PICHA:KUZAMA KWA KIVUKO CHA MTO KILOMBERO

January 28, 2016

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari 3. 
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw Leph Gembe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, kuzama kwa kivuko hicho kulichangiwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma wakati huo hivyo kupoteza uelekeo wake. 

Alisema ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa 1 usiku wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga. 
Mkuu huyo wa wilaya amesema taarifa alizopewa ni kwamba kivuko hicho kilikuwa na abiria 30 na wote waliokolewa baada ya kupewa majaketi ya usalama baada kivuko hicho kuanza kupoteza uelekeo kutokana na upepo mkali. 
Hata hivyo amesema kuna mashaka ya mtu mmoja kuwa alizama na wanaendelea kufuatilia kupata ukweli wake. 
Ameyataja magari yaliyozama kuwa ni pamoja na gari moja la CRDB, gari la kampuni ya mitiki, fuso moja pamoja na bajaji.
Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.
Matukio Bungeni katika picha bungeni Dodoma leo

Matukio Bungeni katika picha bungeni Dodoma leo

January 28, 2016

mh1
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh2
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
mh3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka ajali hiyo.
mh4
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh6
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh7
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh8
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
mh9
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh10
Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais
picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

January 28, 2016

ak1 
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp aliyemtembelea ofisini kwake leo tarehe 28 Januari, 2016, Mjini Dodoma.
ak2
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp  aliyemtembelea ofisini kwake. Katikati ni Katibu wa Balozi huyo.
ak3
ak4
Spika wa Bunge Mhe. Job Y. Ndugai akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Yasemin Eralp aliyemtembelea ofisini kwake Mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Bunge)
SERIKALI YAENDELEA KUREJESHA MALI ZILIZOPATIKANA NA UHUJUMU UCHUMI

SERIKALI YAENDELEA KUREJESHA MALI ZILIZOPATIKANA NA UHUJUMU UCHUMI

January 28, 2016

DI1
Mkurugenzi wa upelelezi Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athumani akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam.
DI2
Mkurugenzi wa Upelelezi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) Bw. Alex Mufungo akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam pembeni yake ni Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP Biswalo Mganga.
DI3
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishina Diwani Athuman hayupo pichani wakati wa mkutano wa kuelezea mikakati na malengo ya Serikali katika kupamabana na kudhibiti wahalifu wa kuhujumu uchumi uliofanyika leo jijini Dar  es salaam.
Picha zote na Ally Daud -MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………
NA MAGRETH KINABO NA ALLY DAUD – MAELEZO
Serikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu ana makosa hayo.
Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Hayo yalisemwa na  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo Mganga wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi   jijini Dar es salaam, ambapo  alisema kuwa hatua hizo zimechukuliwa mara baada ya  upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi kukamilika na kumbaini mhusika.
Aidha Mganga aliongeza kwamba  mhusika  hushtakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo  watumishi wa umma.
“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya kulipa faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika na makosa hayo” alisema  Mganga.
Alisema kufuatia mkakati huo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini (20) ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuziwa au kutaifishwa.
Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu.
Mkoani Kilimanjaro kesi mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani  kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine  zenye uzito wa kilogram tatu zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo cha maisha.
Kesi nyingine ni namba 46 ya mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu, mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gram 3191.11 na thamani ya Sh. Milioni 143, watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa huru.
Mganga alizitaja baadhi ya kesi nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni  Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila mmoja.
Kesi nyingine  ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2016 iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid Ngaza aliyetiwa hatiani  kwa  kosa la kukutwa na meno ya tembo nane iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, wilaya ya Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30 na kullipa faini ya Sh. bilioni 1.2.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf , Hiace pamoja na nyumba  kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya kuhujumu uchumi.
Aidha,  Mganga alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshirikikuficha mali ya mtu mwingine inayohusiana na uhalifukwa njia yoyote ile pia anaweza kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema kuwa atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na mali zake kutaifishwa.
“Mhalifu akibainika na mshataka ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha taslimu” alisema Kamishna Athumani.
Aidha, Kamishna Athumani aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina ya wake zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia za uhalifu.
“Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza Kamishina Athuman.
Mbali na hayo, Mkurugenzi wa upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.
Tangu mwaka 1990, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kama kipaumbele katika mfumo wa haki jinai wa kupigana na uhalifu.  Haisadii sana katika jitihada za kupambana na uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini au kwenda jela ikiwa ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au mali iliyopatikana kwa uhalifu huo.
Zaidi, fedha zilizoibwa na wanasiasa wala rushwa pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa na kuelekezwa katika maeneo muhimu yenye mahitaji.
Sheria ya Utaifishaji wa Mali Haramu ilipitishwa na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa Kimataifa pamoja na mikataba ya Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi yetu.

