Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akionesha
Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya
kukabidhiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa
niaba ya Wabunge. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika,
Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto)
akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson(wa pili kulia) Mwongozo wa
watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa niaba ya Wabunge.
Wakishuhudiawatatu kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa pili kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba. Makabidhiano hayo yamefanyika
ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)
akimweleza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson(wa kwanza kulia) umuhimu wa
Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa Wabunge mara baada
ya kumkabidhi Mwongozo huo kwa niaba ya Wabunge ili waweze kusoma, kuelewa na
kuelimisha wananchi namna ya kutumia vema huduma na bidhaa za mawasiliano
nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson(wa kwanza kulia) kuhusu Mwongozo wa
watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya kukabidhiwa na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Wabunge. Makabidhiano
hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kushoto na akikabidhiwa Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar
Francesca Morandin akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa
Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kwa Wizara ya
Afya Zanzibar ili zisaidie kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za
Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa
Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka shirika la
UNICEF ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara
hiyo.
Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
……………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuhudumia Watoto UNICEF limetoa msaada wa Komputa aina ya Laptop 200 kwa
Wizara ya Afya ya Zanzibar ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa
za Afya kwa wizara hiyo.
Laptop hizo zenye thamani ya zaidi
ya Shilingi Milioni 400 zimetolewa ikiwa ni mwendelezo wa UNICEF
kuiunga mkono Serikali katika kuimarisha huduma za matibabu hasa ya
akinamama na watoto.
Akikabidhi Msaada huo katika
Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazi mmoja Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar
Francesca Morandin amesema upatikanaji wa taarifa sahihi ni jambo muhimu
linalofaa kupewa kipaumbele.
Amesema uwepo wa taarifa sahihi za
Wajawazito na watoto huisaidia Serikali kujua idadi ya ongezeko la watu
wake hali inayopelekea kupanga mipango vyema ya matibabu kulingana na
idadi ya watu husika.
Amewataka Watendaji kwa ujumla
kuunga mkono juhudi zinazotolewa na UNECO ili kuhakikisha afya za Watoto
na Wajawazito zinaimarika.
Francesca ameongeza kuwa Shirika
hilo la UNICEF litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za
kimatibu na kuipongeza Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea
kutoa matibabu bure kwa wananchi wake.
Amefahamisha kuwa Zanzibar inapiga
hatua mbele kwa upande wa Matibabu na kupongeza juhudi zinazofanywa na
Serikali kuwashajiisha Wajawajizito kushiriki huduma hizo muhimu katika
maisha yao. “Zanzibar zaidi ya asilimia 99 ya Wajawazito hushiriki
katika Kliniki mbalimbali walau mara moja katika kipindi chao cha
ujauzito. Hii inawezekana kwamba imechangiwa na juhudi za Serikali za
kuyafanya matibabu bure”Alipongeza Francesca.
Kwa upande wake Waziri wa Afya wa
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amelishukuru Shirika la UNICEF kwa
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika sekta ya Afya.
Amemuahidi Mwakilishi huyo kwamba Msaada uliotolewa utatumika vyema ili kutimiza malengo ya Shirika hilo.
“Cha bure mara nyingi vitu vya
bure havitunzwi vyema lakini Laptop hizi lazima tujitahidi kuutumia
vyema..Laptop ziendelee kudumu na taarifa zinazohitajika zote kuanzia
Dawa, Wajawazito, Watoto nakadhalika zote ziwekwe kwenye mfumo
unaotakiwa”Alisema Waziri Kombo.
Waziri Kombo amesema Zanzibar
inaendelea kupokea pongezi kutoka pande zote za Dunia kwa namna Serikali
inavyojitahidi katika kutoa huduma bora za matibabu na hivyo msaada huo
utazidi kuimarisha huduma hizo.
