WAZIRI MPINA AKAMATA MELI YA UVUVI HARAMU NA KUITOZA FAINI YA MILIONI MIA SABA SABINI

February 01, 2018
 Waziri wa Mifugo  na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia  mzigo wa mapezi  ya samaki aina ya papa wakati Kapteni Han Ming Chuan wa Meli ya Buah Naga 1 akifungua mfuko wenye Mapezi yaliyokamatwa kinyume na  Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John Mapepele
 Waziri wa Mifugo  na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia pezi  la samaki aina ya papa wakati alipokagua Meli ya Buah Naga 1 yenye Mapezi yaliyokamatwa kinyume na  Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John Mapepele
 Waziri wa Mifugo  na Uvuvi Luhaga Mpina akitoka kwenye Meli ya Buah Naga 1 baada ya kuikagua ambapo ilikutwa na mapezi ya samaki aina ya papa kinyume na  Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John Mapepele
Meli ya Buah Naga 1 iliyokamatwa eneo la Mtwara ikiwa na kilo 90 ya mapezi ya samaki aina ya papa yaliyokamatwa kinyume na  Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John Mapepele
Na John Mapepele, Mtwara
Waziri wa Mifugo  na Uvuvi Luhaga Mpina ameridhia utozwaji wa faini ya dola za kimarekani laki tatu na nusu sawa na shilingi milioni mia saba  na sabini iliyotozwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu (DSFA)  kwa Meli ya Buah Naga 1 kutoka nchini Malaysia  kwa kosa la kukutwa  mapezi ya  samaki aina ya papa kilo 90 huku miili ya samaki hao kutupwa baharini kinyume na kanuni ya 66 ya kanuni za bahari kuu za mwaka 2009 na kifungu namba 18(2) cha  Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2007.

Akizungumza  baada ya kukagua meli hiyo leo mjini Mtwara, Waziri Mpina alisema kuwa  wamiliki  wa meli hiyo wanatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku saba ambapo kama hawatalipwa watapelekwa mahakamani mara moja na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aidha Mpina amesema Serikali imetaifisha tani nne na nusu za samaki ambazo zitauzwa mara moja kwa njia ya mnada na kwa kuzingatia taratibu mbalimbali za Serikali.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa meli hiyo, kwa Waziri, Kiongozi wa Kikosi Kazi maalum cha kudhibiti uvuvi haramu, Kamishna  Frederick Milanzi wa Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini amesema kwamba Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan raia wa Malaysia  alikutwa  na bastola  aina ya Bereta na risasi kumi ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha sheria.

Amesema kuvua na kutupa mizoga ya samaki baharini siyo tu kwamba wanahujumu  raslimali za uvuvi baharini bali pia wanachangia  katika uchafuzi wa mazingira ya baharini.
Pia Waziri Mpina amesisitiza kuwa Serikali haipo tayari kufanya kazi  na wawekezaji wababaishaji  kwenye sekta ya uvuvi na kwamba kuanzia sasa  hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa  yeyote atakayejaribu kuhujumu raslimali za uvuvi na kujihusisha na uvuvi haramu.

Aidha Waziri Mpina  ametoa onyo kali kwa wawekezaji wa uvuvi kwenye bahari ya Tanzania kuacha kutumia mwanya wa kupewa kibali cha kuvua na kujihusisha na  makosa mbalimbali.
Ameyataja  baadhi ya makosa  hayo kuwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa silaha, binadamu, madawa ya kulevya na nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo. Pia usafirishaji wa  mazao ya misitu na samaki.

Kwa upande wake, Bw. Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Divisheni ya Mashtaka Makao Makuu Dar es Salaam na Mkuu wa Dawati linalohusiana na Makosa ya Mazingira, amesema makosa ya namna hii ni makubwa na endapo kiwango hicho cha pesa hakitalipwa kama ilivyoamriwa, taratibu za kiupelelezi zitakamilishwa na kapteni wa Meli hiyo atafikishwa mahakamani kwa makosa yaliyoainishwa ambapo anaweza kupewa adhabu ya kifungo na meli hiyo kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali. 

