AWAMU YA KWANZA YA UANDIKISHAJI WA WACHEZAJI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA KITUO CHA MICHEZO CHA NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY WAANZA RASMI LEO

February 14, 2015

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia kuendelea leo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu utakaowakwamisha kusajiliwa.
Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota 30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo inayosubiriwa kwa hamu nchini.
“Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani Februari 28,” alisema Magori.
Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji, kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali watakaofungua darasa la akademi hiyo.
Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar es Salaam kufanya hivyo.
Magori aliongeza kuwa, watoto watakaopata nafasi ya kuingia katika akademi yao watasoma na kujifunza soka, ambapo watakaozivutia timu mbalimbali barani Ulaya watauzwa na wale watakaokwama, watauzwa Afrika, ikiwamo kuunda timu ya NSSF.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa uzinduzi wa mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF–Real Madrid Sports Academy.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).
 Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati), usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
Mtoto Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali akishuhudia.
Baadhi ya wazazi wakiondoka katika uwanja wa Karume baada ya kuandikisha watoto wao.

Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (wa pili kulia) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kushoto) wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo.
Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.

Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.
Vijana wakiingia katika uwanja wa Karume kwa ajili ya zoezi la kujisajili na hatimaye kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mwakilishi wa FIFA katika masuala ya michezo hapa nchini, Henry Tandau (katikati) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
Mtoto Issa Hashim akijaziwa fomu na Aisha Hashimu.
RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA WIZARA YA HABARI,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA WIZARA YA HABARI,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO

February 14, 2015


1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao siku moja cha Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo  kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana,[Picha na Ikulu.]
3
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo na Idara zake mbali mbali  wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Said Ali Mbarouk (hayupo pichani) alipokuwa  akitoa taarifa ya Wizara ya  utekelezaji wa mpango kazi   kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana  chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
8
Waziri wa Habari,Utamaduni ,Utalii na Michezo  Said Ali Mbarouk alipokuwa  akitoa taarifa ya Wizara ya  utekelezaji wa mpango kazi   kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 jana katika kikao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar   mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahya Mzee (kulia)

YANGA YAIADHIBU TIMU BDF XI FC YA BOTSWANA KWA BAO 2-0, UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

February 14, 2015

 Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0 zilizotiwa kimiani na Mshambuliaji Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na 55. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
 Golikipa wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
 Winga machachari wa Yanga,Saimon Msuva akiangalia namna ya kumtoka beki wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana,Othusitse Mpharitlhe wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
Beki wa Yanga,Mbuyu Twite akirusha mpira kwa ustadi mkubwa.
Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiichezesha ngome ya timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana katika mtanange wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.
huchukui mpira hapa.....










Kiungo mchezeshaji wa timu ya Yanga,Haroun Niyonzima akichanja mbuga mbele ya mabeki wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana katika mtanange wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.

Rais Kikiwete azindua Sera ya Elimu,Afungua maabara Shule ya Sekondari ya kata

Rais Kikiwete azindua Sera ya Elimu,Afungua maabara Shule ya Sekondari ya kata

February 14, 2015

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa wakiangalia jaribio la Sayansi lililokuwa likifanywa na mwanafunzi katika shule ya sekondari ya kata ya Majani ya Chai huko Kipawa jijini Dar es Salaam.Awali Rais Kikwete alizindua maabara za sayansi katika shule hiyo na baadaye alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik.
(picha na Freddy Maro)
RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZINZA

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZINZA

February 14, 2015

1. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu mjumbe maalum wa Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi.
2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribidhiwa ujumbe maalum Ikulu kutoka  Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilishakutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi
(picha na Freddy Maro)

SHIRIKA LA EQUALITY FOR GROWTH (EfG) LA ZINDUA MRADI WA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFANYABIASHARA SOKONI NA OFISI ZAKE WILAYANI LUSHOTO MKOANI TANGA, FEBRUARY 13, 2015

February 14, 2015


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
 Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na maofisa wa EfG.
 Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
 Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
 Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
 Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine Kisigila.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (kushoto), akifurahi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali ya EfG.
………………………………………………………………………..
Doto Mwaibale
 
WAJASIRIAMALI wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila ya kutoa elimu hiyo.
Mwito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo  mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne Shauri. 
“Ninyi Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika maeneo yenu” alisema Dk. Shelukindo
Alisema elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu ya uongozi na usimamizi wa vikundi.
Alisema EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
Alisema EfG  inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa mafunzo  ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria kwa jamii.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa  takribani siku tano.
” Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara sokoni” alisema Magigita.
Alisema mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.
Alisema pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)