NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATAKA VIFAA VYENYE THAMANI YA SH 14 BILIONI VIFUNGWE HARAKA

January 22, 2018


Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(wa pili kuli) akiwapongeza wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kozi walizosomea

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(katikati),Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(wa pili kulia),Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wasichana.
Arusha.Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameuagiza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) uwe umefunga vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Sh 14 bilioni ndani ya wiki nne badala ya siku 67 ili vianze kutumika mara moja.

Ametoa agizo hilo kwenye mahafali ya tisa ya wahitimu 465 wa fani mbalimbali za ufundi jijini hapa  kuwa ukarabati na upanuzi wa karakana ufanyike ndani ya muda alioutoa ili vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

"Nilipotembelea Chuo hiki Desemba 2,mwaka jana nilitoa maagizo mharakishe ujenzi na ukarabati wa miundombinu itakayotumika kufunga vifaa hivyo kutoka Austria,nafarijika kusikia kuwa utaanza mara moja kwani Wizara ilishatoa kibali cha kutumia watalaam wenu wa ndani na fedha mnayo,"alisema Ole Nasha

Alisema sekta ya elimu ya ufundi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2015 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate maendeleo.

Ole Nasha aliongeza kuwa elimu ya ufundi ina mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda na nchi zilizoendelea kama Japan na China zimefikia hapo zilipo kwa kutilia mkazo elimu ya ufundi.

"Katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 hadi 2020/21 tunalenga  kuongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi(Veta) kutoka 150,000 hadi 700,000  na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyotoa elimu ya Kati kutoka 40,000 hadi 80,000,"alisema

Kuhusu idadi ya wasichana wanaosoma elimu ya ufundi kuwa ndogo alivitaka vyuo vyote vya ufundi nchini kuweka mikakati ya kuongeza udahili ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele maalum kwa kwa wanafunzi wa kike wanaomba kujiunga.

Pia aliagiza Mamlaka ya Elimu nchini(TEA)kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi cha Sh 1.7 bilioni kilichotengwa kwaajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana katika Chuo hicho ili kupunguza pengo katika wavulana na wasichana.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Masudi Senzia alisema wahitimu 465 wamemaliza katika ngazi za Astashahada ya awali,Astashahada ,Stashahada na Shahada  huku wahitimu wa kike ni 101 sawa na silimia 21  na wahitimu wa kiume  ni 364 sawa na asilimia 78.

MBUNGE MGIMWA NIPO TAYARI KUNYIMWA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2020

January 22, 2018
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa  akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao  kwa ajili ya faida ya maisha yao.

“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema walimu

Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.

“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.

Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu

Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

January 22, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Barala la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 22, 2018

PICHA NA IKULU

WATALII MILIONI 62 WALITEMBELEA AFRIKA 2017

January 22, 2018

Na Jumia Travel Tanzania


Idadi ya watalii duniani imekuwa kwa kiwango cha 7% mwaka 2017 na kufikia idadi ya milioni 1,322, kwa mujibu wa matokeo ya hivi karibuni yaliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).

 

Kulingana na takwimu zilizoripotiwa kutoka sehemu tofauti duniani, inakadiriwa kwamba idadi ya watalii waliowasili duniani kote imeongezeka kwa 7% mwaka 2017. Hii ni ishara nzuri au zaidi ya kiwango kilichokuwepo cha 4% kilichodumu tangu mwaka 2010, hivyo kuonyesha matokeo mazuri ndani ya miaka saba. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa Afrika ambazo Jumia Travel ingependa kukushirikisha, ukuaji katika mwaka 2017 ulikadiriwa kuwa wa 8%. Ilijiimarisha kama ilivyokuwa kwa mwaka 2016 na kuwa na matokeo mazuri yaliyofikia idadi ya watalii milioni 62 kutembelea kutoka mataifa tofauti duniani. Licha ya changamoto mbalimbali hususani za kisiasa, nchi za Kaskazini mwa Afrika zilirejea kuwa na matokeo mazuri kwenye sekta ya utalii ambapo idadi ilikuwa kwa 13%, wakati nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zenyewe idadi iliongezeka kwa 5%.

