KILELE CHA NANE NANE BANDA LA TIGO -NGONGO LINDI

August 11, 2017
Baadhi ya wananchii wakiwa wamezunguka Banda la Tigo wakipata Huduma Mbalimbalia katika maonesho ya kilimo ya Nane nane yaliyopo Ngongo Mkoa wa Lindi.

Meneja wa kanda ya Kusini wa Kampuni ya Tigo  Uthman Madata akigawa Kofia Katika Banda la Tigo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo ya Ngongo Mkoani Lindi

Meneja wa kanda ya Kusini wa kampuni ya mtandao wa  Tigo Uthman Madata akimuonesha Simu ya Mkononi Aina ya Tekno S1 Mwanafunzi wa Sekondari ya Lindi Charles Shirima katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane  yaliyofanyika Mkoani Lindi.

.Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane

.Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane​



The Commonwealth Secretary General Rt Hon Barones Patricia Scotland QC meets Zanzibar President, visits some of the Isles attractions

August 11, 2017
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC (left) accompanied by Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Ambassador Celestine MushyDirector of  Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs and Regional Affairs head to the plane ready to take off  for their one day trip of  Zanzibar
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the crew before boarding
Top Zanzibar government officials receive The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia atScotland QC at the Karume International Airport in the isles
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC signs the visitor's book upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her right is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and left is Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her left  is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC arrives at the Zanzibar State House accompanies by Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein receives The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC fields questions from journalists at the State House
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC poses for a souvernier photo with Isles based ITV and Radio One journalist Farouq Karim  at the State House
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is taken to a tour of Stone Town with The House of Wonders in the background
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for a group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for another group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage take a guided walking tour through spice plantations
During the Spice tour the Baroness  and her entourage saw how the spices, herbs and fruits are cultivated, with the  tour guide describing in detail all about them as well as tropical fruits such as cloves, lemongrass, nutmeg, cinnamon, turmeric, vanilla, coconuts, papaya, chilli, black pepper, jackfruit, cardamom, cassava and oranges.
The  tour guide describes in  detail  how the spices, herbs and fruits  can be used
Visibly happy with the tour, our visitor is
More spices and herbs are shows
Even lipstick from plants was applied 
Some of the many tourists taking the spice tour cool off the day with coconut juice under clove trees
The baroness joins in
Neatly packed spices and herbs are on display
The visitors take their leave after a satisfying spice tour
Off to the State House where a sumptious luncheon in her hnour awaits
After  the luncheon and on behalf of the entourage Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro thanks their host President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein 
Thank you, Your Excellency, for the sumptious luncheon....
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein  leads the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC outside for souvenir photos.
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein take the first photo with the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC are joined by the Zanzibar Chief Secretary Dr.  Abdulhamid Yahya Mzee (left)  Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma, Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Minister for Finance and Planning Dr. Khalid Salum Mohamed
The VVIPs are joined by the rest of the entourage
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein bids farewell to the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC
At the airport The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan meets the Baroness
The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan bids farewell to  the Baroness
Its time for the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC to depart
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is bid farewell 
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  bids farewell to Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma

The Baroness waves goodbye...
....and blows kisses to her hosts
Salutes welcome them back to Dar es salaam
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the police officers
"...What a tour"
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC caps off the day with a courtesy call on  Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam
The Baroness greetsb Prof Sifuni Mchome, Permanent Secretary in the Ministry of Justice and Constitutional Affairs
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  holds talks with   Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam.

UMMY MWALIMU ATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ‘NIPO TAYARI’

August 11, 2017
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mapema leo Agosti 11, 2017, imetangaza matokeo ya washindi wa shindano la Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu ‘Nipo Tayari’.
Akitangaza washindi hao mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amepongeza wadau mbalimbali kwa kuweza kufanikisha zoezi hilo  zikiwemo Halmashauri zote zilizoshiriki.
“Mashindano ya afya na usafi wa mazingira kwa mwaka huu 2017 hapa nchini yaliweza kushirikisha Halmashauri zote zaidi ya 185 huku, Halmashauri 73 zikishindanishwa Kitaifa baada ya mchujo ngazi ya Mkoa.
Mchanganuo wa Halmashauri hizi ni; Majiji Manne, Manispaa 21, Miji 21 na Halmashauri za Wilaya 27.
Kila mwaka, Wizara yetu  imekuwa  ikiratibu mashindano haya Kitaifa nchini kote ikiwa na lengo la kuinua hali ya afya na usafi wa mazingira katika ngazi ya Kaya na taasisi ili kulinda na  kuboresha afya ya jamii.”  Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy Mwalimu amewatangaza washindi wa kwa upande wa Halmashauri za Majiji na Manispaa ambapo Manispaa ya Moshi ikiibuka kidedea kwa kupata asilimia 78.5, mshindi wa Pili, Jiji la Arusha, Asilimia 78.1 na mshindi wa tatu, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Asilimia 67.2.
Kwa upande Halmashauri za Miji, mshindi wa kwanza ameibuka Halmashauri ya Mji wa Njombe huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama na mshindi wa tatu ni  Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Washindi wa Halmashauri bora inayotekeleza kwa ufanisi Kampeni hiyo hususani katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora,  mshindi wa kwanza ni Halmashauri ya Wilaya ya Meru,  kwa mshindi wa Pii imechukuliwa na Wilaya ya Njombe huku wa tatu ni Halmashauri ya Wilaya ya Makete.
Waziri Ummy Mwalimu amewatangaza washindi wa Kijiji bora kinachotekeleza kwa ufanisi hiyo ya usafi ni Kijiji cha Kanikelele kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mshindi wa pili, Kijiji cha Nambala kutoka Halmashauri ya wilaya ya Meru, na cha tatu ni Kijiji cha Lyalalo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Aidha Vijiji hivyo viliweza kupatikana baada ya kushirikisha jumla ya Vijiji na Mitaa 80 huku Kaya zake zikiwa zimefanikiwa kujenga na kutumia vyoo bora pamoja na sehemu za kunawia mikono kwa maji na sabuni.
Washindi wengine wa shindano hilo ni pamoja na Hospitali Bora kwa usafi ambapo Mshindi wa kwanza ni Arusha Lutheran Medical Centre, mshindi wa pili, Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisco na Ifakara – Morogoro na wa tatu, Hospitali ya Rufaa Mount Meru.
Aidha, Waziri Ummy Mwalimu amewatangaza washindi kwa upande wa Hoteli, ambapo Hyatt Regency Dar es Salaam the Kilimanjaro, iliibuka mshindi wa kwanza huku wa pili  ikienda Mount Meru Hotel, Arusha  na ya tatu ni Aden Palace Mwanza.
“Wizara itatoa zawadi ya gari la kubebea taka (trekta lenye tela) kwa Halmashauri ya Mji wa Njombe ambayo imeibuka mshindi wa kwanza kundi la Miji.
 Aidha zawadi ya gari mpya aina ya Nissan itatolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira, na zawadi za pikipiki aina ya YAMAHA kwa washindi wote waliosalia ili kutoa motisha kwa mabwana Afya wote.
Pia zawadi nyingine zitakazotolewa kwa washiriki katika makundi yote ni pamoja Vikombe na Vyeti maalum ambapo Wizara tutaandaa siku maalum kwa ajili ya kukabidhi zawadi hizo na tunawapongeza kwa ushindi” alimalizia Waziri Ummy Mwalimu.
Katika kuongeza ufanisi wa mashindano hayo, Wizara iliunda kamati maalum ambayo iliratibu na kusimamia zoezi zima la uhakiki wa Mashindano huku wajumbe wakitoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais– TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi – Muhimbili, Chuo Kikuu cha Ardhi,  pamoja na wadau wa Maendeleo wanaojihusisha na shughuli za Afya na usafi wa Mazingira hapa nchini huku wakizingatia vigezo hali bora ya usafi wa mazingira kwa ujumla.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa tukio hilo Jijini Dar es Salaam,  la kutangaza washindi wa shindano la Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu ‘Nipo Tayari’. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa tukio hilo Jijini Dar es Salaam,  la kutangaza washindi wa shindano la Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu ‘Nipo Tayari’.  Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Usafi wa Mazingira, Theophil Likangaga.
Mratibu wa kampeni ya mashindano hayo ya Usafi wa Afya ya Mazingira, Bw. Anyitike Mwakitalima akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo. Anayemfuatia ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalumu na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Usafi wa Mazingira, Theophil Likangaga
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa na nembo ya kampeni ya NIPO TAYARI ambayo inahamasisha usafi wa mazingira hasa usafi wa kunawa mikono na matumizi sahihi ya vyoo.
Mwanahabari wa mtandao wa Michuzi Media, Chalila Chibuda akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Mwanahabari wa Tumaini TV akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwa pamoja na baadhi ya wadau wa Wizara ya Afya katika habari na nembo hiyo ya NIPO TAYARI
Mratibu wa kampeni ya mashindano hayo ya Usafi wa Afya ya Mazingira, Bw. Anyitike Mwakitalima akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Wadau mbalimbali wakiwa wamebeba nembo ya NIPO TAYARI
Wadau mbalimbali wakivalishwa nembo maalum ya NIPO TAYARI  kwa ajili ya kuhamasisha Afya ya Mazingira ikiwemo usafi wa mikono na vyoo bora vya kisasa
Wadau mbalimbali wakivalishwa nembo maalum ya NIPO TAYARI  kwa ajili ya kuhamasisha Afya ya Mazingira ikiwemo usafi wa mikono na vyoo bora vya kisasa





--

Andrew Chale

Blogger Personality | Journalist | Activist | Online Editor dewjiblog | Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals 2007 to present.

           chalefamily@yahoo.com

Telephone: +255222122830 Fax: +255222126833
Golden Jubilee Towers, Ohio Street,20th Floor
Po Box 20660, Dar es Salaam,Tanzania