NDEGE YA JESHI LA MAREKANI YAANGUKA AFGHANISTAN NA KUUA 12

NDEGE YA JESHI LA MAREKANI YAANGUKA AFGHANISTAN NA KUUA 12

October 06, 2015

Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules iliyoanguka.
Ramani inayoonesha eneo ambapo ndege hiyo ilipata ajali.
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules imeanguka usiku wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Jalalabad nchini Afghanistan na kuua watu 12.
Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus ameiambia AFP kwamba watao kati ya waliokufa walikuwa wanajeshi wa Marekani, watano walikuwa raia wa kawaida na wawili walikuwa ni Waafghan.
Msemaji wa kundi la wapiganaji la Taliban, Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara inayoonesha ndege hiyo kama ilishambuliwa.
Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.
Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste kubadilishwa mapema mwaka huu.
Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.
MWIGULU NA JANUARY MAKAMBA BUMBULI

MWIGULU NA JANUARY MAKAMBA BUMBULI

October 06, 2015

Mwigulu Nchemba na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Bumbuli Mh.January Makamba wakiwasili Kata ya Usambara kwaajili ya Mkutano wa hadhara wa kampeni .
Wajumbe wa timu ya Kampeni ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi wakiteta Jambo.
January Makamba akimsikiliza Mwananchi wake kwa Makini.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Funta.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Tamota wakati wa kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi hii leo Jimbo la Bumbuli.
January Makamba akizungumza na Wananchi wake namna alivyotekeleza ahadi zake zilizopita na anavyokwenda kusimamia ilani ya Uchaguzi kwa miaka 5 ijayo kwa wananchi wa kata ya Tamota.Moja ya jambo kubwa la kimaendeleo kwa kata ya Tamota ni kupata umeme uliofika makao makuu ya kata hiyo.,
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Mbonde hapa Bumbuli.
January Makamba For Bumbuli.
Picha na Sanga Festo Jr.

FAINALI YA BSS 2015 KUFANYIKA OKTOBA 9 MWAKA HUU JIJINI DAR ES SALAAM

October 06, 2015

 Mwandaaji  wa   Bongo Star Search, Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani)  juu ya fainali ya (BSS) itakayofanyika Ijumaa ya Oktoba 9 mwaka huu katika ukumbi wa King Solomoni Hall uliopo karibu na Nyumbani Lounge au Eaters Point  eneo la Namanga  kuanzia saa moja jioni kikao hicho kimefanyika leo Jiji Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko  wa Huawei  Samson Majwala.
 Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko  wa Huawei, Samson Majwala  akisisitiza jambo katika kikao hicho kulia ni Meneja Masoko wa Huawei  Lyadla Nangaki.
 Baadhi ya Wandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini  Mwandaaji  wa Bongo Star Search Rita Paulsen.
 Mshiriki wa (BSS  1O3) kutoka Arusha   Nassib Fonabo akionesha umahili wake wa kucharaza gita mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa (BSS) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwandaaji  wa   Bongo Star Search Rita Paulsen leo jijini Dar es Salaam

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA MKUTANO NA AKINA MAMA ZAIDI YA 300 KUPAMBA NA KIPINDUPINDU SHINYANGA

