TRL KUSAFIRISHA SARUJI YA TANGA KWA NJIA YA RELI

March 24, 2016
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogoso kulia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Saruji ya Simba Cement,Reinhardt Swart  wakitiliana  saini ya makubaliano baina yake na Kampuni ya Saruji ya Simba iliyopo Jijini Tanga kwa lengo la Kampuni hiyo kuanza kusafirisha shehena za mizigo kwa kutumia njia ya reli ili kuokoa athari za uharibifu wa Barabara zinazojitokeza kwa sasa kutokana na usafirishaji kwa kutumia malori
Waziri wa wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa kushoto akibeba Mfuko wa Saruji na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Saruji ya Simba Reinhardt Swart kulia baada ya utiaji wa saini ya makubalinao saini ya makubaliano baina yake na Kampuni ya Saruji ya Simba iliyopo Jijini Tanga kwa lengo la Kampuni hiyo kuanza kusafirisha shehena za mizigo kwa kutumia njia ya reli ili kuokoa athari za uharibifu wa Barabara zinazojitokeza kwa sasa kutokana na usafirishaji kwa kutumia malori

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akishuka kwenye ngazi mara baada ya kupakia mfuko wa saruji saini ya makubaliano baina yake na Kampuni ya Saruji ya Simba iliyopo Jijini Tanga kwa lengo la Kampuni hiyo kuanza kusafirisha shehena za mizigo kwa kutumia njia ya reli ili kuokoa athari za uharibifu wa Barabara zinazojitokeza kwa sasa kutokana na usafirishaji kwa kutumia malori.




SERIKALI imetia saini ya makubaliano baina yake na Kampuni ya Saruji ya Simba iliyopo Jijini Tanga kwa lengo la Kampuni hiyo kuanza kusafirisha shehena za mizigo kwa kutumia njia ya reli ili kuokoa athari za uharibifu wa Barabara zinazojitokeza kwa sasa kutokana na usafirishaji kwa kutumia malori.

Makubaliano hayo yalitiwa saini na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL)Masanja Kadogosa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Saruji ya Simba Reinhardt Swart wakishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa.

Akizungumzia hatua hiyo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kwa sasa serikali inatumia shilingi milioni moja kwa kila kilometa moja ya Barabara kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na gharama ambazo zingetumika kwa ajili ya kuboresha njia za reli.

Prof.Mbarawa alisema Kampuni hiyo itakuwa ikisafirisha tani 35,000 sawa na tani 500,000 kwa mwaka  ambapo TRL itakusanya shilingi milioni 40 kwa kila mzigo jambo ambalo litarudisha uhai wa njia za reli na kuondoa uharibifu wa Barabara.

“Kwa mwezi magari haya makubwa yaani malori yanayobeba mizigo yanafanya zaidi ya tripu 3,500 sawa na tripu 35000 kwa mwaka sasa jiulize ni kwa namna gani Barabara zinaharibika na kusababisha gharama kubwa sana za ukarabati kwa serikali ….hivyo tunaamini mazungumzo yetu yataenda vizuri na kufika tulikokusudia”,alisema Waziri huyo.

Aliwataka watumishi wa Kampuni ya Reli (TRL)kufanya kazi kwa bidii hasa kwa kutambua kuwa kampuni hiyo ndiyo moyo wa uchumi wa nchi katika sekta ya usafirishaji na kamwe serikali haitamvumilia mtumishi mzembe kwenye sekta hiyo.

“Lazima wafanyakazi mshirikiane na kila mmoja ajitume katika kutimiza wajibu wake bora niwe na wafanyakazi wachache hata ishirini wenye kuliko kukaa hapa na watu wanaoiba dizeli na oili kama mtu hawezi na aondoke hatuwezi kuendelea kufanya kazi kwa mazoea na kuharibu shirika hili ambalo ni tegemeo la kiuchumi kwa Taifa”,alisisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRL Masanja Kadogosa akizungumza hivi karibuni alisema kuwa kwa mwaka 2014/2015 Kampuni ya Saruji ya Simba Tanga ilisafirisha shehena ya mizigo tani 44,000 ambapo kutoka Julai hadi Disemba 2015 ilisafirisha tani 24,960.

