TANZANIA NA KUWAIT ZASAINI MAKUBALIANO YA SAFARI ZA ANGA

TANZANIA NA KUWAIT ZASAINI MAKUBALIANO YA SAFARI ZA ANGA

March 29, 2016

1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan.

2Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
3Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan mara baada ya kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait leo jijini Dar es salaam.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait (Kushoto katikati).Wengine katika picha hiyo ni Maafisa kutoka Tanzania na Kuwait. 
Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO.

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA HATI YA KIWANJA KWA BOHARI YA DAWA (MSD)

March 29, 2016
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari tano Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa MSD kupitia Wizara hiyo Dar es Salaam leo mchana.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akisalimiana Naibu Katibu Mkuu wa  Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Moses Kusiluka wakati wa hafla hiyo ya kukadhiana hati hiyo ya kiwanja. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, William Lukuvi.
 Salamu zikiendelea. Hapa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango Miji, Profesa John Modestus.


 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (mbele kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Waziri Lukuvi na Mkurugenzi wa MSD, wakiangalia hati hiyo.



Viongozi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo, Amina Ramadhani, Ofisa Ardhi Mkuu, Mwamasage na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya.

Na Dotto Mwaibale

RAIS Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5 kwa Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Luguluni nje kidogo ya jiji la  Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa ili kuondoa upotevu wa fedha kwa maghala ya kukodi.

Ujenzi wa maghala katika kiwanja hicho utaokoa kiasi cha sh. bilioni 4 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya malipo ya maghala ya kukodi yaliyopo Mabibo Ubungo jijini pamoja na kanda mbalimbali  nchini.

Akizungumza wakati wa akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu Dar es Salaam leo mchana,  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema, Rais ametoa ardhi hiyo ili kuepusha gharama zisizo na sababu kwa MSD.

Alisema agizo la rais fedha zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kukodi maghala hayo, zinapaswa kununua dawa ili kila Mtanzania apate huduma bora za kiafya.

“Rais aliniagiza niwape eneo, leo nimetekeleza agizo hilo kilichopo muanze ujenzi kama mlivyoomba kwa ajili ya kujenga ghala la dawa, naamini mtaanza mara moja balada ya kuendelea kukodi maghala na  badala yake fedha zote zitumike kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba,” alisema Lukuvi na kuongeza;

“Kiwanja hiki ambacho kilikuwa cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kilichokuwa na ukubwa wa ekari 200, tumewapa ekari tano kama uhitaji wenu ulivyokuwa, nimewasamehe kodi ya premium na badala yake kiasi cha Sh16.7 hamtalipa na gharama mtakayotakiwa kulipa ni sh. milioni 2 pekee ili muanze ujenzi mara moja.”

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa  (MSD) Laurean Bwanakunu alisema tayari wameshazungumza na Bodi ya wadhamini, Wizara ya Afya na wahisani hivyo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja Julai Mosi.

“Tunamshukuru sana Rais kwa sababu ombi hili limefanyiwa kazi kwa haraka sisi kama MSD tulishindwa kuhimili mikiki kutokana na gharama kubwa iliyokuwa ikielekezwa katika malipo ya ghala la kukodi pale ubungo mwaka wa fedha ulioisha tulilipa kiasi cha Sh3.5 bilioni na tukitarajia mwaka huu mpya wa fedha inafikia Sh4 bilioni kwa sababu ya malipo kwa dola,” alisema Bwanakunu.

Alisema katika eneo hilo jipya lililopo Luguluni wanatarajia kujenga zaidi ya maghala matano yenye ukubwa wa sikwea mita mita 5000 yatakayogharimu kiasi cha sh. bilioni 10nkila mojawapo, “ujenzi huu utakapokamilika kanda zitakazonufaika ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuwa eneo hilo walilopata wanaweza kujenga kiwanda cha maji.


Waziri Mbarawa azitaka taasisi na idara kutumia kituo cha kuifadhi taarifa cha Taifa.