October 06, 2015


Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako wanawake/akina mama zaidi ya 300 wa manispaa ya Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa wa Shinyanga.Mkutano huo umeitishwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Akina mama hao waliojitokeza kwa wingi leo jioni Oktoba 06,2015 wameweka mikakati mbalimbali ya kutokemeza ugonjwa kipindupindu ambapo Jana pekee wagonjwa 9 wamelazwa katika kambi maalum jirani na hospital ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambapo kati ya hao 9 wawili wamefariki dunia.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mkutano wake na wanawake zaidi ya 300 katika manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema wanawake ni jeshi kubwa na ni walimu wakubwa katika familia hivyo wana nafasi kubwa ya kupambana na kipindu pindu kwa kuimarisha na kuhamasisha usafi kwa akina baba,watoto na hata wanawake wenzao.
"Kipindu pindu ni hatari sana...kinaua lazima tupambane nao kwa nguvu zote..nimewaita ili kila mmoja ajue Shinyanga tuna janga..sasa kila mtu achukue hatua,ugonjwa huu unatokana na uchafu..akina mama mna nafasi kubwa sana katika hili...."alisema Matiro.
Akina mama wakiwa wamenyoosha mikono...kwamba wako tayari kupambana na kipindupindu.....
Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwaeleza akina mama hao kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni uchafu yaani kula au kunywa kinyesi cha mtu mwingine hivyo ili kuhakikisha ugonjwa kipindu pindu ni vyema wananchi wakajenga vyoo,kuepuka kunywa maji yasiyochemshwa,kula vyakula vya moto,kuosha matunda kabla ya kula sambamba na kuepuka kunywa pombe za kienyeji.
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo alisema ugonjwa huo unazidi kuenea kwa kasi katika manispaa ya Shinyanga ambapo jana pekee wagonjwa 9 walifikishwa katika kambi maalum ya wagonjwa wa kipindu pindu jirani na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Afisa afya huyo alisema ili kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa katika manispaa ya Shinyanga tayari wamepiga marufuku tabia ya akina mama lishe na baba lishe kutembeza vyakula mtaani,unywaji pombe za kienyeji,kuzuia matanga kwenye familia yoyote iliyopatwa na kifo pamoja na kula vyakula kwenye sherehe yoyote.
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa aliwataka wakazi wa Shinyanga kufika haraka hospitali pindi wanapoona dalili za ugonjwa wa kipindupindu ikiwemo kuharisha na kutapika mfululizo.
Mkutano unaendelea
Nakuzelwa aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufunika vyoo vya shimo,kuepuka kula vyakula kwenye mikusanyiko ya watu wengi,kuacha kutembeza vyakula mtaani,kuuza vyakula shuleni,kununua mboga zinazouzwa chini badala ya kwenye meza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza juu ya matumizi ya vyoo majumbani kwani chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kipindupindu ni kunywa au kula kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuchanganyikana na vyakula ama maji anayokunywa binadamu.
Akina mama kutoka manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini ambapo walikubaliana kuimarisha usafi ili kutokomeza ugonjwa hatari wa kipindupindu
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kipindu pindu zilizotajwa ukumbini ni pamoja na kuharisha na kutapika mfululizo.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Akina mama wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa mitaa katika manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa akina mama katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga
Mmoja wa akina mama hao akichangia mawili matatu katika mkutano huo
Katika mkutano huo pia ilibainika kuwa wananchi wengi mjini Shinyanga hawana vyoo hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu
Wanawake hao pia walisisitizwa kujenga tabia ya kuwaelimisha wanaume juu ya umuhimu wa kujenga vyoo
Mkutano unaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia kuhusu amani ya nchi ambapo alisema serikali imejipanga vyema kukabiliana na watu waliojiandaa kufanya vurugu ikiwemo kuzuia wanawake na wazee wasipige kura siku ya uchaguzi mkuu nchini utakaofanyika Oktoba 25,2015.

DAWASCO YAZINDUA RASMI KAMPENI YA “MAMA TUA NDOA KICHWANI”

October 06, 2015

                 SIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limezindua rasmi kampeni yake mpya inayojulikana kama “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kampeni ambayo ni endelevu inayolenga kuboresha huduma ya Maji safi na salama maeneo yote  ya jiji la Dar es salaam, pamoja na miji yote ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, huku ikimhakikishia mwanamke kumpunguzia adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa mtendaji mkuu wa Dawaso, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni hiyo ina malengo ya kusogeza huduma ya Maji karibu kwa kuhakikisha inaongeza wigo wa huduma ya Maji safi na salama kwa kujenga vituo takribani 18 ambavyo vitakuwa vikitoa huduma ya Maji kwa wateja wake kwa muda wa saa 24 kupitia wakala wake.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhandisi huyo pia alitoa rasmi kibali cha kuuza Maji kwa watu wote wenye visima na magari makubwa (Maboza) huku akifanya usajili bure kwa wauzaji hao wa Maji na wamiliki wa visima waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hizo, aliwataka wenye matanki kuacha kuchota Maji sehemu ambazo sio rasmi kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha afya ya watumiaji wa huduma hiyo.

“Ni maarufuku kwa wenye matanki kuchota maji sehemu ambazo sio rasmi, sehemu ambazo hazijasajiliwa, ni marufuku kuuza maji bila kuwa na leseni kuanzia sasa kwani kwa kufanya hivyo mnahatarisha afya ya watumiaji wa maji hayo” alisema Luhemeja.

Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa, usajili huo utarahisisha upatikanaji wa huduma ya Maji kwa kupeleka huduma hiyo mpaka kwenye makazi ya wananchi hao huku ikiwahakikishia kupata Majisafi na salama hivyo kuondokana na magonjwa ya milipuko yakiwamo kipindupindu.
“Uzinduzi huu unalenga kupunguza usumbufu wa Maji majumbani pamoja kupunguza kuuziwa Maji machafu yanayosababisha magonjwa ya mlipuko” alisema Mhandisi Cyprian.

Kutokana na wafanya biashara hao kuchoka Maji sehemu ambazo hazieleweki, uongozi wa Dawasco umewatengea maeneo maalum ambayo watakuwa wakiyatumia kama vituo vya kuchotea maji, baadhi ya maeneo hayo ambayo yatakuwa vituo vya magari makubwa (maboza) kuchotea Maji  ni kama Kimara, mbezi, kibamba ccm, Bunju na namlandizi.

