KAMISHNA WA SENSA HAJJAT AMINA MRISHO SAID ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KITETO MKOANI MANYARA

KAMISHNA WA SENSA HAJJAT AMINA MRISHO SAID ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KITETO MKOANI MANYARA

June 08, 2015
0001
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
0002
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kulia kwake ni mume wake Alhajj Abeid Omary Khamis.
………………………………….
Na. Mwandishi wetu Dar es Salaam
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kiteto lililoko mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hajjat Amina Mrisho Said amesema iwapo atateuliwa na CCM kuwa mgombea wa Jimbo la Kiteto, atahakikisha anatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuleta maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo. Ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 – 2020 na kufanikisha ujenzi wa Chuo cha VETA jimboni ili vijana waweze kupata elimu ya stadi za kazi na hatimaye waweze kujiajiri. Kuhusu suala zima la ufugaji, Hajjat Amina amesema atahamasisha uendelezaji wa ufugaji wenye tija kwa kuifuatilia Serikali ili iweke miundombinu katika maeneo yote ya wafugaji jimboni. Vipaumbele vingine ni pamoja na kuhamasisha ujenzi wa Soko la Kimataifa la Mazao hasa mahindi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya stakabadhi ya mazao gharani na kuwashirikisha wananchi wote katika kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao. Hajjat Amina Mrisho Said kitaaluma ana Shahada ya Uzamili wa Mifumo ya Kompyuta na amewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa na Pwani ambapo kwa sasa ni Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAZINDUA HUDUMA ZA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO- Maombi na malipo ya leseni kufanyika kupitia mtandao

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAZINDUA HUDUMA ZA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO- Maombi na malipo ya leseni kufanyika kupitia mtandao

