RAIS DKT. SAMIA AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA (CGP) JEREMIAH YORAM KATUNGU

July 31, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Kamishna wa Magereza CP. Jeremiah Yoram Katungu cheo Kipya cha Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 31 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WASISITIZWA KUZINGATIA BAADHI YA VIPAUMBELE KATIKA KUTEKELEZAJI MAJUKUMU YA KILA SIKU

July 31, 2024

 



Na Mwandishi Wetu,Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuzingatia vipaombele ambavyo ni muhimu kupewa msukumo katika utekelezaji wa shughuli kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Ameyasema hayo mapema leo tarehe 31 Julai, 2024 Jijini Arusha alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mazingativu (Retreat) kilichohusisha watendaji na watumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na Taasisi zake.

Akiongelea kipaombele cha kwanza ambacho ni Kuratibu Ujenzi wa Majengo ya Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, Waziri Mhagama alisema, Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2024/25 itaendelea na uratibu wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara, Taasisi pamoja na miundombinu mbalimbali katika Mji wa Serikali wa Mtumba, pamoja na kutoa vibali vya ujenzi kwa Taasisi za Serikali zinazoendelea kuhamia Makao Makuu ya Chama na Serikali Dodoma, ikiwa na nia kuhakikisha kuwa Awamu ya Tatu ya ujenzi wa Mji wa Serikali inakamilika kwa wakati na watumishi wanahamia katika majengo hayo ndani ya mwaka wa fedha 2024/25 na kuelekeza kuwa  Uratibu huo uimarishwe sambamba na kuweka ufuatiliaji wa karibu wa ujenzi pamoja na ununuzi wa samani za majengo yote.

Akiongelea suala la Kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali, Waziri Mhagama Alibainisha kuwa, Kulingana na muundo mpya wa Ofisi ya Waziri Mkuu ipo Idara mpya iliyoundwa ambayo jukumu lake kubwa ni kusimamia masuala yote ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Utendaji wa Serikali kwa ujumla kuanzia ngazi za Wizara na taasisi zake, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Aidha Waziri Mhagama Aliipongeza Idara hiyo kwa kazi kubwa inayoendelea kuifanya na kusema kuwa hadi saa imeandaa Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini nchini na imekamilisha Mwongozo wa Menejimenti ya Tathmini nchini na Mwongozo wa kufanya tathmini ya utayari wa masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Taasisi za Serikali. 


“Baada ya kazi hiyo nzuri sasa tunahitaji kuona matokeo ya utendaji unaotokana na kuimarishwa kwa ufuatiliaji na tathmini, Masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kutiliwa mkazo ni ufuatiliaji wa maoni na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo hutoa mwelekeo wa utendaji wa Serikali.” Alisisitiza Waziri Mhagama.

Aliendelea kusema kuwa, Hatua hii itajenga imani zaidi kwa wadau kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti matumizi mabaya ya mali za umma na kuelekeza kazi ya kukamilisha Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali (Government Wide Integrated Monitoring and Evaluation System) ikamilike mapema kabla ya mwezi Disemba, 2024 na ili mfumo huo uanze kufanya kazi na kuwezesha upimaji wa utendaji wa Serikali kufanyika kwa urahisi, haraka na ufanisi mkubwa.

Akiongelea kuhusu Kuimarisha Uwezo wa Uchapishaji wa Nyaraka za Serikali, Waziri Mhagama alipongeza jithada za maboresho yanayoendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya, ununuzi wa mashine mpya saba na matengenezo ya mashine zaidi ya 13.

“Nawapongeza wataalam waliobuni na kuandaa maandiko yaliyowezesha kupata mafanikio haya kwa muda mfupi, Naendelea kutoa wito kuwa shughuli za uchapaji wa nyaraka zote za Serikali ufanywe na Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali na ufuatiliaji ufanyike kwa Taasisi ambazo zinakiuka masharti ya Waraka uliotolewa kwa Watendaji wote.” Alisisitiza Waziri Mhagama.

Akizungumza kuhusiana na Vita dhidi ya biashara haramu na Matumizi ya Dawa ya kulevya, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kupongeza hatua mbalimbali za udhibiti wa dawa za kulevya nchini akitolea mfano wa mafanikio yaliyopatikana na kusema kuwa ni kiashiria kikubwa cha utendaji mzuri wa Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini.

 

“Dhahiri kwamba nchi yetu imejipatia heshima ndani na nje ya nchi kwa kuwa na mifumo imara ya udhibiti wa dawa za kulevya na tumeweza kuwalinda watu wetu dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.” Alisema

Aidha, Waziri Mhagama alibainisha kuwa, ni azma ya Serikali ya Awamu ya Sita (6) chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa biashara ya dawa ya kulevya inakomeshwa, kwani ina madhara makubwa sana kwa jamii ya Watanzania na inaathiri nguvu kazi ya Taifa na kutoa wito wa kuendeleza jitihada za  kuendeleza mapambano, sambamba na kuweka msukumo wa utekelezaji wa Sera mpya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2024.

