WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA TRILIONI 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA TRILIONI 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND

January 30, 2024











Na. WAF – Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa kiasi cha Tsh. Trilioni 1.4 kutoka Global FUND ili kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote kwa malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030.

Upokeaji wa msaada huo umefanyika leo Januari 30, 2024 chini ya Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa pamoja wameshuhudia utiji saini wa makabidhiano ya msaada huo baina ya Global Fund na Serikali ya Tanzania.

“Msaada huu wa fedha unalenga kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote lengo likiwa ni kutekeleza malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030″.
Amesema Waziri Ummy
- Advertisement -


Waziri Ummy amewashukuru Global Fund kwa msaada huo mkubwa katika Sekta ya Afya na kwa kuridhia ombi la Sekta ya Afya kutumia frdha za msaada kutoka Global Fund kwa ajili ya kusomesha na kuwaajili wataalam wa Afya ngazi ya jamii (Community Health Workers) wapatao elfu Tano kwa kipindi cha miaka Mitatu ijayo ambapo wataalam hawa watasaidia kuleta mabadiliko ya utoaji wa huduma za Afya nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Global Fund katika sehemu ya High Impact Africa 2 Bw. Linden Morrison ameipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya Nne Kati ya nchi zinazopokea fedha hizo kutoka Global Fund.

“Lakini pia naipongeza Tanzania kwa kuendelea kutumia vizuri fedha hizo za msaada kutoka GLOBAL FUND ambapo Tanzania imefikia asilimia 92 ya utumiaji wa fedha hizo na hali hii inapelekea kuzifikia afua nyingi katika maeneo ya Kifua Kikuu, UKIMWI nà Malaria”. Amesema Bw. Morrison.

WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA BODI, MENEJIMENTI KWA KUING’ARISHA STAMICO

WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA BODI, MENEJIMENTI KWA KUING’ARISHA STAMICO

January 30, 2024



Waziri ya Madini, Mhe.Anthony Mavunde,akiipongeza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),mara baada ya kufanya kikao cha pamoja na bodi hiyo kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Micheal Isamuhyo,akizungumza wakati wa kikao cha Waziri ya Madini, Anthony Mavunde na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.


Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha pamoja na Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

Na Gideon Gregory Dodoma.

Waziri ya Madini,Mhe. Anthony Mavunde,ameipongeza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kwa kuendelea kukuza sekta ya madini nchini kwa kununua mitambo mikubwa ya kuchoronga miamba pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogo kukua.

Waziri Mavunde ametoa pongezi hizo leo Jijini Dodoma Januari 30,2024 alipokutana na Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO na ambapo amesema kuwa shirika hilo limekuwa liking’ara zaidi na kuwa moja kati ya mashirika ya umma yaliyopiga hatua kiasi cha kutoa gawio la bilioni 8 kwa serikali.

“Nitumie nafasi hii pia kuipongeza menejimenti ya shirika hili pamoja na wafanyakazi wake kwa kufanya kazi kwa bidii na kuliwezesha shirika lenu kuongeza mapato yake kutoka billion 1.4 hadi billion 61 kwa kipindi cha miaka minne iliyopita,”amesema.

Aidha amesema kuwa kazi kubwa imefanyika kuhakikisha STAMICO inafufuka kutoka kuwa moja ya mashirika yaliyotakiwa kufutwa hadi kuwa moja ya mashirika yenye tija kwa Taifa.

“Serikali sasa tunajivunia utendaji mzuri wenye tija wa shirika hili. Naipongeza bodi, menejimeti na wafanyakazi wa STAMICO kwa kazi nzuri mnayoifanya,” amesema Mavunde.

Aidha Waziri Mavunde amesema kuwa shirika la madini Tanzania STAMICO linao uwezo mkubwa wa kutatu tatizo la umeme nchi kwa ajili ya kuwagusa watanzania

“STAMICO kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati anaamini wakishirikiana wanaweza kuwasaidia Watanzania kupata umeme wa uhakika.”amesema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Micheal Isamuhyo amemshukuru Waziri Mavunde pamoja na uongozi mzima wa wizara kwa jinsi wanavyoshirikiana na shirika hilo katika mambo mbalimbali katika kuiletea maendeleo nchi pamoja na wizara hiyo.

Pia amemuahidi waziri huyo kutekeleza maagizo yote aliyowapatia hasa ikizingatiwa yanalenga kuendeleza sekta ya madini nchini.

