MSAADA TUTANI: UZINDUZI WA KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION (KFDF) WAFANA

May 23, 2016
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kariakoo family Development Foundation Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi polisi mstaafu Jamal Rwambow akiogea machache na  amekitaka  chama hicho kujali maendeleo ya jamii ya cha hicho kinachowajumuisha wzawa na waliowahi kuishi na wanaoishi eneo lote la Kariakoo jijini Dar es salaam kwa lengo la kushirikiana mambo mbalimbali ya limaendeleo na kijamii.
Mwenyekiti wa kariakoo family development fund mh.mohamed bhinda akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa City Lounge jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kariakoo Family  Development Foundation, Mohamed Bhinda akiwa na Jamal Rwambow (mwenye suti nyeusi) wakikata keki mara baada ya kuzindua  umoja huo.
Wakongwe wa Kariakoo Senpai Yusuf Kivuli (kushoto) na Senpai Waheed  wakiwa katika shoo  ya Goju Ryu Karate  katika uzinduzi wa Kariakoo Family Development Foundation.
 Mkurugenzi wa MMG, Ankal Muhidin Issa Michuzi akilishwa keki katika uzinduzi wa Kariakoo Family Development  Foundation 
Picha ya Pamoja ya Wanakariakoo na Mgeni Rasmi.
WAAMUZI 40 KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

WAAMUZI 40 KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

May 23, 2016
Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeteua waamuzi 40 watakaochezesha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) inayoanza leo Mei 23 katika vituo vinne tofauti hapa nchini.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27, imegawanywa katika makundi manne ambako bingwa katika kila kundi atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2017/18.


Timu tano zitapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya washindi katika vituo vyote vinne, mshindwa bora katika vituo vya Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda daraja kwa kuangalia vigezo vya wingi wa pointi, wastani wa mabao, mabao kufunga na mabao ya kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa kuwa kina timu shiriki sita.

Waamuzi walioteuliwa kuchezesha ligi hiyo kwa kituo cha Njombe ni Elasto Msaliwa, Klement Manga, Mashaka Lulambo, Lazaro Mbogoro, Michael Mkongwa, Alex Chitalula, Maulid Makiwa, Michael Kilango, Edina Ndelwa na Haidal Kisingile.

Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa, Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es Salaam.

Kituo cha Morogoro walioteuliwa ni Athuman Lazi, Mohammed Theophil, Seleman Kinugane, Fikiri Yusuph ‘Magari’, Nicolaus Makangara, Mwarabu Mumba, Emmanuel Muga, Herry Shao, Shaban Juma na Makongo Katuma na timu zinazoshiriki ni Stend  FC ya Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo FC(Lindi), Muheza United ya Tanga, Stand Misuna FC ya Singida, Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC ya Temeke, Dar es Salaam.

Kituo cha Singida wako Meshack Suda, Abdallah Mwinyimkuu, Sarah Bongi, Lucas Mathias, Amani Mwaipaja, Siyachitema Kawinga, Theophil Tegamaisho, Shaaban Msangi, Aboubakar Irume na Frederick Ndahani na timu shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi SC (Arusha), Kitayosce FC (Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Murusagamba FC (Kagera), Fire Stone (Manyara) na Tomato FC (Njombe).

Kituo cha Kagera walioteuliwa ni Jonesia Rukyaa, Jamada Ahmada, Ringston Rwiza, Grayson Buchard, Grace Wamala, Edgar Lyombo, Yahaya Juma, Adrian Karisa, Getrude Kahawa na Ahmada Simba na timu shiriki ni Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela City (Shinyanga), Ambassador FC (Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa (Kigoma).

