RC KANAL THOMAS ATAKA GST KUSOGEZA HUDUMA ZA MAABARA RUVUMA

September 19, 2023












*Amepokea Vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania kwa shangwe*

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas ametoa wito kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kufungua tawi katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa Makaa ya Mawe ikiwemo Mkoa wa Ruvuma. 

Kanal Thomas ameyasema hayo Ofisini kwake wakati akipokea toleo la Vitabu vipya vinavyoonesha Madini yapatikanayo Tanzania vya Mwaka 2023 vilivyoandaliwa na GST.

Amesema uzalishaji wa Makaa ya Mawe unafanyika kwa kiwango kikubwa mkoani humo ambapo wafanyabiashara wanatumia mianya ya kuto kuwa na maabara ya kutambua ubora wa Makaa hayo kupunguza bei ya bidhaa hiyo, hivyo ameiomba GST kusogeza huduma hiyo ili kuwapunguzia adha ya kusafirisha sampuli kupeleka nje ya nchi kwa ajili ya vipimo.

Aidha, amesema ameuongoza Mkoa huo kwa muda mrefu na hakuwahi kujua kuwa Mkoa huo una Madini mengi mbali na yale waliyozoea kuona yanavunwa ambapo ameahidi kusambaza taarifa za Madini yapatikanayo Mkoani humo kwa wadau mbalimbali pamoja na kuhuisha taarifa za madini kwenye website ya Mkoa  kwa lengo la kutafuta Wawekezaji.

Kwa upande wake, Meneja wa Sehemu ya Jiolojia Solomon Maswi amesema, jukumu kubwa la GST ni kufanya tafiti za madini, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na madini na kuratibu majanga ya asili ya jiolojia.

"Leo tumekuja ofisini kwako mahususi kukukabidhi Vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania ili uweze kujua rasilimali zilizopo mkoani kwako ambalo ni agizo la Waziri Mkuu ili kuvutia uwekezaji mkubwa katika eneo lako," amesema Maswi.

Pamoja na Mambo mengine, Maswi amesema Mkoa wa Ruvuma una madini mbalimbali tofauti na wadau wajuavyo kuwa ni Makaa ya mawe, urani na vito pekee, hivyo Kitabu hicho kinaonesha Madini hayo katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata mpaka Kijiji na hivyo kitasaidia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha Wawekezaji kuja kufanya utafiti wa kina.

PROF. BISANDA: WAHITIMU NI CHACHU YA MAENDELEO

September 19, 2023

 

WAHITIMU (Alumni) ni Rasilimali muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ikiwemo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda, pembeni ya kikao cha Baraza la Seneti kilichoketi Septemba 18, 2023 Makao Makuu ya Chuo, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

"Wahitimu ni wadau wakubwa katika kuleta chachu ya maendeleo katika Chuo chetu kwani kupitia wao tunaweza kupata mrejesho wa kile wanachofanya na kuboresha mitaala yetu kwa lengo la kukidhi mahitaji ya soko la ajira. Pia, Alumni ni mabalozi na wajumbe wa kukisemea vizuri Chuo na kukifanya kifahamike kwa jamii na kisha kutoa mchango wake wa kukuza na kuendeleza Rasilimali watu kwa maendeleo ya Taifa letu." Amesema Prof. Bisanda.

Kutokana na umuhimu wa Alumni, Prof. Bisanda, amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimepanga kufanya Mkutano mkubwa wa Alumni wote utakaofanyika Septemba 21, 2023 jijini Dodoma kwenye Kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania cha jijini hapo, kuanzia Saa Mbili Kamili Asubuhi.

Kupitia Mkutano huu Alumni wote watapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kutoa mrejesho wa namna gani masomo waliyosoma yamewasaidia katika soko la ajira, kutoa huduma bora kwa wananchi na changamoto walizokumbana nazo ili tuendelee kuimarisha mtaala hasa katika kipindi hiki ambapo tunaendelea na kazi ya Mapitio ya Mitaala ya programu zetu zote.

Prof. Bisanda ametumia fursa hii pia kuwaalika Alumni wote kushiriki mkutano huo adhimu ambao utakuwa na mambo mengi mazuri yakiwemo ya uchaguzi wa viongozi na kupanga mikakati ya kuendeleza Chama cha Alumni cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.



MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WAHITIMU VYUO VIKUU NCHINI KUANZA SEPTEMBA 25,2023

September 19, 2023

 NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) inatazamiwa kuwafikia vijana wahitimu takribani 1,200 katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania ambayo yanatarajia kuanza Septemba 25 hadi Oktoba 12,2023 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika Mikoa mingine ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Lindi, Kusini Pemba na Mjini Magharibi mafunzo hayo yataanza Oktoba 16 hadi 20,2023.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ubunifu na Ujasiriamali, Prof. Hannibal Bwire amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vijana uelewa, taarifa, maarifa, Ujuzi na uwezo wa kuainisha fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia fursa hizo kwa kuanzisha ajira kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.

"Utoaji wa Mafunzo haya ni mojawapo ya harakati za UDSM katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini". Amesema Prof.Bwire

Aidha amesema kuwa washiriki watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa biashara na kuungana na taasisi za Serikali na binafsi zinazotoa huduma kwa wajasiriamali kama vile SIDO, TBS, TRA, BRELA, TANTRADE, Manispaa za mikoa husika na baadhi ya washiriki waliokwishapata mafunzo hayo mwaka 2019, 2021 na 2022.

Amesema Mafunzo yatatotolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa,na washiriki wa mafunzo hayo watajigharamia usafiri na malazi na gharama nyingine zitagharamiwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

"Tunawahimiza washiriki wanaopenda kujiunga na mafunzo haya kujisajiri kujaza fomu ya maombi iliyo mtandaoni kwenye tovuti ya udsm-gep.ac.tz/ na kwa mwaka huu tunahamasisha vijana na vikuundi walio hitimu Elimu ya juu na ambao hawana Elimu ya juu fursa hii imetolewa tu kwa mikoa ya Dar es Salaam,Iringa na Lindi"Amesema.

Kwa upande wake Mratibu-Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Winnie Nguni amesema mafunzo hayo yanalenga kumuimarisha kijana kuweza kutengeneza bidhaa ambayo itauzika na kuweza kumfikisha katika mahala ambapo anaweza kusaidia na wengine kupitia biashara yake.

Dkt.Winnie amesema mpaka sasa wamehudumia Zaidi ya Vyuo 70 na katika mikoa mingi vijana wengi wana uhitaji wa mafunzo hayo.

"Kijana akiwa na biashara yake akiendesha kisomi mafanikio yake ni makubwa kuliko yule ambaye hakupata nafasi ya kusoma elimu ya juu"Amesema.

Nae Mwezeshaji wa Mafunzo ya Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Biashara, Dkt.Theresia Busagara amesema kupitia mafunzo hayo chuo kina kuwa kimetoa fursa nzuri ya usimamizi wa fedha hivyo kuwa rahisi kwa urejeshaji wa mikopo na usimamizi wa kifedha kwa wahitimu wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yamebeba kauli mbiu isemayo "BADILI CHANGAMOTO KUWA FURSA",iliyo lenga kubadiri Mtizamo wa Vijana ili kuziona changamoto na kuzigeuza kuwa Fursa.

Mkurugenzi wa Ubunifu na Ujasiriamali, Prof. Hannibal Bwire akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.
Mratibu-Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Winnie Nguni akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.

Mwezeshaji wa Mafunzo ya Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Biashara, Dkt.Theresia Busagara akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.

DRC KONGO KUJIFUNZA UONGEZAJI THAMANI MADINI TANZANIA

September 19, 2023




 
Afisa Biashara kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Nchini Bw. Marcel Kasongo Yampanya amewasilisha nia ya Serikali ya Kongo kuleta Vijana wengi nchini Tanzania kujifunza Uongezaji Thamani wa Madini ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) cha jijini Arusha.

Ameyabainisha  hayo  wakati wa mazungumzo yake na viongozi wa kituo cha TGC baada ya kukitembelea  Septemba 19, 2023 katika ziara iliyolenga kujifunza na kuona namna ya kushirikiana na kituo hicho katika masuala ya Uongezaji Thamani Madini ya Vito  pamoja na kuhakikisha ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili katika kukuza sekta hiyo ndogo.

Ziara hiyo  inakuja wakati ambapo  nchi ya Kongo imeonyesha nia ya kukuza sekta ya madini ya vito na kuleta vijana wa Kongo kujifunza kutoka kwa wataalam  wa Tanzania ambao wamekuwa wakiongoza katika  utoaji wa mafunzo ya uongezaji thamani wa madini ya vito kwa upande wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Aidha, sehemu kubwa ya wakufunzi wa kituo hicho tayari wamepata utaalam wa shughuli hizo kutoka nchi mbalimbali zilizoendelea katika eneo hilo ikiwemo Thailand, India na China.

