WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE,AKARIBISHA SHINDANO HILO KUFANYIKA BUNGENI DODOMA 2018

July 09, 2017
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian  tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.
 Msanii Dullah Aka DY akitumbuiza wakati wa Fainali hizo
 Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa fainali za Shindano la Bongo Style na kuipongeza Asasi ya Kiraia ya FASDO kwa ubunifu mkubwa.
 Mratibu wa FASDO Nchini Tanzania Bi. Joyce Msigwa akizungumza wakati mambo mbalimbali yanayohusu Asasi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio waliyoyapata kama kuendesha shindano la Na mimi nipo pamoja na FASDO CUP na mengine mengi yahusuyo asasi hiyo.
Ilikuwa ni 'Surprise' Kati kati ya Sherehe za Shindano la Bongo Style ambapo Mratibu Mkuu wa FASDO na Muasisi wa Asasi hiyo isiyo ya kiserikali Bi. Lilian Nabora(Aliyevaa Gauni Jekundu) alipofanyiwa Hafra fupi ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo alitimiza miaka 50. Waliomsindikiza ni 'Team' ya FASDO pamoja na washiriki wa shindano hilo kwa mwaka 2017.
Mratibu Mkuu na Muasisi wa FASDO Lilian Nabora akiongea wakati wa fainali za Bongo Style, alisema kuwa wamewekeza sana katika mitandao ya kijamii na hasa tovuti ya www.fasdo.org ili kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania nzima ambao wanauwezo na wanajiamini kuwa wanavipaji katika mambo mbalimbali wapate kujiunga katika taasisi hiyo,aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata washindi ulipitia mchujo mpaka kuwapata washiriki bora 30,kisha 15, mpaka kufikia washindi watatu(3) "Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wanaokadiliwa kuwa 1,500 na mpaka sasa bado tunawahimiza wapate kujiunga nasi" alisema Bi. Lilian.
 Waliokaa katika Meza ni Majaji Upande wa ubunifu wa mavazi, na walio mstari wa mbele ni Majaji upande wa Miswada ya Filamu na upigaji picha.
Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaonesha Mavazi yao waliyo yabuni wao wenyewe
 Wageni waalikwa  wakifuatilia sherehe za Fainali za shindano la Bongo Style
 Mwenyekiti wa FASDO Bw. Stanley Kamana akitoa neno la Shukurani wakati wa Fainali za Bongo Style
 Washiriki wa Shindano la Bongo Style kwa Mwaka 2017 wakiwa wanafuatilia mambo mbali mbali wakati wa Shindano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya FASDO Bw. Tedvan Nabora akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria katika Fainali za shindano la Bongo Style
Picha ya pamoja ya  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe,Uongozi na Team ya FASDO,Majaji na washindi wa Bongo Style Competition kwa mwaka 2017.
Picha zote na Laden Tedvan Nabora.

SERIKALI INAVYOMSHINDA ADUI 'MARADHI'

July 09, 2017
 Dk. John Pombe Magufuli, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Vifaa vya tiba vya kisasa kabisa katika moja ya Hospitali hapa nchini

*****
Mara baada ya kupata Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitangaza vita dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Mwalimu Nyerere alisema wazi kuwa ili Taifa letu liendelee halina budi kupambana dhidi ya maadui hao.

Kwenye mapambano dhidi ya 'ujinga' tumeshuhudia Serikali ikijenga shule za msingi kwenye kila kijiji na mtaa, Serikali ikijenga shule za sekondari kwenye kila kata; Serikali ikitoa elimu bure kuanzia ngazi ya  shule ya msingi mpaka Sekondari; Serikali ikitoa mikopo ya elimu ya juu kwa wenye sifa vyuoni; Serikali ikiboresha miundo mbinu ya maabara, maktaba na madawati; Serikali ikihakikisha Waalimu wanakuwepo wa kutosha na wakiwahudumia kwa kuwapatia mishahara na makazi.

