CRDB YATANGAZA NEEMA KWA BODABODA, BAJAJI

December 20, 2023

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati wa halfa hiyo 


MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kulia akigawa riflect kwa Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Tanga katikati  ni Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji na kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kushoto akimkabidhi seti ya  sofa msindi a Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi inayoendeshwa na Benki hiyo kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat

Na Oscar Assenga, TANGA


BENKI ya CRDB imetangaza neema kwa wafanyabiashara wa bodaboda pamoja na bajaji kwamba hivi sasa hauitajiki kuwa na nyumba,gesti wala shamba kama dhamana ili kuweza kupata mkopo wa bodaboda.

Neema hiyo imetangazwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadat wakati wa halfa ya kugawa zawadi ya Sofa seti kwa mshindi katika kampeni yao ya Tisha na Tembo Kadi iliyokwenda sambamba na ugawaji wa Riflect kwa Waendesha Bodaboda”,

Alisema kwamba wanachotakiwa ni kufika kwenye tawi lolote la benki hiyo na kumueleza Meneja wamefika kuchukukua bodaboda na dhamana yao na Bajaji ni ile kadi ya hicho kifaa.

Aidha alisema kwamba wameweza kutoa mikopo hiyo ili kuwaepusha wananchi na mikopo kausha damu na wamewapelekea riba nafuu sana kutokana na ombi la mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.

“Bodaboda na waendesha bajaji wanasahauliwa sana lakini sisi kama benki ya CRDB tumeamua kuwawezesha wafanyabaishara wa bodaboda na bajaji hauitajiki kuwa na nyumba,sham,ba wale gesti “Alisema

Meneja huyo alisema kwamba benki hiyo wamejiwekea malengo ya kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi kwa kushirikiana na makundi yote ya wajasiriamali wakubwa,wa kati na wachini kabisa.

Alisema kwa sababu wanaamini kanzuri ya ijumaa inaandaliwa Alhamisi na wafanyabsiahara wakubwa wanaandaliwa tokea chini hivyo leo wanakwenda ramsi na mambo matatu ikiwa ni kutimiza agizo la RC Kindamba kushirikisha jamii ya wafanyabiashara wadogo wadogo katika suala la mitaji na biashara kwa ujumla.

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliishukuru Benki hiyo kwa kuamua kuwezesha makundi hayo huku akitoa wito kwa watakao kupata mikopo wakaitumie kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili waweze kufanya marejeshe kwa wakati.

Kindamba alisema kwamba pamoja na hayo lazima waendelee kutunza uaminifu ambao Benki ya CRDB wamewapa kwa kuhakikisha wanarejesha mkopo huo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika nao.

“Hasa wakina baba usije kupewa fedha ukaenda kuongea jiko watu wa Pwani tunajua wenyewe…fedha hiii ikatumike kwenye madhumuni yaliyokusudiwa”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya DC –aliomba wafanyabiashara ndogo ndogo na maafisa usafirishaji waweze kutumia mikopo hiyo ili kuweza kujikwamua


RC MANYARA ATAKA UHAKIKI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO HANANG' UFANYIKE KWA UWAZI

December 20, 2023

 


Na  John Walter-Babati   

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema zoezi la  kuhakiki waathiriwa wa maafa ya maporomoko ya udongo,mawe na magogo Hanang' linaendelea ili kuwathibiti wasiokuwa waaminifu wanaotaka kujinufaisha kupitia misaada inayotolewa na serikali kupitia wadau mbalimbali.

Mkuu huyo wa mkoa ameelekeza zoezi hilo lifanyike kwa uwazi kuwatambua walioathiriwa na maafa hayo yaliyotokea Desemba 3 mwaka huu.

Sendiga amesema kuwa ofisi za  kata zitakuwa vituo vya kutolea misaada na kuwaelekeza  waathiriwa wa maafa ambao hawajaorodheshwa  kama waathirika wanaohitaji kuendelea kupatiwa misaada, kufika katika ofisi hizo  kujiandikisha.

Katika hatua nyingine matumaini ya maisha ya awali  kwa wananchi wa wilaya ya  Hanang'  yamerejea  huduma mbalimbali kama maji zimerejea ambapo mkuu wa mkoa anasema serikali inaendelea kurejesha huduma katika maeneo ambayo bado huduma hizi hazipo.

Kwa upande wa miundombinu, Sendega amethibitisha ujenzi wa soko   jipya  kwani  eneo la mwanzo  katika soko la  zamani limebainika kuwa katika mkondo wa maji.