Aidha, ziara hiyo ya Afisa biashara wa Kongo imekuja ikiwa zimepita siku chache tu baada ya ujumbe wa Tanzania kutembelea shughuli za uongezaji thamani madini katika viwanda vikubwa, vya kati na vidogo nchini Thailand ambapo shughuli hizo zimeshamiri kwa kiasi kikubwa. Katika ziara hiyo, Mratibu wa Kituo hicho pia alikuwa sehemu ya ujumbe huo.

Katika ziara ya hivi karibuni  nchini  Thailand, Wizara ya Madini kupitia kituo hicho ilifanya mazungumzo  na taasisi kadhaa kuhusu  namna ya kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uongezaji thamani  ikiwemo  kiwanda kikubwa chenye uzoefu wa miaka 50 katika  shughuli za uongezaji thamani madini ambapo wadau nchini humo walifungua milango kwa watanzania  kujifunza ili kuwa bora katika eneo hilo.

Katika kikao hicho, Kaimu Mratibu wa TGC Bw. Daniel Kidesheni amepokea ahadi ya balozi na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri kati ya taasisi hizo mbili. Amesisitiza umuhimu wa kubadilishana uzoefu na kuendeleza teknolojia za kisasa ili kuhakikisha kuwa sekta  ndogo ya madini ya vito inachangia  katika ukuaji wa uchumi na maendeleo katika nchi hizo.

Katika ziara hiyo,  Bw. Kasongo  amepata fursa ya kutembelea karakana mbalimbali za TGC, ikiwa ni pamoja na maabara za kisasa zinazotumika kwa uchunguzi wa madini ya vito, usonara na ukuataji na ung’arishaji wa madini ya Vito.

Ziara hiyo ya Afisa biashara kutoka ubalozi wa Kongo nchini Tanzania imekuwa hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ndogo ya madini ya vito.

MABEHEWA YA SGR KUKAMILIKA KWA WAKATI KOREA

September 19, 2023

 Na. Saidina Msangi, WF, Busan, Korea Kusini


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, na Treni ya mwendokasi vinavyotengenezwa na kampuni za Hyundai Rotem na Sing Sung Rolling Stock Technology (SSRST) za Korea Kusini.

Alisema hayo mara baada ya kutembelea kampuni hizo zilizopo katika mji wa Changwon, Korea ya Kusini, zilizoingia mkataba na Serikali ya Tanzania, wa kutengeneza mabehewa 59 na vichwa vya treni 17 pamoja treni za Mwendokasi (Electric Multiple Unit) 10.

‘‘Kwa kampuni zote mbili maendeleo ni mazuri kwa hatua iliyofikiwa na wametueleza kuwa wanatarajia kukamilisha utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni kama ilivyoainishwa katika makubaliano, na kwa kweli tuliyoyaona yako katika hali nzuri’’alisema Bi. Amina.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa sekta husika kuhakikisha kuwa inatoa mafunzo kwa watakao husika na kuendesha, kuhudumia treni hizo wanajengewa uwezo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma bora kwa uendelevu.

‘‘Tunashauri wenzetu watakaosimamia uendeshaji wa treni hizi kwa Tanzania wajengewe uwezo wa uendeshaji na utunzaji ili mabehewa na vichwa viendelee kuwa na ubora huu kwa ajili ya huduma na pia yaweze kudumu kwa muda mrefu’’, alisisitiza Bi. Amina.

Ujumbe wa Tanzania ulikuwa Busan Korea ya Kusini kuhudhuria mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini ambapo Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Majaribio Dongjin Son, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni ya mwendo kasi, ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea kiwanda hicho Changwon, Korea Kusini. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akipewa maelezo na Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Majaribio wa Kampuni ya Hyundai Rotam, Dongjin Son, pamoja na kutazama hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mabehewa, wakati ujumbe wa Tanzania ulipotembelea kiwanda hicho Changwon, Korea Kusini.
Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa moja ya kichwa cha treni, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni ya Hyundai Rotam, Kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni Changwon, Korea Kusini.
Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa moja ya kichwa cha treni wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni ya Hyundai Rotam, kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni Changwon, Korea Kusini.
Muonekano wa moja ya behewa linaloendelea kutengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea kampuni hiyo kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini.
Muonekano wa ndani wa moja ya behewa linaloendelea kutengenezwa katika kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea Kampuni hiyo kuona maendeleo ya utekelezaji wa utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara hiyo na viongozi wa Kampuni ya Hyundai Rotam, wakati ujumbe wa Tanzania ulipotembelea kampuni hiyo, kuona maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, Changwon, Korea Kusini. Kulia kwake ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje. Bw. Melckzedeck Mbise, Kamishna Idara ya Fedha za Nje Bw. Rished Bade na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Nuru Ndile.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Korea Kusini)
WAZIRI NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

WAZIRI NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

September 19, 2023

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha  ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea  kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM.

Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya  wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea  umezalisha  ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za  kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati  na kuwa na  tija kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.

Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri pamoja na viongozi na watendaji yake na Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea Itracom Fertilizer mara baada ya kukagua utekelezaji wa sheria za kazi katika kiwanda hicho tarehe 18 Septemba, 2023 jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kiwanda cha Itracom, Kimramzilo Nkurikiye.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoani Dodoma akiambatana na Viongozi wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wengine  katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa kiwandani hapo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Intracom Fertilizer Limited Dkt. Keneth Masuke (kushoto) wakati wa ziara hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiangalia Mchanga aina ya Phosphete unaotumika kutoa sumu kwenye udongo kabla ya kupanda mazao. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha Itracom Fertilizer Limited wakati wa ziara hiyo.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited, Kimaramuziro Nkurikiye akitoa taarifa kuhusu kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye UlemavuProf. Joyce Ndalichako (kushotokatika kiwanda hicho Mkoani Dodoma.

Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa (kushoto) akitoa taarifa ya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria za kazi katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako katika kiwanda hicho Mkoani Dodoma.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

BANDARI YA KILWA KUCHOCHEA UCHUMI

BANDARI YA KILWA KUCHOCHEA UCHUMI

September 19, 2023

 


Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Bandari ya Kilwa iliyopo mkoani Lindi imekua ikitumika zaidi kwa shughuli za utalii na kwa kiasi kidogo shughuli za uvuvi.

Kwa kuwa mkakati wa Serikali ni kukuza sekta za uvuvi na utalii nchini, imeanza kutekeleza mradi wake wa kimkakati wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa, sambamba na kusaidia wananchi kunufaika na raslimali za bahari.

Akizungumza leo katika Wilaya ya Kilwa eneo la Kilwa Masoko wakati akiweka jiwe la msingi katika Bandari ya Uvuvi Kilwa na kugawa boti za kisasa 160 kwa wavuvi, ikiwa ni mradi wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 280 Mhe. Rais Samia amesema kuwa Serikali imefanya tukio muhimu la kihistoria kwa kujenga Bandari hiyo ya kwanza ya Uvuvi nchini.

” Boti hizi 160 zimetolea kwa mkopo wa masharti nafuu na unalenga kutoa ajira na kuongeza kipato cha jamii. Boti ndogo zitatumiwa na akina mama kulima mwani na kubeba mizigo, na zile kubwa zinakwenda kwenye kina cha maji
marefu “, ameeleza Rais Samia.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema kuwa Serikali haitarajii boti hizo kuleta ugomvi katika vikundi vya wakulima na wavuvi bali zitumike kuimarisha uchumi wao.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa kati ya boti hizo zipo ndogo na zenye ukubwa wa mita14 na uwezo wa kuhifadhi samaki hadi tani moja na nusu.

“Tunakushuru Mhe. Rais kwa kutupa fedha shilingi bilioni 11.5 zitakazowasaidia wavuvi na kazi imeanza. Leo unajenga bandari ya kwanza ya wavuvi, bandari hii inakwenda kuinua uchumi kupitia sekta ya uvuvi kutoka asilimia 1.8 hadi kumi kufikia mwaka 2036, hiyo itawezekana kwa kuwakaribisha wawekezaji wakubwa duniani”, ameeleza Waziri Ulega.

Amefafanua kuwa bandari hiyi itakua na karakana ya meli, sehemu ya kuegesha meli kubwa kumi zenye urefu wa mita30. Aidha, meli kutoka maeneo mbalimbali duniani zitaweza kuweka nanga pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika ikiwemo kuongeza chumvi kwenye samaki kabla ya kusafirisha.

Manufaa mengine ya bandari hiyo ni uwezo wa kuhifadhi boti ndogo, sehemu ya kuegesha mitumbwi isiyopungua 200, sehemu ya kuegesha mashua na kutoa fursa ya kutoa ajira kwa vijana takribani 30,000.