Pia amependekeza kuwepo kwa mwongozo wa uendeshaji mashauri (Standard Operating Procedures) kwa makosa yanayofanyika baharini ili uweze kutumiwa na wadau mbali mbali kuanzia ukamataji wa chombo husika, upelelezi wake, namna bora ya kutunza chombo hicho na uendeshaji wa mashauri yanayotokana na operesheni zote zinazofanyika baharini. 

Alisema mwongozo utasaidia kuimarisha kesi zote zinazoenda mahakamani kuanzia inapofunguliwa mpaka kufikishwa mahakamani na wadau wote watajua kwa urahisi namna ya kusimamia utekelezaji wa majukumu yao.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (DSFA) Hosea Mbilinyi amesema Mamlaka yake imegundua kuwepo kwa  baadhi ya wawekezaji wasiofuata taratibu na Sheria  za kufanya shughuli za uvuvi katika bahari ya Tanzana  ambapo amesema tayari Mamlaka imeshawapiga faini ya dola za kimarekani laki moja kwa meli tatu zilizofanya makosa katika sikuza hivi karibuni.

Katika siku za hivi karibuni Waziri wa Mifugo na Uvuvi ameunda  timu iliyoshirikisha  wataalam kutoka katika vyombo mbali vya Serikali kuendesha operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu nchini ambayo  licha ya kupata mafanikio makubwa imetoa hamasa kwa wavuvi  kuanza kusalimisha  zana haramu za uvuvi  na kuziteketeza.
BALOZI WA CUBA NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

BALOZI WA CUBA NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

February 01, 2018

????????????????????????????????????
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisalimiana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
????????????????????????????????????
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa na changamoto zinazolikabili Jeshi hilo Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
????????????????????????????????????
Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades akizungumza jambo wakati mazungumzo yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto), Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo hawapo pichani na Katibu wa Balozi na Mkalima, Sultan Hamud Said (Kulia) Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
????????????????????????????????????
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa katika picha na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam wengine ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Michael Shija wanne kutoka (kulia), Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage wa kwanza (kulia) na Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko wa tano kutoka (kulia). Balozi huyo wa Cuba alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
????????????????????????????????????
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiagana na Balozi wa Cuba hapa nchini, Profesa Lucas Domingo Hernades Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo asubuhi tarehe 01/02/2018.
Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

February 01, 2018

l1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.
l3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.
l4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim  Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora –  Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. 
l5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim  Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora –  Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na Majaji  Wastaafu baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. 
l6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Ngwilimi  baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.
Picha na IKULU

TATU MZUKA YAZINDUA KAMPENI YA VALENTINE DAY,UKISHINDA,UNAYEMPENDA NAYE ANASHINDA

February 01, 2018
 Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga,akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kampuni hiyo kuzindua kampeni mpya ya Valentine  ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’  , ambayo inaanza rasmi leo hadi februari 18,2018.Pichani kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwae Nandy pamoja na Aslay (kushoto) ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo
 Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi kipya Aslay akighani moja ya wimbo walioimba pamoja na msanii mwenzake aitwaye Nandy 'subah lakheri' kama sehemu ya kionjo kwa wanahabari walioshiriki mkutano huo mapema leo jijini Dar.
 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Aslay na Nandy kwa pamoja wakiimba wimbo wao wa 'subah lakheri'mbele ya wanahabari waliofika kwenye mkutano huo mapema leo jijini Dar
 Picha ya pamoja


• Zaidi ya milioni 300 kutolewa katika msimu huu wa Valentine

 Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka, leo wamezindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo inaanza rasmi leo hadi tarehe 18 ya mwezi wa pili.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, bwana Sebastian Maganga, alisema Tatu Mzuka imekuwa na utaratibu wa kuwa na kampeni zinazoendana na misimu ya sherehe za kitanzania.

‘Kwa msimu huu wa Valentine peke yake, zaidi ya shilingi MILIONI 300 zitatolewa kwa washindi wetu watakaocheza kuanzia tarehe 1 hadi 18 ya mwezi huu’ alisema Maganga.

