WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KUTANO WA ROTARY CLUB ARUSHA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KUTANO WA ROTARY CLUB ARUSHA

May 04, 2017
ro2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivishwa beji ya uanachama wa Rotary Club na Dk. Manoj Desai kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ro3 ro4
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Rotary Club kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ro1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania  (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ro5
Washiriki wa Mkutano mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) wakishangilia mara baada ya Waziri Mkuu kutangaza kuwa yeye na mke wake, Mary Majaliwa wanajiunga na Rotary Club katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TUME YA UCHAGUZI YAMTEUA NDG. CATHERINE RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA

TUME YA UCHAGUZI YAMTEUA NDG. CATHERINE RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA

May 04, 2017
 DSC_0428
KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikaochake cha tarehe 04 Mei, 2017imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge kuwa Mbunge wa VitiMaalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujazanafasiiliyoachwawazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweponafasiwazi ya Mbunge wa VitiMaalumkupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwaMbunge wa VitiMaalumMhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.
Imetolewaleo tarehe 04 Mei, 2017 na:-
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

MAVUNDE:VIJANA MILIONI 4 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA VITENDO

May 04, 2017

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa vitendo kutoka Kwa Chama Cha Waajiri nchini ATE kwa kushulikiana na Shirika la Kazi Duniani ILO leojijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akionyesha Vitabu vya programu vya mafunzo kwa vitendo mara baada ya kuzindua programu hiyo katika ukumbi wa Hyatt Kempiski leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akikata utepe kuashiria uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Chama cha Waajiri nchini ATE, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa ATE nchini , Almas Maige(MB) akishuhudia uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la kazi Duniani (ILO) ukanda wa Afrika Mashariki ,Dk Mary Kawar akizungumza wakati wa ufunguzi proamu hiyo
Katibu Mtendaji wa ATE ,DK.Aggrey Mlimuka akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE), Almas Maige(MB) akichangia jambo katika mkutano huo uliowashirikisha wadau mbalimbali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani Yaadhimishwa Zanzibar

May 04, 2017

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmoud Thabit Kombo akipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya na Jumiya ya Wakunga, Wauguzi na Wadau wa Afya Tanzania wakati wakipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo Zanzibar.  
Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao

Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
MC wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Zanzibar akisoma utaratibu wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar 


Kaimu Msaidizi wa Mrajisi wa Wauguzi na Wakunga Zanzibar Ndg. Rajab Mussa akisoma kiapo cha wauguzi na wakunga wakati wa hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar yalioaza kwa maandamano ya Wakunga na Wauguzi Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakunga Zanzibar Bi Amina Abdulkadir Rajab akizungumza wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimishwa katika ukumbi wa Sanaa rahaleo kwa maandamano yaliopokelewa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
Mwakilishi wa Jumuiya ya Tanzania Midwives Assossiotion Bi Priscilah Godwin akitowa salamu za TAMA wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wauguzi Zanzibar Bi Valeria Rashid akitowa salamu za jumuiya yao wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
Rais wa Jumuiya ya CHORA (Construction Health and Relief Acts) Bi Carol Mcdonald akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNFPA Bi Sabina Luoga akitowa salamu za Shirika lake wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya Zanzibar akiwahutubia Wauguzi na Wakunga wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, na kutowa nasaha zake kwa Wauguzi na Wakunga katika utowaji wao wa huduma kwa Mama na watoto, wakati wa kutowa huduza zao katika jamii.   

Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Afya Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani.
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani wakimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmuod Thabit Kombe akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa waugunzi na wakunga katika kutowa huduma kwa wananchi wakiwa katika ukumbi wa sanaa rahaleo
Viongozi wa Wakunga na Wauguzi wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani huadhimishwa kila mwezi wa Mei 5, Duniani kote, hafla hiyo ya maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar.
Imeandaliwa na Othmanmapara.Blog.com
Zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com

Story ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia

May 04, 2017
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.

Balozi wa Tanzania Saudi Arabia atumia Sikukuu ya Muungano kutangaza Utalii

Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia
SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Balozi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Prince Muhammad bin abdullahman wakikata keki ya sherehe.
Balozi Mgaza kushoto akikata keki
Balozi Mgaza akihutubia katika hafla hiyo

Alisema kutokana na sera hizo pamoja na kusimamia vyema rasilimali za utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga mbalimbali za wanyama ni sehemu thabiti ya utalii kwa wageni, wakiwamo wananchi wa Saudi Arabia.

“Nchi yetu ina mbuga za wanyama 16 ambazo zimekuwa zikitunzwa na kuhifadhiwa vema kama sehemu ya kuhakikisha kwamba rasimali hiyo inakuza uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nchi yetu ina wakaribisha wote kutembelea kujionea mambo mbalimbali yanayovutia katika utalii pamoja na kuwekeza katika sekta muhimu zikiwamo za viwanda ambazo ndio agenda kuu kwa sasa nchini mwetu,” Alisema Balozi Mgaza.

Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimishwa wiki iliyopita Aprili 26 ambayo hutumiwa kama kioo cha kuangalia matunda yanayojitokeza kutokana na Muungano huo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.