Laptop hizo zitagawiwa katika
Vituo vyote vya matibabu Unguja na Pemba ili kuimarisha usimamizi wa
mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Kangi Lugola akisalimiana na Uongozi wa Mamlaka ya maji Safi na
usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) alipofanya ziara ya kutembelea
Ofisi hizo mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Kangi Lugola akifafanua jambo alipokua akiongea na Wafanyakazi
wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA)
mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Kangi Lugola akielekeza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) David
Palangyo wakati wa ziara ya kutembelea mabwawa ya kuhifadhi maji taka
yanayotumiwa na DUWASA katika eneo la Swaswa mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Kangi Lugola akiwa pamoja na Ujumbe toka DUWASA akikagua
mabwawa ya kuhifadhi maji taka katika eneo la Swaswa na Ilazo mjini
Dodoma ambapo alifanya ziara.
Sehemu ya mabwawa ya kuhifadhia
maji taka inayotumiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira
mjini Dodoma (DUWASA) katika eneno la Swaswa.
………………………………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola hii leo amefanya ziara ya
kushtukiza katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini
Dodoma (DUWASA) ikiwa ni pamoja na kutembelea miundombinu ya Mamlamka
hiyo.
Waziri Lugola amesikitishwa na
namna Mamlaka hiyo ilivyoshindwa kuhimili kiasi cha maji taka
yanayozalishwa katika Mji huo wa Dodoma na kutitiririka katika makazi
ya watu bila kutibiwa (Treated).
Katika ziara hiyo Naibu Waziri
Kangi Lugola ameitaka Mamlaka hiyo kuja na mpango wa haraka wa kudhibiti
maji hayo kwa lengo la kudhibiti usafi wa Mazingira na Ustawi wa
Wananchi. “DUWASA mmekuwa mkitiririsha maji taka bila kuyatibu kwenye
makazi ya watu, na kwenye kilimo cha mpunga, na mmepelekea baadhi ya
watu kuyahama makazi yao.” Lugola alisisitiza.
Aidha Waziri Lugola ameitaka
DUWASA kuhakikisha mabwawa mawili yaliyotelekezwa eneo la Swaswa
yanakarabatiwa ili kuhimili kiwango cha uharibifu wa mazingira kabla ya
tarehe 31/12/2018, na kuwataka kuimarisha ulinzi kuzunguka mabwawa yote
ili watu wasichepushe maji katika mashamba yaliyopo pembezoni mwa
mabwawa hayo.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Lugola ameitaka Mamlaka hiyo ya DUWASA kutumia gari ya matangazo
na kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa kutoa elimu kwa
wananchi wa maeneo hayo juu ya athari ya matumizi ya maji hayo machafu
DUWASA pia imetakiwa kupata
kibali kutoka kwa Mamlaka ya Bonde la Maji ya Wami-Ruvu cha kutiririsha
maji taka kwenye mazingira na kuhakikisha maji hayo yanatibiwa kwa
kiwango kinachoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kufanya Tathmini ya
Kimkakati ya Mazingira kuendana na ongezeko la watu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA
Bw. David Pallangyo amesema kuwa walipokea mabwawa hayo kutoka kwa
iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mwaka 2002 na kukiri
kutiririsha maji hayo bila kuyatibu katika mazingira.
Bw. Palangyo amebainisha kuwa
Ofisi yake ina mkakati wa muda mrefu wa kujenga mabwawa makubwa zaidi
eneo la Nzuguni ili kukidhi mahitaji ya sasa na kuendana na ongezeko la
idadi ya watu baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga(CCM) Alhaji Mustapha Mhina Selebosi akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani leo kwenye ukumbi wa Halmashauri kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Naibu Meya wa Jiji hilo,Mohamed Haniu
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudio Mayeji akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo,Alhaji Mustapa Mhina Selebosi anayefuata ni Naibu Meya Mohamed Haniu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja
Naibu Meya Mohamed Haniu akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi
Waheshimiwa madiwani wa Jiji la Tanga wakifanya dua kabla ya kuanza kikao hicho
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi katika akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia na Naibu Mstahiki Meya Mohamed Haniu wakipitia taarifa mbalimbali wakati wa kikao hicho leo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi katika akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga ,Mohamed Haniu
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Hamisi Mkoba akipitia kabrasha wakati wa kikao hicho
Katibu wa CCM wilaya ya Tanga katika akifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa kikao hicho
Baadhi ya waheshimiwa maduwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho kwa umakini
Sehemu ya wataalamu katika halmashauri ya Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho
Diwani wa Kata ya Maweni (CCM) Calvas Joseph akiuliza swali katika kikao hicho
Sehemu ya waheshimiwa madiwani wa Jiji la Tanga wakiangalia makabrasha kabla ya kuanza kikao hicho
Sehemu ya wataalamu kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwa makini kufuatilia taarifa mbalimbali kulia ni Ramadhani Possi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na
Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.
