SERIKALI WILAYANI KOROGWE YAAPA KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI

June 27, 2017
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative kulia ni Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu na 
Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada
nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka
Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu kushoto akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka
Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka akizungumza katika halfa hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Gorge Nyaronga akizungumza katika halfa hiyo  
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
Robert Gabriel kushoto akimpatia zawadi ya kitenge

Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu akimshukuru kwa msaada wa ujenzi wa madarasa na vyoo na uzio
Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu katikati akitazama kitenge chake
Risala ya shule hiyo ikisomwa

 Sehemu ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa


 Wanafunzi wa shule ya Msingi Jitengeni  wilayani Korogwe wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative


SERIKALI wilayani Korogwe Mkoani Tanga imepania kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mimba za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali watakaobinika kuhusika na matukio hayo ili kuweza kuondosha hali hiyo kwenye jamii.

Lakini pia imesema watakaohusika kuwa kichocheo cha ndoa hizo zifanyike wakiwemo wazazi kutoka pande zote mbili watafikishwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake zaidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Mhandisi,Robert Gabriel wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
.

Alisema hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha wanakomesha vitendo vinavyofanya na baadhi ya vijana vya kuwa sha wishi wananfunzi wa kike na kuwapatia ujauzito hivyo kupelekea wasichana hao kukatisha masomo yao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hivi sasa  lazima wawe wakali na watu wanaocheza na maisha ya watoto ya wanafunzi ambao asilimia kubwa masomo yao yana haribiwa mara tu baada ya kushawishiwa na kupewa ujauzito.

Alisema hatua ya kurubuniwa watoto wa kike kwenye masomo haiwezi kuvumiliwa hasa kipindi hiki ambacho hawatakuwa na nafasi tena ya kujiendeleza katika shule za serikali pindi watakapo jifungua.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkuu wa shuele ya msingi Jitengeni,Mafikiri Twinzi alisema umalizikaji wa madarasa hayo utapunguza kero kwa wanafunzi shuleni hapo ambapo awali walikuwa wakikaa wanafunzi 100 hadi 120 kwenye chumba kimoja.

Alisema shule hiyo iliyo na wanafunzi 816 imekuwa na tatizo la
uchakavu wa madarasa hali iliyopelekea kuwajengea woga wanafunzi wa kuangukiwa na kuta za shule hiyo.

Naye kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka alisema taasisi hiyo lengo lake ni kuisadiana na  serikali katika kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya na maji.

Aidha alisema baada ya kumalizika kwa ujenzi wa madarasa hayo,matundu ya vyoo,uzio pamoja na kuweka mabomba ya maji na sasa mpango uliopo ni kuendelea kuvunja madara manne mengine yaliyochakaa shuleni hapo ili kujenga upya na kutoa fursa kwa wanafunzi kujisomea bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yeyote ile.

UMMY MWALIMU AMPONGEZA NA KUMSHUKURU RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

UMMY MWALIMU AMPONGEZA NA KUMSHUKURU RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

June 27, 2017
IGA1
Matukio mbaljmbali zikionyesha matukio wakati wa ugawaji Viuadudu vya  kutokomeza Mbu wa Malaria Mjini kibaha.Pichani ni Waziri Ummy Mwalimu akigawa Viuadudu hivyo kwa Halmashauri kumi na moja
IGA2Na. Catherine Sungura na Benson Mwaisaka,WAMJW- Kibaha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amempongeza na kumshukuru  Mhe.Dkt. John Pombe  Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa  kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya malaria kwa kununua lita laki moja na kusambazwa kote  nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ugawaji  wa Viuadudu vya kutokomeza mbu wa malaria kwa halmashauri kumi na moja zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichpo Mjini Kibaha
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

June 27, 2017
wami1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN  alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
wami2 wami3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRNalipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
wami4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB)waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
wami5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la   wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
wami6 wami7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la   wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
 PICHA NA IKULU

KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

June 27, 2017

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa amekaa na watoto wa kituo hicho.
 Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.
 Ofisa  Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Grace Zikwaze, akizungumza na watoto hao.
 Keki maalumu ya hafla hiyo ikikatwa kwa pamoja. Kushoto ni Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobald Truphone na katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya Trumark.