Upande wa mapambano dhidi ya umaskini Serikali imekuwa ikitoa ajira rasmi na zisizo rasmi; Serikali inaboresha kilimo kuwa cha kibiashara na chenye tija zaidi; kujenga viwanda; kuhimiza uwekezaji nchini; kuboresha mikataba ya madini n.k

Hata kwenye upande wa adui maradhi mapambano ya adui huyu bado ni makali Serikali ikijitahidi kumshinda.

Katika vipindi mbalimbali tumeshuhudia Serikali ikijenga vituo vya afya, zahanati na hospital kwenye maeneo mbalimbali nchini; kujenga hospitali ya Moyo nchini ambapo inafanya mpaka upasuaji mkubwa wa moyo.

Tumeshuhudia Serikali ikiendelea kununua vifaa tiba, mashine, vitanda, kupambana na maleria, kifua kikuu, ukimwi na magonjwa mengineyo hatarishi.

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AWASILI CHATO KWA AJILI YA KUKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

July 09, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita. Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita. PICHA NA IKULU.

IDADI YA WATANZANIA WANAOTUMIA SIMU KUFANYA HUDUMA MITANDAONI YAONGEZEKA

July 09, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Ripoti ya Utalii ya mwaka 2017 iliyozinduliwa na Jumia Travel nchini Tanzania imebainisha kuwa idadi ya watanzania wanaotumia simu katika kufanya huduma za hoteli kwa njia ya mtandao imeongezeka na kufikia takribani asilimia 60.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita imebainisha kuwa mpaka kufikia mwaka 2016 watumiaji wa intaneti walikuwa ni zaidi ya milioni 19 kutoka milioni 17 ilivyokuwa mwaka 2015.
 
Ongezeko hilo limechochewa kwa kiasi kikubwa na kukua na kuenea kwa matumizi ya intaneti nchini (takribani asilimia 40 ya watanzania wamefikiwa na intaneti nchini kote) lakini pia maendeleo ya kasi kwenye sekta ya mawasiliano ya simu ambapo mpaka hivi sasa watanzania zaidi ya milioni 40 wanatumia huduma za simu za mkononi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Meneja Mkaazi wa kampuni hiyo inayojishughulisha na hudumza za hoteli na usafiri barani Afrika, Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa kukua kwa sekta hiyo ni ishara nzuri kwa maendeleo ya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.

“Hakuna anayeweza kubisha kwamba dunia yote kwa sasa imehamia mtandaoni kwani ndiko kwenye urahisi na unafuu mkubwa. Inatia hamasa kuona kuwa watanzania nao hawako nyuma katika kuyapokea na kuendana na mabadiliko hayo. Hivi sasa karibu kila mtanzania ana simu ya mkononi tena ya kisasa ambayo ina uwezo wa kutumia intaneti. Lakini cha kuvutia zaidi ni kwamba kwa namna gani watu wanavyoutumia mtandao huu kwa manufaa yao zaidi badala ya kufanya mambo hayana tija kwao,” alisema Bi. Dharsee.

“Jumia Travel katika ripoti yetu tuliyoiwasilisha inaonyesha kwamba watanzania wanautumia vizuri mtandao wa intaneti kupitia simu zao za mkononi kwenye kufanya huduma zetu. Hii inamaanisha kwamba wameweza kugundua faida zinazotokana na wao kufanya hivyo badala ya kwenda moja kwa moja mahotelini kuulizia huduma. Kupitia mtandao wetu mteja anaweza kujionea huduma za mahoteli zaidi ya 1000 ndani ya wakati mfupi na kuchagulia ile inayomfaa sehemu yoyote ya Tanzania. Kwa kuongezea, ripoti yetu imebainisha kuwa miongoni mwa huduma zinazouliziwa sana na wateja pindi wanapoulizia hoteli ya kwenda ni upatikanaji wa mtandao wa intaneti. Hivyo basi hii ni fursa kubwa kwa watoa huduma kuhakikisha kuwa huduma hii inapatikana kwa uhakika na kuboreshwa zaidi,” alimalizia Bi. Dharsee.