"Tunajenga soko lingine kwa sababu lile soko lililopo pale pameonekana ndio mkondo mkubwa wa maji unapita, maji yameshatengeneza njia  pale yawezekana yakarudi tena  kesho  au keshokutwa, kwa hiyo tumeanza sasa hivi miundombinu ya utengenezaji wa  soko lingine  ambalo tuna imani ndani ya muda mfupi litakuwa tayari na wananchi watarudi kuendelea  kufanya shughuli zao" amema mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga.

RAIS SAMIA AMTUA MAMA NDOO KICHWANI LUDEWA KWA VITENDO

December 20, 2023

 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kimkakati ya ukaguzi wa Miradi ya Maji Wilayani Ludewa.

Akitembelea miradi mbalimbali DC Victoria amesema kuwa Lengo la ziara hii ni kuhakikisha kuwa Wana-Ludewa wanapata huduma ya Maji bora, safi, salama na yenye kutosheleza Sambamba na kuonesha kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Maji Ludewa.

Aidha, katika ziara hiyo imethibitika kuwa Wilaya ya Ludewa inaendelea kutekeleza miradi saba (7) ya maji yenye gharama ya Tsh. 13,866,290,252.86

Kukamilika kwa miradi hii kunalenga kuongeza huduma ya maji kutoka asimia 74.3% hadi asilimia 79.7 eneo la vijijini na asimia 100% kwa wakazi wa mji wa Ludewa.

Pia; amepokea Taarifa za miradi Wilaya nzima na kutembelea Miradi iliyopo Kata za- Mavanga, Ludewa, Iwela, na Manda katika kukagua hali ya upatikanaji wa maji na hali za miradi. 

Sambamba na hapo- ametembelea Vyanzo vya maji vya Mavanga, sambamba na kumkagua mkandarasi anayelaza mabomba eneo la Nyamapinda, na kutembelea ujenzi wa ofisi ya vyombo vya usimamizi wa watumia maji ngazi ya jamii CBWSO- na kukagua vituo vya ugawaji wa maji kwenye jamii. Pia amekagua zoezi la uchimbaji visima linaloendelea kata ya Manda. 

Katika hatua nyingine, DC Mwanziva amesitiza juu ya adhma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya kumtua mama ndoo kichwani, ameasa uelimishwaji wa jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ili vinufaishe vizazi vijavyo- sambamba na kutunza miundombinu yote ya maji.

Mwisho, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amesisitiza wakandarasi waliopewa dhamana za kutekeleza miradi ya Maji Wilaya ya Ludewa kufanya kazi kwa ufanisi, ubora na kwenda na wakati ili kukamilisha miradi husika. 

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratius- Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Ludewa. 

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ludewa Eng. Jeremiah Maduhu. 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Ludewa Eng. Enock Ngoyinde.







POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

December 20, 2023

 Na Abel Paul,Jeshi la Polisi-Arusha.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wamefanya ukaguzi wa kushtukiza ili kubaini kama wananchi wanalipa nauli halali zilizotangazwa na Serikali mapema mwezi huu ambapo wamebaini baadhi ya wamiliki na mawakala wa mabasi kuwapandishia nauli wananchi huku mamlaka hiyo ikiwapiga faini kwa kosa la kuzidisha nauli hizo.

Akiongea katika ukaguzi wa nauli hizo mapema leo katika kituo cha mabasi yaendayo Mikoani na nchi Jirani Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema wapo katika ukaguzi wa nauli kutokana na malalamiko ya wananchi kupitia simu na mitandaoo ya kijamii kuhusiana na kupanda kwa nauli.

Ameongeza kuwa kwa sasa ukataji tiketi ni kwa mfumo wa kielektroniki ambapo amesema kuna mifumo mipya inayorahisisha kuangalia bei elekezi ya serikali huku akiwaomba abiria kutumia mifumo hiyo ili kutokuumizwa na nauli kandamizi ambazo zinatozwa na  baadhi ya mawakala na wamiliki wasio waaminifu.

Kwa upande wake Afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA Mkoa wa Arusha Bw. Joseph Michael amesema kuwa wamefanya ukaguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuangalia utekelezaji wa masharti ya leseni za latra kwa mujibu wa usafirishaji huku akitoa onyo kwa wamiliki na mawakala kutokata tiketi bila kutumia mfumo wa kieletroniki.

