MISA TANZANIA GOVERNING COUNCIL PICKS SALOME KITOMARY AS INTERIM BOARD CHAIRPERSON

April 12, 2017
TANZANIA NCHI YA KWANZA KUWA NA RELI YA KISASA YA MASAFA MAREFU AFRIKA

TANZANIA NCHI YA KWANZA KUWA NA RELI YA KISASA YA MASAFA MAREFU AFRIKA

April 12, 2017
A 8
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Tanzania inatarajiwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na reli ya kisasa inayotumia umeme na mafuta itakayokuwa na uwezo wa kusafiri  masafa marefu kwa mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa.
Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ya leo huko Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa reli hiyo itakuwa ya kisasa zaidi barani Afrika na itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuchochea fursa za biashara ndani na nje ya nchi.
Awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ambayo itahusisha kipande cha kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro utagharimu jumla ya shilingi trilioni 2.8 na utatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 30.
Dkt Magufuli alitoa mfano wa nchi zenye reli za mwendokasi lakini masafa mafupi barani Afrika kuwa ni Morocco ambayo inasafiri kwa mwendokasi wa kilomita 220 kwa saa na Afrika Kusini inayosafiri mwendokasi 150 kwa saa.
Dkt Magufuli alieleza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na treni itakayosafiri masafa marefu kwa mwendokasi wa km 160 kwa saa.
Alifananua kuwa mradi huo wa ujenzi wa reli unatekelezwa kwa fedha za Tanzania ambapo tayari serikali imeshawalipa wakandarasi malipo ya awamu ya jumla ya shilingi bilioni 300.
Akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa reli hiyo, Rais Magufuli alisema kuwa reli hiyo itasaidia kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwa haraka na kuwafikia wateja ndani ya muda mfupi.
Vilevile, reli hiyo itarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo pamoja na kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani ya Kusini.
Sambamba na hayo, Rais Magufuli alisema kuwa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kuimarisha sekta nyingine za uchumi ikiwemo utalii, viwanda, kilimo, pamoja na kutoa ajira kwa watanzania ambapo kutakuwa na ajira muda zipatazo 600,000, na ajira za kudumu 30,000.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema kuwa reli hiyo ya kisasa inayojengwa na wakandarasi kutoka muungano  wa kampuni mbili za nchi ya Uturuki na  Ureno  itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 10,000 kwa mara moja  na kutumia saa 2 kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na saa 7 na dakika 40 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Naye, Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya ujenzi kutoka Uturuki ya Yapi Merkezi Bw.  Emre Aykar alisema kuwa reli hiyo itaimarisha zaidi uhusiano wa Uturuki na Tanzania na kuongeza kiwango cha shughuli za biashara nchini.
“Tunaahidi kujitahidi kumaliza mradi kwa wakati na katika kiwango kinachotakiwa” alisema Bwana Aykar.
Reli hiyo ya kisasa inatarajiwa kujengwa pembeni ya reli ya kati ambayo ilijengwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Wajerumani na Waingereza miaka 112 iliyopita.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATAMBULISHA HUDUMA YA UWEKAJI AKIBA KWA WANACHAMA WA HIARI WA MPANGO UJULIKANAO KAMA “LAPF JIONGEZE SCHEME” KUPITIA MITANDAO YA M-PESA NA TIGO-PESA

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATAMBULISHA HUDUMA YA UWEKAJI AKIBA KWA WANACHAMA WA HIARI WA MPANGO UJULIKANAO KAMA “LAPF JIONGEZE SCHEME” KUPITIA MITANDAO YA M-PESA NA TIGO-PESA

April 12, 2017
A
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji akiba kwa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika Makao makuu ya Mfuko mjini Dodoma .
A 1
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
A 2
Meneja mwenye dhamana na Skimu ya uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze Scheme) Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa ili kuweka akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma.
A 3
Afisa huduma kwa wanachama wanaoweka akiba kwa hiari (LAPF Jiongeze Scheme) Bw. Juma Venerando akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulivyojipanga kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa wanachama.
A 4
Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Mkoani Dodoma Bw.  Gideon Morris akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za Tigo-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote kuweka akiba ya hiari Kwenye Mfuko wa LAPF.
A 5
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Mkoani Dodoma Bw.  Balikulije Mchome akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za M-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote kuweka akiba ya hiari katika Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
A 6
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo mbalimbali yaliyotolewa kwenye utambulisho wa huduma za uwekaji wa akiba ya hiari kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mkutano uliofanyika mjini Dodoma.