March 29, 2016

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao. 
Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa usalama mkubwa wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumza na wadau hao juu ya matumizi ya kituo hicho kuhifadhia taarifa. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya matumizi ya 'National Information Data Centre' 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura pamoja na Ofisa Mkuu Idara ya Ufundi TTCL, Senzige Kisonge wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Mkuu wa Idara ya Compyuta NSSF, Yahaya Madenge (kulia) akiuliza swali kupata ufafanuzi juu ya usalama wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi akiuliza kupata ufafanuzi juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi na kumlinda mteja wake. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye tai ya mistari miekundu) akizunguka na baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali vitengo vya IT kuwaonesha miundombinu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ilivyojengwa kisasa kumlinda mteja wake na taarifa zinazohifadhiwa katika kituo hicho. 
 Baadhi ya mashine kubwa za kisasa za kufua umeme katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mitungi ya gesi ya kuzimia moto endapo ukitokea inayofanya kazi kwa kujiongoza yenyewe mara tukio la moto linapojitokeza katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi moja ya vyumba maalumu vya usalama katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi (kulia) moja ya mitambo ya kisasa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 

Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mashine zinazofanya kazi ya kupooza mitambo katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kilichopo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao.

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI

March 29, 2016
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.
 Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mwanahabari kutoka TBC, Angela Msangi (kulia), akiuliza suala katika mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, imeitaka Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini.

Pia imeitaka Serikali kudhibiti bandari bubu na njia za panya ambazo huingiza sukari kinyume cha sheria na kuua viwanda vilivyopo na kuifanya Tanzania kununua sukari kutoka nje ya nchi na kuua uchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk.Mary Nagu alisema kwa sasa upatikanaji wa sukari ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ambapo kunamapungufu wa tani 80,000 hadi 100,000.

Alisema mapungufu hayo yanatokana na viwanda vinavyozalisha sukari nchini kuzalisha tani 302,0000 huku mahitaji ya sukari kwa nchi nzima ni tani 402,0000.

Alisema kwa sasa kuna viwanda vitano tu ambavyo huzalisha sukari ambayo haitoshi kwa matumizi ya wananchi nchini hapa na kusababisha mapungufu hayo.

Hata hivyo alisema pamoja na viwanda hivyo kuzalisha chini ya kiwango kinacho hitajika katika kipindi hiki cha mwezi Machi hadi Juni viwanda hivyo hufungwa kwaajili ya kupisha ukarabati hivyo kwa kipindi hicho sukari inayotumika ni ile ambayo ilizalishwa katika kipindi kilicho pita.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vema Serikali ikahakikisha inaagiza sukari hiyo mapema ili kuweza kuziba pengo la mapungufu ya sukari katika kipindi muafaka ili isiweze kugongana na sukari iliyopo na kusababisha kuua uzalishaji nchini.

"Hivyo kutokana na mapungufu hayo ili kufidia mapungufu hayo kati ya utumiaji na uzalishaji sukari inaagizwa kutoka nje, hivyo ikiagizwa tani 80,000 hadi 100,000 kuna kuwa hakuna mapungufu.

"Baada ya kupata taarifa ya mapungufu hayo kutoka katika bodi ya sukari tukaona humuhimu wa kumuomba Rais, kutoruhusu mapungufu ya sukari yatokee katika kipindi hichi ambacho viwanda vya sukari vinafungwa na kusimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Machi hadi Juni kwa kuagiza mapema," alisema.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na mapungufu hayo lakini pia kumekuwa na wafanyabiashara wabinafsi wamekuwa wakitumia vibaya mapungufu hayo kwa kuingiza sukari zaidi ya kiwango kinacho hitajika bila kujali uchumi wa nchi unavyodidimia.

"Katika wafanyabiashara hao wapo ambao wanaingiza sukari kwaajili ya kupeleka katika nchi nyingine lakini sukari hiyo inabaki humuhumu bila kuuza na baadae kuuza kwa bei kubwa hivyo kuua uchumi wa nchi," alisema.

