ADC KANDA YA KASKAZINI WACHAGUA VIONGOZI WA KUKIWAKILISHA MKUTANO MKUU TAIFA.

September 16, 2013
Burhani Yakub,Tanga.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha Alliance Democratic Change(ADC) Kanda ya Kaskazini,jana kilifanya uchaguzi na kuwapata wajumbe 10 watakaoiwakilisha  mikoa yao kutano mkuu wa chama hicho Taifa.

Waliochaguliwa katika mkutano huo uliokuwa na ushindani mkubwa ni Doyo Hassan Doyo,Mohamed Siyu, Mwarami Zimbwe,Asia Mgaza,Jamal Ally, Asha Juma, Rehema
Mhando, Rashid Hamza ,Zainab Juma na Hamida Msumeno.

Mkutano huo wa uchaguzi huo uliosimamiwa chini ya uongozi wa AyubMussa Kimangale kutoka tume ya uchaguzi ya Chama hicho ambapo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa ADC,said Miraji Abdallah.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Jijini
Tanga,Miraji aliwataka wajumbe kuwachagua viongozi ambao watamudu mikikimikiki ya chaguzi za Serikali ukiwamo wa Serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema ADC licha ya uchanga wake lakini kimeundwa ili kuchukua madaraka ya Serikali na kimejidhatiti kwa hilo kutokana na ukweli kwamba kimeenea nchi nzima katika kipindi kifupi tangu kuundwa hivyo kinahitaji viongozi watakaojitoa ipasavyo.

“Hatutaki ADC kiwe ni chama chenye viongozi wa huku mikoani wa kushiriki makongamano au Semina,wala kuwa chama cha mkobani au magazetini,tunataka kuchukua uongozi wan chi”alisema Miraji.

MWENYEKITI ADC TAIFA AFUNGUA MKUTANO WA UCHAGUZI MKOA WA TANGA LEO.

September 16, 2013
MWENYEKITI WA CHAMA CHA ADC TAIFA SAID MIRAJI AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA CHAMA HICHO MKOANI HAPA LEO KABLA YA KUANZA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI ULIOFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI WA COMUNITY CENTRE JIJINI TANGA.

KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAWEJE AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO KUSHOTO KWAKE NI KATIBU WA CHAMA CHA PPT MAENDELEO MKOA WA TANGA,RAMADHANI MANYEKO.

WAJUMBE NA WANACHAMA WA ADC KUTOKA WILAYA MBALIMBALI MKOANI TANGA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO TAIFA SAID MIRAJI LEO

HAPA AKIWA AMEPIGA PICHA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA MKOANI HAPA KULIA MWANZO NI MKURUGENZI WA HABARI NA MAHUSIANO CHAMA HICHO,HASSANI DOYO.


       MWENYEKITI WA CHAMA CHA ADC TAIFA,SAID MIRAJI KUSHOTO AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA HABARI NA MAHUSIANO WA CHAMA HICHO,HASSANI DOYO KABLA YA KUANZA UCHAGUZI LEO.


KUSHOTO NI MKURUGENZI WA HABARI NA MAHUSIANO WA CHAMA CHA ADC HASSANI DOYO KUSHOTO KATIKATI NI MWENYEKITI WA CHAMA HICHO TAIFA,SAID MIRAJI.


WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI WAKIHAKIKI KURA KABLA YA KUTANGAZA MATOKEO YA WAJUMBE WATAKAOINGIA KATIKA MKUTANO MKUU.