Nae Bw. Joseph Peter ambaye ni abiria licha ya kupongeza Jeshi la Polisi na mamlaka hiyo  amesema kuwa wao wamekuwa wakikata tiketi za mkono bila kufahamu madhara huku akiwaomba kutooa elimu zaidi ili kupunguza changamoto wanayoipata katika kukata tiketi ambazo zipo katika mfumo wa kimtandao.




SERIKALI INATAMBUA MCHANGO MKUBWA WA SKAUTI TANZANIA-RAIS DKT. MWINYI

December 20, 2023


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili zinatambua mchango mkubwa wa Chama cha Skauti Tanzania kwa namna wanavyojinasibisha na Serikali kwa kufanya mambo makubwa na mazuri katika jamii hususan katika kundi kubwa la vijana.

Ameyasema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzani uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar.

Amesema kuwa Chama cha Skauti kinafanya kazi kubwa ya kuwajengea uwezo vijana kuweza kujitambua kuwa na maadili mema na kuwakuza kiuzalendo ili kutengeneza Taifa ambalo litaendelea kuwa na viongozi bora ambao watasukuma mbele maendeleo ya Taifa.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa Viongozi wa Serikali zote mbili wanaridhishwa na Chama cha Skauti kwani ni chama pekee ambacho ni tofauti na Asasi nyengine hapa nchini kwa kulea vijana kwa kuzingatia misingi, kanuni na taratibu maalumu kupitia elimu isiyo rasmi inayozingatia tunu za kizalendo na maadili yanayoendana na Taifa letu.

Aidha Rais Dkt Mwinyi amekitaka Chama Cha Skauti Tanzania kuendelea kuwasimamia vijana kwa kuwapa elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamiii kwa kuitumia katika kujielimisha ili kukuza uwelewano kwani matumizi mabaya ya mitandao yanaweza kupelekea kushindwa kufikia malengo katika maisha yao ya baadae.

Sambamba na hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhakikisha Skuli na Vyuo vinakuwa na Skauti na Walimu wanaopewa mafunzo bora ya kuendesha uskauti katika maeneo yao.

Dkt. Mwinyi ametowa wito kwa Viongozi wa Skauti nchini kuzingatia utekelezaji wa Sera ya Usalama dhidi ya madhara ya ya unyanyasaji (Safe From Harm Policy) na kuhakikisha vipengele vitakavyoingzwa katika katiba ya Skauti vinaendana na matakwa ya Sera hiyo ili kuendana na agizo lililotolewa katika Mkutano Mkuu wa Skauti Duniani uliofanyika mwaka 2021ambao ulisisitiza utekelezwaji wa Sera hiyo.

Nae Raisi wa chama cha Skauti Tanzania ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Mhe. Profesa Adolf Mkenda amesema miongoni mwa Taasisi muhimu nchini ni Skauti taasisis ambayo inafanya kazi ya kuwalea vijana katika malezi yaliyo bora, kuwaweka pamoja katika kufanya maamuzi pamoja na kuwafundisha uzalendo wa kulitumikia Taifa lao.

Mhe. Mkenda amesema Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania utatoa fursa ya kufanya mchakato wa upatikanaji wa katiba ambayo ndio muhimili Mkuu wa chama hicho itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili sambamba na kusimamia malengo ya maendeleo ya Skauti Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ambae pia ni makamo wa Rais wa Skauti Tanzania Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema uwamuzi wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Skauti hapa Zanzibar sio tu kudumisha Muungano bali ni utayari wa kuwasaidi Viongozi wakuu wa nchi katika kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa baadae.

Amesema kuwa ni dhahiri faida ya uwepo wa Skauti nchini inaonekana kwani vijana wanaopitia katika chama hicho wanalelewa katika maadili mema ambayo yanawasaidia katika jamii na katika Ujenzi wa Taifa letu.

Mapema Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg Rashid Kassim Chapa amesema chama cha skaut ni hazina kubwa ambayo ni chimbuko kuu la viongozi wengi wenye uzalendo na nchi yao.

Amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya Chama cha Skauti Tanzania lakini bado kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa maeneo ya makambi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo Skauti na uhaba wa Ofisi za kufanyia kazi kwa ngazi za Mikoa na Wilaya.

Mkutano huo Mkuu wa siku Moja (1) wa Chama cha Skauti utajikita katika kuangalia mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya Skauti, utunzaji wa mazingira na utawala bora kwa kuweka mikakati imara itakayosaidia kuboresha Uskauti Tanzania.