MBINU ZA KUONGEZA MAPATO HOTELINI MSIMU AMBAO WATEJA NI WACHACHE

May 04, 2017

 Na Jumia Travel Tanzania

Kama biashara zingine, kuna msimu pia wateja hukauka mahotelini na wanakuwa ni wa kuhesabika tu. Kwa kawaida biashara ya hoteli huwa ni ya msimu yaani kipindi ambacho kunakuwa na sikukuu au mapumziko ndicho watu hufurika. Na hii ni kwa sababu kwamba wasafiri wengi huwa ni watalii ukilinganisha na wafanyabiashara.
Kipindi hiki ndicho wamiliki/mameneja wa hoteli hutakiwa kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kuwa wanawavutia wateja. Zipo mbinu kadhaa ambazo Jumia Travel ingependa kukushirikisha hizi chache ili kukabiliana na kipindi hiko kikifika ukiwa umejiandaa:     

Zitambue tabia za wateja wako. Kitu cha kwanza kabisa kukizingatia ni kujua tabia za wateja wanaopenda kutembelea hotelini kwako. Tumia taarifa ulizonazo kwenye kumbukumbu yako kuangalia wengi ni wa aina gani, vipindi wapendeleavyo kutembelea na huvutiwa na huduma zipi zaidi. Kwa mfano, meneja wa hoteli ya Kendwa Rocks anaweza kulitumia tukio la ‘Full Moon Party’ kujifunza hadhira inayofika pale na namna ya kuwavutia tena endapo tukio hilo halitokuwepo.      

Buni na toa ofa maalum za kuvutia. Baada ya kutambua ni wateja wa aina gani hupenda kutembelea zaidi hoteli yako, unaweza kubuni ofa maalum kuwalenga wao. Kwa kawaida kuna watu wanapenda kwenda kupumzika hotelini kipindi wateja wanakuwa sio wengi sana kwa sababu ya utulivu na gharama kushuka. Kama meneja wa hoteli unaweza kuitumia fursa hii kubuni ofa zitakazowavutia wateja wa aina hii. Itumie orodha ya wateja ambao wanaipendelea hoteli yako mara kwa mara kuwajulisha juu ya ofa hizo. Kwa sababu huwezi kujua kama wasipokuja wao wanaweza kuzipendekeza kwa marafiki, ndugu na jamaa zao.

Chunguza matukio yanayotarajia kutukia eneo ulilopo. Kipindi cha msimu ambao wateja sio wengi ni vema kutafiti shughuli ambazo zitawavutia watu kutembelea hotelini kwako. Unaweza kujua matukio yanayoendelea eneo ulilopo kupitia njia mbalimbali kama vile tovuti zinazoweka mtangazo nakadhalika. Ukishafahamu hayo jaribu kuwasiliana na waandaji ili ujue unaweza kushiriki kwa namna gani. Unaweza kushiriki kama washiriki wengine ili kuitangaza hoteli yako au kama mdhamini pengine hata kwa kutoa fursa kwa tukio hilo kufanyika hotelini kwako. Unaweza kuona kama ni gharama kufanya hivi lakini kuna faida nyingi kwani hoteli itajulikana kupitia matangazo, wahudhuriaji na pia huduma zako kutumika wakati wa tukio.
Boresha mwonekano na taarifa kwenye tovuti ya hoteli. Lakini pia kipindi ambacho pilikapilika za wateja zinakuwa sio nyingi sana hotelini, unaweza kukitumia kwa kuboresha mwonekano na taarifa mbalimbali kwenye tovuti. Kwa mfano, huduma, picha, matukio na habari unazoona zinafaa kwa wateja wako kuzifahamu.

Tumia fursa ya wateja wanaoependa kutembelea hotelini kwako. Kama ulikuwa haufahamu wateja wanaweza kutumika kama njia mojawapo ya kujitangaza na kuvutia wengine wapya. Mara nyingi watu huamini na kushawishika kiurahisi kutokana na maneno wanayoambiwa na watu wao wa karibu. Kwa kutumia orodha uliyonayo unaweza kuwaomba kuwataarifu wenzao na kisha kuwapatia ofa hotelini kwako kama chachu.

Tumia barua pepe kuwafikia wateja wako. Makampuni mbalimbali hutumia mbinu hii pia ambapo huwa na kumbukumbu ya anuani za wateja wao. Nadhani hata wewe utakuwa ushawahi kupokea jumbe za namna hiyo zikikutaka kutumia huduma fulani. Kwa hiyo baada ya kuandaa ofa zako kadhaa unaweza kuzituma kwa wale wateja ambao unajua huwa wanakuja hotelini kwako mara kwa mara.