Akizungumza
baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis
Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya
mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.
Pamoja na
kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa
Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo. Pichani Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi
na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo
Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa
Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini
Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika
ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake
Kilimani mjini Dodoma
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na
Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.
Akizungumza
baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis
Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya
mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.
Pamoja na
kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa
Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo. Pichani Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi
na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo
Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa
Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini
Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika
ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake
Kilimani mjini Dodoma
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na
Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.
Akizungumza
baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis
Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya
mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.
Pamoja na
kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa
Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo. Pichani Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi
na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo
Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa
Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini
Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika
ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake
Kilimani mjini Dodoma
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Na Karama Kenyunko , Globu ya Jamii Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul “Diamond Platzum” mapema leo
asubuhi amefika katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande
wa Ustawi wa Jamii kwenye mahakama ya watoto kwa ajili ya usuluhishi
juu ya matunzo ya mtoto wake aliyezaa na mlimbwende Hamisa Mobeto.
Alianza kuingia Diamond akafuatiwa na Hamisa baada ya muda kidogo ambapo walikaa kwa zaidi ya saa moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza usuluhushi huo, Diamond alisema,
“Kiasi
cha pesa tunavyoviandika kama kama hivi, tunazungumza tu, lakini watoto
hawahitaji mahitaji mengi, wakati mwingine mtoto wako una uwezo wa
kumpa hadi Shilingi milioni 100 na huwezi kusema simpi kwa sababu
niliandikisha nitampa Laki Moja haimsaidii”.
Alisema wao kama
wazazi wameweka mazingira mazuri ya kumlea mtoto wao kwa kadri ya uwezo
wataokapata, kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora wakipata
watakula nae wakikosa watalala
“Nyuma ya stori hii nimejifunza
kwamba siyo kila mtoto ambaye haishi na baba au mama yake basi asiyeishi
nae anatatizo nae, hata mi nimejifunza pia kwa mimi na baba yangu,kuna
vitu wazazi wanavifanya vinakuwa siyo fresh,vinatengeneza story, mtoto
baadae akikua hajui story ya nyuma anajua mzazi mmoja anamatizo akajua
dingi noma lakini siyo tu”.
Aidha Diamond amesema ni vema wazazi
wote wawili watumie busara kuangalia namna gani wanasuluhisha ugomvi
hasa hasa pale wanapokuwa wameitilafiana, watumie busara kutafuta njia
ya kusuluhisha bila kuwaumiza watoto
"Nitahakikisha mtoto wangu
akue katika mazingira mazuri, asome kadri ya uwezo nitakaokuwa nao,
kwani maisha ni kupanda na kushuka kuna wakati unakuwa hauna unasema leo
mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha
ndivyo yalivyo amesema Diamond.
Amesema, “Kiumakini hakukuwa na
vita kati yetu sisi wawili, ila kwa upande wa mwenzangu kulikuwa na watu
wanaingiza chuki ilimradi kutengeneza mazingira ya kumkomoa Diamond
kitu ambacho tumeona hakimsaidii mtoto.
“Tumekubaliana na
tumeyamaliza na tumeweka misingi mizuri ya kumlea mtoto wetu, kwani
mwisho wa siku hata mahakama haiwezi kunambia nimlipe Milioni 5 nitaitoa
wapi, nina kazi mie, Mahakama imenipa kazi au kuna mtu amenipa kazi...?
au eti mtoto umjengee nyumba, ulinipa mie nyumba alisema Diamond.