TUKITAKA NCHI YA VIWANDA TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA

April 12, 2017
 ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali Jijini Tanga wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu wilaya ya Tanga ambapo kiwilaya lilifanyika kwenye shule ya Sekondari Tanga Don Bosco iliyopo eneo la Maweni jijini Tanga inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga.
 ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi wa pili kulia akimkiliza mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo wakati alipokuwa akifafanua jambo
a
 ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi katikati akionyesha jambo na Sista ambaye anafanya kazi kwenye shule hiyo 
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi amesema iwapo Serikali  inataka nchi  ya viwanda hawana budi kuweka msukumo mkubwa kwenye kupiga vita dawa za kulevya vitendo ambazo zimechangia kwa asilimia kuwaharibu vijana wengi hapa nchini.
Banzi aliyasema hayo  wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu wilaya ya Tanga ambapo kiwilaya lilifanyika kwenye shule ya Sekondari Tanga Don Bosco iliyopo eneo la Maweni jijini Tanga inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga.

Alisema ili kutimiza azma hiyo ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi lazima kuwepo na juhudi kubwa za kuuteketeza mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini uliyoharibu vijana wengi ambao wangekuwa nguvu kazi kubwa ya Taifa la kesho.

“Kama tunataka kuifanya nchi kuwa ya viwanda maana yake kila mmoja apate elimu ya madhara ya dawa za kulevya lengo kubwa likiwa kuliondoa tatizo hilo kwa vijana ambalo limekuwa likipoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kutumika katika shughuli mbalimbali lakini pia kuwepo kwa mapambano ya kupiga vita hali hiyo “Alisema.

“Lazima kuwepo kwa dhamira ya dhati na mipango ambayo itawezesha kuutokomeza mtandao wa dawa za kulevya unaoangamiza vijana wengi ambao wangewezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujiingizia kipato halali na kuendesha maisha yao bila kuwa tegemezi “Alisema Askofu Banzi.

“Vijana tuachane na matumizi ya dawa za kulevya ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha kuharibu vijana ili kuendana na sera ya maendeleo ya viwanda kwa kuyapiga vita”Alisema.

Akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira,Askofu Banzi aliitaka
jamii kuacha kukata miti ovyo,kuchimba mahandaki ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira.

“Kwani suala la ukataji miti ovyo limekuwa tishio kubwa hapa nchini na kuifanya kugeuka  jangwa kitendo ambacho kimeweza kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira kwa jamii hivyo lazima tuachana na jambo hilo“Alisema.

Awali akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Don Bosco Gregory Mhuza alisema waliamua kupanda miti ili kuhakikisha wanatunza mazingira ambayo ni muhimu kwa jamii.

“Sisi kama shule leo hii tumepanda miti lakini tutahakikisha
tunaitunza na kuilinda kwa vizazi vya sasa na vijazo ili kuiepusha
nchi yetu kukumbwa na janga “Alisema.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Maweni,Wales Janga alisema uzinduzi wa Juma la Elimu kwa kupanda miti katika shule hiyo ni ishara ya kuthamini uwepo wa mazingira kutokana na usemi usemao tunza mazingira yakutunze hivyo jamii haina budi kufanya hivyo ili kuendena na suala hilo.

“Pamoja na kupanda miti pia tutatembelea maabara ya ufundi kwani shule hii ni shule ya Ufundi ili tuweze kuona namna vijana wetu wanajifunza katika masomo yao ya ufundi kuelekea Tanzania ya Viwanda ya Mwaka 2025 “Alisema.

Alisema kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii majukumu yake katika suala zima la elimu duni kwani baadhi yao wamelipokea suala la elimu bila malipo tofauti na kujisahau kuwa wao ni mdau namba“Alisema.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO

April 12, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akiwa ameshika majina hayo.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza

BOHARI YA DAWA (MSD) YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI FURSA NCHIN

April 12, 2017

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

BOHARI ya Dawa (MSD) imeshiriki Jukwaa la Biashara, lililoandaliwa na Kampuni ya magazeti ya TSN,jijini Mwanza.

Katika Jukwaa hilo,MSD pia imeshiriki maonesho ya vifaa tiba.

Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo jijini Mwanza jana Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (pichani kulia) amewahakikishia wadau wa Mwanza fursa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha dawa nchini,endapo watakidhi ubora unaohitajika.

Amesema,hatua hii inafuatia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi na taasisi za Umma katika uwekezaji.

Bwanakunu amefafanua kuwa uanzishwaji wa viwanda nchini utapunguza gharama za uagizaji dawa na vifaa tiba toka nje ya nchi, kuokoa fedha za kununua nje,kusafirisha,kugomboa na  kupata dawa kwa muda mfupi.