SERIKALI KUENDELEZA MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

January 14, 2017
 
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akimkabidhi zawadi Mkaguzi wa Polisi, David Mabula.
 Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki kutokana na ufanyakazi bora.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
 Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
 Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
 Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau 
kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari  wakiwa kwenye hafla hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kupambana wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

Mwigulu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Serikali imejipanga  kupambana na dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la kitaifa ambapo vijana wengi wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.

Mwigulu alisema serikali ya awamu ya tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye kwamisha jitihada za kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga kuupunguza kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2019.

Aliongeza kuwa kanuni na sheria zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani ya jeshi la polisi zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi. 

Akitolea mifano kadhaa alisema askari polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi hilo anapaswa kupewa fedha za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na suala hilo si la kumuonea huruma askari husika bali ni haki yake.

Alisema kwa upande wa askari polisi aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa mapambano dhidi yake na wahalifu askari huyo anapaswa kulipa fidia yake kwa wakati badala ya kuunda tume ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa katika mapambvano hayo.

"Mambo mengine hayahitaji mpaka uwe na elimu kubwa askari amepambana na majambazi mbele ya watu lakini majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake anashindwa kulipwa eti mpaka iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji Mwigulu.

Alisema kwa muda mrefu askari anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia kwa nauli na fedha za kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila ya sababu za msingi.

Alisema hali hiyo kama askari husika anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza katika tamaa na kutumia silaha aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba wahusika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwani mshahara na posho kwa askari hao ni haki yao.

Mwigulu alisema serikali kupitia Rais Dk. John Magufuli imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa askari polisi ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba na kuona namna ya kubadilisha sheria ambazo zinaonekana hazina tija kwa wakati huu katika kuliongoza jeshi hilo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA PAMOJA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGAZO NA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

January 14, 2017
AQT
 
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan (katikati)akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye
ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
iWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani
 Baadhi wa Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DC MUHEZA ASHIRIKI JOGGING,AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO.

January 14, 2017

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akishiriki kwenye mazoezi ya Jogging leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza,Desderia Haule

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye mazoezi hayo kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kujenga afya.


 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki mazoezi ya kuruka ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza



 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye kukumbia ikiwa ni kufanya Jogging inayofanyika kila mwezi wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza, Desderia Haule wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu katika Jogging ambayo hufanyika kila Jumamosi ya kwanza ya  mwezi kwa ajili ya kuimarisha miili na kuwaweka fiti wa kwanza kulia ni Mwandishi wa Azam TV mkoani Tanga,Mariam Shedafa akishiriki mazoezi hayo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew mara baada ya kumalizika mazoezi hayo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Jogging hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatenga maeneo  ya viwanja vya michezo ili kuwezesha vijana kushiriki kwenye michezo jambo ambalo linaweza kuwasaidia kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha.

Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya mazoezi kila Juma mosi ya pili ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili ya watumishi na vijana ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanaweza kuwanyemelea.

Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo kunapunguza fursa kwa wananchi na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hata kuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu ya kujipatia ajira.

“Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa vijana wengi ambao asilimia kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wa maisha”Aliseam Hajat Tumbo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa kufanya mazoezi hasa kwa watumishi wa Serikali.
 
Alisema ili kuweza kukabiliana na magonjwa hayo yasiyoambukizwa kama ugonjwa wa Moyo,sukari na shindikizo la damu lazima kauli ya makamu wa Rais ya kuhamasisha kufanyike mazoezi nchi nzima itekelezwe kwa vitendo na si maneno.

“Laima tubadilike kwa kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa hayo ambayo yamekuwa pigo kwa wananchi na hasa watumishi wa Umma,inatulazimu tupambane kukabiliana na hali hiyo kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zetu”Alisema Dk Mathew.

Naye Katibu Tawala Wilaya hiyo Desderia Haule ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilya alisema zoezi hili litakuwa ni endelevu na Serikali itatenga maeneo ya kutosha ya viwanja kwa ajili mazoezi na kukuza vipaji vya vijana .

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AHUDHURIA MCHEZO WA KUMUENZI MCHEZAJI WA MBAO FC ALIYEFARIKI UWANJANI

January 14, 2017
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, jana akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Mhe.Nape Nnauye, kwenye mchezo wa hisani kati ya timu za UMISETA wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Na Binagi Media Group
Mhe.Wambura, alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA na kwamba imejipanga vyema ili kuiendeleza michezo hiyo mwaka huu 2017 kwa kuondoa dosari zote zilizojitokeza hapo awali na kusababisha kuahirishwa mwaka jana.

Lengo la mchezo huo ilikuwa ni kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 20 ya Mbao Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Isamail Khalifan Mrisho ambaye Disemba 04 mwaka jana, alifariki dunia akiwa uwanjani kwenye mchezo baina ya na timu yake na Kagera Sugar huku kiingilio kilichopatikana kwenye mchezo huo kikiwasilishwa kwa familia ya mchezaji huyo.

Mchezo huo uliandaliwa na taasisi ya soka nchini iliyomlea mchezaji huyo ya The Football House kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mama Angelina Mabula iitwayo Angeline Foundation.

Hadi dakika 90 zinatamatika, timu ya kombaini ya Nyamagana iliibuka mshindi kwa ushindi wa mabo2-1. Mabao ya Nyamagana yalifungwa na Rajesh Kotecha na Kuzaifa Mdabiru huku Ilemela wakipata bao la kufutia machozi baada ya mchezaji wa Nyamagana Jefta John kujifunga.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masele, alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inaendeleza mchezo wa soka ambapo imeanzisha timu kwa kila soko la machinga wilayani humo hatua ambayo itasaidia kuukuza mchezo huo.
Mkurugenzi wa taasisi ya The Football House, Mbaki Mutahaba, alisema taasisi hiyo itaendelea kumuenzi mchezaji wake Ismail Khalifan Mrisho huku akiwasisitiza vijana kutumia vyema vipaji walivyonavyo kama ilivyokuwa kwa Mrisho ambaye ameacha alama ya soka nyuma yake baada ya umauti kumkuta.
Kaka wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, aitwaye Athman Kitwana, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya familia kwa namna ambavyo wadau mbalimbali walivyojitoa kumwendeleza kipaji chake, kusaidia kwenye msiba wake na namna wanavyoendelea kumuenzi baada ya umauti.
Wazazi wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, kushoto ni  Rehema Mfaume (mama) na kulia ni Khalifan Mrisho (baba). 

HALMASHAURI YAIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA SHULE YA MSINGI HAZINA MISION KWA KUTOKUWA NA VIWANGO VYA UANDIKISHAJI

January 14, 2017


Na Woinde Shizza,Arusha

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya
msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa mara baada ya uongozi wa shule
hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza  watumishi
wake pamoja na  mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika uandikishaji wa shule.

Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja mara baada  siku chache zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi na walimu  wa shule hiyo na hivyo kutakiwa
kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya maagizo hayo kwa muda waliopewa.

Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo kaimu afisa elimu  shule za msingi katika jiji la arusha Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya
marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.

Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao, kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja
na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.

"Kwa kuwa uongozi  wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mlioagizwa ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu
katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice

Wananchi wa eneo hilo akiwemo  Diwani wa kata ya baraa Elifasi Ndetika akizungumzia  uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo  alisema kuwa ni halali kabisa kwani walikuwa na malundano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu
lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea marekebisho yakawepo.

SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM

January 14, 2017
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akitoka kukagua chumba namba cha kuhifadhia mizigo kilichoungua moto jana usiku.