June 08, 2015

????????????????????????????????????
Kikundi cha Ngoma za Asili cha Simba kutoka Dodoma (kushoto)  kikitumbuiza mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (kulia katikati, aliyevaa koti la kahawia) kabla ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao uliofanyika mjini Dodoma.
????????????????????????????????????
Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa (Kulia)  akielezea mfumo wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao  unavyofanya kazi kabla ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (wa pili kutoka kushoto, aliyekaa meza kuu).
????????????????????????????????????
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja (Kulia) akielezea mafanikio  katika uboreshaji wa huduma za utoaji leseni kwenye uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisoma hotuba ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia  ya mtandao. Wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja na wa kwanza kushoto  mbele ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa nne kutoka kulia, waliokaa mbele); Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja ( wa tano kutoka kulia, waliokaa mbele) na Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria uzinduzi huo.
…………………………………………………………………
Greyson Mwase na Samuel Mtuwa, Dodoma
Wizara ya Nishati na Madini imezindua mtandao utakaowezesha wachimbaji wa madini kutuma maombi ikiwa ni pamoja na kufanya malipo ya leseni za madini unaojulikana kwa jina la Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP). Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika mjini Dodoma, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema kuwa lengo la mtandao huo ni kuwezesha shughuli za uchimbaji madini kufanyika katika uwazi na kukomesha rushwa. Akielezea hatua mbalimbali katika uboreshaji wa huduma za leseni zilizopitiwa na Wizara Simbachawene alisema mwaka 1990 leseni zilishughulikiwa kwa njia ya mkono hadi kufikia mwaka 2005 ambapo Wizara ilianzisha mfumo wa kompyuta katika utoaji wa leseni uliojulikana kwa jina la MapInfo ambao bado ulitegemea uchambuzi kwa njia ya mkono. Alisema ili kuboresha huduma ya utoaji wa leseni za madini, mwaka 2007 Wizara ilianzisha mfumo wa utoaji wa leseni za madini uliojulikana kama Mining Cadastral Information Management System (MCIMS) ambao uliwezesha ofisi za madini kuunganishwa kwa njia ya mtandao na kuwezesha uchambuzi wa maombi ya leseni kufanyika kwa njia ya kompyuta. Alisema mfumo huo ulirahisisha sana upokeaji na uchambuzi wa maombi ya leseni na kurahisisha usimamizi wa leseni za madini. Aliendelea kusema kuwa kupitia mfumo huo Wizara imeweza kupokea na kuchambua wastani wa maombi 1,400 ya leseni kubwa na 5,000 ya uchimbaji mdogo kwa mwaka. Alisema mfumo huo umewezesha utolewaji wa wastani wa leseni 500 kubwa za madini na leseni zipatazo 1,500 za uchimbaji mdogo kila mwaka. Waziri Simbachawene aliendelea kusema kuwa kuanzia mwaka 2010 Wizara iliendelea kuboresha mfumo wa flexicadastre chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini (SMMRP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Alisisitiza kuwa maboresho hayo yalikuwa ni pamoja na kuwezesha uondoaji wa mlundikano wa maombi ya leseni, kuhuisha takwimu za leseni za madini na pia kuweka tovuti maalumu iliyowezesha wananchi kupata taarifa ya leseni za madini, maboresho yaliyochochea ari ya wananchi kufuatilia masuala ya leseni kwa njia ya mtandao, na kuweka uwazi katika usimamizi wa sekta ya madini kwa mujibu wa Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI) Aliongeza kuwa kufikia Mei, 2015 jumla ya leseni 3,500 za utafutaji mkubwa wa madini, leseni 14 za uchimbaji mkubwa wa madini, leseni 389 za uchimbaji wa kati na leseni 39, 921 za uchimbaji mdogo wa madini zilitolewa. Alisisitiza kuwa kwa sasa Wizara imeamua kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao kama utekelezaji wa agizo la serikali la kuhakikisha kuwa malipo ya serikali yanafanyika kwa njia ya kielektroniki. Simbachawene aliongeza kuwa mfumo huo mpya utawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi na kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki. Alisema mfumo huu pia utawawezesha wateja kuoanisha ramani za maeneo ya leseni na ramani za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Aidha, Waziri Simbachawene aliwataka wamiliki wa leseni na wananchi wote kwa ujumla kujisajili katika mfumo huo kwa kuwa lengo la Wizara ni kuhakikisha kuwa huduma zote za leseni zinakuwa kwa njia ya kielektroniki ifikapo Agosti 31, mwaka huu. Pia aliwataka makamishna wa madini pamoja na watendaji wake kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu mzuri wa kuwasajili wachimbaji wadogo ili nao waweze kutumia huduma hizo la kielektroniki bila kikwazo. Wakati huo huo akielezea faida za mfumo huo, Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa mfumo huu unawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi, kupata historia ya leseni zao, kuhuisha leseni zao, kuongeza ukubwa wa maeneo ya leseni zao na kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki. Mhandisi Masanja aliongeza kuwa mfumo huu utawawezesha wamiliki wa leseni kuwa na usimamizi wa leseni zao kwani utakuwa ukimjulisha mmiliki wa leseni lini leseni yake inatakiwa kulipiwa na lini leseni yake itaisha “Mfumo huu pia umesheheni takwimu mbalimbali za madini ikiwa ni pamoja na ramani za maeneo ya leseni na ramani za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)” Alisema Mhandisi Masanja Aliongeza kuwa, mfumo huu utawapunguzia mzigo watalam wa Wizara kwa kuwa wateja wenyewe wataingiza maombi ya leseni na hivyo wataalam kufanya uchambuzi kwa haraka zaidi na kupata muda wa kutosha kusimamia leseni zilizopo. Alisisitiza kuwa mfumo huu umelenga kuondoa upotevu wa fedha za serikali kutokana na vitendo vya rushwa na makosa mengine ya kibinadamu. Akielezea hatua iliyofikiwa ya usajili wa wateja katika mfumo huo, Mhandisi Masanja alisema tangu kuanzishwa kwa mfumo huo mwaka 2013 hadi sasa ni wateja 140 tu kati ya wateja wapatao 400 wamesajiliwa na wachimbaji wadogo 20 kati ya wamiliki wapatao 4,000 wamesajiliwa katika mfumo huo na kuwataka wadau wote waone umuhimu wa kujisajili na kutumia huduma hizi ili kuondoa matatizo ya ucheleweshaji wa kushughulikia maombi yao. Mhandisi Masanja aliongeza kuwa kuanza kutumika kwa mfumo huu kunaiweka nchi ya Tanzania katika nchi chache za Afrika zilizo na mfumo wa kisasa wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao.