TUME YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

December 20, 2023

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Desemba 19, 2023 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Bw. Ramadhani Kailima akizungumza wakati wa kikao hicho cha Baraza.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi NEC, Livini Avith akizungumza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiimba wimbo wa wafanyakazi pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Bw. Ramadhani Kailima (wa pili kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi NEC, Livini Avith wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano huo.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano huo.


Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano huo.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Barza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mara baada ya Naibi Waziri kifungua Baraza la Wafanyakazi wa Tume 19 Desemba, 2023 jijini Dodoma.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepongezwa kwa maandalizi mazuri ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Tume leo tarehe 19 Desemba, 2023 jijini Dodoma.

“Hongereni sana kwa kuendesha vizuri zoezi la uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mlilolifanya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023. Tumeona mmejipanga na mpo tayari kwa uboreshaji,” amesema Mhe. Nderiananga ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Baraza hilo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi,Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ambayepia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima alilijulisha Baraza hilo kwamba uboreshaji wa majaribio umefanyika kwa mafanikio.

Bw. Kailima amesema katika uboreshaji huo wa majaribio, Tume ilifanikiwa kupima uwezo wa vifaa na teknlojia ya uboreshaji ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la zoezi hilo.

“Tumefanikiwa kupima uwezo wa vifaa na teknolojia japo hatukupata watu waliotumia mfumo wa kujiandikisha kwa njia ya mtandao. Changamoto tumezigundua na tunazifanyia kazi kwa ajili ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari,” amesema Bw. Kailima.

Tume ilifanya uboreshaji wa majaribio kwenye Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, mkoani Mara na Kata ya Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora kwa siku saba kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Katika hatua nyingine, Mhe. Nderiananga amewaasa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana, kuepuka mambo ya utovu wa nidhamu na kudumisha utamaduni wa kujengeana uwezo wa kiutendaji.

“Mnayo nafasi kubwa katika kuwahamasisha watumishi wenzenu ili waweze kuwa na ufanisi kazini, ufanisi huo utatokana na ushirikiano mzuri kati ya watumishi na viongozi,” amesema.

Mhe. Nderiananga amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea kuitisha mabaraza ya wafanyakazi kwa kuwa ni jambo la kisheria na linalolenga kuweka mazingira mazuri na ustawi wa wafanyakazi.
TASAF YAJENGA NYUMBA YA MADAKTARI ZAHANATI YA RAMADHAN MKOANI NJOMBE

TASAF YAJENGA NYUMBA YA MADAKTARI ZAHANATI YA RAMADHAN MKOANI NJOMBE

December 20, 2023




Timu ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiongozwa na Mtaalam wa Mawasiliano Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Bi. Zuhura Mdungi wakikagua ujenzi wa nyumba ya watumishi iliyojengwa na TASAF katika Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan Halmashauri ya Mjombe mkoani Mjombe wakati wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko huko mkoani humo.

Ukaguzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan mjini Njombe ukiendelea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa nyumba ya watumishi wa zahanati katika mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bashir Nyapini Sanga akizungumza kuhusu mradi huo.

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari akifafanua jambo mbele ya Wahariri waliotembelea mradi huo.
- Advertisement -



NA JOHN BUKUKU NJOMBE.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa nyumba ya watumishi na zahanati katika mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bashir Nyapini Sanga ameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo has a nyumba ya watumishi ambayo itaanza kutumika hivi karibuni.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi ya TASAF mkoni mkoani Mjombe amesema kukamilika kwa nyumba hiyo ya watumishi kutasaidia kupunguza changamoto wanazozipata wagonjwa hasa wanapoumwa wakati wa usiku wakiwemo wakimama wajawazito pindi wanapotaka kujifungua.

“Kukamilika kwa nyumba ya mganga itawasaidia mama zetu wanapokuja hapa kituoni kupata huduma stahiki na kwa wakati lakini pia itaondoa kero ambayo anaipata mganga kukaa mbali na kituo kunakopelekea kuamshwa usiku kutoka alipo mpaka hapa kituoni ambapo kunaumbali”amesema.

Aidha amesema kuwa TASAF iliingiza fedha kiasi cha shilingi milioni 66,591,375.89 kwa ajili ya kusapoti mradi huo lakini haikutosha hali iliyopelekea kuongezewa tena fedha kiasi cha shilingi milion 15.