Mwaka 2017 ulitawaliwa na ukuaji endelevu kwenye maeneo mengi na kwa maeneo yaliyokumbwa na changamoto miaka iliyopita yaliimarika na kurejea hali zao za kawaida. Kwa kiasi kikubwa matokeo haya yamepelekewa na mabadiliko kwenye uchumi wa dunia na uhitaji mkubwa kutoka kwenye nchi nyingine na masoko mapya ya kitalii, hususani kuongezeka kwa matumizi makubwa kwenye nchi kama vile za Brazili na Urusi ambazo kwa miaka michache iliyopita zilikuwa zimeshuka kidogo. 

“Utalii wa kimataifa unaendelea kukua na thabiti, na kuifanya sekta ya utalii kuwa imara katika kuendesha shughuli za maendeleo ya uchumi. Ikiwa ni sekta ya tatu katika kuleta mapato ya kigeni duniani, utalii ni muhimu katika kutengeneza ajira na ustawi wa jamii duniani kote,” alisema Katibu Mkuu wa UNWTO Bw. Zurab Pololikashvili kwenye taarifa hiyo. “Bado tukiendelea kukua lazima tufanye kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha kwamba ukuaji huu unainufaisha kila jamii kwenye eneo walilopo, na tunakuwa sambamba kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu.” 

Ukuaji unatarajiwa kuendelea kwa mwaka 2018 

Kasi ya ukuaji imara uliopo hivi sasa inatarajiwa kuendelea mwaka 2018, tena katika kasi endelevu zaidi baada ya miaka 8 ya upanuzi wa kutosha kufuatia changamoto za kiuchumi na fedha mwaka 2009. Kulingana na mienendo ya sasa, matarajio ya kiuchumi na mtazamo kutoka kwa jopo la wataalamu wa UNWTO, UNWTO inatazamia idadi ya watalii kimataifa kwenye maeneo mbalimbali duniani kukua katika kima cha 4% mpaka 5% mwaka 2018. Kwa kiasi fulani hii ni juu kwa 3.5% ya ongezeko la wastani wa kawaida uliotazamiwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 mpaka 2020 na UNWTO katika utabiri wake wa Utalii Kuelekea 2030. Ulaya na Amerika zote zinatarijiwa kukua kwa 3.5% mpaka 4.5%, Asia na Pasifiki kwa 5% mpaka 6%, Afrika kwa 5% mpaka 7% na Mashariki ya Kati kwa 4% mpaka 6%.

 

Utalii Tanzania katika mwaka 2017


Mwaka 2017 ulikuwa ni wenye neema na mafanikio kwa upande wa Tanzania kwani ilishuhudia matukio makubwa kama vile kuja kwa watu mashuhuri kutembelea vivutio vya kitalii kama vile; Will Smith (mwanamuziki na mcheza filamu), David Beckham (aliyekuwa mcheza soka wa vilabu vya Manchester United, Real Madrid, AC Milan na PSG), Mamadou Sakho (aliyekuwa mchezaji wa Liverpool), Morgan Schneiderlin (mchezaji wa Everton) pamoja na ziara ya kikosi kizima cha timu ya Everton kutokea ligi kuu ya Uingereza.


Ujio wa watu hao mashuhuri nchini Tanzania ulisaidia kuipaisha sekta ya utalii kwani katika matembezi yao waliweza kushirikisha dunia uzuri wa nchi na vivutio tulivyonavyo duniani. Na kwa kiasi kikubwa ulizaa matunda kwani wengi zaidi waliendelea kumiminika. 

Mbali na watu hao mashuhuri pia viongozi mbalimbali wa kiserikali kutembelea kwenye vivutio vya kitalii nchini kulileta hamasa kwa wananchi pia. Mwezi Oktoba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu alipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Ngorongoro ambapo aliwahimiza watanzania kuendeleza juhudi za kuhifadhi na kutunza mazingira ya eneo hilo ili kuendelea kunufaisha kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. 

