SERIKALI IPO KWEYE HATUA ZA MWISHO ZA KUANZA UJENZI WA BARABARA YA TANGA-PANGANI

March 05, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionyeshwa eneo la uwanja wa ndege itakakopita barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipima eneo la barabara inayohitajika katika eneo la hifadhi ya uwanja wa ndege wa Tanga.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo katika makutano ya barabara ya mchepuko eneo la Duga.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya gati ya Bandari ya pangani ambayo  inajengwa kwa gharama ya sh. bilioni 2.3.
Muonekano wa gati inayojengwa katika bandari ya Pangani iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya daraja la Mto Pangani ambalo upembuzi yakinifu wa ujenzi wake umekamilika na litaanza kujengwa hivi karibuni.
 
SERIKALI ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tayari kazi  iliyobaki ni kupata mzabuni wa kuendesha mradi huo.
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa ujenzi  wa Barabara hiyo utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 na kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.
Mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja katika  Mto Pangani lenye urefu wa mita 550 ambalo linategemewa kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya kuimarisha shughuli za utalii katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa Prof.Mbarawa ni kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo serikali itawalipa fidia wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa tathimini kwa mujibu wa sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.
“Nasisitiza kwamba kama sheria inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai kila mwenye haki na anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili hatalipwa na hii itakuwa ni kulingana na tathmini iliyokwishafanyika......”,alisema Waziri huyo.
Alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa Barabara hiyo kwamba ndiyo kiini na moyo wa uchumi wa wilaya ya Pangani hasa kwa kutambua namna ambavyo ina vivutio vingi vya kitalii hatua itakayolenga kuwaongezea fursa za kibiashara wananchi na kukuza Pato lao.
“Daraja hili litakuwa na uwezo wa kupitisha magari na watembea kwa miguu kwa wakati mmoja na hivyo ni mkombozi wa wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa walikuwa wakitegemea kuvuka ng’ambo ya pili ya mto kwa kutumia kivuko tu ambacho wakati mwingine kinakumbwa na hitilafu”,alifafanua Prof.Mbarawa ambaye yupo mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.
Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake baada ya kukagua Kivuko cha Mto Pangani,Barabara ya Tanga,Saadani mpaka Bagamoyo na eneo linalotakiwa kujengwa Daraja,Prof.Mbarawa  aliuagiza Uongozi wa Wakala wa ufundi na Umeme(Temesa)kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za utendaji wa kivuko kwa kila siku.
Aliwaagiza kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya elektroniki ili kuepusha vitendo vya ubadhirifu wa fedha wakati serikali ikiwa kwenye mpango wa ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Suala la kutumia mashine za kieletroniki halina mjadala habari ya kutumia vitabu vya risiti ili muongeze sifuri mbele hatuzitaki....hapa kuna shida kuna siku I naandikwa imeingia shilingi milioni moja lakini Benki zimeenda laki nane na hamsini hii laki moja na hamsini zinaishia wapi hili ni tatizo”,alisema.
Hata hivyo alisema ipo haja kwa Temesa kuajiri manahodha wa vivuko ambao wanafanya kazi kwa viwango vya kitaaluma ambavyo vinakubalika badala ya kutumia Wazee ambao wanafanya kazi kwa mazoea.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Dk Hamisi Kigwangala aongoza Matembezi ya " KUTOA AHADI YA UWIANO SAWA WA KIJINSIA "

March 05, 2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akijiandaa kuanza matembezi ya shamrashamra za kuelekea  siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiwa sambamba na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea  siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.

Mwenyekiti wa Tanzania Women of Achievement , Sadaka Gandi akiongea na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea  siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiongea na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea  siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washirikimatembezi ya shamrashamra za kuelekea  siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.





DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 05, 2016
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
Mshairi,  Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.

Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia  walimu hao.

"Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye" alisema Makonda.

Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.

Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.


RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

March 05, 2016

kj1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016PICHA NA IKULU
kj2
Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
kj3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
kj4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
kj5
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, MarehemuMzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi, 
kj6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
kj7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Muskumu Bwana Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na 
Wasukuma ni watani.
kj8
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
kj9
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayang Bw. Khamis Mgeja akiongea na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete,  kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
kj10
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
kj11
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi  wakimsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua jambo huko Msoga Mkoani Pwani.
kj12
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
kj13
Kada wa Chadema Hamis Mgeja akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
kj14
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.PICHA NA IKULU

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI JUU YA MWELEKEO WA HALI YA MVUA NCHINI.

March 05, 2016
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati) akitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa ambae ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mamla ka ya Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji, kujiandaa juu ya namna ya kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.

Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Alisema Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.

Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Bonyeza HAPA Kutazama Semina Kwa Wanahabari.

WWF KUSAIDIA UJENZI WA MAJIKO SANIFU KATIKA SHULE TATU ZA MANISPAA YA MOSHI NA KUWEKA SOLAR KATIKA ZAHANATI YA MSARANGA

March 05, 2016
Shule ya Sekondari , J.K Nyerere iliyopo manispaa ya Moshi ni moja kati ya shule zitakazonufaika na msaada wa kujengewa majiko sanifu na Shirika la kimataifa la Mazingira (WWF-Tanzania) 
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozana na wa wakuu wa idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea shule ya sekondari J.K Nyerere .
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako wakiwa katika jiko la shule hiyo kuangalia namna ambavyo wanaweza kupunguza matumizi ya kuni kupikia.
Matumizi ya kuni ni makubwa katika shule za msingi ambazo zimekuwa zikitumika kupikia hali inayochangia ongezeko la uharibufu wa mazingira kwa kukata miti.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha wageni katika shule hiyo ,katikati ni mkuu wa shule hiyo , Parfectius Mushi akimtizama na kulia ni afisa kutoka WWF ,
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako (kulia) akiwa na kaimu mkuu wa shule ya msingi Langoni ,Mwl Hamad,alipotembelea kujionea namna gani wanavyoweza saidia katika ujenzi wa majiko sanifu. 
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa ameongozana na wakuu wa idara za Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutembelea jiko lilopo katika shule ya msingi Langoni mjini Moshi.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akimueleza jambo Meneja Mradi wa ICLEI Africa Irina Velasco walipotembelea jiko la shule hiyo.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha wageni katika shule ya msingi Msandaka alipotembelea shule hiyo.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozwa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Danford Kamenya wakielekea kutizama jiko la shule hiyo.
Jiko la shule ya msingi Msandaka.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Msandaka katika manispaa ya Moshi.
Baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wakiwa katika chombo maalumu cha kuhifadhia nafaka shuleni hapo.
Diwani wa kata ya Ng'ambo ,Genesis Kiwhelu akisalimiana na Irina Velasco wa ICLEI alipowapokea katika zahanati ya Msaranga ambapo ujumbe wa WWF ulifika kuangalia namna ya kuisadia zahanati hiyo vifaa vya Nishati ya Umeme unaotokana na jua.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitembelea katika zahanati hiyo.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akisikiliza maelezo kutoka kwa mganga kiongozi wa zahanati ya Msaranga Dkt Para.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako na ujumbe wake wakiwa katika eneo la kata ya Ngangamfumuni ambako WWF imepanga kuotesha miti.
Afisa Habari wa manispaa ya Moshi,Ramadhan Hamisi akieleza jambo kwa ujumbe huo mara baada ya kutizama eneo litakalo oteshwa miti.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.