Mkoa Wa Tanga Wapokea tuzo Mikoa Inayofanya Vizuri katika Sekta Ya Elimu Nchini

May 24, 2014

        Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akipokea tuzo ya Elimu Kwa Mkoa wa Tanga kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga  Bw. Salum Mohamed Chima mapema wiki hii ofisini kwake iliyokabidhiwa na Mhe. Mizengo. P. Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Wiki ya Elimu nchini iliofanyika Dodoma Mei 2014. Mkoa wa Tanga umekuwa wa kwanza kitaifa kwa kuwa  na shule nyingi zililizofanya vizuri mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba 2013, kidato cha nne 2013 na Kidato cha sita 2013.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima  ( kushoto) wakati akikabidhiwa Tuzo hiyo na Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Elimu Bw. Ramadhani C. Chomola mara baada ya kuiwasilisha kutoka Dodoma
Tuzo yenyewe; Hongera Sana Mkoa wa Tanga

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani C. Chomola

   Furaha na vifijo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa kutolewa habari njema ya Ushindi wa Mkoa wa Tanga.

TANAPA YATAJA MAJINA 10 YA WANAHABARI WATAKAO WANIA TUZO

May 24, 2014


Meneja uhusiano wa mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA),Paschal Shelutete akizungumza wanahabari kuhusiana na tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAANDISHI 10 WAFIKA FAINALI TUZO ZA HABARI ZA TANAPA ZA 2013.

Jumla ya Waandishi wa Habari 10 wamefanikiwa kufikia hatua ya fainali ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013.
 
Wanahabari waliofanikiwa kufika hatua ya fainali ni pamoja na Frank Leonard (Habari Leo), Jackson Kalindimya (Nipashe), Humphrey Mgonja (Radio SAUT FM), Raymond Nyamwihula (Star TV) na Vedasto Msungu (ITV).
 
Wengine ni pamoja na Kakuru Msimu (Star TV), Gerald Kitabu (The Guardian), Salome Kitomari (Nipashe), David Rwenyagira (Radio 5) na Cassius Mdami (Channel Ten).
  
Hafla ya utoaji Tuzo za Habari za TANAPA itafanyika siku ya Jumanne tarehe 27 Mei, 2014 jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
  
Hafla hii itaenda pamoja na Mkutano wa kila mwaka baina ya TANAPA na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini inayotarajiwa kuanza wiki ijayo jijini Mwanza.
  
Jumla ya kazi zilizotumwa kwa ajili ya kushindanishwa mwaka huu ni 114 tofauti na kazi 34 za mwaka jana. Ongezeko hili la asilimia 235 lililazimu Jopo la Majaji kutumia muda mwingi zaidi wa kupitia kazi zote na kupata washindi. Kati ya kazi 114 zilizotumwa, kazi zilizohusu Uhifadhi ni 64 (sawa na 56%) na kazi zilizohusu Utalii wa Ndani zilikuwa 50 (sawa na 44%). 
 
Tuzo za Uandishi wa Habari za TANAPA hutolewa kila mwaka kwa nia ya kuwashirikisha wanahabari kushindanisha umahiri wa kazi zao katika kuelimisha jamii umuhimu wa dhana ya Uhifadhi kwa maeneo yaliyotengwa kisheria kama Hifadhi za Taifa na uhamasishaji wa Utalii wa Ndani kwa faida ya uchumi wa nchi yetu.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
23.05.2014

HIVI NDIVYO HUSSEIN,OBINA NA RAZACK KHALFANI WALIVYOSAINI MIKATABA YA KUJIUNGA NA COASTAL UNION

May 24, 2014
 Mshambuliaji Mpya wa timu ya Coastal Union,Husein Sued akisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kujiunga na timu hiyo yenye makazi yake barabara ya kumi na moja jijini wanashuhudia katikati ni
Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi na wa kwanza kulia ni Meneja wa timu hiyo,Akida Machai,Picha na Oscar Assenga,Tanga.
                                      HAPA AKITIA SAINA YA DOLE GUMBA

KUSHOTO NI RAZACK KHALIFANI AKISAINI MKATABA MPYA WA KUJIUNGA NA TIMU YA COASTAL UNION YA TANGA KULIA NI KATIBU MKUU WA TIMU HIYO,KASSIM EL SIAGI


Mchezaji mpya wa timu ya Coastal Union ya Tanga,Iker Bright Obina kulia akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara kwenye ukumbi wa klabu hiyo,wanaoshuhudia katikati ni Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,kushoto ni Mwenyekiti wa Coastal Union,Hemed Aurora “Mpiganaji”,

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA MCHANA WA LEO

May 24, 2014


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijibu hoja za wabunge kabla Bunge halijapitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Maofisa wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiwa pamoja na Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakifuatilia kikao cha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa 
Mwaka 2014/2015.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2014/2015.
Wabunge wa Afrika Mashariki wakiwasili Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe.James Mbatia akifurahia jambo na Mhe.Shyrose Banji Mbunge wa Afrika Bunge la Afrika ya Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mhe.Samia Suluhu (kushoto) na Mhe.Celina Kombani.
Mbunge wa Chalinze,Mhe.Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Shyrose Banji