Lakini katika mwaka huo pia tulishuhudia mabadiliko kwenye sekta ya utalii ambapo Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala aliteuliwa na Mh. Rais John Magufuli kuwa Waziri wa Utalii na Maliasili ambapo kupitia uongozi wake mpya tunaona mabadiliko na jitihada za dhati katika kuendeleza sekta hii ambayo ina mchango mkubwa katika pato la ndani la taifa na ajira. 

Kwa upande wa miundombinu, serikali kwa kiasi kikubwa imeendelea kuimarisha sekta ya mawasiliano kama vile barabara, reli, maji na anga ambapo imefanya uwekezaji mkubwa. Sehemu nyingi nchini zimekuwa zinafikika kwa urahisi kutokana na maboresho ya barabara huku uwekezaji mkubwa ukiwekwa katika ujenzi wa reli na kuzifufua za zamani. 
Yapo mengi ya kuvuna kutoka kwenye sekta ya utalii kama vile ajira na fedha ambazo zinasaidia kukuza pato la taifa. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Benki ya Taifa (BoT), mapato ya nje yaliyotokana na sekta ya usafiri, hususani sekta ya utalii, yameongezeka kwa zaidi ya ilivyokadiriwa na kufikia shilingi bilioni 128.8. Mapato hayo yamekuwa na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2,156.9 katika mwaka ulioshia mwezi Novemba 2017, kutoka Dola za Kimarekani 2,101.2 mnamo mwezi Novemba mwaka 2016, ambapo imechangiwa na kuongezeka kuja kwa watalii.

Waziri Makamba akutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira

January 22, 2018
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kulia) akifuatilia hoja za wabunge  katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira hii leo mjini Dodoma.
 Sehemu ya waheshimiwa wabunge, Mhe. Mussa Ramadhani Sima na Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest wakifuatilia mawasilisho juu ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini, katika kikao cha Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira. Kikao hicho kimejumuisha pia wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo Mhe. Makamba amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kutotumia mifuko ya plastiki nchini.

TIgo wakabidhi zawadI kwa washindi wa promosheni ya mawakala

January 22, 2018
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akimkabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Mil 2 mshindi wa kwanza wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini ,Hassan Kusaga ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akimkabidhi mfano wa Hundi ya kiasi cha Sh Mil 1 mshindi wa Pili wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini ,Mwakilishi wa kampuni ya Real Statonary ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.


Washindi wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini  wakiwa katika picha ya pamoja  ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.


Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo,Henry Kinabo akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Promosheni ya Wakala wa Tigo kwa kanda ya Kaskazini  ,Promosheni hiyo iliyowashindanisha Mawakala wote wa mtandao wa Tigo  ilianza Desemba 1,mwaka jana ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 300 zimetolewa kwa washindi.


Waziri Dk. Kigwangalla kufungua onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika, Dar

