MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI MKOANI TANGA JINSI ILIVYOFANYIKA.

August 13, 2013
Vijana wakiwa kwenye maandamano  kusherehekea siku ya vijana duniani ambayo hufanyika kila tarehe 12 Agosti . Maadhimisho haya ni ya kwanza Mkoani Tanga .

Kundi la burudani liitwalo Msisimko group likitumbuiza kwa igizo

Kundi la Muziki wa kizazi kipya liitwalo  Nguvumali group likitumbuiza kwenye maadhimisho hayo

Kaimu Katibu Tawala Bi. Monica  Kinara ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiongea na vijana juu ya umuhimu wao katika jamii


Mtaalamu wa  wa viungo visaidizi na viungo bandia Bw. Richard Mbawala kutoka shirika  Y.D.C.P ( Youth with Disability Community program linaloendeshwana kanisa la Freee Pentecostal Church of Tanzania akimwelezea Mgeni Rasmi shughuli zao.

Baadhi ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na vijana wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanga.

Mwanafunzi  Yona Kishosha wa mwaka wa pili  kutoka shule ya ufundi  VETA   katika fani ya unyoshaji wa bodi za gari  akionyesha moja ya vifaa vya gari vinavyotengenezwa chuoni hapo.


Baadhi ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na vijana wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanga.