RC MAGALULA AWATISHA MZIGO MADC WAPYA TANGA.

February 27, 2015

          
               NA MWANDISHI WETU,TANGA.

 MKUU wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula amewataka wakuu wa wilaya mpya za Handeni na Lushoto mkoani hapa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kwenye maeneo yao ikiwemo kuipatia ufumbuzi migogoro ya ardhi na viwanja ambayo imeonekana kuleta manunguniko kwa wananchi.

Badala yake amewataka kuhakikisha wanasimamia haki kwa usawa ili kuweza kuondoa migogoro hiyo kwenye maeneo husika ikiwemo kuzipatia ufumbuzi changamoto nyengine ambazo

Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni
Mkoani Tanga Husna Rajabu Msangi akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Said Magalula
Alitoa wito huo jana wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya ya Handeni,Husna  Rajabu na Mariam Juma wa Lushoto ambao waliteulwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hizo katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Alisema kuwa kimsingi wakuu hao wapya wanapaswa kwenda kufanya kazi kubwa kwenye wilaya walizopangiwa ili kuweza kuonyesha namna ya uwajibikaji wao katika jukumu hilo kubwa ambalo walipewa na Mkuu wa nchi.

   “Naombeni msimuangushe Rais akawa na maswali mengi kwa uteuzi aliowapa hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa kusimamia shughuli za maendeleo kwenye wilaya zenu lengo likiwa kuzipa maendeleo “Alisema RC Magalula.

Aidha aliwataka kwenda kushirikiana na wananchi katika maeneo wanayokuwa wakiongoza ili kuweza kuchangia harakati za maendeleo kwa jamii zinazowazunguka.
 
Mkuu mpya wa wilaya ya Lushoto mkoani
Tanga,Mariam Juma akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula
jana,
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kuacha kukaa maofisini badala yake watoke na kwenda kukaa vijijini ili kuweza kubaini changamoto ambazo zinawakabili wananchi ili kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Hata aliwataka waweke mikakati mazuri ya kutenda haki kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuangalia jinsi ya kutatua migogoro iliyopo maeneo yao kwa kufuata sheria zilizopo.

   “Acheni kukaa maofisini kusubiria kuletewa taarifa badala yake tokeni mkaangalie changamoto zinazowakabili wananchi lengo likiwa kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi haraka lakini pia jiepusheni na tabia ya umangi meza“Alisema RC Magalula.

Awali akizungumza baada ya kuapisha Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni,Husna Rajabu Msangi alisema kuwa atahakikisha anatenda haki wakati akifuatilia na kushughulikia masuala ya migogoro ya ardhi kwa kutafuta ukweli ili kuweza kutenda haki kwa kushirikiana na viongozi wenzake.

“SUMATRA TANGA YATOA ONYO KALI KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MAJINI.

February 27, 2015


MAMLAKA ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema kuwa haitasita kuwafutia leseni pamoja na kuvifungia vyombo vya majini vitakavyoendelea kutoa huduma hiyo bila kufuata sheria ikiwemo kukaguliwa na kupewa cheti cha ubora.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Mfawizi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Walukani Luhamba wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG  ambapo alisema kuwa vyombo vingi vinavyotoa huduma kwenye maeneo hayo vimekuwa hazikaguliwi hali ambayo ni hatari kwa usalama wa watumiaji.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwa na vyombo vilivyokaguliwa na kufanya kazi zao kwa kufuata sheria zilizopo hapa nchini jambo ambalo litapunguza ajali za mara kwa mara zinazotokana na ubovu wa vyombo hivyo.

Luhamba alisema kuwa watahakikisha kila chombo ambacho kinatoa huduma zao kwenye eneo la majini wanakuwa na leseni za kutoa huduma kwenye maeneo hayo pamoja na vyombo hivyo kufanyiwa uhakiki wa kina.

   “Tunasema kuwa wamiliki watakaoshindwa kupeleka vyombo vyao kukaguliwa hatutawaacha tutahakikisha kuna kula nao sahani moja ikiwemo kuvifungia vyombo hivyo kwani hatutakubali wafanya kazi bila kukaguliwa “Alisema Luhamba.


Aidha alisema kuwa lazima ufike wakati wamiliki kuacha kufanya kazi kwa mazoezi kwa sababu hali hiyo inaweza kuwapa matatizo wananchi wanaovitumia hasa nyakati inapojitokeza ajali.

Hata hiyo alisema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na idara nyengine watashirikiana kwa pamoja ili kuweza kupambana na wale wote ambao watashindwa kufuata sheria hizo kwa kuwachukulia hatua.

Hatua za mwisho za Maandalizi Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2015

February 27, 2015

Maandalizi ya mwisho ya kukarabati maeneo mbalimbali ya uwanja wa Chuo kikuu kutakapofanyika mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni.
Mabango mbalimbali yakiwa yamewekwa maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi kuashiria kuanza kwa shamrashamra za mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Baadhi ya wageni wakijiandikisha kukimbia mbio ndefu za kilometa 42 ambapo zoezi la uandikishaji linafanyika katika hotel ya Keys mjini Moshi.
Washiriki wa mbio za Kilometa 21 zinazodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakijiandikisha kwa ajili ya kupata namba maalumu wakati wa kukimbia mbio hizo. 
Baadhi ya wakimbiaji wakijaza fomu kwa ajili ya kukimbia mbio ndefu za km 42.
Wale wa mbio za Km 5 fun run pia walihakikisha wanafanya usajili wa ndugu zao pia.
Katika eneo la kujiadikishia unapata kiburudisho cha Grand Malt mara baada ya kupatiwa namba kwa ajili ya kushiriki mbio hizo.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.