January 22, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho Januari 23.2018, kwenye uzinduzi wa Onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika, tukio ambalo litafanyika majira ya saa 11 jioni katika viunga vya Makumbusho ya Taifa, yaliyopo mtaa wa Shabani Robert, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza wakati wa utambulisho wa tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla amebainisha kuwa, tayari maandalizi ya onesho hilo yameenda sawa na watu mbalimbali watanatarajiwa kushuhudia tukio ambalo ni la siku moja wakiwemo viongozi wa Serikali na Mabalozi waliopo nchini, na
watalii wanatarajiwa kuhudhuria.
Profesa Mabulla amebainisha kuwa, Vioneshwa vyote katika onesho hilo hapo kesho, vimepatikana hapa Tanzania kutokana na tafiti za kisayansi na vimehifadhiwa Makumbusho ya Taifa.
“Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe na
masalia ya wanyama walioishi takribani tangu miaka milioni 4 iliyopita. Pia zipo picha za zamadamu na mazingira waliyoishi wakifanya shughuli zao za kila siku.” alieleza Profesa Mabulla.
Kwa upande wake Mratibu kwa upande wa Tanzania Dk. Agness Gidna amesema Onesho limegawanyika katika sehemu kuu nne zikiwemo Makumbusho ya Taifa la Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Spain Tanzania. Hii ni pamoja na Makumbusho ya Akiolojia ya
Madrid, Taasisi ya Chimbuko la Binadamu (IDEA) Madrid, Chuo Kikuu cha Alcala Madrid na Makumbusho ya CosmoCaixa Barcelona-Spain huku tamasha zima likidhaminiwa na Kampuni ya Simenti ya Twiga.
“Tunawashukuru kampuni ya Twiga Cement kwa kudhamini onesho la Chimbuko
la Binadamu Afrika (The Cradle of Humankind in Africa). Pia kutakuwa na Semina na onesho hili ni matokeo ya tafiti mbali mbali zinazofanyika bonde la Olduvai na Laetoli, Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro.” alieleza Dk Agness.
Aidha Dk.Agness ameongeza kuwa, Onesho hilo litakuwa katika pande nne ikiwemo sehemu ya kwanza inahusu ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dkt. Mary D. Leakey. Nyayo hizo ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ni ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea
wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopia.
Sehemu ya pili inahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu (Genus Homo) ambapo kuna masalia ya zamadamu Zinjanthropus au Paranthropus boisei na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo (Oldowan) zilizotumika katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 2 iliyopita.
Sehemu ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus. Jamaii hii inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko jamii zilizotangulia. Kuna masalia ya zamadamu Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na ushahidi wa ulaji wa wanyama wakubwa kama vile tembo na nyati wa zamani takribani miaka million 1.7 iliyopita.
Sehemu ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea hapa Afrika miaka laki 2 iliyopita. Kuna masalia ya Homo sapiens na zana za mawe za muhula wa kati na muhula wa mwisho.
Mbali na onesho hilo, pia waandaji hao wa Makumbusho ya Taifa inawakaribisha watu wote kuhudhuria semina na ufunguzi wa onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika.
Kwa upande wa Semina ambayo inatarajia kuanzia majira ya saa tisa kamili itaendeshwa na watafiti wa Kimataifa, akiwemo Prof. Manuel Dominguez-Rodrigo wa Chuo Kikuu cha Complutense, Spain; Prof. Audax ZP Mabulla na Dk. Agness Gidna.
Na Andrew Chale
Waziri Dk. Kigwangalla kufungua onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika, Dar




Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho Januari 23.2018, kwenye uzinduzi wa Onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika, tukio ambalo litafanyika majira ya saa 11 jioni katika viunga vya Makumbusho ya Taifa, yaliyopo mtaa wa Shabani Robert, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza wakati wa utambulisho wa tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla amebainisha kuwa, tayari maandalizi ya onesho hilo yameenda sawa na watu mbalimbali watanatarajiwa kushuhudia tukio ambalo ni la siku moja wakiwemo viongozi wa Serikali na Mabalozi waliopo nchini, na
watalii wanatarajiwa kuhudhuria.
Profesa Mabulla amebainisha kuwa, Vioneshwa vyote katika onesho hilo hapo kesho, vimepatikana hapa Tanzania kutokana na tafiti za kisayansi na vimehifadhiwa Makumbusho ya Taifa.
“Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe na
masalia ya wanyama walioishi takribani tangu miaka milioni 4 iliyopita. Pia zipo picha za zamadamu na mazingira waliyoishi wakifanya shughuli zao za kila siku.” alieleza Profesa Mabulla.
Kwa upande wake Mratibu kwa upande wa Tanzania Dk. Agness Gidna amesema Onesho limegawanyika katika sehemu kuu nne zikiwemo Makumbusho ya Taifa la Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Spain Tanzania. Hii ni pamoja na Makumbusho ya Akiolojia ya
Madrid, Taasisi ya Chimbuko la Binadamu (IDEA) Madrid, Chuo Kikuu cha Alcala Madrid na Makumbusho ya CosmoCaixa Barcelona-Spain huku tamasha zima likidhaminiwa na Kampuni ya Simenti ya Twiga.
“Tunawashukuru kampuni ya Twiga Cement kwa kudhamini onesho la Chimbuko
la Binadamu Afrika (The Cradle of Humankind in Africa). Pia kutakuwa na Semina na onesho hili ni matokeo ya tafiti mbali mbali zinazofanyika bonde la Olduvai na Laetoli, Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro.” alieleza Dk Agness.
Aidha Dk.Agness ameongeza kuwa, Onesho hilo litakuwa katika pande nne ikiwemo sehemu ya kwanza inahusu ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dkt. Mary D. Leakey. Nyayo hizo ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ni ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea
wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopia.
Sehemu ya pili inahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu (Genus Homo) ambapo kuna masalia ya zamadamu Zinjanthropus au Paranthropus boisei na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo (Oldowan) zilizotumika katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 2 iliyopita.
Sehemu ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus. Jamaii hii inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko jamii zilizotangulia. Kuna masalia ya zamadamu Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na ushahidi wa ulaji wa wanyama wakubwa kama vile tembo na nyati wa zamani takribani miaka million 1.7 iliyopita.
Sehemu ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea hapa Afrika miaka laki 2 iliyopita. Kuna masalia ya Homo sapiens na zana za mawe za muhula wa kati na muhula wa mwisho.
Mbali na onesho hilo, pia waandaji hao wa Makumbusho ya Taifa inawakaribisha watu wote kuhudhuria semina na ufunguzi wa onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika.
Kwa upande wa Semina ambayo inatarajia kuanzia majira ya saa tisa kamili itaendeshwa na watafiti wa Kimataifa, akiwemo Prof. Manuel Dominguez-Rodrigo wa Chuo Kikuu cha Complutense, Spain; Prof. Audax ZP Mabulla na Dk. Agness Gidna.
Na Andrew Chale,
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi hiyo kesho Januari 23.2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tukio hilo linalotarajiwa kufanyika kesho Januari 23.2018.
 Balozi wa Spain nchini, Bw. Felix Costales akizungumza katika tukio hilo mapema leo Januari 23,2018. Kulia kwake ni  Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla
Tukio hilo likiendelea 
Mratibu kwa upande wa onesho hilo kwa Tanzania, Dk. Agness Gidna akionesha maandalizi kwa wanahabari (hawapo pichani) namna itakavyokuwa hapo kesho wakati wa tukio
Baadhi wanahabari wakiangalia Vioneshwa ‘visukuku’ wakati wa tukio hilo la utambulisho 
Vionesho ambavyo vinatarajiwa kuwapo kesho katika tukio hilo
Afisa kutoka ubalozi wa Spain akipata maelezo kutoka kwa Mratibu upande wa Tanzania Dk. Agness Gidna  wa Makumbusho ya Taifa. Kulia ni Balozi wa Spain Bw. Felix Costales 
Afisa kutoka ubalozi wa Spain akipata maelezo kutoka kwa Mratibu upande wa Tanzania Dk. Agness Gidna  wa Makumbusho ya Taifa. Kulia ni Balozi wa Spain Bw. Felix Costales 
Vioneshwa kinachoelezea hatua za binadamu wa kale katika makumbusho ya Taifa ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajiri ya kesho
Vioneshwa kinachoelezea hatua za binadamu wa kale katika makumbusho ya Taifa
Vioneshwa ambavyo vinatarajiwa kuwepo kesho.
Moja eneo la bango la Chimbuko la Binadamu wa Kale. (Picha zote na Andrew Chale)









--

Andrew Chale

Blogger Personality | Journalist | Activist | Online Editor dewjiblog | Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals 2007 to present.

Telephone: +255222122830 Fax: +255222126833
Golden Jubilee Towers, Ohio Street,20th Floor
Po Box 20660, Dar es Salaam,Tanzania