NDESAMBURO ATANGAZA KUTOGOMBEA JIMBO LA MOSHI MJINI, AMUACHIA MIKOBA MEYA JAFARY MICHAEL

April 16, 2015


Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakifuatili mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika katika eneo la soko la Manyema.
Katibu mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi na Diwani wa Kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akiwasili katika viwanja eneo la soko la Manyema akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo na Stephen Ngasa wa kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya a manispaa ya Moshi,Jafary Michael akihutubia mamia ya wananchi waliofika katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vilivyoko jirani na soko la Manyema .
Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amekaa chini akifuatilia mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Philemoni Ndesamburo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Clement Kwayu wakati wa mkutano wa hadhara.
Mamia ya wananchi katika mji wa Moshi wakishangilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Msathiki Meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimtambulisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge katika jimbo hili wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
Ndesamburo akizungumza na wananchi wa Moshi mara baada ya kumtangaza mrithi wake katika jimbo la Moshi mjini.
Mamia ya wananchi wakimsikiliza Ndesamburo.
Mstahiki Meya ,Michael akiwa amekaa kando ya Mbunge ,Philemoni Ndesamburo .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA EGYPT NA C P U LEO

April 16, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Mamlaka zinazohusika na  uwekezaji Tanzania na Wawekezajia kutoka Egypt wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mr. Joe Kawkaban kiongozi wa Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawekezajia wa CPU wakati alipokutana na ujumbe huo Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezajia wa CPU baada ya mazungumzo yao Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015. (Picha na OMR)

Bayport Financial Services yazidi kuchanja mbuga, yazindua tawi la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya

April 16, 2015


TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo kwa watumishi wa wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, mwishoni mwa wiki ilizindua tawi lake jipya la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, huku Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Staki Senyamule, akiwataka wananchi wake kukopa kwa sababu maalum.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kulia, akionyeshwa nyaraka za ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mambo ya mikopo katika uzinduzi wa taasisi hiyo katika wilaya hiyo ya Ileje, mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wilayani humo. 

Kufunguliwa kwa tawi hilo si kutainua uchumi wa wananchi wa Ileje watakaotumia fursa ya uwapo wa ofisi hiyo, bali pia kutarahisisha utoaji wa huduma wa taasisi hiyo ya Bayport nchini Tanzania.
Wageni mbalimbali wakiangalia shughuli za uzinduzi wa tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Senyamule.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo jipya, Mkuu huyo wa wilaya Ileje, Rosemary alisema kuwa wananchi wakiitumia fursa ya tawi hilo kutainua pia kiwango cha uchumi cha watu wake.
Baadhi ya wageni waalikwa wakisoma vipeperushi vya taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Alisema suala la mikopo ni jambo jema kutokana na uwezo mzuri unaoweza kuwaendeleza wananchi, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zote zilizoidhinishwa, ambao kimsingi ni watu wanaotakiwa kuendelezwa kwa mambo mengi.
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Bayport Financial Services, Alpha Akim, akizungumza jambo katika uzinduzi wa tawi lao la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

“Kwanza nawapongeza mno wenzetu wa Bayport Financial Services kwa kuamua kuja kufungua tawi hapa katika wilaya yetu ya Ileje, ila ni muhimu wananchi kukopa kwa sababu maalum ili waweze kuendeleza maisha yao kwa kutumia vyema fursa za mikopo Tanzania.

“Tukifanya hivyo tunaweza kupata maisha bora kwa sababu tutajimudu kiuchumi, hivyo ni wakati wetu kufurahia kuanzishwa kwa huduma za taasisi hii hapa kwetu ileje, maana ndio kwanza wanafungua tawi lao hapa,” alisema.

Naye Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim, alisema kufungua kwa tawi hilo pia ni sehemu ya kutoa ajira kwa vijana sanjari na kuongeza kipato kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa kwa kupitia fursa nzuri ya mikopo.

“Watu mbalimbali watapata mwangaza mzuri wa kiuchumi wakiwamo wale watakaopata nafasi ya kufanya kazi nasi, hususan ile ya uwakala, bila kusahau wale watakaokopeshwa bila amana wala dhamana.

“Naomba wananchi na wakazi wa Ileje watumie vyema fursa ya uwapo wa taasisi hii wilayani kwao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wote kwa pamoja tunafanikisha kwa vitendo ndoto ya kukuza uchumi wetu na wa Tanzania kwa ujumla,” alisema Akim, Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Bayport.

Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na utoaji mikopo mbalimbali kama vile fedha taslimu, mikopo ya bidhaa, bima ya elimu kwa uwapendao, ambapo mikopo hiyo inaweza kutolewa ofisini au kwa njia rahisi ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
WATU TISA WALIOHIFADHIWA MSIKITI WA SUNI WAKAMATWA NA MILIPUKO.

WATU TISA WALIOHIFADHIWA MSIKITI WA SUNI WAKAMATWA NA MILIPUKO.

April 16, 2015

RPC MORO KUONESHA MILIPUKO.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akiwaonesha waandishi wa habari ( hawaonekani pichani) milipuko hatari  aina ya ‘ Water explosives gel ‘ iliyokamatwa jana usiku kutoka kwa watuhumiwa  tisa waliokuwa wamehifadhiwa ndani ya  msikiti wa Suni uliopo Tarafa ya Kidatu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Picha kwa hisani ya Michuzi blog