NAIBU WAZIRI MPINA ATEMBELEA BAADHI YA TAASISI ZA MUUNGANO ZANZIBAR

August 14, 2017


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitia sahihi katika kitabu cha wageni katika Ofisi za Makao Makuu ya jeshi la Police kisiwani Zanzibar, Mpina yupo kisiwani humo katika ziara ya kutembelea baaadhi ya maeno ya Muungano, kulia ni kaimu kamishna wa jeshi la Police Zanzibar kamanda Juma Yusuph Ali.


Naibu Waziri Mpina akiongea na viongozi wa Jeshi la Police kisiwani Zanzibar (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo, kulia ni kaimu kamishana wa Jeshi hilo Zanzibar kamanda Juma Yusuph Ali.


Katika picha baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Police katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo kisiwani Zanzibar wakimsikiliza  Naibu Waziri Mpina, ambaye hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao.


Katika picha, Naibu Waziri Mpina akishikilia moja ya Jalada la miaka ya nyuma la maombi ya hati ya kusafiria huku akiuliza swali katika maktaba ya  Jeshi la Uhamiaji katika Ofisi ya Makao makuu ya jeshi hilo kisiwani Zanzibar


Naibu Waziri Mpina katika Picha ya Pamoja na viongozi wa Jeshi la Uhamiaji kisiwani Zanzibar na maafisa wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, baada ya kumaliza ziara yake katika Ofisi hizo .


Kulia Naibu Waziri Mpina akijibu swali la mwakilishi wa ITV na Radio one Zanzibar Farour Kareem (kushoto) kwa niaba ya waandishi wa habari  hawapo pichani, katikati ni Kamishna wa Jeshi la Uhamiaji Zanzibar Bw. Johari Masoud Sururu.
NA EVELYN MKOKOI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara katika baadhi ya taasisi za Muungano kisiwani Zanzibar.
Katika ziara yake alipotembelea ofisi za jeshi la Uhamiaji kisiwani humo Mpina alisema kuwa, Taasisi za Uhamiaji na jeshi la Police ni muhimu sana katika ustawi wa muungano wa Tanzania Bara na Visiwani kwani Muungano huu unategemea sana amani, na hauwezi kuwepo muungano kama kuna vurugu na uvamizi wa wahamiaji haramu.
Alisisitiza kuwa ni lazima taasisi hizo kutembelewa na kuziona mara kwa mara namna zinavyofanya kazi na kuona changamoo zao ili serikali iweze kuzifanyia kazi na kuwawezesha waweze kufanikisha majukumu yao vizuri na katika usimamizi wa sheria kwa ujumla wake.
“ Nataka niseme dhahiri kuwa taasisi hizi zinautendea haki Muungano kutokana na wao wenyewe wanavyotimiza majukukumu yao pamoja na changamoto zinazowakabili na kuiweka nchi katika utulivu na usalama.” Alisisitiza Mpina.
Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa “ nimeona jinsi ambavyo wanasimamia na kutekeleza majukumu yao nimeona namna ambavyo wanatoa vibali vya kusafiria, nimeelezwa kwamba kwa siku moja wastani wa maombi ya vibali vya kusafiria ni kati ya maombi 80 mpaka 120 lakini wao wana uwezo wa kutoa vibali zaidi ya 150 kwa siku hiyo ni zaidi ya maombi yanayotolewa na wanatoa vibali hapa hapa zanzibar haya nimafanikio makubwa katika Muungano wetu”. Alisema
Kwa upande wake kaimu kamishna wa jeshi la Police Zanzibar kamanda Juma Yusuph Ali, alisema ili kukabiliana na changamoto za kiusalama kisiwani humo kunahitajika juhudi na ushirikino wa pamoja kati ya wananchi jamii na wadau . Alitoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi la Police ili kuweza kuzitatua Chngamoto hizo.
Katika ziara yake kisiwani Zanzibar Naibu Waziri Mpina alitembelea Ofisi za uhamiaji, Jeshi la Police na Ofisi za wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Africa mashariki.