“Mradi huu mpaka ninavyozungumza umegharimu kiasi cha shilingi milioni 81,591,375 ambapo mpaka sasa imetumika shilingi milioni 78,716500 lakini kwenye mradi huu nguvu kazi ya umma ambayo kukiithaminisha na fedha gharama yake inakua milion 8,76,000 “amesema

Akizungumzia changamoto amesema mpaka kufika hapo ulipofika hakuna changamoto kubwa waliyokutana nayo ambayo imeshindwa kutatuliwa na kamati kwa kushirikiana na serikali ya mtaa.

“Changamoto kubwa tuliyokutana nayo ni kusita sita kwa wazabuni kufanya kazi kwa madai ya kucheleweshewa fedha na kutokana na utaratibu wa malipo ya serikali “amesema.

Kwa upande wa mganga mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari amesema ujenzi wa nyumba za wahudumu wa afya utawasaidia kutoa huduma za dharura hasa kwa wakinamama wajawazito ambao wanafika kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma.

“Asilimia kubwa ya wajawazito uchungu unaanza jioni lakini kutokana na changamoto tuliyonayo hapa watumishi tulikuwa hatuishi karibu na zahanati lakini pia zahanati haina uwezo wa kulazza wagonjwa zaidi ya kupumzishwa kwa saa12 lakini tutakapo kua tunakaa hapa tutapata nafasi nzuri ya kuwahudumia wananchi”amesema.

Sambamba na hayo Dkt. Rehema ameiomba TASAF kusaidia kukamilisha ujenzi jengo la mama na mtoto ili kuzuia kero inayotokana na kukosa chumba cha kutosha cha kuwasaidia wajawazito ambapo sasa hivi chumba ni kidogo kinachoweza kumsaidia mjamzito mmoja tu ambapo kwa muda wa mwezi mmoja wanawazalisha akinamama 10 ambao wanaenda kujifungua katika zahanati hiyo.

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari akimpima presha mhariri kutoka ETV na EFM Bi. Scholastica Mazula katika Zahanati hiyo ambayo pia imejengwa na TASAF.

Wahariri wakipata maelezo wakati walipokagua nyumba ya watumishi ya Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan.

Muonekano wa nyumba mpya ya watumishi ya Zahanati ya Mtaa Ramadha mjini Njombe.



Hili ndiyo jengo la Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan mjini Njombe. 

NAIBU WAZIRI MWINJUMA ATOA MAAGIZO TAMRISO

December 20, 2023

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' ametoa maagizo matatu kwa Kampuni ya kukusanya na kugawa mirabaha (Tamriso).

Maagizo hayo ni kutoa elimu kwa wasanii wa muziki, wakusanyaji na wanaokusanyiwa mirabaha kabla ya kuanza zoezi la ukusanyaji mirabaha January 14 mwakani.

Akizungumza Leo Disemba 19,2023 alipofanya ziara katika ofisi ya Tamriso Mikocheni Jijini Dar es Salaam,amesema kabla ya ugawaji wa mirabaha elimu inatakiwa kutolewa kwa watu hao wawili, waweze kufahamu na kuepuka malalamiko.

Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo wameziwasilisha kwake na ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara.

"Ziara yangu katika ofisi ya Tamriso kwa lengo kujadiliana namna kazi ya kusanyaji wa mirabaha."

Amefafanua kuwa muda si mrefu wasanii wataenda kunufaika kutokana na kazi zao.

Mwenyekiti wa Tamriso, Jane Gonsalves amesema watahakikisha wanazingatia maagizo waliyopewa na Naibu Waziri kwa lengo kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mirabaha.

"Utoaji wa elimu kwa wasanii, wakusanyaji wa mirabaha na wanaokusanyiwa utafanyika na utakuwa utakuwa endelevu kufanyika.''

KAMATI YA PIC YAITAKA TANESCO NA TRC KULINDA MIUNDOMBINU YA TRENI YA KISASA (SGR)

December 20, 2023


Na Zuena Msuya, DSM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeliagiza Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Shirika la Reli Nchini (TRC), kutunza Miundombinu ya mradi wa Treni ya Kisasa kwa serikali imetoa fedha nyinyi kutekeleza mradi huo na wao ndiyo wenye dhamana ya kuuendesha na kuusimamia mradi huo.

Kauli hiyo imetolewa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Augustine Vuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua chanzo cha umeme wa Gesi Asilia utakaotumika kuendesha treni hiyo ya kisasa katika eneo la kinyerezi, tarehe 19 Desemba, 2023, mkoani Dar es Salaam.