UDSM YAJA NA VIPAUMBELE KUIMARISHA TAFITI NCHINI KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

January 30, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii wameadhimia kufikisha Tafiti zinazofanyika kusikika na kuchapishwa katika majarida ya Kimataifa kwa kuboresha machapisho na kuongeza nguvu katika majarida ya ndani kwa lengo la kuwa na maendeleo endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 30,2024 katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Christine Noe amesema ni vizuri kuzipatia thamani tafiti zinazofanywa nchini,kwa kuweka mazingira ya kuzipandisha katika viwango vya kimataifa katika majarida ya ndani.

"Kila kitu unachokiona cha kimataifa kimeanzia katika mataifa fulani, kwahiyo na sisi tunachojifunza kikubwa ni vizuri kukipa thamani ya Kimataifa vitu na tafiti, kama tutaboresha machapisho yetu na tukipandisha majarida yetu kimataifa italeta sifa kwa nchi". Amesema Prof. Noe.

Aidha Prof. Noe ameeleza kuwa majarida ya ndani yasipopewa nguvu nchi itapoteza kitu kikubwa na kukosea kuwa na maendeleo endelevu katika tafiti zinazofanywa.

"Tunashukuru wenzetu wamefanya tafiti na takwimu ya ile michakato kwahiyo tunaendelea kujadiri mambo haya maana ndio yanayo Jenga hata ile mijadara ya kitaifa "Prof. Noe ameeleza.

Pamoja na hayo amesema kuhusiana na changamoto ambazo wanakumbana nazo katika tafiti kufikia katika majarida makubwa ya nje ambapo imebua bidii ya kuandaa taarifa za tafiti zinazofanywa katika viwango vikubwa.

Kwa Upande wake Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Autonoma Barcelona-Prof. Dan Brockington amesema kuwa katika tafiti za kimataifa mafanikio makubwa yanapatikana kwa kushirikiana na mataifa mengine kwa kuongeza elimu na kutoa matokeo kwa pamoja ili kuinua ujuzi kwa watu wote.

Aidha ameeleza kuwa tafiti za nchini zimetawaliwa na ukimya mkubwa kwa sababu haziifikii jamii ya ulimwengu ingawa zipo katika viwango vya kimataifa ambapo amesema kasoro nijambo ambalo lipo katika tafiti nyingi ulimwenguni na jambo la msingi ni kutatua changamoto hizo.

Naye Mhadhiri Idara ya Sosholojia na Anthropolojia Kikuu Cha Dar es Salaam- Bw. Egidius Kamanyi amesema kuwa wamefahamu mapungufu ya machapisho yaliyokuwa yamechapishwa ambapo italeta mageuzi ya kukuza majarida ya ndani na kukuza katika viwango vya tafiti.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Autonoma Barcelona-Prof. Dan Brockington akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Autonoma Barcelona-Prof. Dan Brockington akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Autonoma Barcelona-Prof. Dan Brockington akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Autonoma Barcelona-Prof. Dan Brockington akisisitiza jambo wakati akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Christine Noe akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam
Mhadhiri Idara ya Sosholojia na Anthropolojia Kikuu Cha Dar es Salaam- Bw. Egidius Kamanyi akizungumza katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilichofanyika leo Januari 30, 2024 UDSM Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

CCM YAWATAKA VIJANA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

January 30, 2024

 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku kikiahidi kuwapa fursa kwa kuwapitisha kwa kuwa wanao uwezo wa kuongoza.



Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana katika mkutano mkuu maalumu wa ukaribisho wa wananchama wapya 1,167 wa Seneti ya Vyuo Vikuu wa DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki.


Kinana alisema Chama kinawategemea vijana kwa kuwa wanayo chachu ya mawazo kwa Chama, hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka bali watambue kuwa wao ni taifa la leo.


Alisema Chama kinawategemea kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa, hivyo watambue wao ni watu wa kisasa, wasomi na wanakwenda na kasi ya upatikanaji wa taarifa hususan kupitia mitandao ya kijamii.


"Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri, kutujenga na kutukosoa, tunakutegemeeni sana, toeni mawazo. mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, nawasihi vijana jitokezeni na gombeeni katika nafasi zote," alisema.


