Jamii Media, CIPESA Wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

July 14, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala huo.[/caption]   [caption id="attachment_80340" align="alignnone" width="800"] Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.
KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma za ICT. Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.   Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.
___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MFUMO WA HCIMS ILI UWEZE KUTUMIKA NA WATUMISHI WENGI ZAIDI

July 14, 2017
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo pichani) leo alipofanya ziara ya kikazi  katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es Salaam. 
 Mhudumu wa Afya kutoka Hospitali ya Magomeni Bi. Rukia Mkapa akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Paschal Mugayana kutoka shule ya Sekondari ya Njechele  akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea kusanifu na kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCIMS) ili uweze kutumika kutoa taarifa za msingi kwa watumishi  wa umma wengi zaidi kwa lengo la kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika sekta ya umma nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni – Kata ya Kawe, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kairuki amesema Mfumo wa HCIMS awali ulikuwa unapatikana Ofisi ya Rais–Utumishi pekee, lakini baadae ukakasimishwa kwa Maafisa Utumishi lakini sasa lengo ni kuwafikia watumishi wa umma waweze kuona taarifa zao ili kupata taarifa sahihi na za uhakika katika kanzidata. Amesema Tovuti ya Watumishi, Watumishi Portal, imeanzishwa maalum ili watumishi wa umma wajisajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi yenye anuani www.utumishi.go.tz na kuona taarifa zao za msingi.
Waziri Kairuki, pamoja na hilo, amesema mfumo wa HCIMS umegatuliwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hivi sasa ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kufanya maamuzi kwa haraka zaidi.
 “Kwa kuwa mahitaji ya watumishi wa umma ni mengi hivyo tumeona ni vema tukakasimu Mfumo huu na kwa watumishi wa umma katika kada nyingine ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri Kairuki ameongeza kuwa tayari mafunzo kuhusu namna ya kutumia mfumo yalikwishatolewa kwa Maafisa Elimu na Makatibu wa Afya wapatao 633.
 “Tumeamua kuanza na sekta hizi kwa sababu ni sekta zenye watumishi wa umma wengi zaidi ukilinganisha na sekta nyingine lakini tutaendelea kugatua mfumo wa HCIMS ili ufike katika sehemu nyingi zaidi za kutolea huduma (Service Delivery Points).” Mhe. Kairuki ameongeza.
Mhe, Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo ni siku yake ya tano aliyoitumia kukutana na Watendaji na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe.
Lengo la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS-UTUMISHI
14.07.2017
MASAUNI AWATAKA MAAFISA UHAMIAJI, POLISI KUONGEZA KASI KUCHUNGUZA NA KUWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU TANGA

MASAUNI AWATAKA MAAFISA UHAMIAJI, POLISI KUONGEZA KASI KUCHUNGUZA NA KUWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU TANGA

July 14, 2017
PIX 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kulia) kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) alipokua anatoa taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwataka Maafisa Uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakuliamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akitoka kulikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga ambalo linahitaji matengenezo ili kulirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, Masauni alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba (kulia) kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa haraka iwezekavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zena Saidi, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake, mkoani Tanga wakati kiongozi huyo alipofanya ziara yake kikazi mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwahasa viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwahakikishia kero zote walizompa atahakikisha anazifanyia kazi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba.Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA

July 14, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda ( kushoto) akikabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Kimisha kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa.

Baadhi ya Kompyuta hizo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (wakwanza kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa kizungumza mchache katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda amepokea Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka kwa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA,ikiwa kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri unaofanywa na Ofisi hiyo.

Upatikanaji wa Computer hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya shauku na utafutaji wa RC Makonda kwa ajili ya kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam, ambapo itakumbukwa hivi karibuni Mh.Makonda alifanya mkutano na Watumishi wa sekta ya Ardhi wa Manispaa zote na moja ya kero kubwa iliyo bainishwa kuwasumbua wananchi ni namna ya kupata kibali cha ujenzi jambo lililomkera RC Makonda.

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA NHC KWA UTENDAJI

July 14, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai 13, 2017. 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa  njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017. 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi akiwa na Mbunge wa Masasi Rashid Chuwachuwa (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Ndanda Costancia Bernad, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanganga, wakati alipo simama, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi mipira, wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

Wananchi wa kijiji cha Nanganga wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipo simama katika kijiji hicho, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Wananchi wa kijiji cha Mtama wakishangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtama,Nape Mnauye alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtama, wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

…………………………………………………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.

Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5.

“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.”

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.

Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

MKURUGENZI KAYOMBO AKUSANYA MILIONI 150 KWA MWEZI KATIKA SOKO LA NDIZI-MABIBO ILIHALI AWALI ZILIKUSANYWA MILIONI 10 KWA MWEZI

July 14, 2017
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifatilia kwa makini mkutano
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akitafakari kwa makini changamoto mbalimbali za wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ziara ya kikazi katika soko la Ndizi-Mabibo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika katika Soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dra es salaam
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifurahi mara baada ya kuambiwa wataendelea na shughuli zao katika soko hilo.

TANAPA YAMPATIA DK JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

July 14, 2017
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi  Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe  pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Habari zaidi zitaletwa punde. (NA  RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Na Richard Mwaikenda
Jane ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.

Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.

Akizungumza katika hafla hiyo jane anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.

Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.

Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.

Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe, Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Lembeli, Balozi wa Uingereza nchini, mabalozi mbalimbali pamoja na waalikwa.
Dk. Jane akikabidhiwa cheti cha kutambua mchange wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine

 Jane akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe
 Jane akikabidhiwa picha ya Sokwe
 Mama Mongela akimvisha Jane zawadi ya vitenge
 Dk Jane akitoa maelezo kuhusu maisha ya Sokwe
 Waziri Maghembe akipata maelezo kuhusu maisha ya Sokwe yalivyo
 Wasanii wa Tanapa wakitumbuiza kwa wimbo 


 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Mjeshi Mstaafu, Jenerali Waitara akitoa shukrani nyingi kwa Dk Jane kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuiletea Tanzania sifa lukuki duniani
 Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini wakati Waziri Maghembe akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alisema kuwa Dk. Jane ambaye wakati anaaza utafiti yeye alikuwa darasa la pili, lakini utafiti wake umeiletea sifa kubwa Tanzania na utakuwa ni urithi wa kipekee maishani
 Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini

 Profesa Magembe akihutubia katika hafla hiyo ya kumpatia tuzo Dk. Jane
 Baadhi ya mabalozi waliohudhuria hafla hiyo
 Dk Jane akielezea historia yake na jinsi alivyofanikiwa kufanya utafiti huo wa sokwe


 Lembeli akitoa neno la shukrani
 Jane akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi waliohudhuria hafla yake pamoaja na viongozi mbalimbali


 Jane akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari baada hafla kumalizika