Vuma amesema TANESCO na TRC wahakikishe kuwa wanatunza na kulinda mradi huo kwa namna tofauti tofauti ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakuwa endelevu na kuleta tija ilikuyokusudiwa na kwamba Kamati haitegemei kusikia wala kuona miundombinu hiyo inaharibika kwa sababu ya uzembe.

“Wakati Mradi huu unaanza ulikuwa kama ni ndoto, lakini sasa ndoto hiyo imekamilika na mradi huo uko tayari kwa ajili ya matumizi, Kamati imeona nia ya dhati ya Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukamilisha miradi mikubwa ambayo iko katika Taifa letu, na imeona nia yake ya dhati ya kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kwa sababu uwekezaji mkubwa katika miradi hii ya uchukuzi ni dhahiri kwamba itawakomboa watanzania kwa kuzingatia usafiri wa Treni ni wa gharama nafuu ukilinganishwa na njia nyingine za usafirishaji hivyo kunyanyua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa kwa ujumla”, alisisitiza Mhe. Vuma.

Naye Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wameshukuru kamati hiyo kufika katika eneo la mradi na kwamba wamepokea maelekezo yaliotolewa kuwa kutunza miundombinu kwa kuwa Serikali imetoa fedha nyingi sana kuwekeza katika miundombinu hiyo.

Amesema TANESCO watashirikiana na TRC kuhakikisha miundombinu hiyo inatunzwa na kutumia wataalamu wa ndani ambao wamepatiwa mafunzo maalum kutunza miundombinu hiyo kwa weledi mkubwa ili kuwanufaisha watanzania.

Pia amewataka Watanzania ambao wanaishi pembezoni mwa mradi huo kuendelea kulinda na kuitunza miundombinu hiyo kwa kuzingatia uzio uliowekwa na pia kupita maeneo mahsusi yalioruhusiwa kwa ajili ya usalama wao.

Katika mradi huo kumewekwa utaratibu mzuri wa kuwawezesha Wananchi kupita katika vivuko maalumu ili kuwaruhusu kuendelea na Maisha yao mengine ya kila siku.

Amewahakikishia Watanzania kuwa umeme utakaotumika katika mradi huo ni wa uhakika kutokana na miundombinu thabiti iliyowekwa maalumu kwa ajili ya mradi huo.

“Niwatoe hofu na wasiwasi Watanzania kuwa umeme utakaotumika katika mradi huo utatoka katika vyanzo viwili ambavyo ni umeme wa maji kutoka Kidato, Mtera na Julius Nyerere na ule Gesi Asilia kutoka Kinyerenzi hivyo hakutaweza kutokea changamoto ya umeme, vilevile kuna kila kituo cha umeme kwa kila baada Kilomita 50 ili kufatilia mwenendo wa Umeme katika mradi huo”, alisema Mhe. Kapinga.

Kamati imezipongeza TANESCO na TRC kwa namna ambavyo wamesimamia ujenzi wa Mradi huo na kukamilika,wameishauri TRC kukamilisha haraka maeneo machache yaliobaki, na kuhakikisha kuwa mabehewa ya Treni yanakuja na kuanza kutumika kwa sababu miundombinu iko tayari na wameanza majaribio ya kichwa cha treni cha mwendokasi.

Kamati imewasihi Wafanyabiasha wawekezaji na watanzania kutumia fursa adhimu za mradi huo.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga  akizungumza na wakati wa ziara ya Makamu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ya kukagua chanzo cha umeme wa Gesi Asilia utakaotumika kuendesha treni hiyo ya kisasa katika eneo la kinyerezi, tarehe 19 Desemba, 2023, mkoani Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Augustine Vuma akizungumza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua chanzo cha umeme wa Gesi Asilia utakaotumika kuendesha treni hiyo ya kisasa katika eneo la kinyerezi, tarehe 19 Desemba, 2023, mkoani Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma,  Augustine Vuma( kulia) wakibadilishana mawazo na  Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga(katikati) wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua chanzo cha umeme wa Gesi Asilia utakaotumika kuendesha treni hiyo ya kisasa katika eneo la kinyerezi, tarehe 19 Desemba, 2023, mkoani Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma,  Augustine Vuma( katikati) na  Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga(kulia) wakipata maelezo ya namna Umeme utakavyofanya kazi katika Treni ya Kisasa( SGR) wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua chanzo cha umeme wa Gesi Asilia utakaotumika kuendesha treni hiyo ya kisasa katika eneo la kinyerezi, tarehe 19 Desemba, 2023, mkoani Dar es Salaam.