Kadogosa alisema katika kufufua Kampuni hiyo ya TRL serikali imewekeza kiasi cha  Dola za Kimarekani Milioni 100 sawa Bilioni 200 za kitanzania huku ikilenga kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo matengenezo ya miundo mbinu ya njia za reli.

Naye MKurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha saruji Swart alisema kuwa hatua hiyo itapunguza gharama za usafirishaji wa shehena za mizigo ya saruji ambapo katika safari zake wanatarajia tani 20,000 za saruji kutoka Pongwe kwenda Kigoma na tani 15,000 kutoka Pongwe kwenda Mwanza.

“Uzalishaji wa saruji kwa mwezi ni tani 105,00 na tunatarajia kusafirisha tani 35,000 kila mwezi kwenda mikoa mingine tukiamini njia hii itakuwa ni nafuu zaidi,”,alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwahakikishia wamiliki wa kiwanda hicho kwamba serikali ya mkoa imejipanga vizuri kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama wa mizigo yao ili kusitokee hujuma wakati wa usafirishaji.

“Tunajua kuna hujuma za wizi wa mizigo na mataruma ya reli lakini kama mkoa tutahakikisha tunapambana na hali hiyo kwa hali na mali ,”alisisitiza Shigella.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN

March 24, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyi Haji Makame mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na usalama vikiimba wimbo wa Taifa kwenye uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jeneral Devis Mwamunyange wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na Yamoto bendi katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na Bendi ya muziki ya Yamoto katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa Amaan mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar mara baada ya kuapishwa. Picha na IKULU

SHEREHE YA KUAPISHWA RAIS MTEULE WA ZANZIBAR

March 24, 2016

WanaChama cha Mapinduzi na Wananchi wakiwa pamoja wakisherehekea kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,pia wakiwepo Waandishi wa Habari kushuhudia mambo mbali mbali yanayoendelea katika zoezi la kuapishwa kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya Brass Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya kuapishwa rasmi kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu ya saba.
Viongozi mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa leo katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
Waaandishi wa Habari Wapigapicha wakijaribu kufanikisha kazi yao kupata matukio mbali mbali wakati wa Sherehe za kumuapisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa unaoashiria mwanzo wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa rasmi leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Mkuu wa KMKM Hassan MUssa Komodoo wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.[Picha na Ikulu.]

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA MSD

March 24, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.

Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya wametembelea Makao makuu ya Bohari ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam.  Katika ziara yao kamati imeishauri serikali kutenga bajeti ya dawa na vifaa tiba kulingana na mahitaji. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema bado hakuna viwanda vya ndani vya kutengeneza dawa ,na vichache vilivyopo havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya MSD.

Katika hatua nyingine,wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge ya masuala ya UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa,huku wakihimiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie deni la serikali. Aidha, walisema kulipwa kwa deni kutasaidia MSD kununua dawa muhimu kwa wakati.

Kuhusu deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa kazi.

Hata hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari serikali imeshaahidi kupunguza deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa fedha.


VIJANA WAANDAA MSAFARA WA HISANI KWA KUTUMIA MAGARI KUPINGA UJANGILI NA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI

March 24, 2016
Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea makamilisho ya maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard.
Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele akiongea na waandishi wa habari kuelezea kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard
Wawakilishi wa Bongo Ride charity cruise wakisikiliza kwa makini maswali ya waaandishi wa habari katika mkutano huo kuhusu kuhusu ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani.

Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele akiteta jambo na Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani.

