AWADH MASSAWE ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA TPA

October 18, 2015
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Rais Dkt. Jakaya Kikwete amemteua Bw. Awadh Massawe (pichani kushoto)kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa tukio la kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayosemekana kuwa kubwa katika ukanda huu wa Afrika mara itakapomalizika.

Akihutubia wakati wa tukio hilo, Dkt. Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Bw. Massawe afuatilie tu barua yake rasmi ya uteuzi.

“Mimi nilishalimaliza hilo, fuatilia tu barua yako ya ajira,” alisema Rais huku akishangiliwa na umati.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Massawe amekuwa akifanya kazi kama Kaimu katika nafasi hiyo tangu mwezi wa Pili mwaka huu na kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. 

Pia kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja Bandari ya Dar es Salaa.

Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.

Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamis ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya  kuboresha ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.

Pia mwisho wa mwezi wa Sita mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka, Zambia.

Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao katika bandari ya Dar es Salaam.

Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kugharimu dola bilioni 10, kutaongeza uwezo wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12 za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua 1,500.

Bandari hiyo mpya inatarajiwa kuhudumia tani 600,000 za mizigo na makasha 1,000 kwa mwaka na kuajiri watu 1,000.

Awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha gati nne ambapo mbili kati ya hizo zitatumika kwa huduma ya makasha pekee, moja kwa ajili ya mizigo mingine.

Tayari TPA iko katika hatua za mwisho kabisa kulipa fidia kwa wanavijiji zaidi ya 2,000 walioachia ardhi yao kupisha mradi huo.

Mradi huo utatekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu za serikali ya Tanzania, China Merchants Holdings International (CMHI) ya China na State Government Reserve Fund (SGRF) ya Oman.

WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAMUAGA RAIS KIKWETE

October 18, 2015


Picha zote za juu zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha cha Mikutano cha Julius Nyerere ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya hafla ya kumuaga Mhe. Rais.
Rais Kikwete akifunua kitambaa ambapo nyuma yake kuna picha ya Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje linalokusudiwa kuanza kujengwa hivi karibuni. Rais Kikwete alifunua kitambaa hicho kuashiria kuanza ujenzi wa jengo hilo.
Rais Kikwete akipiga makofi kuonesha furaha yake kuwa Wizara ya Mambo ya Nje itapata ofisi za kisasa hivi karibuni
Rais Kikwete akiongozwa kuelekea ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya kufanya hafla ya kumuaga. Wanaomuongoza ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa kulia kwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akitoa neno la kuwakaribisha wageni waalikwa akiwemo Rais Kikwete katika hafla ya kumuaga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akitoa utambulisho wa wageni waalikwa wakiwemoWaheshimiwa Mabalozi waliostaafu.
Balozi Mstaafu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa
Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara/Vitengo, Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa wameketi kwa ajili ya kushuhudia matukio ya hafla ya kumuaga Rais Kikwete.
Sehemu ya watumishi wa Wizara waliohudhuria hafla ya kumuaga Rais Kikwete
Watumishi wa Wizara katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete
Mtumishi wa Wizara akisoma utenzi wa kumsifu na kumpongeza Rais Kikwete namna alivyoongoza Taifa la Tanzania kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 10 ambacho kinakamilika Oktoba 2015.
Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K.Membe akisoma hotuba yake katika hafla hiyo. Hotuba ya Waziri Membe iligusia mafaniki ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata katika kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wakubwa, kuongeza uwakilishi nje ya nchi,kujenga ofisi za kibalozi na utatuzi wa migogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Membe wakionesha Tuzo aliyotunukiwa Rais Kikwte na Wizara ya Mambo ya Nje.
Picha za juu zinaonesha zawadi mbalimbali ambazo Rais Kikwete amekabidhiwa wakati wa hafla hiyo
Rais Kikwete akiongea na watumishi wa Wizara na wageni waalikwa. Katika mazungumzo yake Rais Kikwete alisisitiza umuhimu wa watumishi wa Wizara kudumuisha na kuimarisha mahusiano mazuri na nchi zote duniani. Alisema katika kipindi cha uongozi wake mafanikio makubwa ya kidiplomasia yamepatikana hivyo ni vyema watumishi wa Wizara wakayaendeleza kwa kiwango cha juu zaidi.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Waziri Membe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Wakuu wa Idara/Vitengo na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi

Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu

WATOTO BADO WANAENDELEA KUDHULUMIWA UTOTO WAO- UMOJA WA MATAIFA

October 18, 2015

 Picha hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake,  pamoja na kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji  wenye hadhi. Pamoja na  Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya kupinga watoto  kutumika kama askari, bado  taarifa za hivi karibu za Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika baadhi ya maeneo kama askari,  huku wengine wakiingizwa katika  biashara haramu  zikiwamo za ngono.
 Vickness Mayao kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na  Watoto,  akichangia majadiliano kuhusu haki za mtoto wakati wa Mkutano wa   Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati iliyokuwa ikijadili kuhusu   haki za mtoto ambapo  akizungumza kwa  Niaba ya Serikali   Bi. Mayao amesema Serikali  inaendelea na uboreshwaji wa Sheria mbalimbali zinazolinda haki ya Mtoto  huku  ikisisitiza kwamba wajibu wa kwanza wa kumlinda mtoto  dhidi ya  madhara yoyote  ni ya Wazazi wenyewe.  aliyekaa nyuma ni Afisa mwingine kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na Watoto Bi. Grace Mbwilo
 .Pamoja na  kufanyika kwa  mikutano ya Kamati ya Tatu ya Baraza  Kuu la  Umoja wa Mataifa,  Mikutano  ya Kamati nyingine zikiwamo ya Pili inayohusika na masuala ya  Uchumi na Maendeleo pia imekuwa ikiendelea na vikao vyake. Pichani (katikati)ni Bw. Ahmed Makame Haji Kamishna wa  Tume ya  Mipango kutoka Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar akiwa katika  moja wa Mikutano ya Kamati ya   Uchumi na Maendeleo  wapo  pia Bi. Halima Wagao kutoka Wizara ya Fedha ( ZNZ na Bi. Mtumwa Idrissa kutoka  Tume ya Mipango ( ZNZ)
 Bw. Suleiman Said Ali. Afisa  Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala ya  misaada  ya  ulipuaji wa mabomu ya  Ardhini,  Bw.  Ali pia alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa  Makoloni 17 ambayo bado  hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia  mambo yake yenyenyewe likiwamo  Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani Afrika.

MAALIM SEIF BUBUBU

October 18, 2015

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kwageji Bububu, Maalim Seif amesema atarekebisha mfumo wa ushuru katika bandari ili kuepusha wafanyabiashara kulipa ushuru mara mbili wanaposafirisha mizigo yao kuelekea bandari ya Dar es Salaam.

Amesema hali hiyo imekuwa ikiwadhoofisha wafanyabiashara wa Zanzibar, jambo amesema ataliwekea utaratibu mzuri, ili wafanyabiashara waweze kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu.

Akizungumzia wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo wale wa Jua kali, Maalim Seif amesema atawaekea mazingira mazuri kuweza kufanya shuguli zao.

Amesema chini ya uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawanyanyaswi, na watawekewa maeneo maalum ya kufanya biashara zao, na kwamba hakutokuwa na ulipaji wa kodi zisizotambulika katika maeneo yao.

Aidha ameahidi kuanzisha benki ya uwekezaji, ili kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

Nae afisa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, amewataka wanachama hao kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia wasioweza kupiga kura wakiwemo wagonjwa, wazee na wenye ulemavu,  ili kila aliyejiandikisha aweze kupiga kura kwa mgombea anayemtaka.

Aidha amewataka kuelimishana juu ya namna ya upigaji kura, ili kuepuka uharibifu wa kura na kupiga kura kwa usahihi.

 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika viwanja vya Kwageji Bububu.
  Wafuasi wa CUF wakisikiliza na kushangilia hotuba ya mgombea Urais wa Chama hicho katika viwanja vya Kwageji Bububu.
 Imail Jussa Ladhu, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF, akihutubia kwenye mkutano huo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

NIMESTUKA WAWASTUA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA

October 18, 2015

Masnii, Ray Kigosina akiwasalimia wakazi wa mwanza.
Timu nzima nimestuka ni
Kundi la wasanii wanaomuunga mkono Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli. wakiwastua wakazi wa  Mwanza.
MGOMBEA UWAKILISHI JIMBO LA TUNGUU, MBUNGE NA MADIWANI WAENDA KIJIJI KWAO SIMAI MUHAMMED UZI MTONGANI KUOMBA KURA.

MGOMBEA UWAKILISHI JIMBO LA TUNGUU, MBUNGE NA MADIWANI WAENDA KIJIJI KWAO SIMAI MUHAMMED UZI MTONGANI KUOMBA KURA.

October 18, 2015

1
Mwenyekiti wa CCM wadi ya Tunguu Omar Azan Jecha akiwasalimi wananchi wa wadi ya Bungi waliofika kwenye Mkutano wa kuwanadi wagombea wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano uliofanyika kiwanja cha mpira cha Uzi Mtongani Mkoa wa Kusini Unguja.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

2
Mgombea uwakilishi Jimbo jipya la Tunguu Simai Muhammed Said (alievaa miwani waliokaa chini) akiwa na wananchi wa kijijini kwao Uzi wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wadi ya Tunguu Omar Azan Jecha (hayupo pichani) alipokuwa akiwatambulisha wageni waliofika kwenye Mkutano huo.
3 4
Mgeni rasmin Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Zanzibar anaemaliza muda wake Mhe. Ramadhan Shaaban akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo jipya la Tunguu Khalifa Salum Suleiman wakati wa Mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa mpira wa Uzi Mtongani jana Oct 17.
5
Mgombea uwakilishi Jimbo jipya la Tunguu Simai Muhammed Said akiwasalimia wananchi waliofika kwenye Mkutano uliofanyika kijijini kwao Uzi.
7

Mgeni rasmin Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Zanzibar anaemaliza muda wake Mhe. Ramadhan Shaaban akimnadi mgombea udiwani wa wadi ya Bungi Said Mtaji (Askari) katika Mkuno wa kampeni uliofanyika uwanja wa mpira wa Uzi Mtongani Mkoa Kusini Unguja.

6
Mgeni rasmin kwenye Mkutano huo Mhe. Ramadhan Shaaban akinadi mgombea uwakilishi Jimbo jipya la Tunguu kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Simai Muhammed Said wakati wa Mkutano wa wadi ya Bungi uliofanyika Uzi Mtongani Mkoa Kusini Unguja.