SPIKA WA BUNGE AKABIDHI KIKOMBE MECHI YA BUNGE NA NMB

SPIKA WA BUNGE AKABIDHI KIKOMBE MECHI YA BUNGE NA NMB

May 07, 2017
bu1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (Kushoto)akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge, Mheshimiwa Sixtus Mapunda mara baada ya mechi kuisha na timu ya Bunge kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa bila dhidi ya NMB,  mechi hiyo ilifanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
bu2
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (Kulia) ambae pia ni mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Bunge kabla ya kuanza mechi ya mpira wa pete kati ya Timu ya Bunge na Timu ya NMB iliyofanyika jana katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
bu3
Wachezaji wa timu ya Mpira wa pete wa Bunge na NMB wakipiga picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi yao ambayo ilifanyika jana katika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI

May 07, 2017
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.

Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.

TEMESA WAPEWA SEMINA YA UKIMWI NA TACAIDS

TEMESA WAPEWA SEMINA YA UKIMWI NA TACAIDS

May 07, 2017
TEM1
Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akizungumza wakati akitoa semina kuhusu Ukimwi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya TEMESA jijini Dar Es Salaam.
TEM2
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir  (hayupo pichani) wakati akitoa semina kuhusu maambukizi mapya ya Ukimwi iliyofanyika ofisini hapo.
TEM3
Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akisisitiza jambo wakati alipokua akitoa semina ya Ukimwi kwa wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar Es Salaam.
TEM4
Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akisisitiza jambo wakati akitoa takwimu kuhusu viwango vya maambukizi ya Ukimwi kimkoa kwa wafanyakazi wa TEMESA katika semina iliyofanyika makao makuu ya wakala huo jijini Dar Es Salaam.
TEM5

RC NDIKILO AHIMIZA WILAYA YA KISARAWE KUFUFUA ZAO LA KOROSHO

RC NDIKILO AHIMIZA WILAYA YA KISARAWE KUFUFUA ZAO LA KOROSHO

May 07, 2017
KOR1
Mkulima wa korosho huko Sungwi, wilayani Kisarawe mkoani Pwani akimwelezea mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, (aliyefunikwa mwamvuli) namna alivyoanza kilimo hicho .(picha na Mwamvua Mwinyi) 
KOR2
Mtaalamu wa zao la korosho, wilayani Kisarawe, Ayubu Isele, akimwelezea mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, hatua wanazochukua kufufua zao hilo wilayani hapo. (picha na Mwamvua Mwinyi) 
……………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, ameitaka wilaya ya Kisarawe kufufua zao la biashara kama ilivyokuwa miaka ya 1995 ambapo wilaya hiyo ilikuwa ikisifika kwa kulima zao hilo.
Aidha amepiga marufuku kang’omba kwani inasababisha hasara kwa wakulima wa korosho badala yake utumike mfumo wa stakabadhi ghalani.
Mhandisi Ndikilo,pia ameonya wizi unaofanywa na baadhi ya vyama vya ushirika vya msingi vya korosho,(AMCOS) kwa wanunuzi .
“Ambapo katika msimu uliopita sh. mil. 385 zilipotea katika wilaya ya Rufiji, Kibiti, Mkuranga na Bagamoyo na kati ya fedha hiyo mil. 4.633 ziliibiwa na AMCOS za Kisarawe”alibainisha .
Aliyasema hayo baada ya kutembelea shamba la korosho na mihogo la mzee George Haule huko Sungwi.
Mhandisi Ndikilo, alieleza kwamba, zao la korosho liwe ni azimio la baraza la madiwani wilayani humo.
Alisema kwa kulima korosho kwa wingi kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea umaskini.
Mkuu huyo wa mkoa alifafanua kuwa,endapo mkulima akipanda miche 100 kwa miaka mitatu anapata tani 4 sawa na mil. 16 .
“Ndani ya miaka mitatu ni lazima utajirike, tuibue Kilimo hiki kwani kinatija kwa wilaya na mtu mmoja mmoja “alisema mhandisi Ndikilo.
Akizungumzia ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya AMCOS  alisema kati ya mil. 385 wilaya ya Kisarawe ni mil. 4.633 na kati ya hizo Amcos ya Maneromango ni mil. 3.72 na ya Mzenga ni laki 4.64 .
Aliwaasa kuacha tabia ya wizi kwa wanunuzi na kuhujumu zao hilo la biashara.
Mhandisi Ndikilo,alisema vyama vilivyojihusisha kutapeli wanunuzi vitoe sababu za msingi kwa wakuu wa wilaya kueleza ubadhilifu huo na wakibainika kufanya wizi vyombo vya sheria vifanyekazi yake.
Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema, wataalamu kutoka bodi ya korosho ndio wana hakiki ubora wa korosho katika vyama vyote vya msingi vilivyokusanya korosho kwa kushirikiana na CORECU na kisha kuandaa muongozo kwa wanunuzi.
Alisema muongozo wa mauzo namba 1 wa mwaka 2015,kifungu namba 4.4 wa bodi ya korosho Tanzania  kinasema mnunuzi ataruhusiwa kuhakiki ubora wa korosho zilizopo kwenye ghala baada ya kufanya utaratibu wa kulipa korosho .
Twamala alisema sababu zinazotolewa na vyama hivyo kuwa ni unyaufu na sio upotevu alisema ni visingizio. 
Nae mtaalamu wa zao la mikoroshi wilayani Kisarawe, Ayubu Isele, alisema kwasasa wanayo miche 35,000 ambayo inasambazwa bure kwa wakulima wilaya nzima.
Alisema zao la Korosho miaka ya 1995-1996 katika wilaya hiyo lilishamiri na wakulima kunufaika.
Mkulima wa zao la korosho mzee Haule, alisema alianza Kilimo hicho mwaka 2005 ,na miche 662 na sasa ameongeza miche 342 .
Alisema zao hilo ndio ajira yake na linamuingizia kipato kwa kiasi kikubwa.
ENG. NGONYANI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UYOVU- BWANGA.