Mkuu wa matukio Kelvin Edes ( Wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia maelezo ya wawakilishi  wa Bongo ride charity cruise kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani



Dar Es Salaam, 24 Machi 2016 Vijana wa Bongo Ride, kwa ushirikiano wa vijana wenzao wa Team Tezza na TanzaniaZalendo wanayo furaha kuwatangazia umma wa watanzania kukamilika kwa maandalizi ya msafara(cruise) wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,
Ujangili hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni umeongezeka ikiwa ni matokeo ya mahitaji makubwa  ya pembe za ndovu,pembe za kifaru na pia ngozi ya chui na bidhaa mbalimbali za wanyamapori.
Hivi sasa biashara ya wanyamapori na rasiliamali za asili imeshika nafasi ya nne kwa biashara haramu inayowafaidisha wengi duniani,baada ya madawa ya kulevya ,silaha na usafirishaji wa binadamu inakadiliwa kuwa na thamani ya dola zaidi ya 284 billion za kimarekani.
Hali hii inatisha licha ya kuwaeimisha vijana kuwa wanaweza kuwa mabalozi wa kulinda wanyamapori pamoja na rasilimali za nchi yao,pia wanatakiwa kutuma ujumbe watu waweze kuchukua hatua kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa amesema “ tumezindua awamu  ya tatu ya Bongo Ride Charity Cruise ikiwa ni matokeo ya kuweza kusaidia jamii.Tukiwa na washiriki zaidi ya mia 2 wa hapa nchini na zaidi ya washiriki  elfu 2 Afrika mashariki. Katika awamu yetu ya kwanza tulifanya msafara wa hisani kusaidia wagonjwa waliopata ajali katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani kwa kuwapatia mashuka yakutandika pamoja na kujifunikia na pia Mwaka jana tuliweza kwenda Mkoani Morogoro na kusaidia watu waishio na virusi vya UKIMWI Morogogo (WAVUMO) ikiwa nia ni kuhamasisha amani na upendo katika nchi yetu na awamu hii tumeamua kufanya ”YOUTH AGAIST POACHING” ili kufikisha ujumbe kwa vijana wenzetu na serikali kwamba tnapinga ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani kama wazalendo na wapenda maendeleo.
“Malengo yetu ni kuwa na tukio la kihistoria tukiwa na nia ya kumfanya kijana wa Kitanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio vilivyomo ndani ya nchi pamoja na kuwa balozi mzuri na mzalendo wa Nchi yake” Aliongeza Magesa
Mkuu wa matukio wa Bongo Ride Kelvin Edes akiongea alisema Tunategemea kuwa na siku tatu za mbio hizi za hisani za magari kuanzia Dar es salaam kuelekea Arusha tukiwa  na washiriki  zaidi ya mia 200 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Pia tutakuwa na muda wa kuongea na vyombo vya habari, kutembelea shule na kuzunguka  katikati ya mji kuweza kuongeza uelewa juu ya janga la ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
“Siku ya pili tarehe 26 tutaungana na washiriki mbalimbali wa Arusha na tutaelekea Hifadhi ya wanyama Tarangire na kujionea mambo mazuri ya hifadhi hiyo na kujifunza zaidi. Jambo hili litasaidia zaidi watu kuwapa hamasa ya kwenda kujionea vivutio vya hifadhi za ndani na kumfanya kijana  ajionee utajiri uliomo ndani ya nchi yake.
Tunaamini kabisa kasi ya kuuliwa kwa maalbino imepungua kwasababu wao wenyewe wanaweza kuzitetea nafsi zao, lakini Tembo, Kifaru na wanyama wengine wanaokumbwa na janga la ujangili hawawezi kuzitetea nafsi zao na kuomba msaada, Hivyo sisi kama vijana tumejitolea kuwa mstari wa mbele kupaza sauti zetu na kutetea haki zao kwani nao wanastahili kuishi, ”Aliongeza
Meneja Mawasiliano wa Bongo Ride  Krantz Mwantepele alinukukuliwa akisema kuwa vijana wakipaza sauti zao itaamsha matumaini kuwa imefika wakati kuwa ujangili ni jambo linalotakiwa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukomeshwa .
“Sisi kama vijana tunaumizwa na kuongezeka kwa matukio haya ya ujangili ,uhujumu wa rasilimali ni matukio yote yanayopangwa na watu wenye tamaa za mafanikio ya haraka  na kutamalaki kwa rushwa miongoni kwa viongozi na wanajamii.”
Pia Mkurungezi na mwanzilishi wa Team Tezza Kenan Richard aliongeza kuwa vijana wanataka sauti zao zisikilizwe, kwa maana hawataki kuwa kizazi kitakachowasimulia wajukuu zao  kuwa hawakufanya jambo lolote juu ya haya na wanaomba vijana wenzetu na viongozi wa dunia kuungana nasi ili kupinga biashara haramu ya ujangili.