Mbali na utoaji wa leseni na usajili wa magari, wamiliki na wauzaji wa magari hayo, walitumia fursa hiyo katika kuchagua viongozi ambao watakuwa wakiwasilisha taarifa za wauzaji na wamiliki hao wa magari ya Maji kwa uongozi wa DAWASCO, huku uongozi wa Dawasco nao wakiwasilisha taarifa zake kwa wafanya biashara hao kupitia viongozi hao waliochaguliwa.

Katika uchaguzi huo Ndugu, Mayunga alichaguliwa kuwa mwenyekiti, ambapo nafasi ya ukatibu ilikwenda kwa Ndugu  Duwa Said. Pia walichaguliwa wajumbe wengine 8 ambao watakuwa wakiwawakilisha wenzao katika kikao cha kamati kuu ya wafanya biashara hao (water by tankers)
Maadhimisho ya Wiki Huduma Kwa Wateja wa Tigo Yaendelea

Maadhimisho ya Wiki Huduma Kwa Wateja wa Tigo Yaendelea

October 06, 2015

1
Msimamizi mkuu wa Duka la Tigo Nkurumah, Lulu Kikuli akimkabidhi zawadi simu Grace Joachim mkazi wa Tandale ikiwa ni sehemu maadhimisho ya wiki ya wateja wa Tigo.
7
Msimamizi mkuu wa Duka la Tigo Nkurumah, Lulu Kikuli akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa habari wa TV1 Robert Latonga.
2
Meneja wa ubora huduma kwa wateja wa Tigo Bi. Mwangaza Matotola,akiwakabidhi fulana wateja wa tigo kwenye maadhimisho ya wiki ya wateja yaliyofanyika Dula la Tigo Nkurumah.
3
 Mtaalam wa huduma kwa wateja wa Tigo Jackson Jerry (kushoto), Meneja wa Kitengo huduma kwa Wateja Tigo, Halima Kasoro (katikati) na Meneja wa ubora huduma kwa wateja wa Tigo Mwangaza Matotola (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja.
4 5
Mwandishi wa habari wa TV1 Robert Latonga akifanya mahojiano na mteja wa Tigo, Hamadi Maliwata mkazi wa Mbagala kwenye maadhimisho ya wiki ya wateja wa Tigo.
6
Wateja wakiendelea kupata huduma.
LOWASSA AHANI MSIBA WA MZEE KISUMO, KIJIJINI KWAKE USANGI, MKOANI KILIMANJARO

LOWASSA AHANI MSIBA WA MZEE KISUMO, KIJIJINI KWAKE USANGI, MKOANI KILIMANJARO

October 06, 2015

1
Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la maua katika kaburi la aliewahi kuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, alipokwenda kuhani msiba Nyumbani kwa Familia ya Kisumo, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro Oktoba 6, 2015.
3
Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema,Mh. Edward Lowassa, akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika kuhani msiba wa aliewahi kuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, alipokwenda kuhani msiba Nyumbani kwa Familia ya Kisumo, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro Oktoba 6, 2015.
4
Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema,Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Kaka wa Marehemu Mzee Peter Kisumo, Mzee Daniel Mchangila, wakati alipofika kuhani msiba wa aliewahi kuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo, alipokwenda kuhani msiba Nyumbani kwa Familia ya Kisumo, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro Oktoba 6, 2015. Kulia ni Mama Mdogo wa Marehemu Mzee Kisumo, Bi. Nashati Mbawa.
Picha na Othman Michuzi.

DK. Shein Aendelea na Mikutano yake ya Kampeni Zanzibar Akiwahutubia Wananchi wa Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini B.

October 06, 2015

Mama Fatma Karume akishuka jukwaani baada ya kuwahutubia Wananchi na Wana CCM katika viwanja vya mpira bumbwini makoba wakati wa mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, mkutano uliofanyika katika Jimbo la Bumbwini Unguja.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mama Fatma Karume baada ya kuwahutubia Wananchi na kumuombea Kura kwa Wananchi wakati wa Mkutano huo wa Kampeni katika Wilaya ya Kaskazini B uliofanyika viwanja vya mpira bumbwini makoba.
Umati wa Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mpira bumbwini makoba wakihudhuria mkutano wa mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein. 
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Salim Turky (Mr White) akiwa katika mkutano wa mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya bumbwini makoba wakimsikiliza Mgombea.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe Haji Omar Kheri akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein, katika viwanja vya bumbwini makomba na kumuombea Kura Dk Shein, ili kuendeleza amani na utilivu na Masendeleo ya Wazanzibar.
Kada wa CCM Balozi Amina Salim Ali akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein 
Baadhi ya Wagombea wa CCM wakifuatilia mkutano wa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika viwanja vya mpira bumbwini makoba.