Alipohojiwa
baada ya kumalizika kwa usuluhishi, wakili wa Hamisa Mobeto,Walter
Goodluck amesema, "leo tulikuja kwa usuluhishi na wamesuluhishwa Ila
sasa wamesuluhishwa nini na nini hilo tutalijua badae", amesema
Novemba
10, mwaka jana na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo upande wa
watoto ya watoto, Devotha Kisoka, aliitupilia mbali kesi aliyofunguliwa
Mobeto juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul kwa kuwa ilifunguliwa kwa
kutumia kifungu ambacho si sahihi.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine akiiomba matunzo ya mtoto.
Pia alikuwa akiiomba mahakama imuamuru Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akifika katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya
mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto. Hamisa Mobeto akiwa kwenye mahakamani kisutu leo
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kutoka ustawi wa jimii kwa ajili ya
kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto
leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa akimunesha mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa Serikali utakaoshirikisha Wizara yake, Wizara ya Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.
Dk. Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na kujifunza juu ya mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.
"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto ambazo zimekuwepo.
"Niwaombe sana wakati Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro huu ni vema tukafuata sheria zilizopo, tuzingatie mipaka iliyowekwa ili tusiingie kwenye migogoro, lakini kwa sasa siwezi kwa namna yeyote ile kutamka neno la kujibu maombi ya mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na wananchi yaliyotolewa hapa leo.
"Kama Serikali tutakaa, Wizara yangu, Wizara ya Ardhi na Tamisemi ili tujue kiini cha mgogoro huu tufanye uamuzi kuwa ni maeneo gani yaongezwe katika hifadhi kwa ajili ya wananchi au ni vitongoji vipi vifutwe, tutaleta majibu, na jambo hili tutalifanya kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea mtu ili kumaliza mgogoro huu," alisisitiza Dk. Kigwangalla.
Awali akimkaribisha Waziri huyo kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ikengwa, Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Ashatu Kijaji alisema kutokana na ukweli kuwa Serikali ya awamu ya tano inasikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi, ni vema Waziri huyo akatumia hekima na kuangalia uwezekano wa kuwapa wananchi hao Kilomita 12 za mraba kutoka kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kibinadamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi alisema mgogoro baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero ulinza mwaka 2006 kufuatia zoezi la kuanzishwa kwake pamoja na lile na uwekagi wa vigingi vya mpaka na vijiji jirani kutoshirikisha wananchi na viongozi wa halmashauri za vijiji hoja ambayo ilipigwa na Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso.
Aidha alisema wananchi wa vijiji hivyo wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kilimo na ufugaji, hivyo akamuomba Waziri huyo pamoja na Serikali kwa ujumla kutumia busara kuwamegea wananchi wa vijiji hivyo eneo la Kilomita 12 za mraba kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.
Naye Meneja wa Pori hilo, Emannuel Bilaso alisema Pori la Akiba Mkungunero lilianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 307 la mwaka 1996 baada ya kupandishwa hadhi kutoka Pori Tengefu. Alisema mchakato wa kupandisha hadhi pori hilo ulishirikisha wananchi na viongozi wa vijiji na wilaya ambapo mihutasari mbalimbali ilisainiwa.
Alisema pori hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazochochea mgororo huo ikiwemo kijiji kimoja cha Kisondoko kusajiliwa kimakosa ndani ya hifadhi hiyo pamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchi kuwa hawakushirikishwa kwenye uanzishwaji wa pori pamoja na madai mengine kuwa pori hilo limeingilia mipaka ya vijiji hivyo.
Pori la Akiba Mkungunero ambalo lina ukubwa wa Kilimita za Mraba 557.9 lina umuhimu mkubwa kiuchumi na kiikolojia kwa kuwa ni chanzo muhimu cha mto Tarangire ambao ni uhai wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ikolojia nzima ya ziwa Manyara. Pori hilo pia ni sehemu ya mapito na mazalia ya wanyamapori pamoja na makazi ya wanyamapori adimu duniani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kondoa muda mfupi baada ya kuwasili wilayana humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteja jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi wakati wa ziara yake ya kikazi jana katika Pori la Akiba Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea mabango ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisondoko kuhusu Pori la Akiba Mkungunero na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko wilayani Kondoa jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na mmoja wa wahifadhi wa Pori hilo wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.