WAZIRI MKUU ATINGA BANDARI YA TANGA

WAZIRI MKUU ATINGA BANDARI YA TANGA

February 19, 2016

tan1
Waziri  Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na  Mhandisi wa Mamlaka  ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tan2
 Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua  bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tan3
Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa  maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo kesho (Jumamosi) saa 6 mchana.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga leo mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani kurejea Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo. Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat  (meli ndogo).
“Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe  (self propelled) “
“Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?” alihoji Waziri Mkuu
“Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa,” aliongeza.
Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. “Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,” alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.
“Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.
Waziri Mkuu amerejea jijini leo jioni.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA KIKAO CHA TATU CHA BARAZA KUU LA PILI LA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TIA).

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA KIKAO CHA TATU CHA BARAZA KUU LA PILI LA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TIA).

February 19, 2016

tk1
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akiwahutubia wajumbe wa Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
tk2
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kikao cha tatu cha Baraza Kuu la Pili la wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
tk3
Baadhi ya wajumbe wa Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
tk4
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) baada ya kufungua kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Morogoro.
WITO umetolewa kwa watumishi wa Umma kufanya kazi kwa uadilifu na kutimiza wajibu wao kikamilifu katika sehemu zao za kazi.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
Dkt. Kijaji amesema kuwa, Serikali haitamvumilia mtumishi wa ngazi yeyote wa wizara ya Fedha na Mipango atakayeshindwa kutimiza wajibu wake kikamilifu ikiwa ni pamoja na kushindwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa Taasisi hiyo kuendelea kusimamia kwa karibu kazi zote na kutathimini utendaji kazi wa watumishi wake.
“Haipendezi kukuta meza ya Mkurugenzi imejaa majalada huku watumishi wa chini yake wakiwa hawana kazi za kufanya” alisema Naibu Waziri huyo.
Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa, wakati umefika kwa kuwapatia watumishi hao kazi za kufanya ili nao wapate uzoefu ambao tayari viongozi waliopo ngazi za juu  wameshaupata.
Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango amewataka watumishi wa Serikali wakiwemo wa Wizara hiyo kila mmoja wao kuwajibika  katika nafasi yake kwani suala hilo ni  muhimu katika kuleta tija sehemu ya kazi.
“Sasa ni wakati wa watumishi wa umma  kujituma pamoja na kufanyakazi kwa bidii kwa kuwa mmepewa dhamana ya kuwatumikia watanzania wote “ amesema Naibu Waziri huyo.
 Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Joseph Kihanda, amesema kuwa Taasisi imejiimarisha katika utoaji wa elimu yenye ubora ili kuwawezesha wahitimu kufanya vizuri katika masomo yao na baadaye katika sehemu zao za kazi.
Amesema jitihada zao za kutoa elimu bora zimethibitishwa na bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) na bodi ya Wataalamu wa manunuzi na ugavi (PSPTB).
Hata hivyo Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa muda mrefu ikiwemo ya uhaba wa majengo kwani kwa kipindi cha miaka minane Taasisi hiyo imekuwa ikiomba ruzuku Serikalini kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini bado haijapata ruzuku hiyo.
Pia ameitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi ambapo uwiano wa wahadhiri haulingani na wanafunzi.
Hali hiyo inatokana na Taasisi kupata vibali vichache vya kuajiri wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji kutoka Utumishi ikilinganishwa na maombi ya Taasisi.
Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wabunge kutoka nchini Sweden.

Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wabunge kutoka nchini Sweden.

February 19, 2016

ngo1
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza  na Wabunge kutoka nchini Sweden (hawapo pichani) leo jijini Da es salaam wakati wa mkutano uliofanyika Wizarani hapo, kuhusu ushirikiano wa  kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden. Kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad.
ngo2
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya Serikali wakati wa mkutano na Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi nchini.
……………………………………………………………………………………………..
Waziriwa Fedha na Mipango,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa Sweden katika ukumbi wa Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina Tanzania na Sweden.
Katika mazungumzo yake na wabunge hao ambao wamewasili nchini kwa  ziara ya kikazi, Dkt. Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na inafanyakazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma stahiki kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema Serikali imejipanga kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kuiwezesha nchi kujiendesha yenyewe na kuacha kutegemea misaada ya wahisani.
Aidha, amefafanua kuwa Tanzania imejipanga kuongeza vyanzo vya ukusanyaji mapato pamoja na kuboresha  vyanzo vilivyopo na kuhakikishakila Mwananchi anayestahilikulipakodistahikianalipa kwa wakati.
“Ni aibu kwa nchi yenye rasilimali za kutosha Wananchi wake kuishi katika hali ya umasikini, tunachotakiwa ni kuboresha kilimo kwa sababu wananchi wengi ndicho wanachotegemea”, alisema.
Akizungumzia vipaumbele vya Serikali katika mkutano huo, Dkt. Mpango alisema mkazo umewekwa zaidi katika kufanya mapinduzi ya viwanda, ambapo nchi inaanzakuboresha viwanda vilivyopo hususani vile ambavyo hutumia rasilimali zinazopatikana nchini kama zile zinazotokana na kilimo.
Aliongeza kuwa katika kuboresha viwanda pia Serikali ipo katika hatua za kuboresha soko la ndani na nje ya nchi kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo.
Dkt. Mpango alisema sambamba na kufanya mapinduzi ya viwanda, Tanzania imejipanga kuboresha miundombinu ambapo mpaka sasa kuna miradi mbalimbali ya maendeleo imeanzishwa kama mradi wa umeme vijijini.
Alisema katika suala la umeme, nchi imeazimia kujikita katika uzalishaji wa kutumia vyanzo vingine kama gesi asilia, jua na upepo kuliko kutegemea maji pekee.
Kuhusu sekta ya usafirishaji, Dkt. Mpango amesema Serikali imejipanga kuboresha bandari zote nchini na kuzifanya ziwe za kisasa ili kuhamasisha biashara za ndani na nje ya nchi kupitia bandari hizo.
Hata hivyo, Dkt. Mpango alikiri kuwa uboreshaji wa reli ya kati ni changamoto kwani reli hiyo haiwezi kuboreshwa kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali pekee, hivyo Serikali inajitahidi kutafuta njia za kufanikisha ujenzi huo.
Katika mkutano huo, Dkt. Mpango alizungumzia suala la huduma za kijamii alisema, nchi imejipanga kutoa elimu inayoendana na soko la ajira na Serikali imeanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo ili kuwawezesha wananchi wengi kupata elimu.
Akizungumzia suala la uchumi, Dkt. Mpango alisema hali ya uchumi kwa sasa ni nzuri kwani pato la ndani la Taifa limefika asilimia 7 katika miaka ya hivi karibuni.
Dkt. Mpango alisema ili kufanikisha vipaumbele hivyo, ni lazima maadili na nidhamu ya kazi vifuatwe na watendaji pamoja na watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aliongeza kuwa Serikali ipo msatari wa mbele kupambana na rushwa na haitosita kuhakikisha watu wote wanaohusika na rushwa wanachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande  Wabunge kutoka nchini Sweden, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Kenneth Forslund, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika ukusanyaji wa  mapato ya ndani na kutoa huduma za kijamii.
Tanzania na Swede nzime kuwa na ushirikiano wa muda mrefu ambao umeifaidisha Tanzania katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuendeleza miradi ya afya na umeme hususani vijijini, elimu pamoja na kusaidia kukamilisha bajeti ya kila mwaka.
Imetollewa na Msemaji
Wizara ya Fedhana Mipango
Kitengo cha Habari
19.2.2016

MKURUGENZI WA VODACOM TANZANIA,IAN FERRAO ATINGA CLOUDS FM NA EFM RADIO LEO

February 19, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga(watatu kulia) alipokuwa akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kurushia vipindi vinavyofanywa na kituo hicho, wakati wa ziara maalum iliyofanywa na Uongozi wa kampuni hiyo kwa ajili ya mafunzo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto) na Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mtahaba (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,( katikati ) alipokuwa akifafanua jambo juu ya utendaji mzuri wa kituo Clouds TV na Clouds FM, wakati alipouongoza Uongozi wa kampuni hiyo kutembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia ) akimsikiliza Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba(kushoto) alipokuwa akimuelezea jinsi shughuli mbalimbali za utangazaji zinavyoendeshwa na kituo hicho,wakati wa ziara maalumu iliyoongozwa na Mkurugenzi huyo kutembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao( kushoto ) alipotembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho,katikati Materi Mushi.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo(kushoto)akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kisasa ya EFM, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) Wakati wa ziara maalum ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam,kulia ni Mfanyakazi wa radio hiyo Kasampaida.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Redio ya EFM,Francis Ciza (Majey) baada ya Uongozi wa Vodacom Tanzania kutembelea ofisi hizo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kushoto)wakioneshwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio ya EFM, Denis Sebo progaramu mbalimbali za vipindi vinavyozalishwa na redio hiyo,wakati wa ziara maalum iliyofanywa kituoni hapo na Uongozi wa Vodacom Tanzania kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.0715351938

NDANI YA MASAA 20 WAZIRI MKUU KUTUMBUA JIPU BANDARI YA TANGA (TPA)