Banki ya NMB yashiriki maonesho ya wadau wa kilimo na Biashara Afrika Mashariki

January 28, 2016


Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (wa pili kulia) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (wa pili kulia) akimuuliza swali Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Meneja Mahusiano wa Kilimo cha Biashara wa Benki ya NMB Plc, Christopher Mwalugenge (kulia) akifafanua maswali mbalimbali kwa wateja waliotembelea Banda la Benki ya NMB Plc katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Meneja Mahusiano wa Kilimo na Biashara wa Benki ya NMB Plc, Hamisi Mmomi (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa wateja waliotembelea Banda la Benki ya NMB Plc katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (katikati) pamoja na ujumbe wake wakipata maelezo toka kwa Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) walipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (katikati) pamoja na ujumbe wake wakikaribishwa katika banda la NMB walipotembelea kwenye maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wananchi wakitembelea mabanda anuai katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Pichani ni baadhi ya mashine na magari yanayotumika kwa kilimo wakiwa katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (kulia) akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa mashine kubwa na ya kisasa inayovuna, kukoboa na kupakia mpunga na mahindi kwenye magunia huku ikijiendesha yenyewe shambani, mashine hiyo ipo katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (kushoto) akitembelea mabanda mengine katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

January 28, 2016
 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
 Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo  kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.
 Dimbwi la maji likiwa mbele ya jengo la Yanga.
 Daraja la Jangwani na Kituo cha mabasi ya mwendokasi kikiwa kizingirwa na maji.
 Magari yakipita kwenye dimbwi la maji barabara ya mtaa wa Lindi Ilala.
 Moja ya vibanda wanavyoishi wananchi waliobomolewa eneo la Kinondoni Mkwajuni maji yakipita katikati yake jambo ambalo ni hatari kwa watu wanaoishi ndani humo.
 Nyumba ikiwa imezingirwa na maji eneo la Mchikichini Ilala kufuatia mvua hiyo iliyonyesha leo
Vijana wakiuangalia Uwanja wa Klabu ya Yanga ulivyojaa maji.


KAMANDA WA MATUKIO BLOG YAPONGEZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA COVERAGE NZURI YA UCHAGUZI MKUU 2015

January 28, 2016
 Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.

Mwaikenda, alishiriki kikamilifu katika coverage ya kampeni za miezi miwili za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika mikoa mbalimbali nchini.Kazi zake zilikuwa zinatumika kwenye gazeti la Jambo Leo  analofanyia kazi na kusambazwa pia kwenye blogu mbalimbali nchini.

Pia alikuwa miongoni mwa wapigapicha waliofanya coverage wakati wa kutangazwa kwa matokeo,mshindi wa urais na kuapishwa Rais Dk John Magufuli Novemba 5, 2015, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. (PICHA NA MARGARET CHAMBIRI-NEC)
 Mwaikenda akifurahia kupata cheti hicho




SAPOTI YAKO YAHITAJIKA KWA VIJANA HAWA KATIKA WIMBO HUU

January 28, 2016
waleo - sikuachi
This is Brand new Audio from Tanzanian Artist Called WALEO, Song Called "SIKUACHI" Produced by Fraga Studio:: Uprise Music.

Enjoy the Good Music
Fungwa S.Kilozo Founder of Lindiyetu.com & Kickzacelebrity.blogspot.com P.o.Box 285, Lindi, Tanzania Mob.+255787572019 OR +255713572019 Email: fkilozo@gmail.com or lindiyetu@gmail.com
TANZIA: SWAI AFARIKI DUNIA

TANZIA: SWAI AFARIKI DUNIA

January 28, 2016
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
TFF itawajulisha mipango ya msiba na mazishi ya marehemu Epaphra Swai baada ya kukaa na familia ya marehemu na kupanga utaraibu huo.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

January 28, 2016
1
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) lililofanyika katika ukumbi wa NACTE, jijini Dar es Salaam.(Picha na Philemon Solomon wa Fullshwangwe)
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika jana jijini Dar es Salaam baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
Akizungumza na Mo Dewji Blog, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.
Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
2
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akiwaelezea washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) ambao utafanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017 – 2021.
Naye Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.
Awali Zulmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.
3
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akielezea jambo katika kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
4
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akizugumza kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), Katikati ni Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari.
5
Mmoja wa wanakikundi akiwaelezea wanakikundi wenzake kuhusu kipaumbele ambacho walikuwa wamechaguliwa kukijadili na baadae kuwasilisha mbele ya washiriki wote jinsi kipaumbele hicho kitakavyotumika pamoja na faida zake.
7
Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutoka Ufaransa, Anton De Grauwe akimuelekeza jambo mwana kikundi mwenzake wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vitakavyotumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
8
Baadhi ya wanakikundi wakiwa makini kufuatilia kila jambo ambalo linaendelea katika kongamano hilo la siku mbili ili kupata vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
9
10
11
Picha ya pamoja.