UN NA EU YAWANOA MABALOZI 50 WA MALENGO YA DUNIA IRINGA

November 29, 2016
UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions). Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania. 

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO,PIGA MARUFUKU UUZWAJI WA SARE ZA MAJESHI KWA WATU BINAFSI

November 29, 2016


   

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
  Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga  jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
  Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea  na  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo 
Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016

PICHA NA IKULU

ASILIMIA 40 YA WATANZANIA WAWE KWENYE UCHUMI WA VIWANDA KUFIKIA 2020

November 29, 2016

WATANZANIA takribani asilimia 40 wanatakiwa wawe wamejiingiza kwenye uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020 ili kuweza kusaidia kukuza ajira za vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla. 


 Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali imeazimia kufikisha asilimia 40 ya watanzania kufanya shughuli za uchumi wa viwanda kufikia 2020.
 “Tunataka mpaka kufikia 2020 watanzania takribani asilimia 40 wawe wamejikita kwenye uchumi wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii nan chi yetu kwa ujumla” alisema Waziri Mwijage.
 Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa Uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini kuwezesha kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi ili kukusanya kodi kwa ajili ya kupata huduma bora za kijamii kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania . 
 Kwa upande wa Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambao ni wadhamini wa mkutano huo Bi. Rose Mahendeka alisema kuwa wafanya biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia.
 “Wafanya biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka. Aidha Bi.  Mahendeka alisema kuwa wafanya biashara ambao wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa kutumia msimbomilia wanapasa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuwezesha Tanzania kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda ili kupata huduma bora kwa maendeleo ya jamii.
 Naye Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kutumia msimbomilia wa Tanzania ili kuweza kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata soko la kimataifa na kufikia uchumi wa kati . 
 “Ni lazima kutumia msimbomilia wa Tanzania kwa kila mfanyabiashara na mjasiriamali ili kuweza kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata soko la kimataifa na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda vikubwa na vidogo” alisema Bw. Mazara.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage akiongea na wadau mbalimbali wa biashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kutumia msimbomilia(barcode) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage wa pili kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kulia akimpa mkono wa pongezi Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kudhamini mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kushoto akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Shea illushion kulia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam. Na Mpiga picha Wetu . Dar es salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR ES SALAAM

November 29, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wakati wakiangalia kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo kabla ya Rais Lungu kuondoka nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wakifurahia jambo mara baada ya kuangalia kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo kabla ya Rais Lungu kuondoka nchini.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu kabla ya Rais huyo wa Zambia kuondoka nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wakati akielekea kupanda ndege uwanjani hapo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu ambaye ameondoka nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi. PICHA NA IKULU