JE WAJUA TIMU YA TOTO AFRICANS YA JIJINI MWANZA NDIYO TIMU MASKINI KULIKO ZOTE LIGI KUU NCHINI?

March 09, 2016
Kocha wa Timu ya Soka ya Toto Africas ya Jijini Mwanza inayoshiriki Liku Kuu nchini, John Tegete (Wa pili kulia) akiwa na "Wananzengo" kutoka Jijini Mwanza ambao wanatarajiwa kuwa wadau wapya wa timu hiyo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Kwa Mjibu wa Tegete, Toto Africans ndiyo timu Maskini kuliko zote zinazocheza Liku Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Bajeti yake kwa Mwaka ni zaidi ya Shilingi Milioni 495 lakini mapato yake kwa mwaka ni takribani shilingi Milioni 180. 

Inakadiriwa kuwa hakuna timu nyingine yenye matapo ya chini kama hayo miongoni mwanza timu za Liku Kuu Tanzania Bara hivyo kwa hali hiyo Toto Africans inapitia wakati mgumu katika kujiendesha kuliko inavyofikiriwa.

Pamoja na ugumu huyo, Toto Africans iko nafasi ya Tisa kati ya Timu 16 zinazoshiriki Ligu hivyo hivyo kwa mazingira inayopitia inastahili kuitwa timu bora ambayo haipaswi kutelekezwa na wadau wa soka Jijini Mwanza wakiwemo Wananzengo ambao wameonyesha nia ya kushirikiana na timu hiyo.

MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YAFANYIKA JIJINI MBEYA

March 09, 2016
Baadhi ya maaskofu kutoka makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya wakiwa wamshika Picha ya Rais  na ramani ya Tanzania wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.

Picha ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa imeshikwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya maombi maalumu kwa ajili ya rais na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya

Muongozaji Mkuu wa Maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ,Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi hayo katika ukumbi wa Mkapa .

Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake  katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu. .

Baadhi ya waumini walioshiriki Maombi Maalum ya Kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake yaliyoandaliwa na Jukwaa la wakristo Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la The City of refuge Church Dkt Charles Gadi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu.

Baadhi ya maaskofu  na waumini kutoka jukwaa la Wakristo Mkoa wa Mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt  John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijni Mbeya Machi 8 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo.

kwaya zikiendelea kutumbuiza katika maombi hayo ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Machi 8 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa  kushoto pamoja na Askofu Charles Gadi mwenye miwani  wakiwa katika maombi maalum ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Maombi yakiendelea....

Baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt Maguli na serikali yake .

Picha na Jamiimojablogu Mbeya.....

MWANARIADHA WA TANZANIA ALPHONCE FELIX AREJEA NCHINI BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA TATU KATIKA MASHINDANO YA LAKE BIWA MARATHONI YA NCHINI JAPAN.

March 09, 2016
Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Felix akirejea nchini akitokea nchini Japan kushiriki mashindano ya marathoni yajulikanayo kama Lake Biwa ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu akitumia muda wa saa 2:O9:19.
Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Felix akisalimiana na mdau wa riadha ,Whileam Gidabuday aliporejea nchini akitokea nchini Japan kushiriki mashindano ya marathoni yajulikanayo kama Lake Biwa ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu akitumia muda wa saa 2:O9:19.
Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Felix (katikati)  akiwa na kocha wa timu ya taifa ya riadha Francis John waliporejea nchini wakitokea nchini Japan kushiriki mashindano ya marathoni yajulikanayo kama Lake Biwa ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu.
Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Felix akimkabidhi rais wa shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka ngao ya ushindi wa nafasi ya tatu aliyopata katika mashindano ya Lake Biwa Marathon yaliyofanyika nchini Japan.
Wanariadha wa timu ya taifa ya riadha wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa tatu wa mbio za marathoni za Lake Biwa .Alphonce Felix.
Wanariadha wa timu ya taifa ya riadha wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka pamoja na mshindi wa tatu wa mbio za marathoni za Lake Biwa .Alphonce Felix.
Mwanariadha wa Tanzania ,Alphonce Felix akionesha zawadi aliyopewa baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Lake Biwa Marathon ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu akitumia muda wa saa 2:O9:19.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI FEBRUARI, 2016 WAPUNGUA KWA ASILIMIA

March 09, 2016

 Mkurugenzi wa Takwimu za Sensa na Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Februari, 2016. Kulia ni Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Mwanahabari wa Kituo cha Channel Ten, Bi Faudhia akiwa kazini kuchukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakiwa kazini.

Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei katika Februari mwaka huu umepungua  mpaka kufikia asilimia 5.6  kutoka asilimia 6.5 ya  mwezi Januari.

Akizungumza  katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mkurugezi wa Sensa za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kasi ya upunguaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisiyakula kwa kipindi kilichoishia  cha Februlia, 20 ikilinganishwa na bei za Februari mwaka 2015.


Alisema kuwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Februari mwaka huu umepungua kwa  asilimia 10.3, mafuta ya dezeli kwa asilimia 4.5  na matunda kwa asilimia 7.2.

Kwesigabo alisema pamoja na kupungua kwa  kasi  ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kuna baadhi ya bidhaa zinaonyesha  kuongezeka  katika hicho  ni pamoja na Sukari kwa asilimia 7.1, Mkaa asilimia 4.3, Mchele kwa asilimia 22.9 na viazi 16.3.


Aidha alisema hali ya mfumuko wa bei katika nchi za jilani unaelekea kufanana na nchi za afrika  mashariki ambapo Kenya umepungua hadi asilimia 6.84 kutoka  asilimi7.78 mwaka huu, Uganda umeongezeka kwa asilimia 7.7 kutoka  asilimia  7.6 kwa mwezi  Januari mwaka huu.