KUHUSU BONGORIDE CHARITY CRUISE;
Bongo Ride Charity Cruise ilianzishwa mwaka 2014 ikiwa na lengo la kuisaidia serikali na jamii kiujumla kutatua baadhi ya matatizo yanayoizunguka jamii ya Kitanzania na Afrika kwaujumla kwa njia ya kupaza sauti kuhusu jambo lolote linaloonekana kuwa tatizo kwa namna tofauti.
Nia yetu ni kuzunguka mikoa yote Tanzania na Afrika kwa kutumia njia ya kusafiri kwa pamoja na magari yetu binafsi na kutoa misaada sehemu mbalimbali katika bara letu la Afrika, Pia kumfanya kijana wa Kitanzania kujifunza tamaduni mbalimbali na kukuza wigo wa marafiki wenye msaada kwake ili kuongeza sababu lukuki za kimaendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.

KWA MAELEZO ZAIDI; WASILIANA NA
KRANTZ MWANTEPELE
MENEJA MAWASILIANO  BONGORIDE
NAMBA YA SIMU;0712579102

EMAIL;krantzcharles@gmail.com

BODABODA MKOANI MWANZA WAADHIA KUANZISHWA KWA UMOJA WA KITAIFA WA BODABODA.

March 24, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhura wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.

Katika Mkutano huo, Konisaga ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara kuzidisha juhudi za kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali, badala ya kasi iliyopo ya kutoza faini kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani.

Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye  Kayanda amesema "pamoja na Mambo mengine, Wajumbe wa Mkutano huo walikubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya Bodaboda".
Kwa Habari Zaidi BONYEZA HAPA.

KAMPUNI YA MABIBO BEER YADHAMINI BONANZA LITAFANYIKA LEADERS CLUB JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAM

March 24, 2016
 Mwonekano wa chupa ya bia ya Windhoek inayosambazwa hapa nchini na kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd.
 Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd  Ismail Mzava (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu udhamini wa bonanza lililoandali na Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge litakalofanyika Viwanja vya Leaders Klabu Jumamosi. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Sas  Sangandele. 

Mazoezi yakiendelea katika  Kituo cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge  kilichopo katika Jengo la Tanzanite House lililopo jirani na Kanisa la Full Gaspel.
 Mazoezi yakiendelea kwenye kituo hicho.
 Vyuma vikiinuliwa kwenye kituo hicho.
 Mazoezi yakifanyika.
Hapa ni kazi tu na mazoezi kwa kwenda mbele.

Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Mazoezi cha Power or Fitness cha Mwenge kimeandaa bonanza la michezo mbalimbali litakalofanyika Jumamosi Viwanja vya Leaders Klabu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema bonanza hilo liwatawahusisha watu wa rika zote wakiwepo watoto.

"Bonaza letu litawashirikisha watu wa aina zote na litakuwa la bure na litaanza saa 12 asubuhi hadi jioni hivyo wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongaji vyake tunawaomba wafike kwa wingi kushiriki" alisema Sangandele.

Alisema bonanza hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd kupitia kinywaji chake cha Windhoek linakuwa na michezo ya mpira wa miguu, kufukuza kuku, karate kwa watoto, mazoezi ya viungo na mbio za kilometa tano.

Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Ismail Mzava alisema wameamua kudhamini bonanza hilo kutokana na umuhimu wa michezo ambayo inaleta afya kwa jamii.