Kama sehemu ya kampeni hiyo pia, Maganga alisema pia KILA SIKU kwa siku 18 kiasi cha MILIONI 10 zitakuwa zinatolewa, ambapo MILIONI 5 itakuwa ya mshindi na MILIONI 5 itakuwa ya mtu ambaye mshindi atamchagua.

‘Lakini pia kubwa kuliko, ukicheza kuanzia leo hadi tarehe 18 utapata pia fursa ya bure kuingia kwenye Valentine SUPA MZUKA Jackpot, ambapo mamilioni yatatolewa kwa washindi, ambapo pia mamilioni ya ziada yatakwenda kwa wanaowapenda’ alisema Maganga.

Kwa upande mwingine, Maganga aliwatambulisha Aslay na Nandy kama mabalozi wa kampeni hii, ambao pia watakuwa na matamasha makubwa katika msimu huu wa Valentine ambayo yatafanyika katika mikoa ya Tanga, Arusha na Dar.

‘Tunaomba mashabiki wetu wacheze Tatu Mzuka katika kipindi hiki, kwani wakishinda pia watapata fursa ya kuhudhuria matamasha yetu pamoja na kukaa sehemu ya watu maalumu pia watapata fursa ya kupiga picha na sisi na mambo mengine kibao’ alisema Aslay.

Akizungumza katika uzinduzi huo, msanii Nandy alisema anaamini kila mtu ana mtu anayempenda na ndio maana amefurahia kampeni hii kwani inawakumbusha watannzia misingi yetu ya upendo.

Namna ya kucheza Tatu Mzuka kipindi hiki cha Valentine ni rahisi kwa kutuma shilingi 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako tatu za bahati zikufuatiwa na neno PENDA, na hiyo itakupa fursa za kushinda kila saa, kila siku na pia kuingia kwenye SUPA MZUKA JACKPOT pamoja na kupata fursa ya kuhudhuria matamasha ya Nandy na Aslay.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

KAIMU KATIBU WA IDARA YA VYUO NA VYUO VIKUU NDUGU ZENDA AKABIDHI KADI 1500 KWA KATIBU HAMASA SENETI YA DAR

February 01, 2018
Dar es Salaam
Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndugu Daniel Zenda akikabidhi  kadi 1500 za wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa Katibu wa Hamasa Seneti ya mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Juakali Kuwanya katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya UVCCM, Upanga  jijini Dar es Salaam.

Zenda amesema, kadi hizo amezikabidhi ili zigawiwe kwa wananchama wapya ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi katika Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, kutokana na mwamko mkubwa wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuunga mkono CCM kutokana na kuvutiwa na Utendaji kazi  wa Rais John Magufuli na Serikali yake ya awamu ya tano

Imetolewa na 
Uvccm Seneti Mkoa Dsm. -- Best regards Bashir Nkoromo Blogger & Photojournalist UHURU PUBLICATIONS LTD Dar es Salaam, TANZANIA Cell: +255 712 498008, +255 789 498008, BLOG: theNkoromo Blog Email: nkoromo@gmail.com

KAMISHNA MKUU KICHERE AWATAKA WAFANYAKAZI SIRARI KUENDELEA NA UTOZAJI WA KODI STAHIKI

February 01, 2018
Na: Veronica Kazimoto-Sirari

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere amewataka Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wakiwemo wa mamlaka hiyo wanaofanya kazi katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja cha Sirari kilichopo wilaya ya Tarime mkoani Mara kufanya kazi kwa ushirikiano na kuhakikisha wanaendelea kutoza kodi stahiki.

Akizungumza wakati wa ziara yake kituoni hapo, Kamishna Mkuu Kichere alisema nchi inaendeshwa kwa kodi za ndani hivyo ni muhimu kila taasisi iliyopo eneo hilo kutimiza wajibu wake katika suala zima la ukusanyaji wa kodi.

“Wote mnajua umuhimu wa kodi na pia mnafahamu kuwa, kwa kupitia kodi hizi, Serikali inajenga miundombinu ya barabara, umeme, inasomesha wanafunzi, inajenga shule, inalipa mishahara ya wafanyakazi wake na mambo megine mengi. Hivyo, mfanye kazi kwa bidii na kwa weledi ili mkusanye kodi inayotakiwa kukusanywa kwa mujibu wa sheria bila kumuonea mtu yeyote.” alisema Kichere.