Hii ni mara ya pili kwa Jumia Travel kuwasilisha Ripoti ya Utalii nchini Tanzania ambapo mwaka 2016 walifanya hivyo pia. Miongoni mwa mambo yaliwekwa wazi na ripoti hiyo ni kuendelea kwa kufanya vizuri kwa sekta hiyo kwani mapato yake yameongozeka kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.9 mwaka 2015 na kufikia 2.1 mwaka 2016. Kiasi hiko kimechangia Dola za Kimarekani bilioni 4.6 mwaka 2016 kutokea 4.2 za mwaka 2015 katika pato la taifa.

Kwa upande wa ajira, katika mwaka 2016 sekta hiyo imeajiri watanzania zaidi ya milioni 1.3 (asilimia 11.6). Idadi hiyo inatarajiwa kukua kwa asilimia 4.6 ndani yam waka huu wa 2017 na kufikia zaidi ya milioni 1.4. Hivyo kuifanya mojawapo ya sekta muhimu katika uchangiaji wa uchumi na pato la taifa kwa ujumla.

Mbali na kuwasilisha ripoti hiyo, Jumia iliwashirikisha habari njema watanzania kuwa inasherehekea miaka mitano tangu kuanza kufanya shughuli zake barani Afrika kwa kuwarahisishia waafrika huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Jumia ambayo inaundwa na kampuni tano (Jumia Travel, Jumia Food, Jumia Market, Jumia Deals na Classified pamoja na Jumia Jobs) pia imeujulisha umma kuwa imefanikiwa kuingia kwenye orodha ya makampuni 50 yanayotoa huduma za mtandaoni duniani kwa mara ya pili mfululizo.
 
Orodha hiyo ilitolewa na Taasisi ya Kiteknolojia ya Massachusetts (MIT) ya nchini Marekani ambayo huyatambua makampuni 50, yaliyopo tayari na yanayochipukia katika kutengeneza fursa kwa kutumia teknolojia mpya kwenye kutoa suluhu na kukidhi mahitaji ya masoko mbalimbali duniani.

Mwaka huu 2017, Jumia imeshika nafasi ya 44 ukilinganisha na ya 47 kwa mwaka 2016, ikiwa imetajwa kama kampuni iliyojikita zaidi kutatua changamoto zinatokana na huduma kwa njia ya mtandao barani Afrika. Changamoto hizo ni pamoja na barabara zisizopitika kwa urahisi, tabia zisizotabirika za wateja, kukosekana ueneaji wa kutosha wa mtandao wa intaneti ambapo kitakwimu ueneaji wake ni asilimia 27 tu barani kote.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka

July 09, 2017
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu nchini na sanaa kwa ujumla huku akiwa ndio kiongozii wa juu kabisa hapa nchini kuizungumzia mara kwa mara tamasha hilo la ZIFF. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmo, Dkt. Jakaya Kikwete alishukuru na kupongeza kwa mafanikio waliyopata ZIFF hadi kufikia msimu wa 20, tokea kuanzishwa kwake ambapo imewataka waendelee zaidi na zaidi. “Nashukuru kwa kunialika. Nashukuru kwa tuzo hii kwani sikutegemea na nina wapongeza kwa mafanikio haya ua kutimiza miaka 20. Nawaombeeni muendelee miaka 20 na 20 zaidi vizazi na vizazi mpaka litakapofika mwisho” alieleza Dkt. Kikwete. Dkt. Kikwete alitoa ushahuri kwa uongozi wa ZIFF kuwa na kifua mbele kwa namna filamu zinazopita kwenye tamasha lao kuzifuatilia kwani zimekuwa zikifanya vizuri huko mbele ikiwemo tuzo za Hollywood. Kwani ZIFF imekuwa ni taasisi yenye nafasi muhimu kwa jamii ya watu wa Zanzibar Tanzania . Kwa sasa ni kujipima katika miongo miwili hii ni jinsi gani na kiasi gani ZIFF ilivyojisogeza na kuwa karibu na jamii” alieleza Dkt. Kikwete. Aidha, Dkt. Kikwete alieleza kuwa, tasnia ya sanaa hapa nchini inatakiwa ipande na kuwa juu ili kuendeleza utamaduni wa Mzanzibar na Mtanzania inaenda vipi. Pia amewataka ZIFF kuwa karibu na jamii ili kuweza kujenga ushawishi kwa jamii hiyo na kilamwaka wawe na matamanio zaidi ya tamasha. Awali akitangaza tuzo hiyo, Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo mbele ya jopo la wajumbe wa Bodi ya ZIFF, waliweza kumtangaza rasmi Dkt. Kikwete kutwaa tuzo hiyo kubwa kabisa ambayo utolewa kwa watu wenye kutukuka ambao pia wameifanya mchango mkubwa ndani na nje katika masuala ya Sanaa na tasnia ya filamu. Mwenyekiti wa ZIFF Mahmoud Thabit Kombo aliweza kuwataka wazawa hasa Wazanzibar kuwa na mwamko wa kuthamini cha kwao na hata kujitokeza kudhamini tamasha hilo. “ZIFF imefungua milango yake wazi kwa mtu yeyote kujitokeza na kudhamini tamasha hili. Wazawa tunawakaribisha sana kwani uwepo wa tamasha ili ndio kukuwa kwa uchumi wetu na maendeleo hivyo tujisikie fahari kwa uwepo wake”. Ameeleza Mahmoud Thabit Kombo. Akiwa mgeni rasmi, Dkt. Kikwete aliweza kushuhudia filamu ya uzinduzi wa tamasha hilo ya ‘T-Junction’ iliyoandaliwa na mtayarishaji wake Amir Shivj kutoka Kijiweni Production ya Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, Ngome Kongwe iliweza kufurika umati mkubwa waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo. Imeelezwa kuwa, wageni kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 14,000 wamefika Visiwani Zanzibar huku hoteli mbalimbali zikiwa zimepata faida kwa kipindi hiki, alieleza Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo ambapo ameweka wazi kuwa katika orodha yao ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali huku wengine wakiendelea kufika kila siku. Tamasha hilo linatarajia kumalizika hadi Julai 16,2017. Huku kila siku kukiwa na filamu zinazoonyeshwa Ngome Kongwe na zingine zikioneshwa kwenye kumbi mbalimbali ndani ya viunga vya Unguja pamoja na Vijiji vya Zanzibar sambamba na kutoa mafunzo ya uendeshaji wa filamu na mafunzo mbalimbali katika tasnia hiyo ya filamu. Imeandaliwa na Andrew Chale, MO BLOG-Zanzibar
Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Zanlink wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF 2017, ambalo kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Wadau mbalimbali wa wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF 2017, ambalo kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busara Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la Sauti za Busara, Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
wadau wakiwa kwenye picha ya kumbukumbu
Mwendesha kipindi cha senema zetu akiwa 'mbashara' wakati wa ufunguzi huo
Mmoja wa wageni waliofika kwenye tamasha hilo ambapo alikuwa kivutio kwa muonekano wake wa kama aliyeigiza filamu ya YESU " JESUS'
Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabiti Kombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi wakati wa uzinduzi huo
Mmoja wa wadau wakubwa wa tasnia ya filamu na muziki hapa nchini Dada Sauda Simba akihojiwa 'mbashara' na kipindi cha SINEMA ZETU
Wadau mbalimbali wakipata picha ya ukumbusho kwenye zuria jekundu
wadau wakipata kumbukumbu
Mkurugenzi wa Fabrizio Colombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busara Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la Sauti za Busara, Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
Burudani ikiwendelea
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongzi wengine wakipiga makofi kupongeza bendi iliyokuwa ikitumbuiza
upande wa viongozi na wagei waalikwa wakifuatilia tukio hilo
Wakurugenzi wapya wa ZIFF wakitambulishwa katika ufunguzi huo, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF Daniel Nyalusu na kushoto ni Mkurugenzi wa ZIFF Fabrizio Colombo
Mkurugenzi wa ZANLINK akizungumza katika tamasha hilo
Burudani
Mwenyekiti wa ZIFF 2017, Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Kikwete jukwaani
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshika tuzo yake hiyo ya mtu aliyetukuka wa ZIFF baada ya kukabidhiwa na Bodi ya ZIFF usiku wa Jumamosi Julai 8,2017. Ngome Kongwe, Unguja
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika tukio hilo