani Sakala,Omari Kupe na Frank Masumba.
Katika nafasi ya mwakilishi wa wachezaji mkutano mkuu Taifa kwa mkoa wa Tanga ilichukuliwa na Saa Mumy Mohamed aliyepata kura 14 kati ya 6 alizopat mpinzani wake Adam Issa Semkonde.