Tumia mitandao ya kijamii kuongeza hamasa ya ofa na kampeni zako. Kwa sasa, hakuna njia rahisi na ya haraka zaidi inayowafikia na kuwaunganisha wateja wengi na makampuni kama mitandao ya kijamii. Hakikisha unaitumia vema mitandao hiyo kujenga na kueneza hamasa kwa kile unachotaka kukifanikisha. Watu wengi siku hizi wanatumia zaidi mitandao hiyo kwa kuwasiliana pamoja na kupata taarifa mbalimbali.
Zipo njia tofauti ambazo mahoteli huzitumia katika kukabiliana na kipindi hiki ikiwemo kukitumia kufanya maboresho. Kikubwa ni kutokukubalina na hali ya kwamba msimu huu huwa hakuna wateja au kushusha gharama ili kuwavutia wengi zaidi. Mbinu hizo hapo juu zilizoorodheshwa na Jumia Travel endapo zikizitumika ipasavyo basi hutoona tofauti ya misimu ya wateja kufurika hotelini kwako.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI WA MAKANDARASI MJINI DODOMA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI WA MAKANDARASI MJINI DODOMA

May 04, 2017
Q 1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa muda mfupi kabla ya kufungua mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. Q
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. Q 2 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi  na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya  ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
…………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.
Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo.
Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”
Kuhusu madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha wakandarasi.
Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.
Waziri Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.
Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.
Nae, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.
Msajili huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.
Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango

WAZIRI MWAKYEMBE AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUJIKITA KWENYE HABARI ZA UCHUNGUZI

May 04, 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza. Waziri Dkt.Mwakyembe alimwakilisha Rasi John Pombe Magufuli.

Dkt.Mwakyembe aliwaasa waandishi wa habari kuwa na weledi kwenye utendaji wao wa kazi ikiwemo kujikita kwenye habari za uchunguzi wa kina na siyo hisia alizosema atazilinda na kuzitetea huku akiwahimiza wahariri nchini kuwa na utaratibu wa kukutana na Mkurugenzi wa Habari Maelezo japo mara moja kwa mwezi ili kujadiliana kwa pamoja mafanikio na changamoto za utendaji kazi kwenye tasnia ya habari kwa manufaa ya taifa.

Aidha alionesha utayari wa kufungua milango ya majadiliano kuhusiana na sheria mpya ya vyombo vya habari nchini hususani katika baadhi ya vipengele vinavyolalamikiwa na wanahabari akisema sheria hiyo haijaandikwa kwenye mawe, ishara tosha kwamba kukiwa na mazungumzo, mabadiliko katika sheria hiyo yanaweza kufanyika.
BMGHabari
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza.

Kitomari alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya waandishi wa habari 100 kote duniani waliuawa mwaka 2016kutokana na majukumu yao ya kazi huku pia kukiwa na matukio ya upigwaji na utekaji wa waandishi wa habari ambapo kwa Tanzania zaidi ya kesi 30 za manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ziliripotiwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fikra Makini, Nyakati za Changamoto, Jukumu la Vyombo vya Habari katika kudumisha Amani, Usawa na Jamii Jumuishi".
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi mkazi wa taasisi ya FES nchini Tanzania, Michael Schulteiss, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mkazi wa Mwanza azoa mkwanja wake kutoka Biko

May 04, 2017
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono ya shukrani na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven baada ya kumkabidhi fedha zake jijini Dar es Salaam kama sehemu ya ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko inayoendelea nchini Tanzania na kugawa mamilioni kwa washindi wake.

Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la mchezo bahati na nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limemkabidhi mshindi wake wa wiki ya tatu ya Sh Milioni 10, ambaye ni Pildas Emmanuel, anayeishi jijini Mwanza baada ya kutangazwa mshindi wa wiki katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.

Makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam sambamba na kumfungulia akaunti ya benki ya NMB kwa ajili ya kuingiza fedha hizo kwa mshindi huyo aliyejitambulisha kama mjasiriamali wa vileo jijini Mwanza Tanzania.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel aliyeletwa kwa Ndege kwa ajili ya kumkabidhi fedha zake.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kulia, akishuhudia jinsi mshindi wao wa Sh Milioni wa bahati nasibu ya Biko, Pildas Emmanuel anavyofurahia baada ya kumkabidhi fedha zake mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Na Mpiga Picha wetu.

Alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000, pamoja na zawadi kubwa ya wiki ya Sh Milioni 10 kwa kila mshindi wao, huku wakiwa wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili ambao ni Christopher Mgaya, Nicholaus Mlasu ambao wote wameshapokea fedha zao.

“Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri wananchi wa Watanzania wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa sh 1000.
“Na kila Sh 1000 itakayolipwa itakuwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku mshiriki akiruhusiwa kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili wavune mamilioni ya Biko.

Naye Emmanuel alisema kwamba amefurahishwa na huduma zote alizopewa na Biko ikiwamo ya kumpa fedha zake katika benki ya NMB pamoja na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ndege kutoka Mwanza jambo ambalo halijawahi kumtokea katika maisha yake.

“Ingawa nimepata fedha nyingi ambazo sijawahi kuzishika tangu nizaliwe, pia nimeingia kwenye historia kwa sababu na mimi nimepanda ndege kwa mara kwanza huku fedha zote zikilipwa na Biko, hivyo ni kampuni nzuri na mchezo wao ni mzuri kutokana na malipo ya ushindi kulipwa haraka,” Alisema Emmanuel na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.

Emmanuel aliwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu akitokea jijini Mwanza ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja katika droo iliyoshuhudiwa pia na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.