Kinana alisema Chama kitafanya kila linalowezekena kuwapitisha vijana wengi katika nafasi za kugombea kwani yeye na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan watafanya kila jitihada kuwapitisha vijana wengi.


"Nawasihi nendeni mkagombee nafasi zote na Chama tutatoa maelekezo kufanya linalowezekena kuhakikisha vijana wanapewa nafasi nanyi hakikisheni mnakipa ushindi Chama chenu," alisema.


Kinana alisema CCM ni kubwa, hivyo wanapaswa kukilinda, kujipanga, kuweka mikakati na kugawa majukumu.


Alisema yapo mambo yanayochangia kukipa ushindi Chama ukiwemo utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hivyo aliwataka vijana kuchagua viongozi wenye uwezo na sio wa kubebwa wala kutumia fedha kupata nafasi.


Hata hivyo, alisema Chama kisingependa kupata malalamiko bali kitachagua viongozi kulingana na sifa zao.


Kinana aliahidi kutoa kompyuta, mashine ya kuchapisha na ‘printa’ kwa vijana hao wajitegemee katika seneti yao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abas Mtemvu alisema ofisi ya Chama mkoa itachamgia sh. milioni mbili katika mfuko wa vijana zitakazosaidia kununua vifaa mbalimbali ambavyo vitawawezesha kujitegemea.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza na Viongozi na Wanachama  katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius  Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.(Picha na Fahadi Siraji wa CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi za CCM kwa  Wanachama   1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE patika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius  Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akizungumza na Viongozi na Wanachama  katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius  Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akisalimia Viongozi na Wanachama alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es Salaam.



Wanachama na Viongozi Mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE Mkoa wa Dar Es Salaam.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi za CCM kwa  Wanachama   1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE patika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius  Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
CHATANDA AWATAKA WABUNGE WANAWAKE WA CCM KUTIMIZA WAJIBU WAO KUWATUMIKIA WANAWAKE NA WANANCHI

CHATANDA AWATAKA WABUNGE WANAWAKE WA CCM KUTIMIZA WAJIBU WAO KUWATUMIKIA WANAWAKE NA WANANCHI

January 30, 2024

  Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,akizungumza katika Mkutano na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,akisisitiza jambo kwa Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima wakati wa kikao kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

  Baadhi ya wabunge wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,(hayupo pichani) wakati wa kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu ,Dodoma .

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amefanya Kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima lengo Likiwa ni Kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kuwatumikia wanawake na wananchi Nchini kwa kufanya Mikutano ya Hadhara ya kuisemea Miradi ya Serikali iliyofanywa na Serikali ya awamu sita chini ya uongozi wake Dkt Samia SuluhuHassan.

Akizungumza leo na Wabunge wanawake wa CCM Nchini Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi katika Mikoa yenu basi sasa niwaombe wabunge muendelea kutembelea miradi na kuisemea kwa wananchi ili wajue Serikali yao imefanya nini kwenye maeneo yenu.

Mwenyekiti Chatanda amewaomba Wabunge wanawake wa CCM Nchini kuendelea kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye Uchaguzi na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa ambayo utaaza hivi karibuni.

"Sisi ndio Jeshi la Mama basi niwaombe wanawake wenzangu mwende kwenye Mikoa yenu fanyeni Mikutano ya Hadhara na kuhamasisha wanawake kugombea kwani wanaweza endapo mkiwahamasisha watahamasika kwa kasi"

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema nimefurahishwa sana na baadhi ya wabunge wanawake ambao wanaendelea kupambana katika kuhakikisha wanafanya Mikutano ya Hadhara na kusemea miradi iliyofanywa katika maeneo yenu hivyo niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kusemea Serikali ya Rais samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti Chatanda amesema Wabunge wangu Nawapenda sana sana muendelea kupambana katika kuhakikisha wananchi na wanawake walipo katika maeneo yenu wajue nini Serikali yao inafanya katika kuwaletea Maendeleo.

Nae Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari amewapongeza wabunge wanawake kwa kufanya kazi katika Mikoa yao na kuwaomba kuendelea na juhudi hizo katika kusemea miradi na kusikiliza kero za wanawake na kuweza kutatua kwa wakati.

"Sisi kama viongozi wenu tupo pamoja na nyie katika kutatua changamoto yoyote ambayo inakwamisha kazi zenu na niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kutatua Migogoro na changamoto zilizopo katika maeneo yenu."

Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jokate Mwegelo amewashukuru wabunge wanawake kwa kujitoa kwa wingi kuja kusikiliza Mwenyekiti na kuwaomba yale yote ambayo Mwenyekiti kazungumza basi yafanyiwe kazi ipasavyo kwa Maslai ya Jumuiya yetu ya Wanawake.

WATAALAMU SEKTA YA MIPANGO MIJI WAKUTANA KUJADILI MAPITIO YA RASIMU YA KANUNI MPYA ZA SHERIA YA MIPANGO MIJI

January 30, 2024

 





 

Na Eleuteri Mangi, WANMM

Wadau wa sekta mipango miji wamekutana Jijini Dodoma kujadili rasimu ya marekebisho ya Kanuni za Sheria za Mipango Miji nchini ili ziendane na mabadiliko ya kasi ya ukuaji miji pamoja mchango wake wa sekta hiyo katika hafua muhimu za kuifadhi mazingira. 

Akifungua kikao hicho Januari 30, 2024 jijini Dodoma, Naibu Katibu Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera amesema kuwa ardhi inahitaji kupangwa, kupimwa, kumilikishwa na kuendelezwa ikiwa katika hali nzuri kiuchumi, kijamii na kimazingira.

“Natambua ili kufanikisha azma hii, tunahitaji kuwa na kanuni sahihi za kuongoza upangaji wa miji yetu pamoja na matumizi mbalimbali ya ardhi hapa nchini” Naibu Katibu Bi Kabyemera.

 Upangaji miji unaongozwa na Sheria ya Mipango Miji sura Na. 355 na Kanuni zake za mwaka 2018 ambazo zinahitaji kuboreshwa kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kimazingira, mitazamo ya kimaisha, kimaendeleo pamoja na mitazamo ya kimataifa vimekuwa msingi wa kupitia upya kanuni hizo ili ziendane na hali ya sasa.

Wadau hao ni pamoja na Manejimenti ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi kutoka mikoa ya Tanzania Bara, wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali, taasisi za Serikali pamoja na zisizo za Serikali.

TANZANIA YASISITIZA MPANGO WA MATTEI UZINGATIE MAHITAJI STAHIKI YA AFRIKA

January 30, 2024

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia. Katika Mkutano huo, Mhe. Makamba anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia. Katika Mkutano huo, Mhe. Makamba anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi mbalimbali walioshriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia wakiwa katika picha ya pamoja.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia amesisitiza umuhimu wa mpango wa Mattei kuzingatia mahitaji sahihi ya Afrika ili uweze kuleta matokeo stahiki barani Afrika.

Mheshimiwa Makamba alieleza kuwa mpango huo ukizingatia mahitaji stahiki ya Afrika changamoto nyingi zinazokabili nchi zilizoendelea zinazosababishwa na ukosefu wa maendeleo barani Afrika zitaondoka.

Awali akihutubia katika mkutano wa Nne wa Italia-Afrika, Waziri Mkuu wa Italia, Mhe. Giorgia Meloni amesema mpango wa Mattei utagusa masuala ya usalama wa nishati na matumizi ya nishati mbadala, maendeleo ya miundombinu, usalama wa chakula, elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na kupambana na wahamiaji haramu, ameeleza

Serikali ya Italia inatarajia kushiriki kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo barani Afrika kwa kupitia Mpango wake Mpya wa Mattei.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat ameomba Afrika ipewe muda wa kuchanganua Mpango wa Mattei kwanza kabla ya kuanza utekelezaji wa mpango huo.

"Tunahitaji kubadilisha maneno kuwa vitendo kwa sababu ni vyema tukajadiliana na kuona ni njia gani zinatumika kutekeleza miradi inayopendekezwa katika Mpango wa Mattei ili kuepuka kuwa na furaha na ahadi ambazo hazitekelezwi,” amesema Mahamat.

Viongozi wakuu wa baadhi ya nchi za Afrika, mawaziri, maafisa waandamizi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, wawakilishi kutoka taasisi na mashirika ya kimataifa wafanyabiashara pamoja na mashirika ya kifedha wameshiriki mkutano huo unaoendelea Roma, Italia.

PINDA AWAFUNDA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI MWANZA

January 30, 2024

 Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geophrey Pinda amewafunda watendaji wa sekta ya ardhi katika jiji la Mwanza kwa kuwataka kusimamia sekta hiyo kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozi ya sekta hiyo.