 

Akiongelea suala la Usimamizi na uratibu wa masuala ya Uchaguzi, Waziri Mhagama alisema, Mwaka huu wa 2024 na mwaka 2025 kutafanyika chaguzi mbalimbali, Mwaka 2024 kutafanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Mwaka 2025 utafanyika Uchaguzi Mkuu.

 “Chaguzi hizi zinahitaji maandalizi ya kutosha na uratibu mzuri, hivyo nitoe wito kwa Taasisi inayohusika na maandalizi ya Uchaguzi pamoja na Idara ya Bunge na Siasa kufanya maandalizi na uratibu kwa ukamilifu ili kufanikisha chaguzi hizi.”

Akihitimisha hotuba yake alitumianfursa hiyo kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na maafa ya Mafuriko mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwezi Aprili, 2024, na Mvua za El Nino, na kusema kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na maafa hayo.

“Nitumie fursa hii kupongeza jitihada zilizochukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika kukabiliana na maafa hayo, Tuendelee kufanya kazi kama Timu ili kupata matokeo makubwa zaidi katika kukabiliana na majanga huku jitihada kubwa zikielekezwa katika utoaji wa elimu kwa umma.”

RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI KUMBUKIZI YA 3 YA URITHI WA MKAPA JIJINI DAR ES SALAAM

July 31, 2024

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa wakati walipotembelea mabanda ya Maonesho ya wadau wa Taasisi hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa Tuzo ya Mkapa kuhusu Uongozi thabiti kwa Washindi mbalimbali kutoka Sekta ya Afya Nchini.. Mhe. Rais Samia alitoa Tuzo hizo wakati wa kilele cha Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

TAKUKURU TANGA YAANZA UCHUNGUZI WA MIRADI ILIYOBAINIKA NA MAPUNGUFU

July 31, 2024

 

 Akizungumza kwa  niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024 

 Akizungumza kwa  niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024
 Akizungumza kwa  niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024



Na Oscar Assenga, LUSHOTO.


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Tanga imeanzisha uchunguzi wa miradi minne iliyobainika kuwa na mapungufu kadhaa yaliyopelekea kuanzishwa kwake mchakato huo

Akizungumza leo na waandishi wa Habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda ambapo alisema kwamba waliendelea na ufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo 79 yenye thamani ya Milioni 34,517,081,773.60.

Mapunda ambaye pia ni Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Takukuru Mkoa wa Tanga alisema miradi ambayo ilifuatiliwa ni katika sekta za kipaumbele ambazo ni Elimu, Barabara, Maji na Afya pamoja na ile ambayo ilitembelewa na kuzinduliwa au kuwekwa mawe ya msingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024.

Aliitaja miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya Msingi Kisinga wenye thamani ya Sh.Milioni 50 katika Halmashauri ya Lushoto, Ujenzi wa Zahanati ya Milingano wenye thamani ya Milioni 553,

Mapunda alitaja mradi mwengine ni upanuzi wa kituo cha Aya Mgwashi wenye thamani ya Milioni 500,000,000.00 na mradi wa zahanati ya Maalie wenye thamani ya Sh.Milioni 50,000,000.00.

Wakati huo huo, Mapunda alisema kwamba katika kipindi hicho walifanya kazi ya uelimishaji kwa wajumbe wa kamati za Afya ya Msingi katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali pamoja na Watumishi na Wataalamu wa Sekta ya Afya ambao ni 485 kwa idadi yao katika wilaya za Kilindi,Handeni,Korogwe na Lushoto.

“Katika uelimishaji huo tuliweka kipaumbele ushirikishwaji wadau katika uzuiaji rushwa kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote katika wilaya hizo ambapo wakuu wa wilaya zote walishiriki kufungua mafunzo na kuhimiza uadilifu,uwajibikaji na huduma bora za Afya ya Msingi katika wilaya zao”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kufanya udhibiti na uzuiaji wa rushwa kwenye eneo la ukusanyaji mapato kwa kushirikiana na mamlaka husika kufanya ufuatiliaji wa moja kwa moja kwenye vyanzo vya mapato vilivyoanishwa katika bajeti kwa kuangalia mienendo ya makusanyo ya mapato sambamba na kushauri hatua mbalimbali za kudhibiti upotevu wa mapato wakati wa mchakato wa ukusanyaji.

TCB BENKI YATOA VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 50 SUMBAWANGA

July 31, 2024


*Sumbawanga, 30 Julai 2024* — TCB Benki inajivunia kutangaza mchango mkubwa wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni 50 za Kitanzania (TZS) kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu na afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mchango huu wa hali ya juu unalenga kuboresha miundombinu muhimu kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa elimu bora na huduma za afya katika eneo hilo.