Alisema ni vema Serikali kuhakikisha hairuhusu mapungufu ya sukari kwani mapungufu hayo kwa kuingiza sukari hiyo kwa wakati kwani usheleweshwaji unaweza kusababisha kuuzwa kwa bei ya juu na hivyo kuua uchumi, pamoja na kuifanya nchi ya kununua sukari kutoka nje.

Aidha Kamati hiyo iliitaka Serikali kufunga bandari bubu na kudhibiti njia za panya za uingizaji wa sukari, kutobakiza sukari zinazotakiwa kuuzwa nje ya nchi kubaki nchini na kuwekwa mahali ambapo hapajulikani na baadae kuuzwa kwa bei ya juu kunapokuwa na mapungufu ya sukari.

"Sisi kama kamati tunaendelea kumshukuru rais na tutaendelea kuisaidia Serikali kusisitiza uzalishaji wa sukari ya kutosha na ziada ya kupata sukari kutoka nje uwezekano upo.

"Hivyo tumeapa katika kumsaidia rais katika kuhakikisha sukari inazalishwa ya kutosha na inakuwa na tija, viwanda vinafanya kazi, na nahakika siku moja Tanzania itakuwa nchi ya kuuza sukari nje na badala ya kununua," alisema.

Pamoja na hilo lakini pia ni vema ikahakikisha Tanzania isiwe eneo la kuuza sukari za nchi nyingine na kuua uchumi uliopo na kukuza wa nchi hizo.

Alisema pia Serikali inawajibu wa kufuatilia utaratibu za uingizaji wa sukari kwani kamati hiyo imegundua tatizo hilo lisipotatuliwa bei ya sukari haiwezi kudhibitiwa kutokana na hali ya kisoko.

Alisisitiza kuwa pia ni vema wazalishaji kutumia muda mwingi wa kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji na kununua miwa kutoka kwa wakulima.

Hivyo alisema kama kamati imeona umuhimu wa kuwawezesha wakulima kulima ili viwanda vinapopanua uzalishaji kupata malighafi za kutosha.

ASKOFU CHARLES GADI NA WACHUNGAJI WENZAKE WALIOMBEA TAIFA LIPATE MVUA

March 29, 2016
 Askofu  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni Mchungaji Palemo Masawe.
 Mchungaji Martini Ndaki (kushoto), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza kuu kabla ya maombi. 
Askofu Charles Gadi (wa tatu kutoka kushoto), akiongoza maombi ya kuliombea taifa lipate mvua. Kutoka kushoto ni Mchungaji Denis Komba, Mchungaji Martin Ndaki, Mchungaji Palemo Masawe, Mchungaji Denis Kumbilo, Mchungaji James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, ameliombea taifa lipate mvua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Askofu Gadi alisema,  mabadiliko hayo ya kijiografia yamesababisha kukosekana kwa mvua za kutosha katika mwanzo wa masika wa mwezi wa tatu na kukithiri kwa joto kutokana na dunia kuwa karibu na jua(Equinox).

Alisema mvua za masika ni muhimu sana kwa kilimo, ufugaji, malisho ya wanyama mwitu wa nchini, mazao ya kudumu kama vile kahawa, migomba, michai  na mito yote hayo yanategemea mvua za masika.

“Tukumbuke kuwa kuna kipindi kirefu hupita tangu mvua za masika hadi kukutana na za vuli  ambapo ni karibu ya miezi mitano au sita  pasipo na mvua, hivyo kama kukiwa na uhaba wa mvua za masika maana kipindi cha ukame kitaongezeka kwa miezi saba hadi  miezi minane jambo ambalo ni hatari sana kwa kilimo na wanayama wetu.

“Joto la Equinox limekuwa kali  kuliko wakati mwingine wowote ingawa lilitarajiwa kuchemsha maji ya bahari ili mvua ziwe nyingi lakini hali imekuwa kinyume, hivyo tunawaaasa watanzania wote  bila kujali dini na itikadi ya mtu kuungana kwa pamoja  kumuomba mungu ili ukame huu usiikumbe nchi yetu,” alisema Askofu Gadi.

Alisema ni lazima kuomba ili ipatikane mvua   za kutosha nan chi iweze kujitegemea kwa chakula  ili fedha ambazo zingetumika kuagiza chakula nje ya nchi ziweze kutumika kwenye kuleta maendeleo ya kitaifa.

Aidha Askofu Gadi aliishukuru Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)kwa kuendelea kutoa  taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kijiografia yanayosababisha kuongezeka kwa joto kwa kikwango kikubwa.

Askofu Gadi alifanya maombi hayo kwa kushirikiana na wachungaji wenzake  ambao ni Mchungaji Denis Komba, Martin Ndaki, Palemo Masawe,  Denis Kumbilo, James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 29, 2016
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Mary Lingo (wa pili kulia), akiwaelekeza wajumbe wa kamati hiyo jinsi dawa zinavyotunzwa katika maghala.
 Mkurugenzi wa MSD, Laurean Banakunu (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea MSD leo.
Mjumbe wa kamati hiyo, Azani Zungu akiuliza swali juu ya kuharibika kwa dawa.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko na kuipongeza kwa utendaji wake kazi pamoja na mazingira magumu yanayoikabili.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba amesema Kamati yake itasimamiana kuyafanyia kazi masuala makubwa manne ambayo ni pamoja na bajeti finyu ya dawa, ulipwaji wa deni la serikali, mfumo wa uwajibikaji kati ya Tamisemi na Wizara ya Afya ambao unasababisha utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Afya kutokuwa na mtiririko kutoka juu kwenda chini. 

Jambo la nne ni kuhakikisha utekelezaji wa kuongeza uzalishaji dawa ndani ya nchi kupitia sekta binafsi (PPP).

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangala alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Bohari ya Dawa inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kwa bei nafuu, hivyo Serikali imeweka kipaumbele kuhakikisha deni la MSD linalipwa mapema iwezekanavyo.

Alisema tayari Wizara ya Afya imeiagiza MSD kuandaa bei elekezi kwa maduka maalum ya dawa (prime vendor) ili vituo vinavyokosa dawa MSD vinunue huko bila usumbufu na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameviomba vituo vya Afya kuleta mahitaji yao kwa wakati.

WASHINDI MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 WAKABIDHIWA ZAWADI.

March 29, 2016
Mfanyabiashara Davis Mosha akiwa na mshindi wa kwanza katika mashindano ya Mbio za magari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi,Gurjit Dhan (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Shameer Yusuf (kulia).
Mshindi wa pili katika mbio za magari ,Piero Canobbio (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Silvia Frigo.
Mshindi wa tatu katika mashindano hayo Gurpa Sandhu (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Davie Sihoka.
Mshiriki wa Mbiio za magari kutoka Morogoro Bob Taylor akipokea kikombe baada ya kumaliza akiwa katika top ten.
Zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa washiriki wa mashindano hayo ya Vaisakh Rally ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro.
Mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa mbio hizo.
Zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa washindi pamoja na waandaaji.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya mbio za magari ,Gurjit Dhan (Kulia) akizungumza jambo na mshindi wa pili wa mbio hizo Piero Canobbio kutoka nchini Kenya.
Baadhi ya magari yaliyoshiriki mbio hizo.
Mashabiki wakiwa katika eneo mojawapo wakifuatilia mbio hizo.
Moja ya gari la mashindano kikivutwa mata baada ya kupata hitilafu.
Baadhi ya magari yakiwa katika mbio hizo.
Magari mengine yalilazimika kutembea bila ya gurudumu baada ya kupata hitilafu.
Imendaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini,.
(0755659929)