UVCCM yaipiga Tafu timu ya Umiseta Carton 50 za maji ya Kunywa

June 04, 2013
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga,Ramadhani Chomola akipokea maji toka kwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga,Abdi Makange wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Afisa elimu jiji la Tanga,Mr.Sengasu na kulia kwake ni Afisa Michezo mkoa wa Tanga,Digna Tesha,Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga,Acheni Maulid na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Tanga School

Pokea Mkuu

June 04, 2013
MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Tanga,Abdi Makange akimkabidhi Maji ya Kunywa kwa ajili ya timu ya Umiseta ambayo imeweka kambi katika shule ya sekondari Tanga School kwa Afisa Elimu Mkoa wa Tanga,Ramadhani Chomola wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Elimu Jiji la Tanga,Mr.Sengasu,kulia ni Afisa Michezo mkoa wa Tanga,Digna Tesha na Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga,Acheni Maulid.

Mkacheze vema

June 04, 2013
MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Tanga,Abdi Makange akizungumza na wachezaji wa timu za Umiseta mkoa wa Tanga leo mara baada ya kukabidhi maji ya kunywa cartons 50 zilizitolewa na umoja huo,kushoto kwake ni Afisa Michezo mkoa wa Tanga,Digna Tesha na mwenye shati nyeupe ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga,Acheni Maulid.

Tulifika

June 04, 2013
MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Tanga,Abdi Makange akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari ya Tanga School ambapo timu ya Umiseta ya Mkoa wa Tanga imeweka kambi ambapo alikwenda kuitembelea na kukabidhi maji ya kunywa cartons 50,Picha na Mpiga picha wetu.