WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.

January 31, 2016
NA RAISA SAID,BUMBULI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.

Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo  Kanisa  na Msikiti zimeezuliwa mapaa katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo imesabisha  kaya  hizo  kukosa  mahali pa kuishi , huku wengi wa  waathirika  wakipewa hifadhi  kwenye  nyumba  za majirani zao.

Akizungumza  na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo January 27 mwaka huku saa kumi jioni.

Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi  kuwa  ni Vitongoji vya Kwemchaa,Nazareti,CCM,Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio vimeweza kuathirika na maafa hayo.

Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
 
Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada zaidi.
 
"Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu  mwingine" alisema Makamba

Makamba   aliwataka  wananchi  wote  kupanda  miti ili kuepuka  upepo  mkali  unaosababishwa  na  mvua  zinazoendelea kunyesha  katika  maeneo tofauti
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA JANA IKULU DAR ES SALAAM

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA JANA IKULU DAR ES SALAAM

January 31, 2016

Q1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory
 Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve   kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses  Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi   katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya  Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q22
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akifurahia jambo na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuwaapisha  Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q23 Q24 Q25
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msemaji wa JWTZ Luteni Kanali Ngeleba  Lubinga baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q26
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahman Kaniki  baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016.
PICHA NA IKULU
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA masuala ya Usalama Barani Afrika.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA masuala ya Usalama Barani Afrika.

January 31, 2016

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
(Picha na OMR)
NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. KIGWANGALA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. KIGWANGALA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA

January 31, 2016

2
Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.
3
NaibuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Dawa la MSD jijini Arusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru.
1
Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Arusha. NaibuWaziriwaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe. Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo. Naibu Waziri huyo pia amewahimiza watendaji wa MSD kuwa waadilifu, kuwajali na kuwasilikiza wateja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja, huku akitoaangalizo kwa wale wanao kiuka taratibuza ajira kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhaminiya MSD Prof. IdrisMtulia ameeleza kuwa MSD inaweza kufanya vizuri zaidi endapo changamoto za sheria ya manunuzi, mgawo mdogo wafedha kwa vituo vya Afya, hospitali na zahanati, na mgawo wafedha kuja kwa mafungu zitafanyiwa kazi. Naye Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa MSD itakuwa na maduka manne tu mkoani Dares Salaam, Mwanza, A Arusha na Mbeya ambapo kwa mikoa mingine MSD wanaafanyama wasiliano na hospitali za mikoa ziwe na maduka ya hospitali wanayoendesha wenyewe na kisha MSD iwauzia dawa na kuwawezesha utaalamu wakuendesha maduka hayo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO.

January 31, 2016
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.
Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya .
Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa  mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.
Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

LEO NI HEPI BESDEI YA BLOG YA VIJIMAMBO YATIMIZA MIAKA 6

January 31, 2016



 Vijimambo ilizaliwa Januari 31, 2010 na kuzinduliwa Oktoba 23, 2010 na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar. Picha ni siku ya uzinduzi ukumbi wa Mirage  uliopo Hyattsville, Maryalnd.
Hapa Balozi Mwanaidi Maajar akiwa mgeni rasmi miaka 2 ya Vijimambo iliyofanyika Machi 31, 2012 ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
 
Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyia Julai 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton Inn uliopo Capitol Heights. Maryland.
Mwenyekiti wa Vijimambo akiwapokea wasanii Shilole na Masanja waliokuja kunogesha sherehe ya miaka 3 ya vijimambo.
Mhe. Nyarandu (kulia) akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo iliyofanyika Septemba 13, 2016 Hotel ya Growne Plaza iliyopo Rockville, Maryland.
Wasanii Aunty Ezekiel na Cassim Mganga wakija kunogesha miaka 4 ya Vijimambo, kushoto ni NY Ebra akipata ukodak moment na wasanii hao walipotembelea New York City.
Cassim Mganga na Aunty Ezekiel wakitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York siku walipotembelea pande za New York City, kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Maniongi
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA
Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu

Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu

January 31, 2016
Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu.
IMG-20160130-WA0029
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo
IMG-20160130-WA0030
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akitembelea Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha.
Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo upo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao unaweza kuwashawishi watu wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi.
"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapa,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma, dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko kwenye hospitali binafsi.
"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma wa serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema Dkt. Kingwangalla.
IMG-20160130-WA0032
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
IMG-20160130-WA0027
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangwala akiwa amembeba mtoto mchanga (bado hajapatiwa huduma) na mama wa mtoto huyo Bi. Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
IMG-20160130-WA0028
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuangalia mtoto huyo