Kichere aliongeza kuwa, wafanyakazi wote kituoni hapo wana wajibu wa kukusanya kodi ili kuisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo kwa kutumia mapato yanayokusanywa nchini kupitia kodi mbalimbali.Aidha, Kamishna Mkuu huyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime kwa ushirikiano wanaoutoa kwa TRA.

“Nachukua fursa hii kukushukuru wewe Mhe. Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati yako ya Ulinzi na Usalama na pia napenda kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Glorious Luoga kwa ushirikiano mkubwa mnaoutoa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania,” amesema Kichere.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima alisema kwamba, mkoa wake umepanga utaratibu wa kufanya kikao kila mwezi ili kupitia taarifa ya ukusanyaji mapato mkoani humo.

“Kwa mkoa wa Mara kituo hiki cha Sirari ni muhimu sana na kina maslahi makubwa hususani katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, hivyo sisi kama mkoa tumejipanga kila mwezi kukaa pamoja kupitia taarifa ya TRA ili kupata viashiria vya maeneo muhimu ya ukusanyaji mapato ndani ya mkoa wetu,” alisema Malima.

Naye Kaimu Meneja Msaidizi wa Forodha wa Mkoa wa Mara Laurent Kagwebe ameushukuru uongozi wa mkoa wa Mara kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika suala zima la ukusanyaji mapato mkoani humo na kusema kuwa ushirikiano huo ukiendelea, kuna dalili njema za kuongezeka kwa makusanyo hapo baadae.

“Nikili wazi kuwa, nimekuwa nikipata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya mkoani hapa na kama ushirikiano huu ukiendelea, nina imani kuwa, makusanyo yataongezeka kwa kiasi kikubwa,” amefafanua Kagwebe.

Kituo cha Huduma kwa Pamoja cha Sirari kina jumla ya wafanyakazi 86 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyakazi hao wana jukumu la kulinda afya za wananchi kwa kukagua bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia kituo hicho, kulinda usalama wa raia pamoja na kukusanya mapato ya Serikali.

DK.MPANGO ,MKURUGENZI BENK YA BARCLAYS WATETA UJENZI RELI YA KISASASA,MRADI UMEME WA STIGLER'S GORGE

February 01, 2018
Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Bw. Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR) mradi wa miundombinu ya umeme wa Stieglar's Gorge ili kurahakisha maendeleo ya kiuchumi kupitia viwanda.

Amemweleza kiongozi huyo kwamba Serikali imeimarisha uchumi Mkuu kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao uko katika kiwango chatarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

"Tumewekeza kwenye miundombinu kama vile Elimu, maji, kilimo, afya, madini, na biashara na kwamba katika kipindi kifupi cha miaka 2 zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.

Dkt. Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) ambao amesema utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji (Stiegler's Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakao zalisha megawati 2,100 za umeme utakao kuwa wa uhakika na bei nafuu ili kukuza viwanda.

Alisema kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa hapa nchini badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo nguzo kuu ya kufikia malengo hayo.

"Ili tuweze kufikia azma hiyo tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika na wa bei nafuu ili viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa wingi ndio maana tunaiomba Benki yako iweze kufikiria namna ya kushiriki katika ujenzi wa miradi hii" Alisisitiza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango ameipongeza Benki ya Barclays ambayo pia ni mwanahisa katika Benki ya NBC kwa ahadi yake ya kutaka kuwekeza kiteknolojia katika sekta ya benki nchini hatua ambayo itasaidia kukuza mitaji na mikopo kwa kundi kubwa la watanzania wakiwemo wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa.

Alielezea msimamo wake kwamba katika kukuza uchumi, Serikali inathamini mchango mkubwa wa Sekta Binafsi na imeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba hivi karibuni alikuta na wadau wa Sekta ya Benki ili kusikiliza changamoto zao na pia kuwaeleza mambo muhimu ambayo ingependa sekta Binafsi ifanye ili kufikia malengo yanayokusudiwa.

Awali, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anaye hudumia kundi la benki za Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Bw. Peter Matlare, ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.