Amesema, kwa kufanya hivyo Wizara ya Ardhi itaweza kuepukana na migogoro ya ardhi isiyo na lazima aliyoieleza kuwa imeendelea kuibuka kila kukicha katika maeneo mbalimbali.

Mhe Pinda alisema hayo tarehe 29 Januari 2024 alipokutana na wakuu wa idara na vitengo wanaosimamia sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na wale wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake mkoani humo.


"Ninyi ndiyo wasimamizi wa sekta hii ya ardhi katika jiji la Mwanza hivyo mnao wajibu mkubwa wa kufuata kanuni, taratibu na miongozo ya sekta hii ili kuepusha migogoro ya ardhi" alisema mhe. Pinda

Amewataka wakuu hao wa idara na vitengo kuwa washauri wazuri wa wakurugenzi wa halmashauri zao ikiwemo kuzishauri halmashauri kuwa na benki za ardhi katika maeneo yake.

"Ninachotaka kuwaambia silka yangu ni kuwapitisha katika maeneo mnayoyasimamia na hii itawasaidia kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha"alisema Mhe. Pinda.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi amehimiza suala la upendo miongoni mwa watumishi wakati wote wa utendaji kazi kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuwawezesha wakuu hao wa idara na vitengo kufanya kazi bila kulaumiwa.

Vile vile, Mhe. Pinda amewataka wakuu wa idara na vitengo katika sekta ya ardhi kuwa na mipango madhubuti itakayofanikisha kuzuia ujenzi holela pamoja na kuhakikisha maeneo ya wazi yanalindwa.

Amewaasa watendaji hao kuhakikisha wanatatua mgogoro ya ardhi katika maeneo yao kwa busara ikiwemo kufanya vikao vya kumaliza tofauti kwa amani.

Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Happiness Mtutwa alimshukuru Naibu Waziri wa Ardhi kwa kuwafunda na kuwapa elimu na maelekezo na kusema hilo ni jambo muhimu sana katika kuiboresha sekta ya ardhi.

Alisema wao kama wakuu wamepokea maelekezo na namna ya kuyashusha kwa watumishi wa chini ili mwisho wa siku maeneo wanayoyasimamia yawe salama.

"Nikutoe hofu mhe waziri ofisi ni taasisi na mara nyingi tumekuwa tukifanyia maelekezo tunayopatiwa na nikuahidi kutekeleza maelekezo na ushauri ulioutoa kwetu kwa kuwa ndiyo msingi wa kuiboresha sekta ya ardhi nchini.’’ Alisema Happy.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Gephrey Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo wanaosimamia sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na wale wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake mkoani humo tarehe 29 Januari 2024.
Mhe. Geophrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa na wakuu wa idara na vitengo wanaosimamia sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na wale wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake mkoani humo tarehe 29 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Gephrey Pinda akizungumza na wakuu wa idara na vitengo wanaosimamia sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na wale wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake mkoani humo tarehe 29 Januari 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

KISHINDO KIKUBWA KUWEKWA WAKFU NA KUSIMIKWA KWA ASKOFU JOVITUS MWIJAGE WA JIMBO LA BUKOBA

January 30, 2024

 

Askofu mwijage (katikati) mwenye fimbo akiwa na baadhi ya maaskofu waliohudhuria ibada hiyo
Askofu Mwijage akikabidhiwa fimbo na Kardinali Rugambwa wa Jimbo Kuu la Tabora katika ibada hiyo.
Msemo wa kihaya usemeo “Tikiliwa Igamba”ambalo tafsiri yake ni “tukio ambalo litabaki simulizi” ulidhihirika wakati wa tukio kubwa la kihistoria la kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Jovitus Francis Mwijage, wa jimbo la Katoliki la Bukoba, lililofanyika mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mikimiki na shamrashamra za maandalizi ya tukio hilo kubwa la kihistoria katika jimbo la Bukoba ilianzia kwenye ngazi za familia za wakristo, Vigango, Parokia mpaka jimboni ambako ilihitimishwa na misa takatifu iliyofanyika katika uwanja wa Kaitaba ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu wa Waziri wa Nishati, Mh. Doto Biteko, aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Samia Suluhu Hassan.

