SBL yakabidhi mradi wa maji wa 83m/- Makanya wilayani Same

December 08, 2016
Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Semanyole akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa serengeti breweries Limited .kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasialiano wa SBLJohn Wanyancha  mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha makanya..Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.
Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Senyamule akimtwisha moja ya wanakijiji ndoo ya maji kuashiria kuanza kwa mradi wa maji ulidhaminiwa na Serengeti Breweries Limited katika kijiji cha Makanya.. na kulia ni Meneja miradi wa SBL Hawa Ladha,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.



Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza
Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza

Same, Desemba 9th, 2016- Kampuni ya Bia Serengeti leo imezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 83  katika eneo la Makanya wilayani Same  ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia watu 10,629, mradi huo unajumuisha  kisima  pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji  ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila saa moja.

Akizungumza katika  hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha  alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni mionmgoni mwa  mikakati kama hiyo  ambayo kampuni hiyo ya bia  imeiendesha  katika mikoa ya  Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha  zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

 Wanyancha alisema kwamba mradi wa Makanya  sio tu kwamba  utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia  utaongeza tija katika kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake  ambao  hawatahitaji kutumia saa nyingi  kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule  wakiwa huru.”

 “SBL  ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake  kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Wanyancha akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo wa mahusiano  aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita  imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.

Wanyancha  alisema kutokana na juhuzi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 1000 na hili limechangia  katika kukua kwa kampuni  na kukuza  kipato cha wakulima.”

Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia  malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani  katika kutoa  huduma  ya maji  safi na salama ndani ya nchi.”


Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule aliipongeza SBL  kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika mno, akisema kwamba kampuni hiyo ya bia  imekuwa mstari wa mbele katika kukuza  miradi ya maendeleo nchini  ambayo inawezesha kuwepo kwa jamii  inayozalisha na  iliyo na afya

TAMASHA LA SIFA ZA YERIKO ARUSHA

December 08, 2016


Miaka 25 ijayo, Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii inamaanisha nguvukazi kubwa itakuwa mikononi mwao. Lakini kama watasalia kuwa idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa kwa ukuaji wa nchi.Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye makusanyiko ya kijamii mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa nguvu. Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.

Uwepo wa Tamasha la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto kwenye jamii.Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono Foundation.

Tamasha la Sifa za Yeriko msimu wa kwanza inatarajiwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2016 Jijini Arusha kwenye Kanisa la New Life City Church (Kwa Egon) lililoko Kwa Iddi, na kisha kufuatiwa na Tamasha la pili litakalofanyika tarehe 11 Disemba Kanisa la Tanzania Assemblies of God CCC Upanga Jijini Dar es Salaam ikiwa ni weekend hii. Tamasha hili litahusishwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania, ambapo ugeni kutoka Afrika Kusini utakuwepo. Wageni hawa ni Mercy Manqele, KgotsoMakgalema na Sipokazi Nxumalo.Baadhi ya waimbaji wa ndani ni kama vile, Abednego na The Worshippers, Toddlers International, Yusuphu Nahashon, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,Wengine ni Machalii wa Yesu, The Cahogoz, Voice of Joy, Lilian Kimola, na Bomby Johnson.

LENGO
Lengo la awali nikukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zitatumika
kutafuta eneo la kituo kwa jijini Dar es Salaam na Arusha, pamoja na matengenezo iwapo itanunuliwa nyumba na kuibadilisha kuendana na maono ya jinsi kituo tunavyotaka kiwe kukidhi mambo mbalimbali yatakayokuwa yakipatikana kituoni, kama kujifunza muziki, uimbaji, ushauri nasaha, na utafutaji wa shule za kukuza vipaji ndani na nje ya nchi.ambayo tunatarajia yatawezesha kupatikana kwa kiasi hiki ni kupitia barua za mwaliko kwa watumishi mbalimbali wa dini na taasisi, pamoja na kiingilio kitakachopatikana kupitia matamasha yote mawili.

GHARAMA
Ili lengo la kukusanya milioni 200 kutimia, gharama mbalimbali kutoka kwa waanzilishi na marafiki zimefanikisha katika kuwakaribisha waimbaji hawa kutoka Afrika Kusini, kulipia mahala watakapofikia, matangazo, usafiri wa ndani, chakula, vyombo, muziki na gharama nyinginezo. Hili litasaidia katika ukusanyaji wa kiasi kilichosalia kwa awamu tofauti tofauti. Tunaamini katika ushirikiano katika kutatua matatizo yaliyomo kwenye jamii yetu

Katika Kufanikisha na maono ya kupata fedha katika Tamasha hilo kwa Dar es salaam na Arusha kutakuwa na Kiingilio katika Matamsha hayo,Arusha ni Ijumaa hii Dec 9 pale kwa Egon Wakubwa 5000 VIP 20000 Dar es salaam ni Jumapili hii Dec 11 pale CCC Upanga Opp Chuo cha Mzumbe Watoto 5000 Wakubwa 10000 VIP 30000


Tunategemea support yenu wadau wa vyombo vya habari Bloggers kwa kwa ajili ya kusaidia kutangaza Tamasha hili linalofanyika lengo na maono tuliyo nayo mbele yetu Arusha na Dar es salam kwa wikendi hii.



Best Regards, gospelhabari.blogspot.com Tunu Bashemela Jr Managing Director Kingdom Heritage P.O.Box 11681 kingdomheritagetz@gmail.com +255 712116647 Dar es salaam Tanzania Better Community Better Life

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

December 08, 2016


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.

TAASISI YA AFRICAN RELIEF YAANZISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHUMBI,RUFIJI

December 08, 2016
Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Ndauka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mradi huo
 Vibarua akifyaka vichaka kusafisha shamba hilo
 Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) wakisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Samy  Mohammed Elazeb akisimamia maandalizi ya shamba hilo
 Ndauka na Samy  Mohammed Elazeb wakijadiliana jambo
 Mratibu wa Mradi huo, Peter Ambilikile (kushoto) akifafanua jambo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Samy  Mohammed Elazeb (kushoto),  na mwanakijiji wakiziba maji kwenye mabomba ya kisima kilitolewa msaada na taasisi hiyo kwa Kijiji cha Chumbi C

 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chumbi C, akikinga maji kwa mkono katika kisima hicho
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko, akionesha ukumbi wa Kijiji ambao umejengwa kwa msaada wa Taasisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akionesha jengo la ofisi za kijiji hicho, lililojengwa kwa msaada wa taasisi hiyo.
 Nyumba anayoishi Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho