MKURUGENZI WA JAMII FORUM ASOMEWA MASHTAKA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

MKURUGENZI WA JAMII FORUM ASOMEWA MASHTAKA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

December 16, 2016
1
Mwanzilishi na MKurugenzi wa Jamaii Forum Bw. Maxence Mello akitoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka yake Mello amekosa  dhamana  katika kosa moja baada ya kukosa mdhamini mmoja mwenye sifa  , Hata hivyo katika makosa mawili mengine yanayomkabili alipata dhamana Bw. Mello amesomewa mashtaka hayo leo  kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
2 3
Mwanasheria wa TCRA Bw.Johanes Kalungula akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa.
MASHARTI LIGI KUU YA VODACOM DURU LA PILI

MASHARTI LIGI KUU YA VODACOM DURU LA PILI

December 16, 2016

Duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu.
Katika mechi za kesho, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.
Michezo mingine ya kesho ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.
Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata. 
Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya kuwa na leseni B ya CAF.
Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi husika.
Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. 

“BANDARI TANGA YAIFUNGA MTWARA MABAO 43-16”

December 16, 2016


Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam  na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
 Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam  na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
 Wachezaji wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga wakichuana dhidi ya Makao Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi wa seti 2-0 mchezo uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini Tanga
TIMU ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye michuano ya Bandari inayoendelea mjini Tanga.

Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya Bandari mjini hapa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga ilikuwa ikiongozwa kwa mabao 23 -17 dhidi ya Mtwara.

Halikadhalika Tanga wakiweza kuibuka pia na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao  Makuu kwenye mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.

Katika mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es Salaam iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Makao Makuu kwa mabao 36-13.

Wakati huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye dimba hilo la Bandari mjini hapa.

Kwenye mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha Bandari Mtwara na Maziwa Makuu ambapo timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta zikigawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Ili kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye michezo Bandari Tanga wanaume waliweza kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba.

Wakati wanaume wakiibuka na ushindi huo wanawake nao waliweza kuwaunga mkono wenzao kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly.

Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa jana na Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA) Deusdedit Kakoko ambaye aliwataka wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na maarifa kwenye michezo yao ili kupata ushindi.


MFUKO WA PPF WADHAMIRIA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE WAKIWEMO WANATASNIA WA FILAMU.

December 16, 2016
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Meshack Bandawe, akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara. 

Mafunzo hayo yalanza Disemba 14 na yanafikia tamati leo Disemba 16, 2016 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Musoma. Yameandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kuwajengea uwezo wadau wa filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora.
#BMGHabari
Wadau wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, wakati akiwaeleza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo
Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, akiwasilisha mada kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara
Wadau wa filamu mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Afisa Masoko PPF, Evance Baguma
Wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara wamefurahishwa na mada kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka PPF na kuonesha mwitiko mkubwa wa kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF.

Mfuko wa Pesheni wa PPF umesema umedhamiria kuhakikisha kwamba wananchi wengi walio kwenye sekta zisizo rasmi ikiwemo wajasiriamali wananufaika na mafao ya hifadhi za jamii kupitia huduma ya Wote Scheme.

Meneja wa mfuko huo Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ameyasema hayo Musoma mkoani Mara, wakati akieleza umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo mbele ya wadau wa filamu mkoani humo.

Amesema wananchi wasio kwenye sekta rasmi wakiwemo wajasiriamali wanayo fursa ya kujiunga na mfuko wa PPF na kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu, mikopo ya elimu, maendeleo pamoja na mafao ya uzeeni kwa kila mwanachama kuchangia shilingi elfu 20 kwa mwezi ambazo mwanachama hulipa kadri awezavyo.

Naye Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, amesema lengo la mfuko huo kuanzisha huduma ya Wote Scheme kwa wajasiriamali ni kuondoa dhama potofu kwa baadhi ya wananchi kwamba anayeweza kunufaika na huduma za mifuko ya hifadhi za jamii ni lazima awe mtumishi wa taasisi binafsi ama serikali.

Wadau wengi wa filamu mkoani Mara wamefurahishwa na ufafanuzi wa mfuko huo ambapo wamebainisha kwamba awali walikosa fursa mbalimbali za mifuko ya hifadhi za jamii ikiwemo PPF kutokana ufahamu duni waliokuwa nao.
Tazama picha zaidi HAPA

SIKU YA KWANZA YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI (JWTZ) KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA.

December 16, 2016
Waandishi wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua kuashiria kuanza safari hiyo atika lango la Marangu.
Safari ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutzama madhari ya Mlima Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu mnene.
Wapandaji waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baraidi mapema wakati safari ya kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
Safari ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha. 
Safari ya kupanda vilima vidogo ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro iliendelea.
Maeneo mengine yalikuwa ni ya Madaraja na Mito.
Hatimaye safari kafika eneo la Kisambioni ikiwa ni nusu ya safari ya kuelekea katika kituo cha Mandara ,eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kupata chakula.
Baadae safari ya kuelekea kituo cha Mnadara ikaendeleo.
Maeneo mengine Washiriki walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata nguvu mpya ya kuendelea na safari.
Majira ya saa 12 jioni hatimaye Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku ya kwanza ikafika katika kituo cha Mandara na washiriki wakapata nafasi ya kupata picha ya pamoja na kupumzika kwa ajili ya siku ya pili kuendele na safari ya kwenda kituo cha Horombo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.