Fastjet yatuma salamu za Rambirambi kwa kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.

January 18, 2016
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi  Suleiman S. Suleiman.  




SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Dar es Salaam, 19 Januari, 2016

Uongozi na wafanyakazi wa Fastjet Tanzania  umepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za  kifo cha ghafla cha Mkurugenzi Mkuu wa  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi  Suleiman S. Suleiman.

Tunaungana na familia, marafiki, ndugu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kutuma salamu za rambirambi katika kipindi hiki cha kuomboleza.

Fastjet Tanzania imefanyakazi kwa ukaribu na Mhandisi Suleiman na tunatambua mchango wake katika kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.

Tutaukosa kwa kiwango kikubwa ushauri, uongozi na ushauri wake kutokana na kifo chake.

Tunaomba roho yake ipumzike kwa amani peponi.

Amin.


Imetolewa na Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.


photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
JANET MWENDA NA MARAFIKI ZAKE WA "MENTORING AND NETWORKING" WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA

JANET MWENDA NA MARAFIKI ZAKE WA "MENTORING AND NETWORKING" WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA

January 18, 2016
Picha No 1
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete moja ya vitu vilivyowasilishwa kwenye kituo hicho ndoo ya sabuni ya unga. Kushoto ni Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga na wengine wanaoshuhudia ni watoto wa kituo hicho. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM] Mmiliki na Mwendeshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mmiliki wa programu maalum ya vipindi vya watoto katika kutoa elimu katika televisheni kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’ kwa kushirikiana na marafiki zake wa kundi la “Mentoring and Networking” kupitia mitandao ya kijamii wametoa misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutoa misaada hiyo mapema jana 17 Januari, wakati wa tukio hilo lililofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam, Janet Mwenda ambaye aliambatana na baadhi ya marafiki zake hao wa “Mentoring and Networking” wameweza kutoa misaada hiyo ya vyakula, vinywaji ambavyo vitasaidia kituo hicho.
“Kwa kuja hapa kutoa msaada huu ni kutokana na kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa hapa na kwingineko kote. Naamini msaada huu utasaidia watoto wetu hapa kituoni naamini kwa hiki kidogo kitasaidia kwa siku kadhaa” alieleza Janet Mwenda.
Janet Mwenda ameongeza kuwa, amekuwa akifikiria zaidi kutoa misaada hivyo kufika hapo ni kutokana na kuguswa kwake kwa muda mrefu na amekuwa pia akitembelea kituo hicho kipindi cha nyuma hivyo kuwa miongoni mwa wanafamilia.
Kwa upande wake Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga ambaye aliambatana na Janet Mwenda katika kituo hicho ametoa wito kwa jamii kujitokeza kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo kama hivyo na kuchangia chochote walicho nacho.
Pia amepongeza watu mbalimbali kwa kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo ameomba waendelee kujitokeza zaidi pindi wanapoguswa na masuala ya kusaidia jamii isiyo jiweza.
Naye Mkurugenzi wa kituo hicho, Ndugu Evans Tegete akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alishukuru kwa kuguswa kwa Janet Mwenda na marafiki zake kwani hadi sasa kituo hicho hakina Mfadhili wa kudumu zaidi wakitegemea kuendesha kituo kwa michango ya misaada ya watu mbalimbali wanaofika kituoni hapo.
“Tunashukuru kwa msaada huu. Kwani ni mkubwa sana na utasaidia kuendesha kwa siku kadhaa ndani ya kituo chetu. Kituo chetu kwa sasa tuna watoto na vijana zaidi ya 89 wakiwemo wale wanaosoma shule za Bweni na wa kutwa ambao wapo hapa kituoni.” Alieleza Mkurugenzi huyo.
Pia alieleza kuwa changamoto mbalimbali zinawakabili ikiwemo suala la ada za shule kwa watoto na vijana waliochini ya kituo hicho.
Kituo hicho kinacholea Watoto na vijana wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu kina jumla ya watoto pamoja na vijana 120 kilianzishwa mnamo mwaka 1998 Kwa lengo la kuwasaidia watoto waliokosa malezi na huduma mbalimbali za kijamii. Kituo hicho kinapatikana Kimara Suka pamoja na Kijiji cha Mazizini Msata wilayani Bagamaoyo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo uongozi wa kituo hicho kinawaomba watu binafsi na wafadhili mbalimbali kujitokeza kuwasaidia pindi waguswapo.
Picha No 2
Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa kituo hicho.
Picha No 3
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (kushoto) akipata fursa ya kuwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo hocho cha Watoto Wetu Tanzania, kulia kwake ni Mary Sanga kutoka kundi la marafiki wa “Mentoring and Networking”.
Picha No 4
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga akitoa nasaha na kushukuru wale wote walioguswa kwa kuchangia mpango huo.
Picha No 5
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akipata fursa ya kuwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania.
Picha No 6
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ambapo ameiomba jamii kuwa na tabia ya kusaidia jamii isiyojiweza ikiwemo watoto wanaolelewa kwenye vituo.
Picha No 7
Binti Cecilia Sospita anayelelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania, akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa kituoni hapo kwa msaada uliowasilishwa na Bi. Janet Mwenda.
Picha No 8
Msaada uliotolewa kusaidia kituoni hapo.
Picha No 9
Kijana Samson Furgence akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho.
Picha No 10
Zoezi la utoaji wa zawadi likiendelea.
picha no 11
Watoto na vijana wanaolelewa katika kituo hicho. Wengine ni wageni wa kujitolea "Volunteer" wa kituo hicho kutoka nchini Ujerumani wakiwa pamoja na watoto hao kituoni hapo.
Picha No 12
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga akitoa msaada katika tukio hilo.
Picha No 14
Baadhi ya watoto na walezi wao wakifuatilia shughuli hiyo.
picha no 16
Janet Mwenda akishukuru watu mbalimbali kwa kumtia moyo katika kufanikisha shughuli hiyo.
picha no 17
Baadhi ya watoto hao.
picha no 18
Baadhi ya watoto hao.
picha no 19
Sala maalum ya kuombea vitu hivyo vilivyoletwa kituoni hapo pamoja na Baraka kwa waliofanikisha ikitolea na mmoja wa watoto wa kituo hicho.
 

JAMES KATORO AWASHUKURU WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MANISPAA YA ILEMELA KWA MAAMUZI YAO.

January 18, 2016
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG 
Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Tukio hili limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 
Mchungaji Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 
Diwani wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza James Katoro (CCM) akihutubia katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua kuwa diwani wao. Aliahidi kushughulikia kero mbalimbali zilizo katika Kata hiyo ambazo ni pamoja na kero ya maji, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za msingi na Sekondari.
Salum Abdallah Said ambae ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Kulia ni Jeremiah Mtoni ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Elias Makaranga (mwenye kinasa sauti) ambae alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Katoro katika uchaguzi uliopita akizungumza jambo katika mkutano wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jana.
Wakazi wa Kata ya Kayenze wakifuatilia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata hiyo wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25, mwaka jana.

Tigo kusambaza mtandao wa 4G LTE nchi nzima mwaka huu

January 18, 2016
•             Ni mtandao wa kasi Zaidi na wenye uwigo mpana Tanzania

 Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali imetangaza mpango wake wa kupanua huduma ya intaneti ya 4G katika mikoa yote nchini mwaka huu.

 Huduma hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam  mwanzoni mwa mwaka jana  na  baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro, kwa ufanisi na  hivyo kuufanya mtandao wa 4G kuwa mpana na wa kasi nchini Tanzania.

 Ukichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojia ya 4G LTE ina kasi ya nguvu takribani mara tano ikilinganishwa na teknolojia ya 3G ambayo inatumiwa na watoaji wengine wa huduma hiyo kwenye soko la Tanzania.

Mtandao wa 4GLTE una kasi kubwa kwenye kurambaza (surf) na kupakua vitu mbalimbali  kutoka kwenye intaneti pamoja na kupiga miito ya simu ya skype.
Hali kadhalika  inawezesha wateja kwa kiwango kikubwa  kuwa na uzoefu wa kutiririsha video au kufanya mikutano na inaweza kuhimili  kutumika kwenye  kupata video, mikutano, muonekano wa hali ya juu, blogu za video, michezo mbalimbali  na kupakua video kwenye mitandao ya kijamii.

Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo Shavkat Berdiev


Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo Shavkat Berdiev alisema kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari  kuwa  mipango ya kupanua teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote nchini  inafanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo  ya kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ili kuwawezeshakuendesha maisha ya kidijitali.
“Upanuzi wa mtandao  wa 4G nchi nzima  kwa mara nyingine umeonesha  sio tu kwamba Tigo  inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, bali pia kujikita kwake  kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwa Watanzania wengi kadri iwezekanavyo,” alisema Berdiev.

 Tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dola milioni 120 kwa mwaka kwenye  upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano. Hali kadhalika kuongeza A idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) takribaniu asilimia 67  ya idadi ya watu wazima wanamiliki simu za mkononi  ambapo idadi ya watumiaji wa intaneti hadi mwaka 2014 ilikuwa imeongezeka hadi kufikia watu milioni 9.3.


photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"