Alisema hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Kiafrika na Duniani kwa ujumla ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.

Bw. Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare  akielezea umuhimu wa kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Benki yake wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakifuatilia mazungumzo kati yao na ugeni kutoka  Benki ya Barklays  nchini Afrika Kusini (hawako pichani), mkutano uliofanyika mjini Dodoma
 Ujumbe kutoka Benki ya Barclays uliongozwa na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (kulia), wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati yao na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (hayupo pichani), kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano katika kukuza biashara kati ya Tanzania na benki yake, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Maafisa Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano kulia), Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare (wa sita kushoto) wakiwa katika picha yapamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Benki ya Barclays baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Dkt. Khatibu Kazungu, akibadilisha mawazo na naimbu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays kundi la Afrika, Bw. Peter Matlare, baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya Wizara ya Fedha na Uongozi wa Beni hiyo kutoka Afrika Kusini, Mjini Dodoma

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA ATEMBELEA ENEO LINALOTARAJIWA KUEKEZWA NDANI YA MKOA WAKE

MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA ATEMBELEA ENEO LINALOTARAJIWA KUEKEZWA NDANI YA MKOA WAKE

February 01, 2018

01
Afisa kutoka Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) zone ya Pemba Nd. Ali Shaaban Suleiman akitoa ufafanuzi wa maeneo yanayotegemewa kuekezwa.
02
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi. Salama Mbarouk Khatib akimkaguza   Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Omar Khamis Othman katika eneo linalotarajiwa kuwekezwa Hoteli kubwa ya kitalii eneo la Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
03
Eneo la fukwe Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba linalotarajiwa kuekezwa.
Picha na Mwamize Muhammed Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pemba.
WAKAZI ELFU 16 KONDOA VIJIJINI WAONDOKANA NA KERO YA MAJI

WAKAZI ELFU 16 KONDOA VIJIJINI WAONDOKANA NA KERO YA MAJI

February 01, 2018
IMG_9625
Mmoja wa akina mama wa kijiji cha Mauno, Kata ya Bumbuta, Jimbo la Kondoa Vijijini akiongea na vyombo vya habari kuhusu furaha yao baada ya kisima cha maji kuzinduliwa hatua iliyowaondolea kero ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji
IMG_9636
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, na Mbunge wa Jimbo la KOndoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa mradi wa kisima cha maji pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na viongozi wa dini katika kijiji cha Mauno, wilayani Kondoa.
IMG_9643
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
IMG_9645
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
IMG_9652
Wakazi wa kijiji cha Mauno wakiwa wamemwangusha ng’ombe kwa ajili ya kupata kitoweo ikiwa ni namna ya kujipongeza na kusherehekea baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
……………………
Na Benny Mwaipaja, Kondoa
ZAIDI ya wakazi elfu 16 wa vijiji vitatu vya Mauno, Makiranya na Kinyasi-Majengo, katika Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma wameondokana na adha ya kukosa maji baada ya kuzinduliwa kwa visima viatu vya maji vilivyojengwa kwa msaada wa wahisani kutoka nchini Uturuki kupitia ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa visima hivyo katika Kijiji cha Mauno, Kata ya Bumbuta, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini Dokta Ashatu Kijaji, amesema kuwa kuzinduliwa kwa visima hivyo kunalifanya jimbo lake lifikishe visima 41 hatua ambayo amesema itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika jimbo lake.
Dkt. Kijaji ameushukuru Ubalozi wa Uturuki kwa kuratibu msaada huo wa zaidi ya Dola za Kimarekani elfu 36, sawa na shilingi milioni 81, zilizotumika kuchimba visima hivyo pamoja na kuweka miundombinu mingine zikiwemo jenereta zinazotumika kusukuma maji hayo na kuwezesha upatikanaji wa maji hayo.
“Hivi sasa ujenzi wa visima 15 kati ya 25 vinavyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji unaendelea huku wahisani wakiwa wametujengea visima 36 hivyo kufikisha idadi ya visima 61 katika kipindi cha miaka miwili tu tangu Serikali ya Awamu ya Tano ya  Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani hali ambayo haijawahi kutokea na lengo letu ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote 84 vinapatiwa huduma ya maji ifikapo mwaka 2020” Alisisitiza Dkt. Kijaji
Diwani wa Kata ya Bunbuta Bw. Bashiru Mtolo na mkazi mmoja wa kijiji hicho Bi. Khadija Hussein wamesema kuwa tatizo la maji katika kijiji cha Mauno lilikuwa kubwa na kuwalazimisha wanawake na watoto kwenda umbali mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi yao ya majumbani pamoja na kunywesha mifugo.
“Tunaushukuru Ubalozi wa Uturuki kwa msaada wao huu mkubwa na Mbunge wetu kwa ufuatiliaji wake wa karibu uliowezesha kupatikana kwa visima hivi na vingine ambavyo vimesaidia kwa kiwango kikubwa kutatua kero ya maji na tunaamini mpaka kufikia mwaka 2020, matatizo ya maji katika wilaya yetu ya Kondoa litakuwa historia” alisema Diwani Mtolo.
Naye Mwakilishi na Mwambata wa Ubalozi wa Uturuki hapa nchini Sheikh Muhammad Cicek ameeleza kuwa msaada wa Dola elfu 36 zilizotumika kujenga miradi hiyo mitatu ya visima vya maji umetolewa na wahisani mbalimbali wa Uturuki ikiwa ni kuenzi uhusiano wa muda mrefu kati ya Uturuki na Tanzania.
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo ya maji kutasadia kuwawezesha akina mama na wananchi wa Kondoa kwa ujumla kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji ambayo hata hivyo hayakuwa safi wala salama.
Mohammed Enterprises yazindua shindano la Pindua Ushinde

Mohammed Enterprises yazindua shindano la Pindua Ushinde

February 01, 2018

Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imezindua shindano la Zawadi ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde” litakalofanyika kwa muda wa siku 45, linalotarajiwa kuisha Machi 10 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Masoko MeTL, Fatema Dewji ameeleza namna ya kushiriki shidano hilo, kwamba ili ujishindie zawadi, inatakiwa kununua maji ya Mo Maisha na Masafi yenye ujazo kuanzia Mili lita 600 hadi lita 1.7.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tunawaletea shindano la zawadi ya chini ya kizibo kwa bidhaa za maji. Hii ni kwa maji ya Mo Maisha na Masafi yenye ujazo kuanzia Mili Lita 600, lita 1 na lita 1.7 ambazo huja kwako katika chupa za plastiki. hii haijawahi kutokea popote nchini Tanzania,” amesema.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shindano la Zawadi ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde”
Amesema, Pindua Ushinde inakupa fursa ya kujishindia zawadi ya Maji ya bure au pesa taslimu kuanzia Sh. 1,000 hadi 100,000, ambapo ili kujionea ulichoshinda, unatakiwa kupindua kizibo cha chupa ya maji ya Mo Maisha au Masafi.
“Maji ya Mo Maisha na Masafi ni safi na salama kwa afya yako na hutayarishwa katika mazingira bora ya usafi wa hali ya juu. Pia,chupa zetu ni safi na salama zilizorafiki kwa matumizi yako zimetengenezwa ili kukidhi viwango vya kimataifa. Kumbuka unapokunywa maji yetu unajiepusha na magonjwa yanayoenezwa kwa maji yasiyo safi na salama,” amesema.
Vile vile, Fatema Dewji amezindua Kampeni ya kutunza mazingira inayofahamika kwa jina la “Tanzania Safi” iliyolenga kuhakikisha ardhi haiharibiwi kwa uchafu wa chupa za plastiki.
“Tutatoa ushirikiano kuondoa chupa za plastiki zitakazoonekana mitaani ili zitumike kama malighafi katika uzalishaji viwandani. Hii si mara ya kwanza kufanya kampeni za utunzaji mazingira, awali MeTL ilifanya kampeni ya utunzaji mazingira kwa kusafisha ufukwe wa Coco Beach," amesema na kuongeza.
“Pia tuliendesha kampeni ya kuelimisha jamii namna ya kuepuka magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama ambapo wataalamu wa afya walielimisha jamii.”
Naye Meneja Mauzo wa Kiwanda cha A 1 kilicho chini ya MeTL kinachozalisha Maji ya Mo Maisha na Masafi, Godfrey Mangungulu amesema washindi wa maji bure na fedha kuanzia 1,000 hadi 50,000 watapewa zawadi zao waliponunua maji, na watakaoshinda zaidi ya fedha hizo watachukua bidhaa zao kwenye Kiwanda cha A1 kilichopo Kurasini.
“Tumeamua kurudisha fadhila kwa jamii, kwa zaidi ya miaka 20 tunauza bidhaa zetu , hivyo tumeamua kurudisha sehemu ya mauzo ya bidhaa zetu kwa jamii. MeTL tuajivunia bidhaa bora na usambazaji wetu unafika nchi nzima,” amesema.

MICHUANO TULIA CUP YARINDIMA KIBAMBA

February 01, 2018
MSHAMBULIAJI wa timu ya Kibamba Worious Emmanyel Athanas (kulia) akijitahidi kumtoka beki wa timu ya Mpakani FC, Haruna Ramadhani, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
MSHAMBULIAJI wa timu ya Kibamba Worious (kulia) akijitahidi kumtoka beki wa timu ya Mpakani FC, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
Katibu wa Kamati ya Uratibu wa Michuano ya Tulia Cup Moreen Ngasala akimkaribuisha Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA) Ernest Mgawe (kulia) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mpiga wa Kibwegele, katika ufunguzi wa michuano hiyo
Msanii wa kujitegemea akichangamsha Uwanja kabla ya michuano hiyo kuanza
Kibamba Warious na Mpakani FC wakiwa tayari kwa mtanange
MC akitangaza hatua mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa michuano hiyo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Majige aakisalimiana Katibi wa Siasa na Uenezi Kata ya Kibamba Clement Mgabo walipokutana kwenye uzinduzi wa michuano hiyo
Wadau wa friends Of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo
Mgeni rasmi akienda kukagua timu ili mpambano uanze
  1. Mgeni Rasmi akisalimiana na mwamuzi wa mechi hiyo
Mgeni rasmi akisalimia wachezaji wa timu ya Kibamba Warious
Mgeni rasmi akiwa na baadhi ya viongzi baada ya kukagua timu
Timu zikiwa tayari kwa mpambano
Mmoja wa waraibu wa michuano hiyo Moreen akisoma risala
Mwenyekiti wa Friends of Tulia akizungumza kabla ya mpambano kuanza
Wadau wa Friends of Tulia wakiwa kwenye michuano hiyo
Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA),  Ernest Mgawe akizungumza kabla ya kipute kuanza. "Michezo siyo siasa, inasaidia sana kuweka jamii pamoja hasa vijana. Napongeza sana uamuzi wa kuanzisha michuano hii", alisema.
Mgeni rasmi akizungumza kufungua michuano hiyo ambayo leo kuu ni kuwaweka vijana pamoja na pia kuchangisha vifaa na fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Hondogo katika Kata hiyo ya Kibamba. Mgeni huyo rasmi aliahidi kuchangia mifuko mia moja ya saruji
Wadau wa Friends Of Tulia
Baadhi ya wadau wakiwa na wachezaji
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na baadhi ya wachezaji
Mgeni rasmi akijiandaa kupiga mpira kuanshiria mechi kuanza
Mgeni rasmi akiwa ameshapiga mpira
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na timu zote
mpambano ukaanza
"vipi umenusurika?' refa akimuuliza mchezaji huku akimpapasa baada ya mchezaji wa timu ya Kibamba Warious baada ya  kuchezewa vibaya na mchezaji wa Mpakani FC
Kipa wa Mpakani FC akiuangalia mpira wakati ukiingia kimiani kufuatia penati iliyopigwa na mchezaji wa Kibamba Warious kutokana na mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa rafu katika eneo la hatari
Mpambano ukiwa umeiva
Mdau wa Friends of Tulia akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kuhangamsha uzinduzi wa Tulia Cup
Mwandishi wa Uhuru FM akiwa na mmoja wa wasanii waliofika kutia chachandu michuano hiyo