“Pia, Bandari hii itakuwa na uwezo wa kuhifadhi samaki tani 1300 kwa wakati mmoja, soko la samaki litakalotumika na wavuvi katika ukanda wa kusini na eneo la kuchakata samaki”, amesisitiza Waziri Ulega.

Aidha, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo Mamlaka ya Bandari Tanzania itaendesha shughuli za bandari hiyo kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Mnufaika wa mradi huo, Shukrani Shamte ambaye ni mkulima wa mwani ameipongeza Serikali kwa jitihada hizo za Serikali.

“Tunaikushuru Serikali kwa kutupatia mkopo wa boti ya malipo nafuu, boti hizi zitatusaidia kwenye shughuli za kulima mwani kwenye kina cha maji mengi na kubeba mwani kutoka kwenye maji mengi kuja pwani.

“Wakulima wengi wa mwani tunaomba utuwezeshe boti zingine na mahitaji ni mengi na boti ulizotupa ni chache”, ameeleza Bi. Shukrani.

      

WANANCHI JIMBO LA MBARALI NA KATA SITA WAJITOKEZA KUPIGA KURA, JAJI MWAMBEGELE ATOA NENO

September 19, 2023

 

Mkazi wa Kata ya Nala katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiwa mwenye furaha akionesha kidole chake cha shahada kilichotiwa wino baada ya kupiga kura kuchagua Diwani wa Kata hiyo katika Uchaguzi mgogo unaofanyika Leo Septemba 19,2023 katika Kata hiyo. Aidha wananchi wa Jimbo la Mbarali na Kata zingine sita wanapiga kura kuchagua viongozi wao.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Jaji Mwambegele baada ya kutembelea vituo amesema ameridhishwa na utendaji wa Wasimamizi wa Uchaguzi huo na kuongeza kwamba vituo vimefunguliwa kwa wakati na zoezi linaendelea vizuri kwa utulivu na amani.

Aidha, Jaji Mwambegele amezungumza na mawakala wa vyama vya siasa ambao wamemueleza kuridhishwa na mwenendo wa zoezi la kupiga kura na kwamba hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza. 

Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali unafanyika sambamba na kata sita za Tanzania Bara. Kata zenye uchaguzi ni Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Wananchi wa Jimbo la Mbaràli wakiwa Leo wamejitokeza kupiga Kura kuchagua Mbunge wa Jimbo hilo. 
Wananchi wa Jimbo la Mbaràli wakiwa Leo wamejitokeza kupiga Kura kuchagua Mbunge wa Jimbo hilo. 
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mwanaisha Kwariko akikagua vituo vya kura wakati wananchi wa Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakipiga kura kuchagua Diwani wao Leo Septemba 19,2023.

Wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga Kura.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mwanaisha Kwariko akikagua vituo vya kura wakati wananchi wa Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakipiga kura kuchagua Diwani wao Leo Septemba 19,2023.
Mpiga Kura akipakwa wino baada ya kupiga kura.
Wananchi wakiwa kituoni
Karani muongozaji akihakiki jina la Mpiga kuraWananchi waliona umri mkubwa au wagonja walipewa kipaumbele.
Mpiga Kura mwenye mahitaji maalum akisaidiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura ili aweze kutimiza haki yake ya kumchagua Kiongozi anayemtaka katika kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya Kata Na.2, katika Kata ya Mfaranyaki Halmashauri ya Manispaa ya Songea, leo tarehe 19/09/2023.

Zoezi la kupiga kura likiendelea Kwa amani na utulivu katika vituo mbalimbali katika Kata ya Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Leo tarehe 19 Septemba, 2023
Wapiga kura wakiendelea kujitokeza kwenye vituo vya kupiga kura kwenye maeneo mbalimbali ya Kata ya Old Moshi Magharibi kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo iliyopo Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro unaofanyika leo tarehe 19 Septemba, 2023.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Jaji Asina Omari akitembelea na kukagua upigaji kura katika Kata ya Marangu Kitowo katika Halmashauri ya Rombo.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Jaji Asina Omari akitembelea na kukagua upigaji kura katika Kata ya Marangu Kitowo katika Halmashauri ya Rombo.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akikagua vituo vya kupiga Kura katika Kata ya Mfaranyaki Halmashauri ya Manispaa ya Songea tarehe 19 September siku ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani.
90