BANDARI TANGA YAKABIDHI VITANDA 10 VYA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA WAJAWAZITO WILAYANI PANGANI

April 13, 2018

Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimkabidhi vitanda 10 leo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito ambavyo vimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ambavyo vinagharimu kiasi cha milioni 12.2 kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimkabidhi vitanda 10 leo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito ambavyo vimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ambavyo vinagharimu kiasi cha milioni 12.2 kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimkabidhi vitanda 10 leo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito ambavyo vimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ambavyo vinagharimu kiasi cha milioni 12.2 kulia anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Daudi Mlahangwa
Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimpongezwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya kukabidhi vitanda hivyo katika anayeshughudia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa

Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa katika akimkabidhi Vitanda 10 vilivyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Daudi Mlahangwa kwa ajili ya wilaya ya Pangani kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama akishughudia
Mganga mkuu wa wilaya ya Pangani (DMO) Juma Mfanga kulia akitolea vitanda 10 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Daudi Mlahangwa vilivyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA)
Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wilaya ya Pangani Zainabu Issa katikati ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
Sehemu ya vitanda 10 vilivyotolewa na TPA





WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

April 13, 2018

Watafiti wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada zao za kufanya utafiti.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).

Bw. Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo kupelekea kuongeza makusanyo.

“Nina imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika kupitia utafiti mtakaoufanya”.

Aidha amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.

Naye Mkuu wa Chuo cha Kodi Pro. Isaya Jairo ameishukuru ATAF na TRA kwa kukiamini Chuo cha Kodi kuendesha mafunzo kwa watafiti ambao wametoka nchi mbalimbali za Afrika. Ambapo pia amewapongeza washiriki hao kwa kupatiwa nafasi kushiriki mafunzo hayo akisema kwamba ushiriki wao unadhihirisha utayari wa mamlaka za mapato barani Afrika kutatua changamoto zilizopo kwa kuwa na watafiti wenye weledi na ujuzi.

Awali akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa Bw. Alfred Mregi alisema kwamba Usimamizi wa Kodi katika Afrika unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo watafiti wanategemewa kuzitatua ili taasisi zinazosimamia mapato Afrika ziwe rafiki kwa walipakodi na hatimaye kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani.

“Tunawategemea nyinyi kufanya utafiti wa mifumo ya kodi na kutoa suluhisho na mapendekezo kwa watunga sera na wasimamizi wa kodi”, alisema Bw. Mregi.

Warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti Afrika iliwashirikisha watafiti kutoka baadhi ya nchi za Afrika ambao mapendekezo yao ya utafiti yamekidhi vigezo kwa mujibu wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika ambayo inaratibu Mtandao wa Wasimamizi wa Kodi Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo waafrika kufanya utafiti katika usimamizi, sheria na sera za kodi na kuwaunganisha watafiti hao na wanataaluma.

Washiriki wa warsha hii ambayo ni ya Tatu kufanyika, wameishukuru ATAF na Chuo cha Kodi kwa kuendesha mafunzo hayo wakisema kwamba imewapa uelewa zaidi wa kuendelea na utafiti wao.

Mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa kwa lugha tatu: Kireno, Kifaransa na Kiingereza yaliwashirikisha washiriki 24 kutoka, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Niger, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Togo, Benin, Cape Verde, Tunisia, Ivory Coast, Kenya na Tanzania.
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI LEO TAREHE 13 APRILI, 2018 BUNGENI MJINI DODOMA

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI LEO TAREHE 13 APRILI, 2018 BUNGENI MJINI DODOMA

April 13, 2018


V25A9305
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mheshimiwa Saul Amon (kushoto) leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mwenye miwani), anaefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole na wengine ni Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake ambao ni wageni wa Naibu Spika wa Bunge.
V25A9334
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na mmoja ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Victor Mwambalasw
V25A9240
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Viziwi kutoka Mkoa wa Dodoma pamoja na Shule ya Sekondari Tagamenda kutoka Mkoa wa Iringa wakifuatilia mijadala inayoendelea ndani ya Bunge ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya Mafunzo Bungeni.
V25A9250
Viongozi  Mbali mbali  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake wakifuatilia jinsi muhimili wa Bunge unavyofanya kazi yake, leo katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
V25A9331
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa saba kulia mbele), Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (wa tisa kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya yake leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. Wa nane kulia mbele ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole
(PICHA NA OFISI YA BUNGE

SALAMBA MCHEZAJI BORA MWEZI MACHI LIGI KUU YA VODACOM

April 13, 2018
MSHAMBULIAJI wa Lipuli ya Iringa, Adam Salamba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.

Salamba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salum Kimenya wa Prisons na kipa wa Azam, Mwadini Ally katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo hizo.

Mshambuliaji huyo kwa Machi alionesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kupata mafanikio akifunga mabao matatu kwa dakika 270 alizocheza, ambapo Lipuli ilicheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nane hadi ya saba kwa mwezi huo.

Kwa upande wa Kimenya alicheza dakika 269 na kufunga mabao mawili, akiiwezesha Prisons kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kutoka sare mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya tano hadi ya nne.

Mwadini yeye alicheza dakika zote 270 ambazo timu yake ilicheza kwa mwezi Machi, ikishinda michezo yote mitatu iliyocheza, ikibaki katika nafasi yake ya tatu.

Kutokana na ushindi huo, Salamba atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).

Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco (Januari) na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari).

Tuzo za Mchezo Bora wa jumla wa Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu katika tarehe itakayotangazwa, ambapo licha ya Mchezaji Bora, pia kutakuwa na tuzo nyingine tofauti kwa kategori mbalimbali.