"Kampuni yetu imekuwa ikitoa udhamini mbalimbali katika shughuli za jamii ndio maana tukaona ni vema tukawaunga mkono hawa wenzetu katika jambo hilo muhimu litakalohusisha michezo mbalimbali" alisema Mzava.





Tigo yatoa 300m/- kudhamini wanafunzi wa tehama vyuo vikuu

March 24, 2016
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael.

Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katikati ni Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez,na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael. wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  akipeana mkono na Mmoja wa wanafunzi waliopata udhamini wa tigo  Carolyne Paul, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Udsm shahada ya uhandisi wa kompyuta na teknolojia ya habari   wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati),Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula(kulia) na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael(kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati) akipata "SELFIE"  na ,Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula  na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam   .



Dar es Salaam Machi 23, 2016 Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo wametangaza kudhamini wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa kwa jumla ya shilingi million 310.
Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema fedha hizo zitagharamia ada ya chuo, gharama za kufanya utafiti, malazi na chakula kwa kipindi cha miaka minne cha masomo ya Tehama kwa kila mwanafunzi.
Gutierrez amesema udhamini huo unaowalenga kuwasiadia vijana wenye vipaji katika taaluma ya Tehama kutimiza ndoto zao za kimaisha ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya mawasiliano ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya tehama na kuleta maendeleo nchini.

“Tunaamini kupitia udhamini huu kampuni yetu,  kwa kushirikiana na DTBi, inatoa mchango wake katika kujenga kizazi kijacho cha mabingwa katika sekta ya Tehama ambao watakuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi hii,”Gutierrez amesema akiongeza kwamba tayari kuna makubaliano kati ya Tigo na DTBi unaowapa wanafunzi kutoka DTBi fursa ya kubuni bidhaa mbalimbali vya Tehama ambavyo hutumiwa na Tigo kibiashara na mapato kugawanywa kwa wadau wote.  

 Wanafunzi tisa waliobahatika kupata udhamini wa Tigo ni Erickson Muyungi (UDSM), Fatma Moshi (UDSM), Caroline Paul (UDSM), Michael Lunyungu (UDOM), Robert Charles (UDOM), Isack Kipako (UDOM), Jacqueline Dismas (UDSM), Jumanne R. Mtambalike (IFM) na Joel Mtebe (UDSM).

Akizingumzia zaidi kuhusu mkataba huo kati ya Tigo na DTBi, Mkurugenzi huyo wa Tigo amesema: “mbali na udhamini tunaoutoa kwa wanafunzi wa Tehama tuna mradi wa pamoja uitwao ‘Project Digitize’ ambao umewawezesha wanaTehama chipukizi kuanzisha kampuni zao kuipitia ubunifu wao na ambao wanapata msaada kutoka Tigo katika kuendeleza miradi yao. Hadi leo kuna wanatehama watatu wanaosaidiwa na Tigo kupitia mpango na ambao bidhaa pindi bidhaa zao zitakapoanza kutumika kibiashara, watafaidika kutokana na mgawanyo wa mapato..”
 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi Mhandisi George Mulamula kwa upande wake amesema üshirikiano na Tigo umetoa fursa na njia za kibunifu kwa wanafunzi wa DTBi kupata elimu, kujenga uwezo wao wa Tehama ambavyo vitawasaidia kuonyesha vipaji vyao katika fani hii ndani na nje ya nchi.

Mulamula aliongeza kusema kwamba: “DTBi’s ina malengo ya kuwahamasisha vijana wakiwemo wanawake kujenga tabia za kuwa wajasiriamali Tehama ili kusaidia kukuza sekta binafsi na kuongeza makusanyo ya kodi nchini. Katika kutekeleza azma hii, Tigo imetoa mchango mkubwa kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu kufikia ndoto zao za uzalishaji mali, kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, kuleta nafasi mpya za ajira yote haya yakiwa ni vielelezo vya jinsi ambavyo tehama inaweza kusaidia kukuza pato la taifa.”
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"