ENG. NGONYANI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI UYOVU- BWANGA.

May 07, 2017
unnamed
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akipokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, kuhusu ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokagua barabara hiyo jana, mkoani Geita
A
Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, akitoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.
A 1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mhadisi Mkazi Eng. Juma Msonge, baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita.
A 2
Sehemu ya barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Synohdro, mkoani Geita. Hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 60.
A 3
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Geita, Eng. Harun Senkuku, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ambae alikuwa mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara yake.
…………….
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa Km 45 inayojengwa na Mkandarasi M/S Sinohydro Corporation.
Akizungumza mkoani Geita jana, mara baada ya kukagua  barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amemtaka mkandarasi huyo kahakikisha wanamaliza sehemu iliyobakia kwa muda uliopangwa.
“Nimeridhishwa na kasi yenu, hakika mmepiga hatua sana kwani awali nilipopita kukagua barabara hii haikuwa hivi”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Aidha,  Eng. Ngonyani, amewapongeza wasimamizi wa barabara ya Biharamulo – Bwanga kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU),  kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation  kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyomo kwenye mkataba.
Kwa upande wake, Mhandisi mkazi wa barabara hiyo Eng. Juma Msonge, amemhakikishia Waziri huyo kumaliza barabara hiyo kwa wakati.
Eng. Msonge ameongeza kuwa kwa sasa mradi huo umefika asilimia 60 ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya kuweka matabaka ya lami ambapo ameshaweka km 30 kati ya 45 zilizopo kwenye barabara hiyo.
Naibu waziri  Ngonyani, amemaliza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa.

May 07, 2017

Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania Bw. John Ulanga
Na Pascal Mayalla 
 Taasisi ya TradeMark East Africa inazijengea uwezo bidhaa za Tanzania ili  kuziingiza kwenye masoko ya kimataifa, kwa kuziwezesha kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
Kwa hatua hiyo bidhaa hizo zitakuwa na uwezo wa kuhimili ushindani wa kimataifa na kuingia kwenye masoko ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bara la Afrika na masoko ya kimataifa yakiwemo masoko ya Ulaya na Marekani, amesema Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga kwenye kongamano ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam Jumamosi.
Bw. Ulanga amesema zoezi la kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinafikia viwango vya ubora wa kimataifa, linafanywa kwa kupitia mafunzo ya viwango vya ubora kwa kuzitumia taasisi za TBC, TFDA na GS 1 kwa ajili ya barcode kwa bidhaa za Tanzania, hivyo bidhaa hizo kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya kimataifa kwa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa. 
 Bw. Ulanga amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kwa awamu mbalimbali, ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa ambapo Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani zaidi ya Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia mpango huo. 
 Ulanga amesema walengwa wa mafunzo ya awamu hii ni wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, walio chini ya mwamvuli wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania , (Tanzania Women Chamber of Commerce, TWCC), ambapo mafunzo ya mwanzo ilikuwa ni kuwajengea uwezo ili kuweza kuvuka mipaka na kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata nje ya bara la Afrika, lakini mafunzo ya sasa ni kuwajengea uwezo wa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa. 
Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark  imeamua kuanza kwa kumkomboa mwanamke kupitia  Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kimepatiwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, ikiwemo kuendesha mafunzo hayo nchi nzima. 
“Ukimuwezesha mwanamke, ni kuiwezesha familia nzima, familia zikiwezeshwa ni kuwezesha jamii nzima na jamii zikiwezeshwa na kuwezesha taifa kwa ujumla, hivyo uwezeshaji huo  kwa wanawake ni uwezeshaji kwa taifa kupata maendeleo” Alisema Bw. Ulanga. 
Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa  TWCC, Bibi, Jaquline Mneney Maleko, amewasisitiza wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuzichangamkia fursa za kuwajengea uwezo, zinazotolewa na TWCC kwa udhamini wa Trademark East Africa, Bi Maleko amewaasa wanawake kutafuta zaidi elimu ya ujasiliamali na sio tuu kujikita kwenye kutafuta pesa, mwanamke aliyeelimika, anakuwa na uwezo wa kufanya biashara kubwa zaidi hivyo kutengeneza fedha zaidi kuliko mwanamke asyeelimikaMkurugenzi wa TWCC, Wakili Nourine Mawalla, amesema wanawake wa Tanzania wanajituma sana katika ujasiliamali wa uzalishaji wa bidhaa bora, lakini bidhaa zao zimekuwa zikikosa masoko ya kimataifa kutokana na kukosa viwango vya ubora  wa kimataifa, hivyo kupitia TWCC na TMEA, wanawajengea wafanyabiashara, wanawake wa Tanzania, uwezo wa kikidhi viwango vya ubora wa kimataifa, hivyo bidhaa za Tanzania kukubalika katika masoko ya Kimataifa.
Bi Mwala ameishukuru TradeMark kwa ufadhili wa mafunzo hayo na kueleza uwepo wa soko la Afrika Mashariki ni fursa, hivyo Chama cha TWCC, kinaishukuru TMEA kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuchangamkia fursa za soko hilo, kufuatia wanawake ndio idadi kubwa ya wafanyabiashara, lakini wengi huishia kufanya biashara ndogo ndogo kutokana na kuwa na uwezo mdogo, hivyo chama hicho kinawajengea uwezo na kuwafungulia fursa za kupata mitaji mikubwa, na kuingiza bidhaa zao kwenye soko la Afrika  Mashariki na masoko ya kimataifa.

TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia kuongezeka kwa fursa za upatikanaji  wa  masoko, kuboresha mazingira ya biashara, na kuboresha biashara ya ushindani hivyo kuongezeka kwa kiwango cha biashara hivyo kuchangia  ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini nakuleta maendeleo ya taifa la Tanzania.
TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina  matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.

Serikali inafanyia kazi vikwazo biashara ya Madini - Kamishna wa Madini

May 07, 2017
 Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumza jambo wakati wa Kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito ya Arusha.
Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari (katikati) akiangalia ubora wa Madini ya Tanzanite katika banda la kampuni ya Hadjarat Mining and Gemstone Company Limited. Aiiyeshika kifaa cha kupima ubora wa madini  ni Mkurugrenzi wa Kampuni hiyo.

Na Asteria Muhozya, Arusha
Wadau wa Madini nchini wametakiwa kujikita katika shughuli za ukataji na usanifu wa madini badala ya kusanifiwa nje ya nchi ili kuwezesha  adhma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kupitia  Sekta ya Madini.
Hayo yalisemwa na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi  Benjamini Mchwampaka wakati wa kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3-5 Mei,2017.
Aliongeza kuwa, uwepo wa shughuli za ukataji na unga'rishaji wa madini hayo nchini kutawezesha kuyaongezea thamani ikiwemo kupanua wigo wa ajira kupitia sekta ya madini.
" Tanzania ya sasa ni ya Viwanda. Na sisi sekta ya madini tuwe na viwanda vyetu  vya kusanifu madini yetu hapa hapa nchini. Kwanza tutayaongezea thamani madini yetu lakini pia tutazalisha ajira kwa wingi," alisema Mchampaka.
Aidha, Kamishna  Mchwampaka  aliongeza kuwa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imewasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri  ya  biashara ya Madini nchini ili kuondoa kero  ambazo ni kikwazo  katika biashara hiyo kwa watanzania.
"Tunataka kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa madini wa Tanzania lakini pia tunapenda wafanyabiashara wetu washiriki kwa wingi katika maonesho haya. Ni fursa kubwa ya kibiashara kwao," alisisitiza Mchwampaka.
Akizungumzia Mnada wa Madini ya Tanzanite uliofanyika tarehe 5 , Mei, alisema kuwa,  minada  hiyo  itaendelea kufanywa mara kwa mara kutokana na mchango wake katika sekta husika kwa kuwa pia inasaidia kupata bei halisi ya madini hayo.
Katika mnada wa Madini ya Tanzanite jumla ya kampuni 48 zilishiriki mnada huo ambapo madini ghafi ya  Tanzanite kutoka Kampuni ya TanzaniteOne  yenye jumla ya gramu 691,060.33 ziliuzwa katika mnada huo kwa dola za Marekani 3,161,860, sawa na asilimia 100 ya madini yote yaliyowasilishwa kwa mauzo.
Pia, alizungumzia ujumbe wa Serikali ya Nigeria iliyoshiriki Maonesho hayo na kueleza kuwa, ujumbe huo ulifika kwa lengo la kujifunza namna Tanzania inavyoongeza thamani madini yake ikiwemo pia kubadilisha uzoefu na kuongeza kuwa, lengo ni kuifanya Afrika inufaike na rasilimali zake za madini.
Ujumbe wa Serikali ya Nigeria uliongozwa na Waziri wa Madini  na  Maendeleo ya Viwanda, Abubakar Bwari aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abbas Mohamed pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara wa Madini kutoka nchini humo.