UHAMIAJI TANGA WAANZISHA KUZUIZI MKATA KUWAKABILI WAHAMIAJI HARAMU

June 27, 2017
IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imeanza mikakati ya kukabiliana kwa vitendo na wimbi la wahamiaji haramu kuingia mkoani hapa kwa kuanzisha kizuizi eneo la Mkata wilayani Handeni kwa muda wa saa 24.
Hayo yalibainishwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga DCI, Crispin Ngonyani wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mipango waliojiwekea kuzibiti vitendo vya namna hiyo.

Alisema wameamua kuanzisha mpango huo kutokana na asilimia kubwa ya wahamiaji haramu hao wanapokuwa wamefika kwenye eneo hilo la kizuizi wanashushwa na kupakia pikipiki maarufu kama bodaboda na kuingia mkoani Tanga.

“Kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuweka kizuizi hicho ambacho kimekuwa ni eneo ambalo linatumika kuwafaulisha wahamiaji haramu kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kuzibiti suala hilo kwa vitendo “Alisema.

Aidha pia alisema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti maeneo yote ambayo yamekuwa na mianya ya kutumia kwa ajili ya kupitia ili kuweza kuhakikisha hawaingii mkoani Tanga.

“Lakini pia tuwatake wananchi kuhakikisha wanawafichua wahamiaji haramu pindi wanapokuwa wakiwaona kwenye maeneo yao kwani wamekuwa na madhara makubwa hivyo wanapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika “Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuwepo kwa watu wasiowaelewa kwenye maeneo yao ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.
‘Dunia Maridhawa’ ya TBL Group yaendelea kunyanyua wakulima wa Shayiri nchini

‘Dunia Maridhawa’ ya TBL Group yaendelea kunyanyua wakulima wa Shayiri nchini

June 27, 2017
tiz1
Meneja wa TBL kiwanda cha Arusha,Joseph Mwaikasu akimpatia maelezo
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba utekelezaji wa kushirkiana na wakulima unavyofanyika
tiz2.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba(kushoto)akimsikiliza Afisa Ugani kutoka TBL Group,Joel Msechu(kulia)
tiz3
Wakulima wa Shahiri  kanda ya kaskazini wakijifunza mbinu za kilimo bora katika maadhimisho ya siku yao15.Waziri wa Kilimo,Dk.Charles Tizeba akiongea na baadhi ya wakulima wilayani Monduli
tiz4
Wakulima wa Shahiri  kanda ya kaskazini wakijifunza mbinu za kilimo bora katika maadhimisho ya siku yao15.Waziri wa Kilimo,Dk.Charles Tizeba akiongea na baadhi ya wakulima wilayani Monduli
tiz5
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba(kushoto)akimsikiliza  akitoa maelezo kwa wakulima wa zao la shayiri
……………………………………………………………………………………………
-Wakulima wa shahiri waanika mafanikio waliyoyapata
 
Wakulima wa zao la Shayiri kanda ya Kaskazini wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameeleza kuwa ushirikiano huo umewawezesha kupiga  hatua mbalimbali za maendeleo kwa kuwa wanafanya kilimo wakiwa na uhakika wa kuuza mazao yao kwa bei nzuri.
Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shayiri kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika Kijiji cha  Emairete wilayani Monduli juzi,
Mwenyekiti wa umoja wa wakulima hao ,Bariki Kivuyo,alisema kuwa wanawezeshwa kuanzia kupatiwa mbegu,utaalamu wa kutunza mashamba na kupatiwa madawa na pembejeo za kilimo.
 
“Uwekezaji wa kampuni ya TBL Group katika kilimo ni mkakati ambao umesaidia wakulima wengi ambao hivi sasa wanafanya kilimo cha Shahiri kwa njia za kisasa na uzalishaji umeongezeka zaidi ambapo kwa sasa wanavuna  gunia kumi hadi 16 kwa heka moja badala ya gunia tano walizokua wanapata na kwa kuwa soko ni la uhakika  maisha ya wakulima wengi yamebadilika kuwa bora kwa kujenga nyumba nzuri,kusomesha watoto wao na kununua pembejeo za kisasa za kilimo”.Alisema Kivuyo.
 
Hata hivyo alizitaja changomoto zinazowakabili kuwa ni  pamoja  na miundombinu mibovu ya barabara inayoongeza  gharama za ziada kwa wakulima kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda kiwandani na kuiomba serikali iimarishe barabara zinazoingia na kutoka kwenye mashamba makubwa.

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO

June 27, 2017
Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .