RC GEITA KUWAPIMA MAOFISA UGANI UWEZO WA UTENDAJI KAZI ZAO ZA KILIMO

October 30, 2017

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akimkabidhi mbegu bora ya mahindi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi  wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu za mahindi, mhogo na viazi lishe uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya mkoa huo jana. Kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo   (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na ukame  Wema.






 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Isamilo kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kutoka kushoto ni Mtafiti kutoka COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, Mtafiti Bestina Daniel na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo   (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro,  Ismail Ngolinda, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu ya mahindi.
 wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo
 Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.
 Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.
 Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Salome Renatus akizungumza na waandishi wa habari.

MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA

October 30, 2017
Mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

 Na Fredy Mgunda,Mufindi

Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.

Kimbale alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.

“Sisi walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Kimbale
Aidha Kimbale aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum. 

“Wakurugenzi amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema Kimbale

Kimbale alimpongeza wakurugenzi wa halmashauri ya mufindi na mji wa mafinga kwa kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa pale inapotakiwa tofauti na hali ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.

“Unakuta siku ya wanawake duniani au siku ya walimu duniani bado walimu wananyimwa ruhusa wakati muda huo mkurugenzi amewaruhusu walimu kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi baina ya watendaji wa nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Kimbale


Kimbale aliwapongeza walimu wa manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kunyimwa ruhusa.

Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema haelewi kwanini mara kwa mara swala hilo linakuwa linajirudia maana tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.

Sasa naenda kuandika barua rasmi kwa wakurugenzi ili kutatua kabisa tatizo hilo maana hata kwangu imekuwa kero na mwazoni nilijua wakuu wa shule ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio tatizo naenda kulishughulikia kwa haraka sana swala hili” alisema Williamu

Williamu aliwataka maafisa elimu na wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa kuwapa ruhusa walimu pale ambapo wanapata matatizo maana hakuna haja ya kumnyima ruhusa mtu akiwa anashida na watakiwa kuzifahamu siku za kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie wanapaswa kutoa ruhusa bila kipingamizi.

“Kunasiku kama siku ya mwalimu,siku ya wanawake na siku nyingine za kitaifa walimu wanapaswa kupewa ruhusa kwenda kuhudhuria tukio hilo kutokana na umuhimu wake” alisema Williamu

Williamu alisema kuwa mkurugenzi ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa shule wanatoa wapi hiyo jeuri ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa ngazi za juu wanajua kuwa kunakitu kinafanyika cha taifa.

Williamu aliwataka viongozi wa walimu kuandika barua ya kuomba viwanja ili waweze kulishughulikia swala hilo likiwa kwenye maandishi.

“Andikeni barua yenye idadi na majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa kasumba ya kusema wanaotaka ni kikukindi cha walimu wachache tu na bila kufanya hivyo swala lenu la kuomba viwanja litakuwa gumu kulitafutia ufumbuzi” alisema Williamu
Williamu aliwaomba walimu wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala hilo kwa kuwa sio jambo la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili kufanikishwa swala walimu kupata viwanja.

Naye afisa elimu wa wilaya ya Mufindi alisema kuwa watawatafuta hao maafisa ambao wanawanyima ruhusa walimu wakati swala hilo lilishatafutiwa ufumbuzi.

“Jamani sisi huku sheria tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu wapewe ruhusa sasa sijui ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa nitazungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wenzangu

RAIS MHE.DKT MAGUFULI AHUTUBIA WAKAZI WA NYAKATO MKOANI MWANZA

RAIS MHE.DKT MAGUFULI AHUTUBIA WAKAZI WA NYAKATO MKOANI MWANZA

October 30, 2017
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza mara baada ya kufungua kiwandaa cha Sayona Drinks ltd kilichopo Nyakato.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Katikati ya jiji la  Mwanza wakati akitokea Nyakato.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati mmiliki wa Kiwanda cha Sayona Drinks Subhas Patel alipokuwa akionesha bidhaa mojawapo ya kiwanda hicho.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja  mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakati Kwaya ya Makongoro ilipokuwa ikitumbuza katika viwanja vya Mwatex Nyakato jijini Mwanza
10
Kwaya ya Makongoro ikitumbuiza
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini wimbo wa kwaya ya Makongoro kabla ya kuhutubia mamia ya wananchi Nyakato mkoani Mwanza.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wananchi wa Nyakato mara baada ya kuwahutubia.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato  mara baada ya kumaliza kuwahutubia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato  mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Nyakato jijini Mwanza.
PICHA NA IKULU

KISHINDO CHA MSIMU WA TIGO FIESTA CHAACHA GUMZO MOSHI

October 30, 2017
Wasanii Banarba na Gnako wakishiriki uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo ya TUMEKUSOMA ambayo ni namba maalum (code number) itakayowawezesha wateja wa Tigo kuingia kwenye menyu na kupata huduma mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.
Msanii Bright akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.
Chege akiburudisha kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.

NAIBU WAZIRI LUGOLA AZINDUA OPERESHENI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI NZIMA

October 30, 2017
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa operesheni maalumu ya usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar es salaam.
Zoezi la usafishaji wa mitaro likiendelea katika eneo la Tandale kwa Ali Maua, maeneo hayo yameathirika kwa kiasi kikubwa na mvua za hivi karibuni kutokana na kurundikana kwa taka ngumu.
Sehemu ya Mto Ng'ombe kama unavyoonekana ukiwa umekithiri kwa taka. Hii leo  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (hayupo pichani) ameshiriki katika uzinduzi wa Operesheni maalumu ya kusafisha mazingira kote nchini. Zoezi la uzinduzi wa usafi limefanyika katika Mto Ng'ombe.

DKT.KIGWANGALLA:“SASA TUTAKAMATA MAJANGILI KULIKO KUKAMATA NYARA

October 30, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini.
Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili.
“Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini. Ameeleza Dkt.Kigwangalla
Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili.
“Jana tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla.
Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi.
Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu aliyekamatwa akijipanga kuingia Hifadhi ya Serengeti 
Baadhi ya risasi zilizokamatwa na jangili huyo  
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla akiwa pamoja na Mhifadhi wa Mkuu wa Serengeti William Mwakilema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakiangalia mpaka unahishia pori tengefu la Loliondo-Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti mwishoni mwa wiki wakati wa kukagua maeneo hayo yenye mgogoro na wafugaji.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA JIJINI MWANZA

October 30, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kufungua daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha jijini Mwanza mara baada ya ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wananchi waliohudhuria katika sherehe za ufunguzi wa wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiwaaga mara baada ya ufunguzi wa Daraja hilo la Furahisha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwapungia mkono wananchi waliopo chini ya Daraja la Furahisha (hawaonekani pichani ) Mara baada ya ufunguzi wa daraja hilo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya ufunguzi wa daraja hilo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipanda ngazi za Daraja hilo jipya la Furahisha jijini Mwanza.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA: ZINGATIENI VIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA BARABARA

October 30, 2017
Elias Kwandikwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri,

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Mitambo ya ujenzi ikiwa eneo la kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28, mkoani Tabora.

……………

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa matengenezo.

Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.

“Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Amesisitiza kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.

Kuhusu barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli, Mhe. Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa mkataba wake.

“Lengo la mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kw kuzingatia makubaliano ya mkataba wako.Amesema waziri kwandika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwamnri, amemuhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.

“Kwanza sisi kama mkoa tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji kupatiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Ni Wakenya Rock City Marathon 2017

October 30, 2017
 Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19

Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ambae mbali na kuzindua mbio hizo pia alishiriki katika mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mkenya George Onyacha aliyetumia muda wa saa 02:23:27, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.

Katika mbio hizo zilizoanzia na kuhitimishwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo ilishuhudiwa nafasi ya kwanza hadi ya saba zikishikwa na wakimbiaji kutoka nchini Kenya huku nafasi ya nane ikienda kwa Mtanzania Paschal Mombo alietumia muda wa saa 02:30:43.

Akizungumzia siri ya ushindi wake, mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliomuwezesha kukimbia bila changamoto yoyote Too alisema ni kujituma kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.

“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi na ninashukuru Mungu nimefanikiwa,” alisema.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Alice Gradys Otero aliyetumia muda wa saa 02:48:18 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Tecla Chebet  aliyetumia saa 02:54:28 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Flavious Kwamboka alietumia muda wa saa 02:57:32.
Mtanzania Brabuelia Bryton kutoka mkoani Moshi alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 03:14:41

Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini humo  waliibuka na kitita cha Sh 4 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh 2 mil na washindi watatu Sh Mil 1.

Kwa upande wa mbio za km 21 Peter Limo kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:05:24, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo George Wayaki aliyetumia muda wa saa 01:05:50

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mtanzania Chacha Boy aliyetumia muda wa saa 01:05:59, ikiwa sekunde tisa tu nyuma ya mpinzani wake.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Dorifin Omare aliyetumia muda wa saa 01:17:12 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Alice Mogiare aliyetumia saa 01:18:30 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Maiselina Issa alietumia muda wa saa 01:19:55.

Mtanzania Siatha Romanus kutoka mkoani Arusha alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 01:25:58
Katika mashindano hayo ilishuhudiwa washiriki ambao pia ni wadhamini wa mbio hizo kutoka  makampuni ya PUMA, Tiper, NSSF, RedBull,  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS wakishiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri Shonza alisema aliwapongeza washiriki na waandaaji wa mbio hizo na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kurejesha hadhi ya mchezo wa riadha nchini.

“Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.” Alisema.

Naye Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka mbali  mbali na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizo alisema licha ya wingi wa washiriki kutoka ndani ya nchi bado taifa linakabiliwa na uhaba wa wanaridha wa mbio ndefu yaani km 42 na wachache wanaofanya vizuri kwenye mbio hizo wamekuwa wakishindwa kushiriki mbio kama hizo zinazofanyika ndani ya nchini.

Abrahamu Too kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19.

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana  ambapo alikimbia mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.
 Baada ya uzinduzi kazi ikaanza!
 Mbali na kuzindua mbio hizo pia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (wa pili kulia)alishiriki kikamilifu katika mbio mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

 Mbali na washiriki kutoka ndani ya nchin pia pia washiriki kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China na Marekani nao hawakuwa nyuma.

Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kwenye warsha ya kukabidhi zawadi kwa washindi ambapo pamoja na mambo mengine aliwapongeza waandaaji wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI).


Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mbio za Km 42 (waliosimama nyuma) mara baada ya kuwakabidhi zawadi pamoja na medali. Wengine ni pamoja na Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka(wa tatu kushoto), waandaaji pamoja na viongozi wa mchezo huo.

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 42 kwa upande wa wanawake ambapo washindi wa kwanza hadi watano wote walitoka nchini Kenya.
 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 5 ambazo zilikuwa mahususi kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi pamoja na washiriki kutoka kwenye mashirika mbalimbali (corporate race)