BALOZI WA CHINA AMTEMBELEA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE

June 08, 2015

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youquig alipomtembelea Wizarani kwa mazungumzo ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Mkalimani wa Balozi wa China Bi.Wang Fang akisalimiana na Katibu Mkuu 

Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China huku Maafisa wa pande zote mbili wakinukuu kile kinachozungumzwa.
 Balozi wa China, Mhe.Lu akifurahia jambo na Balozi Mulamula
Balozi Lu Youqing akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Mr.Dong (kulia), Mr.Lin Liang (katikati) na Bi.Wang Fang wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw.Nathaniel Kaaya (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na  Maafisa  Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu (hawapo pichani).
 Picha na Reuben Mchome

VODACOM YALIPA KODI YA SHILINGI BILIONI 46.4

June 08, 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kulia) akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV, IssaKwissa Mwaifuge baada ya kuongea na waandishi wa habari kuhusiana na mwelekeo na malengo ya kampuni ambapo alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015 ambapo alibainisha kuwa Kodi ya malipo iliyolpwa ni kiasi cha shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao kuhusiana na mwelekeo wa kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali Nchini wakimfatilia kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(hayupo pichani)wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imelipa kodi serikalini kiasi cha shilingi bilioni 46.4 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 ambao ulimalizika mwezi Machi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema jijini Dar es Salaam leo kuwa  mbali na kodi ya mapato,Vodacom imekusanya kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT)   zaidi ya shilingi  bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5.

Kiasi cha kodi ya mapato iliyolipwa kwa mwaka wa fedha wa 2014/2014 ni zaidi ya shilingi bilioni 47.1 ambazo ililipa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 na kutangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kama kampuni ya pili kwa kulipa kodi nchini na ikiwa ni kampuni ya kwanza kchania maato ya serikali katika sekta ya mawasiliano.Makampuni yaliyotangazwa kuwa ni vinara wa kulipa kodi na kukusanya kodi za serikali nchini mwaka jana ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Vodacom Tanzania na kampuni ya Sigara Tanzania .

Meza ambaye alikuwa anato taarifa ya utendaji na mwelekeo wa kampuni kwa mwaka 2014/2015 alisema “Vodacom bado imeendeleza dhamira yake ya kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na mpaka sasa tumewekeza kiasi cha shilingi 1.8 trilioni na katika pindi cha mwaka huu tumelenga kuwekeza zaidi shilingi bilioni 200 kwa aili ya kubresha mtandao wetu na kuboresha zaidi bidhaa na huduma zetu tunazotoa”alisema.

Aliongeza kuwa mtandao wa  Vodacom umewafikia  asilimia 99 ya watanzania kupitia minara yake 3300 iliyopo sehemu mbalimbali nchini inayowawezesha wananchi kunufaika na huduma kutoka mtandao huu bora nchini.

Meza alisema pia kuwa kampuni inajivunia huduma yake ya M-Pesa ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kifedha nchini “Huduma hii inatumiwa na zaidi ya watanzania katika  kutuma ,kupokea fedha na kufanya mihamala ya malipo mbalimbali  na inazidi kuwarahishia maisha katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa”alisema Meza na kuongeza kuwa M-Pesa ina mawakala zaidi ya 85,000 na imeunganshwa na mabenki 26 nchini na taasisi zaidi ya 500 zimeunganishwa na huduma hii katika  kufanya malipo na kukusanya fedha.

Katika kukuza teknolojia nchini Meza alisema Vodacom inaendelea kubuni huduma za kuwarahisishia maisha na kupata taarifa,maarifa na burudani mbalimali kupitia  mtandao wa internet.