NE-YO AWAKOSHA MASHABIKI WA MWANZA KATIKA JEMBEKA FESTIVAL 2016

May 23, 2016
Katika kusherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio ya Jembe FM iliyo na makazi yake jijini Mwanza, Mei, 21 kumefanyika tamasha lililopewa jina la JembekaFestival ambalo lilikutanisha mashabiki wa redio hiyo walio mikoa ya kanda ya ziwa kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa msanii wa muziki wa miondoko ya R& B kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith almaarufu kama NE-YO
Licha ya msanii NE-YO pia kulikuwapo na wasanii wa nchini wakiongozwa na Diamond Platinumz ambaye aliambatana na timu yake kutoka lebo yake ya Wasafi (WCB), wasanii wengine ni Fid Q, Baraka Da Prince, Ney wa Mitego, Maua Sama, Mo Music, Stamina, Juma Nature a.k.a Kiroboto, Ruby na wengine wengi.
Tamasha hilo lilifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo pia lilihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa nchini, Flaviana Matata ambao kwa pamoja walionekana kufurahia tamasha hilo la kihistoria kuwahi kufanyika jijini Mwanza.
Kufanyika kwa tamasha hilo kulisimamiwa na mikono ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu, Coca Cola, FastJet, SYSCORP, EF Outdoor, Ndege Insurance Brokers, Jembe FM, Double Tree, KK Security na Mo Entertainment ambao ndiyo waliowezesha kufanyika kwa tamasha hilo.
Kama ulikosa kuja Mwanza hii hapa video ya msanii wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, NE-YO akiimba wimbo wake uliotamba na uanendelea kubamba wa 'Miss Independent".
Video ya Mkali wa Hip Hop nchini Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akichana mistari tamasha la Jembeka na Vodacom jijijni Mwanza.
Video ya mkali wa Ragga na Dance hall, Cool Chata wa JEMBE FM ya Mwanza akiwasha moto Jembeka Festival 2016
Video msanii wa Bongo Flava, Ruby akiimba wimbo wa 'Nivumilie' kwenye tamasha la Jembeka Festival 2016.
Sebastian Ndege
Mkurugenzi mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akizungumza jambo kabla ya kuwatambulisha wageni waheshima walioshiriki kwenye Jembeka Festival 2016.(Picha zote na Modewjiblog)
RC Mwanza, John Mongella
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba, Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula pamoja na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye wakimsikiliza Dr. Sebastian Ndege (hayupo pichani).
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanislaus Mabula
Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula akizungumza machache katika Jembeka Festival 2016 kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye kuwasalimia wakazi wa jiji Mwanza waliofurika katik uwanja wa CCM Kirumba mwishoni mwa wiki.
Nape Nnauye
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) na kubariki tamasha la Jembeka Festival 2016 lililofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.
Costantine Magavilla
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla akisamiana na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye.
Dr. Sebastian Ndege
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye pamoja na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba wakati burudani zikiendelea kwenye Jembeka Festival 2016.
Mh. Nape Nnauye
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) akifafanua jambo kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege (kulia) pamoja Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba.
Jackson StarTimes
Wadau wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.
Jembeka Festival 2016
Vijana wa Mwanza walikuwepo kumshuhudia msanii Neyo Live kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Monica Joseph
Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula (kushoto) na Mtaalamu wa masuala ya fedha nchini, Monica Joseph (wa pili kushoto) walikuwepo kushuhudia tamasha la Jembeka na Vodacom ililoweka historia jijini Mwanza 2016. Kwa picha zaidi bofya hapa

BENKI YA CRDB YAFANYA MKUTANO MKUU WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

May 23, 2016



 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akihutubia mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICC Arusha. 
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akijibu maswali ya wanahisa.

Wanahisa wakiwa katika mkuano.
 Manaibu Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na Saugata Bandyopadhyay wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo.
Mwanahisa akiuliza swali.
Mwenyekiti Abeid Mwasajone akiongoza mkutano wa wanahisa. Katikati ni Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo na Makamu Mwenyekiti, Steven Mashishanga.
Wanahisa wakifuatilia mkutano.
Wanahisa wakijiandikisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na Naibu Mkurugeni Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay.
Wanahisa.
 Wanahisa wakipiga kura kuwachagua wajumbe wa bodi ya wakurugenzi katika benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na mjumbe wa bodi wakijadiliana jambo, Boniface Muhegi (kulia) wakati wa mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Tullyesther Mwambapa, Philip Alfred na Anderson Mlabwa.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tullyesther Mwambapa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA ZIARA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)

May 23, 2016

Mkuu wa Mko wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetico (mwenye tai) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetico akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisi za MUWSA.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na Wakuu idara katika Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Nsere .
Chanzo cha Maji cha Nsere ambacho kiwango cha maji kinatajwa kushuka kutoka lita za ujazo Milioni 12 hadi Milioni 9.5.
Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadick akitembelea maeneo ya chanzo hicho.
Mkuu wa Mkoa Said Mecky Sadick na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri 
Meneja ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) Mhandisi Patrick Kibasa akitoa maelezo ya chanz hicho kwa Mkuu wa mkoa Said Mecky Sadick na ujumbe wake.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya chanzo hicho.
Mkuu wa mkoa Said Mecky Sadick akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea chanzo cha maji cha Shiri.
Mkuu wa Mko wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akitembelea kisima cha maji cha Mawenzi.
Kisima cha Maji cha Mawenzi.
Tani la Maji lililopo katika eneo la Kisima cha Mawenzi.
Mkuu wa Mkoa akiwa katika jengo la kuendeshea mitambo ya visima viwili vipya vya mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) vilivyopo eneo la KCMC.
Ujumbe wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ukiwa katika moja ya visima vya zamani ambacho kinataraji kufanyiwa ukarabati.
Meneja Ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) akitoa maelezo katika tanki la maji la Longuo ambalo litatumika kwa ajili ya kuhidhi maji yatakayotumika kwa wakazi wa Kiborironi na vijiji vya Korini na Kikarara.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.