Wananchi wa Bagamoyo-Bayport

March 09, 2016
By Kambi Mbwana
Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, akizungumza na waandishi wa Habari walipotembelea mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na taasisi yao, katika eneo la Kimara Ng'ombe, Bagamoyo, mkoani Pwani jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu, Bagamoyo

Bagamoyo wapokea vizuri mradi wa viwanja vya Bayport

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
WAKAZI na wananchi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamepokea vizuri mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wakisema kuwa mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuupanua na kuuweka mji wao katika kiwango cha juu kimaendeleo.

Meneja wa Bayport Financial Services wilayani Bagamoyo Francis Ndunguru akionyesha alama za viwanja vilivyopimwa katika eneo la mradi wa Kimara Ng'ombe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinauzwa kwa mkopo kwa watu wote wenye kuhitaji kumiliki ardhi.

Kwa mjini Bagamoyo, mradi huo wa viwanja vya Bayport unapatikana Kimara NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha, Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.
Meneja akionyesha barabara zilivyochongwa kuonyesha ubora wa mradi huo wa Bagamoyo, mkoani Pwani.
Mwandishi wa habari Phillip Daud, akimhoji mwananchi wa Bagamoyo, Mwanaisha Khalfany juu ya ubora wa viwanja hivyo na uwezekano wa Watanzania hususan wakazi wa Bagamoyo kuvichangakia viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati.

Akizungumza na mtandao huu, mkazi wa Bagamoyo, Said Juma, alisema kwamba huduma za viwanja vya Bayport vinavyopatikana kwa fedha taslimu na mikopo si vya kukosa, kwa sababu zitachangia kuuweka mji wa Bagamoyo kwenye kiwango cha juu pamoja na kujibu malalamiko ya wananchi kushindwa kumiliki viwanja kwa njia rahisi na isiyokuwa na gharama kubwa.

“Uwezekano wa kumiliki viwanja Bagamoyo mjini ni mgumu kwa sababu vinauzwa bei ghari, hivyo kwa Bayport kuanzisha huduma hizi kwa watu wote bila kusahau sisi wajasiriamali, hakika ni jambo la kushukuru na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri yenye kutuendeleza sisi wananchi na wateja wao,” alisema Juma na kuwataka watu wa Bagamoyo na Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo.

Mwananchi mwingine aliyekutwa kwenye mradi huo, Bi Mwanaisha Khalfany Sultan, alisema kwa kuanzisha mradi huo wa viwanja mji wao wa Bagamoyo utapanuka na kuongeza idadi ya watu wilayani humo.

“Tunafurahia kwa kiasi kikubwa mno kupata mradi huu wa mikopo ya viwanja vya Bayport tukiamini mji wetu utapiga hatua kubwa, hivyo tunawaomba kila mwenye uwezo wake na hitaji la kujenga achangamkie fursa hii muhimu kwa Watanzania wote, ukizingatia kuwa rasilimali ya ardhi ni muhimu na imekuwa ikiongezeka thamani kwa haraka nchini kote, huku katika eneo la mradi wa Kimara Ng’ombe mahitaji ya maji, umeme na barabara yakipatikana kwa urahisi,” alisema Mwanaisha.

Naye mwananchi Patrick Mwilongo, aligusia ubora wa mradi wa viwanja vya Kimara Ng’ombe akisema kuwa utakuwa umejibu swali na malalamiko ya wanasiasa waliokuwa hawataki Bagamoyo iingie kwenye Mamlaka ya Mji mdogo kwa madai kuwa mji utakuwa mdogo, ukizingatia kuwa endapo eneo hilo litajengwa mji huo utakuwa mkubwa na utapiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Ni miongoni mwa wadau muhimu wa hapa Bagamoyo ambao hakika tumeendelea kuthamani mradi huu kwa sababu utakuwa na tija kwetu sote, hivyo ni wazi tunapaswa kujitokeza kupata viwanja hivi ili tujenge kwa sababu uwezo wa kununua kiwanja kwa fedha taslimu kwa baadhi yetu ni mgumu, ukizingatia kwa masharti nafuu unaweza kupata kiwanja kwa kukopeshwa na Bayport.


Naye Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, alisema kwamba lengo ni kusudio lao kuu kuona mji wa Bagamoyo unakuwa na wananchi wanamiliki viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi, hivyo ni budi kutembelea kwenye tawi lao la MJini Bagamoyo pamoja na matawi yote Tanzania ili kupata viwanja hivyo kwa ajili ya kuweka makazi ya kifamilia, kibiashara na mengineyo.

“Tunawaomba Watanzania wote popote walipo kutembelea ofisi zetu au mawakala wetu walionea nchi nzima ili wapate fursa ya kukopa viwanja hivi kwa mji wa Bagamoyo au vilivyopo kwenye maeneo mengine ya Tanzania, tukiamini Bayport imeendelea kuwa mkombozi wa watu wote kwa kumiliki kiwanja kwa utaratibu rahisi,” alisema Ndunguru, Meneja wa Bayport Bagamoyo.

Mita Moja ya mraba kwa viwanja vya Bagamoyo inapatikana kwa Sh 10,000, Kigamboni (Tundi Songani) Sh 10,000, Kibaha (Boko Timiza) Sh 9000, Kilwa (Msakasa) Sh 2000, Morogoro (Kiegea B) Sh 3500, Chalinze (Kibiki na Mpera) Sh 4500 tu, huku utaratibu wa kuweza kupata viwanja hivyo ukiwa rahisi kwa Watanzania wote, wakiwamo waaajiriwa wa serikali, waajiriwa binafsi na wajasiriamali.