Ili kukamilisha malengo na mikakati ya kuboresha sekta ya mawasiliano nchini kwa mwaka 2015 ameitaka serikali kutoongeza kodi kwenye sekta ya mawasiliano katika bajeti yake ya mwaka huu.Watanzania kwa sasa wanalipa asilimia 33 (kodi ya zuio na ongezeko la thamani kwa muda wa maongezi ambacho ni kiwango kikubwa katika ukanda huu wa Afrika. “Kupata mawasiliano ni moja ya haki ya msingi hivyo kuna umuhimu yanapatikana kwa kila mmoja kwa gharama nafuu”.Alisema
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA TAMASHA LA BULABO KABILA LA WASUKUMA MKOANI MWANZA

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA TAMASHA LA BULABO KABILA LA WASUKUMA MKOANI MWANZA

June 08, 2015

5
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib  Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Machifu wa Kisukuma Charles llago Kaphipa wakati wa sherehe za Kimila za wasukuma kwenye Tamasha la bulabo katika kituo cha bujoro Mkoani Mwanza Jana Tarehe 7/6/2015
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt Mohammed Ghar Bilal  akishika jiwe la kutengenezea chuma wakati wa Uchifu kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Bujora Askofu Fabian Mkoja alipotembelea Maonyesho hayo Kijiji cha Kisesa wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza jana tarehe 7/6/2015 
3
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa kituo cha Bujora Askofu  Fabian Mkoja alipotembelea  Nyumba ya Mtemi wa kabila la wasukuma kwenye kituo cha  Bujora Mkoani Mwanza.
4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwapungia Mkono wananchi wa Kijiji Cha Kasesa wilaya ya Magu wakati alipowasili Uwanjani hapo kuzindua Tamasha la Kimila la wasukuma Mkoa wa Mwanza .
6
Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipiga Ngoma ishara ya Kuzindua Sherehe za  kimila za kabila la wasukuma zilizofanyika  kwenye kijiji  cha kisesaWilayani Magu Mkoa wa Mwanza jana.
 RAIS DK.SHEIN NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA KAMPUNI YA MAGARI MERCEDES- BENZ

RAIS DK.SHEIN NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA KAMPUNI YA MAGARI MERCEDES- BENZ

June 08, 2015
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakiapata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa  anaehusika na ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani,
[Picha zote na Ramadhan Othman,]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakiangalia magari ya aina mbali mbali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anehusika na Ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa na ujumbe wake wakiangalia mashine ya gari aina ya Mercedes -Benz na kupata maelezo kutoka kwa afisa anaehusika na ufundi Adam  Nowak M.A katika kampuni hiyo.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Adam Nowak M.A. Afisa anaehusika na ufundi  wakati alipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg ambaapo yapo tayari kwa mauzo.

WANANCHI WATOA MAONI JUU YA MUWSA KUOMBA KUPANDISHA BEI YA UTOLEWAJI WA HUDUMA YA MAJI KATIKA MJI WA MOSHI.

June 08, 2015
Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
mazingira mjini Moshi,MUWSA wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na
mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama (hayupo pichani) wakati wa
utolewaji wa maoni juu ya bei mpya ya huduma ya maji.
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Moshi
waliofika katika ukumbi wa Hindu Mandal kwa ajili ya kutoa
maoni.
Mkuu wa mkoa a Kilimanjaro,Leonidas Gama
akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na EWURA.
Mkukaguzi wa hesbu wa  ndani wa Mamlaka
ya Maji safi na maji taka mjini Moshi ,MUWSA ,Benson Maro pamojana na
Meneja rasilimali watu  wa MUWSA,Michael Konyaki wakichukua
kumbukumbu wa yale yaliyokuwa yakizungumzwa katika mkutano
huo.
Meneja fedha wa MUWSA ,Jpyce Msiru akichukua
kumbukumbu wa mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa katika kikao
hicho  kulia kwake ni kaimu mkurugenzi wa MUWSA .Mhandisi Patrick
Kibasa.
Kamu mkurugenzi wa MUWSA,Mhandisi Patrick
Kibasa akitoa hoja juu ya mapendekezo ya bei mpya ya utolewaji wa
huduma mpya ya maji.
Watumishi wa MUWSA,Idd Semkunde na Jacob
Ollotu wakifutilia mkutano huo/
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Sharry
Raymond.
Mhandsi ,Patrick Kibasa akitoa ufafanuzi juu
ya mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi kutoka manispaa na
watumiaji wa huduma ya maji wakifuatilia kwa makini.
Baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano
huo.
Mmoja wa wananchi waliofika kutoa maoni yao
aliyefahamika kwa jina la Maulid Darabu akiwasilisha maoni yake katika
mkutano huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kada ya
Kaskazini.

MULONGO AZINDUA MASHINDANO YA U13 TAIFA

June 08, 2015


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Magessa Mulongo leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba amefungua mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13.

Akifungua mashindano haya Mh Mulongo amewataka vijana hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba.

Amelisisitizia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kuongeza juhudi katika kuimarisha soka la vijana.

Katika salam zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano haya ni kuibua timu ya vijana wa umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakua pamoja hapo kusoma na kufundishwa mpira.

Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17,fainali ambazo zitafanyika Tanzania.

Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.

TFF inaishukuru Symbion Power kwa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa vijana

NB: Picha za uzinduzi zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 

-
Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  
 

JAPAN HANDS OVER MICHAKAINI 'A' PRIMARY SCHOOL BUILDING

JAPAN HANDS OVER MICHAKAINI 'A' PRIMARY SCHOOL BUILDING

June 08, 2015
Photo 6
The front view of the newly constructed Classroom block.
Photo 7
The rear view of the newly constructed Classroom block.
Photo 1
Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida posing with from left Chaiman of Parent Committee of Michakaini Primary School, Mr. Nassor HArith Mohammed, Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, Headteacher Ms. Neema Mwalim Khamis, Secretary of the Committee and Head Teacher, in front of the newly constructed classroom block.
Photo 2
Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, posing with Michakaini primary school pupils in front of the newly constructed classroom block.
Photo 3
Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, during the Handing over ceremony.
Photo 4
Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, during the Handing over ceremony.
Photo 5
Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida congratulates Eng. Mansour Kassim, during the Handing over ceremony. Also in the phor Prof. Ibrahim Lipumba.
By Our Correspondent
The Government of Japan which has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) scheme since 1991, over the weekend has handed over two-storey Classroom Block at Michakaini 'A' Primary School in Chakechake town, South Pemba Region
The building which cost about US Dollars 159,037 is a response to a request by the Parents Committee of Michakaini A Primary School to ease congestion at the school.
The building which was constructed under the GGHSP scheme was handed in the presence of Hon. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba – Chairman of the Civic United Front (CUF) andHon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah – Regional Commissioner, South Pemba Region.
Speaking during the handover ceremony at Michakaini ‘A’ Primary School Ambassador of Japan, Masaharu Yoshida said Reconstruction of a Two-storey Classroom Block at Michakaini A Primary School in Chakechake Town, South Pemba Region; it is another contribution from Japan to the people of Tanzania.
“This project was recommended to us by Professor Ibrahim Lipumba, chairman of the Civic United Front (CUF), and I’m happy that he is here today to witness this handing over ceremony.” He lamented.
Narrating a sad story of the school he said situation at Michakaini „A‟ primary school, where pathetic with more than 1,300 pupils sharing only 12 classes, an average of 110 pupils in one class.
Due to the shortage of classes, the school decided to divide the pupils into two sessions, the morning session and the afternoon session.
However, even after two sessions, the average number of pupils per class was still very high at about 58 pupils per class.
“In some classes, the number was more than 80 pupils per class. These pupils could not get lectures of good quality and supervision. I’m glad that after our intervention, whereby the Government of Japan extended a grant assistance of US$ 159,037 (by then approximately equivalent to 250 million Tanzanian shillings), three classrooms, which were old and in a very bad condition, were demolished and the two-storey classroom block with a total of seven classrooms was constructed. “he said.
With these new classrooms, the average number of pupils per class is expected to be at 44 pupils per class.
Therefore, this project will help to create better condition that almost reaches the teacher-pupil ratio of 1:40 recommended by Primary Education Development Plan (PEDP III).
The ambassador believed that the new block will improve the quality of education and supervision to all pupils and will help their dreams to come true.
He also reiterated that the Government of Japan would like to provide continuing support for basic human needs in Tanzania.