MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI TANGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI HUMO LEO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI TANGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI HUMO LEO

February 28, 2016

LU1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo leo Februari 28, 2016
LU2
Chipukizi wa Umoija wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum oleo Februari 28,2016.
LU3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo leo Februari 28,2016.
LU4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
LU5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha na OMR)
MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA

MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA

February 28, 2016

hal1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ma  Mwanaidi Mussa  na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji cha Nandagala wilayani  Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti  watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti  watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

February 28, 2016
IMG_4204
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow.
Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za barabarani.
“Tumeamua kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa … tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
"Tunashukuru sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo," alisema Bi. Helen.
Alizitaja baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba, Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana, Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini Rwanda.
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mbio hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.
Alisema kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika kufanikisha mbio hizo.
Henning Nathow
Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.
Nae Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio na lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi kufanya mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na umasikini.
Alisema wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda watayakabidhi magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada ya hapo watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali ya Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.
“Elimu ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na sisi tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia kupatikana kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Helen Peter
Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Eric Potin
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Eric Potin
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Volkswagen Tanzania
Pichani juu na chini ni kati ya magari 18 yaliyoondoka nchini jana kuelekea Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Volkswagen, Tanzania
IMG_4332
Msafara wa magari aina ya Volkswagen yanayoelekea nchini Rwanda yakitoka kwenye 'showroom' ya Volkswagen iliyopo kampuni ya CFAO Motors Group, barabara ya Pugu jijini Dar.
Volkswagen Tanzania

DC MAKONDA AANZISHA MPANGO WA WALIMU KUPANDA BURE DALADALA NCHINI

February 28, 2016


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu mpango aliouanzisha wa walimu kutotoa nauli kwenye daladala wakati wa kwenda na kurudi nyumbani wanapotoka kazini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DACOBOA), Sabri Mabrouke.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DACOBOA), Sabri Mabrouke (kushoto), akizungumzia mpango huo ambao wameuunga mkono. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Shaban Mdemu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (DACOBOA), William Masanja.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (DACOBOA), William Masanja (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Shaban Mdemu (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
 Mwonekano wa meza kuu katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
............................................................
 Taarifa kwa Umma kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.


Moja ya jambo ambalo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa John Pombe Magufuri imelifanya kuwa kipaumbele kikubwa kwenye mipango yake ya kimaendeleo ni suala la uboreshaji wa sekta ya elimu nchini na ndio maana serikali imeanza utekelezaji wa mpango huu kwa kufuta ada zote mashuleni.

Kimsingi ni ndoto hii ya Mheshimiwa Raisi ambayo nina hakika kila mmoja wetu anaelewa ukubwa wa faida zake kwenye ujenzi wa Tanzania mpya na yenye wasomi na wataalamu wa kila namna tena wanaopatikana bila kuzingatia hali ya kipato cha familia anayotokea mwanafunzi, iliyonifanya mimi kama msaidizi wake katika nafasi ya ukuu wa wilaya nijiulize kila wakati juu ya ushiriki wangu wa kuhakikisha inatimia kikamilifu. 

Maswali ambayo yamenifikisha kwenye wazo la kuboresha sekta hii kwa kuchagua kufanya jambo ambalo wakati serikali ikiendelea kupigania changamoto nyinginezo za kuboresha ajira za walimu ikiwemo upandishwaji wa madaraja na mishahara, basi na mimi katika nafasi yangu nishiriki kwenye mchakato huu mzima kwa kutoa motisha ya usafiri wa bure kwa walimu wote wanaofundisha kwenye shule za serikali zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa tatu. 

Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia. 

Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.

Kwasababu hizo nilizozianisha hapo juu ninaomba kuwatangazia walimu wangu wa shule zote za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari ya kwamba, sasa watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao. 

Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na hatimaye mazungumzo hayo kuitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.

Kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwa wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wameseme ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.

Utaratibu kwa walimu juu ya utumiaji wa fursa ambayo tumeipata utakuwa kama ifuatavyo:- Moja, nimemuelekeza ofisa elimu wa sekondari na shule za msingi, kutoa maelekezo kwa wakuu wa shule zote za serikali zilizopo wilayani kwangu na wilaya nyinginezo za jiji la Dar es Salaam, kutengeneza vitambulisho vya shule zao vitakavyokuwa na picha ya mwalimu, jina lake kamili, jina la shule anayofundisha, namba ya simu ya mkuu wa shule husika pamoja na saini yangu mimi mwenyewe Paul Makonda ili kuepuka udanganyifu.

Nimewataka zoezi hili walifanye na kulikamilisha ndani ya wiki moja ambapo baada tu ya kukamilika itakuwa ni furaha yangu kuwatangazia walimu wote wa shule za serikali jijini Dar es Salaam kuwa, watakuwa wakipanda daladala bure ila tu kwa siku za jumatatu mpaka Ijumaa na kwa muda wa saa kumi na moja asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na kati ya saa tisa mpaka saa kumi na mbili jioni. Ingawa, kila mwalimu atalazimika kuonyesha kitambulisho chake alichotengenezewa kwenye shule yake pamoja na kile cha ajira ya serikali




VIDEO: WAZIRI DKT. MAHIGA AZUNGUMZIA MKUTANO WA WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA UZINDUZI WA BARABARA YA ARUSHA-HOLILI/TAVETA-VOI

February 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na  Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Lekule Laizer baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiendelea kusalimia viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassary katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mhe CAtherine Magige baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa dini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Afande Liberatus Sabas  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamanda wa JWTZ  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Bw. Elishilia Kaaya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia kikundi cha utamaduni cha Chuo Kikuu cha Tumaini cha Makumira mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akipiga ngoma baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia burudani ya ngoma ya Mdumange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia ngoma ya kinamama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akipungia wanannchi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana kwa furaha na aliyekuwa Katibu Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Samweli Kasori mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Picha zote na IKULU