SBL yakabidhi mradi wa maji wa thamani ya shilingi 80m/- kwa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza

October 04, 2017


Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula (aliyevaa kofia) akikata utepe kuzindua kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milioni 80.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh,Angelina Mabula,akifungua kitambaa cha jiwe la msingi la  kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula(aliyevaa kofia) akijaribu kumtiwhsa ndoo mara baada ya kuzindua kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion 

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula(wa pili kulia) na Meneja wa Kiwanda cha bia cha Serengeti Mwanza Shekhar Makasare, wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela jana,anayeshuhudia pembeni ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa SBL Hawa Ladha, wakati wa uzinduzi kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milion 80 .




Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL Mwanza mara bada ya uzinduzi wa   kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.

MBUNGE CHUMI AZIPIGA TAFU TIMU ZA JIMBONI KWAKE KWA KUZIPA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA

October 04, 2017
Mbunge wa Jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano


 Na Fredy Mgunda, Mafinga

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.
  
"Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi

Chumi aliwataka wananchi na wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

“Jamani kushiriki ligi daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia vigumu kuipandisha” alisema Chumi

Aidha Chumi hakusita kuwapongeza viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na mawazo yao.

“Mimi nilijua mwaka huu tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi hiyo” alisema Chumi


WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: WATEJA NA WANACHAMA WA PSPF WAPATIWA HUDUMA ZA ZIADA

October 04, 2017


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WATEJA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanaofika kwenye ofisi za makao makuu jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam ili kujipatia huduma katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, wamekuwa wakifaidika na huduma za ziada zinazotolewa na washirika wa Mfuko huo ambao wameweka kambi kwenye eneo hilo.
Washirika wa Mfuko  walioweka kambi kwenye ofisi hizo tangu Otoba 2, 2017, ili kuwahudumia wateja ambao ni pamoja na Wastaafu na Wanachama wa PSPF ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Benki ya CRDB, Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Benki ya NMB na  Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Menenja wa Huduma kwa Wateja wa PSFP, Bi. Laila Maghimbi amesema.
“Kama mnavyoona, mwaka huu tumeamua kuongeza huduma za ziada kwa wateja wetu, yaani wastaafu na wanachama wanaofika kupatiwa huduma ofisini kwetu, ambapo Mteja baada ya kuhudumiwa pia anaweza kuonana na washirika wetu, ambapo NHIF wanafanya uchunguzi wa afya bure, mabenki nayo yapo hapa kuwaelimisha kuhusu jinsi wanavyoweza kuweka fedha zao na kupatiwa mikopo nafuu ili kuendesha miradi  mbalimbali na hivyo kujiongezea kipato.” Alifafanua Bi. Maghimbi.
Alisema, nia ya Mfuko ni kuhakikisha wanafurahia huduma zitolewazo lakini pia kuonyesha kuwajali wateja wao kwa kuwasogezea karibu huduma muhimu za afya na kibenki.
Wateja wamekuwa wakifurika kwenye ofisi hizo tangu Wiki ya Huduma kwa Wateja ianze Oktoba 2, 2017 na miongoni mwa huduma zitolewazo ni pamoja na wastaafu kufuatilia taarifa za michango yao, kuhakikiwa, kulipwa mafao na kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS).
Aidha wanachama wanaofika kwenye ofisi hizo wamekuwa wakipatiwa maelezo ya namna wanavyoweza kupatiwa mikopo ya viwanja na nyumba za makazi ambapo kampuni mshirika ya PSPF, Ardhi Plan Limited kupitia afisa wake, Bi.Anna Lukindo imekuwa ikifanya kazi hiyo.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa pspf, Bw, Andrew Mkangaa, (wapili kulia), Meneja wa Huduma kwa Wateja, Bi. Laila Maghimbi, (watatu kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward(kulia), wakimsikiliza Daktari kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), kuhusu huduma wazitoazo kwa Wateja na wanachama wa PSPF kwenye ofisi za Mkao makuu ya Mfuko katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Maafisa wa Benki ya CRDB, Afisa Uendelezaji Biashara, Bw. Peter Christopher, (wapili kulia), na Afisa Mikopo kwa watumishi, Bi.Diana Jekela, (kushoto), wakiwahudumia wateja.
 Afisa wa Benki ya NMB GTawi la Sinza jijini Dar es Salaam, Bi. Nadina Mpasha, (kulia0, akimpatia maelezo mteja aliyefika kwenye banda la benki hiyo kwenye ofisi za PSPF.
Dkt. Jason B.B Bagonza, (kushoto), ambaye ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, akihudumiwa na maafisa wa benki ya Posta Tanzania, (TPB), Maafisa Masoko,  Bi. Heavenlight A.Uiso na Bw.Nelson Mwakilasa
 Maafisa wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB), Plc, Mwajuma Gilbert, (kulia) na Michael Kachala, ambao ni maafisa wan huduma kwa wateja, wakitoa huduma.
 Faiza Masoli, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
 Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
 Afisa Huduma kwa wateja, PSPF, Bi.Elizabeth Shayo.
 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akipitia taarifa za Mteja aliyefika kuhudumiwa
 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza na mteja huku akimuonyesha taarifa yake.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akiwaeleza wateja hawa wa Mfuko huo, kuhusu huduma za ziada zinazopatikana kweye eneo hilo.
 Afisa wa PSPF(kulia), akimpatia nyaraka Mwanachama huyu aliyefika kuhudumiwa kwenye ofisi hizo.
 Anna Lukindo, (kulia), kutoka kampuni ya Ardhi Plan Limited, akimpatia maelezo Mwanachama wa PSPF aliyetaka kujua ni jinsi gani anaweza kupatiwa mkopo wa kiwanja.
 Wanachama kushoto, wakihudumiwa na maafisa wa PSPF ambao wako makini katika kuwahudumia wateja wanaofika kwenye ofisi hizo.
 Maafisa waandamizi wa PSPF, Bw. Gabriel P.Maro, (kushoto) na Bw. Abdul Njaidi wakifurahia jamb

SHIRIKA LA WOTESWA LAWANOA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA

October 04, 2017
Na George Binagi-GB Pazzo
Mratibu wa Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa majumbani WOTESAWA, Cecilia Nyangasi (pichani juu) amesema shirika hilo limejiwekea mikakati ya kuhakikisha kwamba hadi kufikia mwaka 2020 kusiwepo na mtoto chini ya umri wa miaka 18 ambaye ameajiriwa kufanya kazi za nyumbani.

Nyangasi ameyasema hayo hii leo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari Jijini Mwanza, yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kusaidia kufikisha elimu katika jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na hivyo kuwakosefa fursa mbalimbali ikiwemo kupata elimu.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuwanusuru watoto wafanyakazi wa majumbani na ukatili ikiwemo wa kingono pamoja na kiuchumi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi bila malipo ama kwa malipo kidogo.

Aidha ametoa rai kwa serikali kuboresha sera, mikakati na sheria zinazomlinda mtoto ili kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kutambua bayana umri wa mtoto anayepaswa kuajiriwa kwani baadhi hutaja umri wa miaka 14 huku nyingine ikitaja umri wa miaka 18.

Nyangasi amebainisha kwamba mwaka jana shirika la WoteSawa lilifanya utafiti katika Kata nne za Jiji la Mwanza ambazo ni Igogo, Mkuyuni, Butimba na Capriont na kubaini kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na utumikishwaji na ili kupambana na hali hiyo shirika hilo lilianzisha mkakati wa kuwafikia watoto waajiriwa, waajiri wao pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kuwaelimisha.

Nao waandishi wa habari, Moses Mathew kutoka gazeti la Daily News pamoja na Rhoby Magira kutoka Redio Afya wamebainisha kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari na makala zinazoielimisha jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwatumikisha watoto kupitia ajira za majumbani.

Itakumbuka kwamba mtoto mfanyakazi wa nyumbani analindwa na sheria kadhaa ikiwemo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, waraka wa mishahara wa mwaka 2013 pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa upande wa waraka wa mishahara wa mwaka 2013, mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni ingwa waraka huo hautaji mwajiriwa huyo anapaswa asiwe mtoto.

Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akisisitiza wanahabari kuungana pamoja katika kuibua na kuandika habari/ makala zenye kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Afisa Habari shirika la WoteSawa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Moses Mathew kutoka gazeti Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Tazama picha zaidi HAPA