WAZIRI MAGUFULI AHUDHURIA MAHAFALI YA KUMI YA KIDATO CHA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA CHATO, AAHIDI MAJENGO YA KAMBI YA MKANDARASI KUWA MALI YA SHULE YA MAGUFULI

April 09, 2015

 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mkoani Geita, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao.
 Wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato Mkoani Geita wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao wakiimba wimbo maalum wa Shule hiyo katika Mahafali ya 10 shuleni hapo.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti mwanafunzi mmojawapo katika mahafali hayo.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya uchanaji wa mbao katika Shule ya Sekondari Chato. Mbao hizo hutumika katika kazi mbalimbali za ujenzi wa shule hiyo. Pia Dkt. Magufuli ameichangia shule hiyo kiasi cha Shilingi Milioni tano.
 Waziri Magufuli akikagua moja ya computer katika shule hiyo.kushoto kwake ni Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mahendeka Mafele.
 Dkt. Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha Skauti cha Shule ya Sekondari Chato kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua  maabara ya shule hiyo.
 Waziri Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chato Mwalimu Mahendeka Mafele kuhusu Ujenzi wa vyoo unaoendelea.
 Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali hayo ya kumi ya kidato cha Sita shuleni hapo.
 Vijana wanaotarajiwa kuhitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakitoa burudani pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Bi Helena Busumilo.
 Waziri Magufuli akifanya ukaguzi wa mabweni shuleni hapo. P
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi bora wa Shule ya Sekondari Magufuli Emanuel Sina Cheti cha Usafi na Utunzaji wa Mazingira kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanafunzi pamoja na wazazi kwenye mahafali hayo ya nne katika Shule ya Sekondari  Magufuli.
 Wanafunzi wa kidato cha Sita katika shule ya sekondari  Magufuli wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mgeni rasmi  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Magufuli iliyopo Bwanga mkoani Geita.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Magufuli wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za asili ya kisukuma katika mahafali hayo.
 Mkuu wa shule ya Sekondari Magufuli Mwalimu Abdalah Haji Siseme akimkabidhi risala mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua kambi ya mkandarasi anayejenga barabara inayopita karibu na shule hiyo. Dkt. Magufuli ameiahidi shule hiyo kuwa pindi mkandarasi atakapomaliza ujenzi wa barabara hiyo atakabidhi majengo hayo kwa shule hiyo ya kidato cha tano na  sita.
Mandhari ya shule ya Sekondari Magufuli. Shule hiyo toka kuanzishwa kwake mwaka 2010 haijawahi kufelisha mwanafunzi hata mmoja.

DKT. MAGUFULI AHIMIZA WAZAZI KUWASIMAMIA VIZURI WATOTO KATIKA ELIMU.
Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chato mkoa wa Geita Dkt. John Pombe Magufuli amewahimiza wazazi na walezi kuwasimamia vizuri watoto wao katika masuala ya elimu ili kuwaepusha na matendo maovu katika jamii. 
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo leo katika mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita ambapo jumla ya wanafunzi 84 wanatarajiwa kuhitimu. 
“Wazazi mnataikiwa kuhakikisha mnawafatilia watoto wenu katika masomo yao na kuacha tabia ya kutoa uhuru mkubwa ambao hutumika vibaya. Inabidi muwabane sana hata wakichukia leo kesho watakuja kufurahi na kuona faida yake” alisisitiza Waziri Magufuli 
Waziri Magufuli aliwaasa pia wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha nne kuhakikisha kuwa wanasoma kwa bidii ili waweze kufaulu kuingia kidato cha tano. 
“Mnatakiwa kuanzia sasa kupanga  mikakati mizuri ya kujisomea kwa muda huu uliobaki na kwa mwaka huu kusiwe na daraja la nne katika matokeo yenu” aligusia Waziri Magufuli 
Kwa upande wa  Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chato, Bi. Hellen Busumilo amewasisitiza wazazi kusaidiana na walimu katika malezi ya watoto na pindi mtoto anapokosea aadhibiwe kwani kwa kutofanya hivo ni kosa linalopelekea watoto kufanya matendo maovu. 
“Usimamizi wa watoto ni jukumu la wazazi wote, mzazi nyumbani  na mwalimu shuleni ili tuweze kuwasaidia watoto wetu hasa watoto wa kike” alisema Bi Busumilo 
Bi. Busumilo aliongeza kuwa kuna haja ya kuwaelimisha na kuwafundisha watoto mambo mbalimbali yatakayowajega kwasasa na badae. 
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Chato, Mwalimu Mafere Mahendeka amemshukuru Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhudhuria mahafali hayo ya 10 ya kidato cha Sita katika shule hiyo.
 “Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa michango yako mbalimbali katika shule yetu, mfano  mwaka 1997 ulisaidia shule hii kumilikiwa na Serikali kwa manufaa ya umma, na kwa mwaka 2003 ulifanikiwa kuweka kidato cha tano na sita”, Alisema Mwalimu Mafere. 
Mwalimu Mafere amemhakikishia Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. John Magufuli kuwa watatumia kiasi cha Shilingi milioni tano alizowapa katika mahafali hayo kwa ajili ya maendeleo ya Shule hiyo na si vinginevyo. 