February 19, 2016



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitembelea bandari ya Tanga (TPA) Leo  wakati wa ziara ya kushtukiza na kuagiza kupatiwa maelezo ya ununuzi wa matishali matatu ambayo hayana uwezo  badala ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali na kutaka ndani ya masaa 20 taarifa hiyo iwe imeshafika ofisni kwake.
Majaliwa ambaye ametua Tanga kwa kushtukiza na kwenda bandari ya Tanga moja kwa moja kujionea mambo yaendavyo pia alitoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza pamoja na jeshi la Polisi kuongeza doria katika mwambao wa Bahari ya Hindi kuzuia mali za magendo pamoja na uingizaji wa Sukari kutoka nje ambayo imepigwa marufuku.
Alisema Mwambao wa Bahari ya Hindi upande wa Tanga ni kinara wa uingizaji wa mali za magendo hivyo kutaka kikomeshwa mara moja shughuli hizo na kuongeza kikosi kazi ya kupambana na mali za magendo










 Injinia wa Mamlaka Bandari Tanzania (TPA), Felex Mafinga, akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa  juu ya ununuzi wa matishali matatu ambayo hayana uwezo  badala ya mawili yaliyoidhinishwa na Serikali hivyo kuagiza kupatiwa maelezo ndani ya masaa 20 iwe imeshafika ofisini kwake.



MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA BAB YAKE WAZIRI WA AFYA

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA BAB YAKE WAZIRI WA AFYA

February 19, 2016

lim1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kaburini katika kaburi la  Baba Mzazi wa Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, jinsia ,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mzee Ali Mwalimu katika  mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la  Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
lim2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimpa pole Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakati aliposhiriki mazishi ya baba mzazi wa waziri huyo mzee Ali Mwalimu, nyumbani kwa marehemu eneo la  Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE MAREKANI

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE MAREKANI

February 19, 2016
UJ01Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.
UJ1Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakizungumza na Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Sweden waliotembelea Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.
UJ02Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
UJ2Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wkiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Sweden waliotembelea Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA MAKUNDI YALIYOSHIRIKI NAYE KWENYE KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015

February 19, 2016

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

 Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.




 Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

WAZIRI NAPE NNAUYE ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MICHEZO TANZANIA(BMT).

February 19, 2016

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo hii kuona utendaji wa Baraza hilo.
 Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar es Salaam kutokana utendaji usiolizisha.
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Dionis Malinzi(kulia) akiongea jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye. Picha na Daudi Manongi.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake. 
Mhe. Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo. 
“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye. 

Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009. 

Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana. 

Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini. 

Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.
NMB yakabidhi milioni 75 kusaidia Mkutano wa Makamanda Jeshi la Polisi

NMB yakabidhi milioni 75 kusaidia Mkutano wa Makamanda Jeshi la Polisi

February 19, 2016


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hilo. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hiloMkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hilo. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hilo.Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi katika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker wakiwa wamesimama wakati wimbo maalumu wa Jeshi la Polisi ukiimbwa na Maofisa Wakuu wa Jeshi hilo wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini.Mgeni rasmi katika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker wakiwa wamesimama wakati wimbo maalumu wa Jeshi la Polisi ukiimbwa na Maofisa Wakuu wa Jeshi hilo wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa wamesimama kwa ukakamavu huku wakiimba wimbo maalumu wa jeshi hilo. Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga. Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa wamesimama kwa ukakamavu huku wakiimba wimbo maalumu wa jeshi hilo. Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa wamesimama kwa ukakamavu huku wakiimba wimbo maalumu wa jeshi hilo. Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga. Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa wamesimama kwa ukakamavu huku wakiimba wimbo maalumu wa jeshi hilo. Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga.Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Benki ya NMB (kulia) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi unaoendelea jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB imesaidia baadhi ya gharama kuwezesha mkutano huo kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kufanyika kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya gharama.Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Benki ya NMB (kulia) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi unaoendelea jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB imesaidia baadhi ya gharama kuwezesha mkutano huo kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kufanyika kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya gharama.Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza machache katika kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kabla ya kukabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 75. Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hilo.Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi mfano wa cheki Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu (kulia). Benki ya NMB imedhamini mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 kwa kuchangia shilingi milioni 75 pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam. Katikati ni mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga akishuhudia tukio hilo.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakipata maelezo juu ya bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NMB. Benki ya NMB imesaidia baadhi ya gharama kuwezesha mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakipata maelezo juu ya bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NMB. Benki ya NMB imesaidia baadhi ya gharama kuwezesha mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016 unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa kwanza kushoto) kwa baadhi ya makamishna wa Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo unafanyika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi. Katikati (mwenye suti nyeusi) ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela.Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP-Ernest Mangu akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa kwanza kushoto) kwa baadhi ya makamishna wa Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo unafanyika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi. Katikati (mwenye suti nyeusi) ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela.Mgeni rasmi katika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga (kushoto), akizungumza leo kabla ya kuzinduwa rasmi kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kinaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi katika mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Muhangwa Kitwanga (kushoto), akizungumza leo kabla ya kuzinduwa rasmi kikao kazi cha maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kinaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na meza kuu.Baadhi ya Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wanaoshiriki mkutano kazi wa Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na meza kuu.