Rais Kagame awasili nchini,apokewa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli

Rais Kagame awasili nchini,apokewa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli

July 01, 2016
KAGA1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
KAGA2 
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
KAGA3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
KAGA4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.
KAGA5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.
KAGA6 
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
KAGA7 
Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JINIA.
KAGA8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.
KAGA9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza  ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
KAGA10 
Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.
KAGA11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame. PICHA NA IKULU
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yajionea urushaji vipindi vya Bunge

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yajionea urushaji vipindi vya Bunge

July 01, 2016


C1 
Mhandisi wa mitambo wa Studio za Bunge Bi. Upendo Mbele akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake  juu ya namna wanavyotekeleza majukumu ya kurusha vipindi kwa kuzingatia sheria na Kanuni za Bunge wakati wa Ziara iliyolenga kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
C2Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kushoto) akifuatilia Kikao cha Bunge mapema Jana wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja .
C4 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof. Amon Chaligha akiwa ndani ya Maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
C5Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Bunge Bw. Didas Wambura (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) na Ujumbe wake wakati wa ziara ya Tume hiyo  Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Frank Mvungi-Dodoma)

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA RWANDA MH.PAUL KAGAME NCHINI

July 01, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kufanya Mazungumzo.Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba ,jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride la heshima uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais Paul Kagame akiwapungi mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli .

Dkt. Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda

July 01, 2016


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, pamoja na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili. 
Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo, akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.
Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.
Wakati mazungumzo yakiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.

TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA USALAMA WA MTANDAO WA TEKNOLOJIA.

July 01, 2016


 Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha  na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akijibu maswali mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akiwasikiliza waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine.
 Washiriki waliohudhuria mkutano huo.
Mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle umefanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya teknolojia walikutana na kujadili matumizi salama ya mtandao. Mambo makuu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba, ni usalama katika matumizi ya mitandao ya teknojia, Usimamizi wa utunzaji wa data na taarifa za siri na jinsi ya kukabiliana na hasara zinazotokana na matumizi mabaya ya mtandao yenye kuleta athari kwa watumiaji. Imeeleza katika mkutano huo kuwa kila mwaka mabilioni ya dola hutumiwa na taasisi mbalimbali kujiweka salama na athari za kimtandao ambapo hata hivyo imeelezwa kuwa wezi wanaojinufaisha kupitia teknolojia kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kufanya uharifu kupitia katika mitandao ikiwemo kuiba taarifa za siri kutoka kwenye makampuni na taasisi. Taarifa zimebainisha kuwa hivi karibuni wizi wa kimtandao uliosababisha hasara ya dola za Kimarekani bilioni 300 umefanyika na kiasi cha dola bilioni100 umefanyika kupitia kadi maalumu za mihamala ya fedha na malipo, bara la Afrika likiwa moja ya wahanga wa wezi huu wa kimataifa. Ripoti ya mwaka huu kutoka taasisi za Verizon kuhusiana na wizi wa kimtandao imebainisha kuwa kuwa wizi wa siri za makampuni ni wa pili kufanyika baada ya wizi wa fedha japo makampuni mengi hayajawa na mwamko wa kuwekeza katika kupambana na tatizo hili kubwa ambalo hivi sasa ni janga la kimataifa. Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklicki amesema kuwa mikakati ya kuzuia wizi huu kuliko athari zinazojitokeza baada ya kuingiliwa katika mtandao na kuibiwa taarifa za siri za kampuni. Alisema wizi huu wa kimtandao ni moja ya changamoto inayozikabili taasisi mbalimbali na makampuni ya biashara na ndio mwanzo wa kutengenezwa bidhaa bandia kwenye masoko na alisisitiza kuwa utunzaji wa taarifa za siri ni jambo la kwanza la msingi kwa kampuni Mkutano huo ambao umedhaminiwa za taasisi za Oracle na CIO Afrika na kuhudhuriwa na watendaji kutoka serikali na taasisi mbalimbali umetoka na maazimio ya kuhakikisha uwekezaji wa kiteknolojia unafanyika katika kuhakikisha wizi huu wa kimtandao unadhibitiwa na makampuni kuwa makini kuhakikisha yanalinda taarifa zake za siri.

Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yafanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa majukumu ya kazi za Mamlaka.

July 01, 2016


Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yafanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa majukumu ya kazi za Mamlaka.
  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa katika kituo cha hali ya hewa JNIA. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa katika kituo cha hali ya hewa JNIA. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi akielezea jambo katika kituo cha hali ya hewa JNIA. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa studio ya kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku unaosambazwa kwenye vyombo vya mbalimbali vya habari. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa studio ya kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku unaosambazwa kwenye vyombo vya mbalimbali vya habari. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.

TAASISI YA METDO YAHIMIZA WAZEE WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUKUMBI KUSAIDIWA.

July 01, 2016

Ashraph Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental Transformation For Development Organisation, walipotembelea Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.

Wafanyakazi wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.

 Taasisi ya METDO kupitia kwa msemaji wake, Ashraph Omary, iliwahimiza wanajamii kwa kushirikiana na taasisi za serikali na binafsi kuwasaidia wazee wanaoishi katika kituo hicho ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo ukosefu wa mavazi, chakula, matibabu pamoja na ujenzi wa uzio kituoni hapo ikiwa ni miongoni mwa changamoto zilizoanishwa kuwakabiri wazee hao.
Imeandaliwa na BMG