Shule ya Sekondari ya Chato ina jumla ya wanafunzi 1018 kuanzia kidato cha I-VI. Shule hii imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kidato cha sita, mfano mwaka 2011 ufaulu ulikuwa asilimia 96 na mwaka 2014 ufaulu ulikuwa asilimia 100.
Wakati huo huo, Dkt. Magufuli ameahidi kuwa majengo ya kambi ya mkandarasi katika barabara ya Bwanga-Uyovu yatakabidhiwa kwa shule ya sekondari Magufuli pindi kazi za ujenzi wa barabara hiyo utakapokamilika. 
Ahadi hiyo ilitolewa na Waziri Magufuli katika mahafali ya nne ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Magufuli ambapo jumla ya wanafunzi 48 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao. 
“Sitafurahi kuona wanafunzi wakipata tabu na walimu wakishindwa kufanya kazi zao vizuri kwa kukosa nyumba za kuishi na madarasa ya kufundishia hivyo huyu mkandarasi akikamilisha kazi za ujenzi wa barabara, hizi nyumba 12 zinabaki kuwa mali yenu”, alisema Dkt. Magufuli. 
Aidha, Waziri Magufuli aliwasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuacha kufikiria changamoto zilizopo shuleni hapo kwasababu wenzao waliowatangulia walifanya vizuri licha ya changamoto hizo
 “Pamoja na changamoto zilizopo mnatakiwa msome kwa bidii na muache mambo mengine kwanza ili ikiwezekana wote hapa mfaulu kuingia chuo kikuu na kuendelea kuiletea sifa shule yenu na Wilaya kwa ujumla”, alisisitiza Waziri Magufuli 
Kuhusu suala la umeme ambalo pia ni changamoto shuleni hapo, Dkt. Magufuli amewataka kuwa na subira kwani tayari suala hilo lipo katika mpango wa Umeme vijiji REA ambapo umeme utafika katika tarafa hiyo ya Bwanga hadi eneo la shule ili kupunguza adha wanayoipata wanafunzi hao. 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo amesema kuwa tarafa ya Bwanga ina watoto 81 ambao mpaka sasa hawajaripoti kwenye shule za Sekondari na ametoa hadi tarehe 13 mwezi huu watoto wote wawe wameripoti shuleni hata kama hawana sare za shule. 
“ili kupata wanafunzi wa kuingia kidato cha tano hatuna budi kuwekeza kwenye elimu ya Sekondari hivyo basi nawasihi sana wazazi mpaka muda huo uliopangwa muwe mmewapeleka watoto shuleni baada ya hapo ni msako utafanyika ili wazazi watakao goma tuwachukulie hatua kali za kisheria.”, alisisitiza Mkuu wa Wilaya ya Chato. 
Shule ya Sekondari Magufuli ilizinduliwa tarehe 21/10/2009 na aliyekuwa Waziri wa Elimu katika kipindi hicho Profesa Jumanne Maghembe. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 140 wa kidato cha tano na cha Sita na imekuwa ikifanya vizuri kati ya shule zenye wanafunzi zaidi ya 30 katika ngazi za Wilaya, Mkoa na Kitaifa.

WASHINDI WA DROO YA MWISHO YA AIRTEL YATOSHA ZAIDI WAKABIDHIWA MAGARI YAO

April 09, 2015

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Tipwa Rashid Mapunda (kushoto), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka wa pili kushoto) ni washindi wengine wa droo hiyo, William Saimon Sondi na Boutrous Hebron Mwanjali.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, William Saimon Sondi (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa droo hiyo, Tipwa Rashid Mapunda (kushoto) na Boutrous Hebron Mwanjali.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akifurahia jambo na washindi wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, (kutoka kushoto), Tipwa Rashid Mapunda, William Saimon Sondi na Boutrous Hebron Mwanjali, baada ya kuwakabidhi funguo za magari yao aina ya Toyota IST, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, William Saimon Sondi katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Tipwa Rashid Mapunda katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni mume wa mshindi huyo, Mzee Simon Tawata Mapunda.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto), akimuelekeza jambo mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’ Tipwa Rashid Mapunda, baada ya kumkabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni mume wa mshindi huyo, Mzee Simon Tawata Mapunda.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Boutrous Hebron Mwanjali katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni mke wa mshindi huyo, Hellena na mtoto wao, Alpha.
Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari

Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari

April 09, 2015


Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura wakiwasha mishumaa maalumu kuwakumbuka raia waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura wakiwasha mishumaa maalumu kuwakumbuka raia waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Mratibu Mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akipata maelezo juu ya mwenendo wa mashauri toka ICTR mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa pichani.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akipata maelezo juu ya mwenendo wa mashauri toka ICTR mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa pichani.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kimya kuwakumbuka raia waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kimya kuwakumbuka raia waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Bendera za mataifa mbalimbali zikipepea nusu mlingoti nje ya ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kuashiria tukio la kuwakumbuka raia wa Rwanda waliouwawa mauaji ya kimbari.
Bendera za mataifa mbalimbali zikipepea nusu mlingoti nje ya ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kuashiria tukio la kuwakumbuka raia wa Rwanda waliouwawa mauaji ya kimbari.
Ofisa Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya Mauji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Sarah Kilemi akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.
Ofisa Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya Mauji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Sarah Kilemi akizungumza katika Maazimisho ya Miaka 21 ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.
Viongozi na mabalozi mbalimbali wakiwa katika Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Viongozi na mabalozi mbalimbali wakiwa katika Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania yamefanyika leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

RADIO ZA JAMII ZASHUKURU KWA KUPOKEA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA NJIA YA SAUTI`

April 09, 2015

Wasimamizi wa redio za jamii wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa redio za Jamii, Joseph Sekiku akiongea machache kabla ya kuwagawia wasimamizi wa redio za jamii wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, akiwagawia wasimamizi wa redio za jamii katiba iliyopendekezwa iliwekwa kwa nji ya sauti.

………………………………………………………………………
Wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa Radio za jamii wamethibitisha kupokea na kuanza kurusha Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya sauti, makala na michezo ya radio iliyoandaliwa na Kampuni ya Focus Media na COMNETA zenye maudhui ya katiba inayopendekezwa.

Wakizungumza na Focus Media ambao ndio waandaaji na wasambazaji wamekiri kwamba wamepokea kwa wakati muafaka, kwani hawakuwa na chanzo sahihi cha kupata maudhui yanayohusu elimu ya uraia na uchaguzi mkuu na kura ya maoni.

Baadhi ya wasimamizi wa radio zilizo katika mtandao wa radio za kijamii Community Media Network of Tanzania ambao wamethibitisha kupokea vitendea kazi hivyo ni Bw. Ali Khamis Mtwana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tumbatu Island Community Radio, Bw. Anton Masai Triple A FM Arusha, Dr. Lazaro Ole Mongoi Mkurugenzi Mtendaji wa IDEA Radio, Henry Bernard, Adelina Lweramla, Jackson Mollel, wa ORS FM Arusha, Edwin Mpokasye, Radio Fadhila Mkurugenzi Radio Kwizera- Ngara.

Vipindi vinapokuwa vikiruka hewani wasikilizaji wamekuwa wakishiriki kwa kupiga simu na kuuliza maswali ilikuelewa zaidi Katiba Inayopendekezwa.

Wengine wanapiga simu kupongeza na mnamichezo ya radio ilivyoratibiwa vizuri na ikielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali muhimu.

ILI KUSIKILIZA VIPINDI HIVI VYENYE MAUDHUI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA TEMBELEA 
www.facebook.com/KatibaInayopendekezwaTanzania

JAJI AGUSTINO RAMADHANI AWAASA VIONGOZI WA DINI KUHUSU KULINDA AMANI YA NCHI

April 09, 2015
Rais wa Mahakama  ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada ya jukumu la viongozi wa dini na kimila katika kulinda amani kwenye semina ya mahusiano ya dini na amani ya nchi iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Regal Naivera mjini hapa



Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga,Anthony Banzi akisisitiza jambo na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu  na Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani wakati wa semina ya mahusiano ya dini na amani ya nchi  iliyofanyika jana mjini hapa kulia ni Sheirh wa Mkoa wa Tanga,Ally Luhuchu