Misa hiyo iliyoongozwa na Kardinali Protace Rugambwa, Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora akisaidiana na aliyekuwa Msimamizi wa Kitume jimbo la Bukoba, Askofu Methodius Kilaini na Askofu Almachius Rweyongeza wa Jimbo la Kayanga, ilihudhuriwa na maaskofu kutoka majimbo mbalimbali nchini, viongozi wa Serikali mkoani Kagera wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Fatma Mwassa ,watawa wa kiume na kike, viongozi wa maadhehebu mbalimbali , maelfu ya waumini kutoka parokia mbalimbali za jimbo Katoliki la Bukoba na majimbo jirani waliojawa na bashasha na furaha ya kumpata Askofu mpya.
Kwaya mbalimbali zikitumbuiza wakati wa kumkaribisha Askofu Mwijage katika makazi yake yaliyopo Ntungamo Bukoba.

Pia ibada hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Acattino.

Vikundi mbalimbali vya kwaya kuanzia za watu wazima mpaka za watoto zilizoimba katika ibada hiyo zingine kwenye maandamano kwenye sehemu za barabara alizopita Askofu Mwijage kutoka Rwamishenye hadi kanisa kuu la jimbo zilileta shamrashamra ya pekee katika mji wa Bukoba na vitongozi vyake bila kusahau wananchi wengi waliojipanga misururu barabarani kumshangilia bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha katika maeneo mbalimbali mjini humo.

Pia kulikuwepo na tukio la mkesha wa ibada ya Masifu ya jioni iliyoongozwa na Askofu Flavian Kassala, wa Jimbo Katoliki la Geita, ambayo ulihudhuriwa na waumini wengi wakiwa wanasubiri tukio hili muhimu la kihistoria kwa shauku kubwa.
Askofu Mwijage akikaribishwa katika makazi yake yaliyopo Ntungamo Bukoba.
Askofu Mwijage akikaribishwa katika makazi yake yaliyopo Ntungamo Bukoba.

Akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan, katika ibada hiyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mh.Doto Biteko, alisema Serikali itampa ushirikiano Askofu Mwijage na kanisa Katoliki ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Dk.Biteko, alisema Rais Samia amehimiza umuhimu wa kujenga Taifa lenye uhuru na haki kwa kuwa haki ulijenga Taifa na kusisitiza kuwa zipo changamoto zinazotukabili kama Taifa ambazo ili kuziondoa kunahitaji kuwepo na ushirikiano miongoni mwetu licha ya kutofautiana kwa mawazo na mitizamo.

Akizungumzia utendaji wa Akofu Mwijage, Dk. Biteko, alisema waumini wa Katoliki wa Bukoba wamempata kiongozi wa kiroho, Mchumi, mlezi na mbunifu anayetegemewa na wengi kuwafundisha na kuwaelekeza katika njia sahihi za kiroho na kimwili.

Awali akizungumza kabla ya kumweka wakfu, Kardinali Rugambwa, amemkubusha askofu Mwijage, kuzingatia nafasi aliyokabidhiwa kuwa ni mali ya Kristo hivyo aishi kwa wito kutekeleza utume wake kwa kumsikiliza Kristo.

“Wapende pia watawa wa kiume na wa kike ukiwaamini na kukuza mchango muhimu katika utume hapa Bukoba, wapende waamini na walei ukiwaalika na ukiwahamasisha kushiriki kikamilifu katika maisha, utume wa kanisa ili jimbo la Bukoba lipate sura ya kisinodi ya kutembea pamoja, ”alisema.

Akiongea katika ibada hiyo, Askofu Mwijage ambaye amechukua nafasi ya Askofu Desderius Rwoma aliyestaafu mwaka 2022 ,aliahidi kushirikiana na mapadri kuendeleza pale alipoacha mtangulizi wake “Kwa mapadri, watawa wa kike na wa kiume wote nawaita kuendeleza jimbo letu,watanguzi wetu walifanya kazi nzuri iliyotukuka ninawaomba tuunganishe vipaji vyetu kuendeleza jimbo kiroho na kiuchumi”,alisisisitiza.

Tukio hilo la kihistoria katika kanisa kwenye jimbo Katoliki la Bukoba liliambatana na habari ya kustaafu kwa aliyekuwa Msimamizi wa Kitume jimbo la Bukoba, Askofu Methodius Kilaini ambaye amelitumikia kanisa kwenye nafasi mbalimbali kwa uadilifu mkubwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50.
Kwaya mbalimbali zikitumbuiza wakati wa kumkaribisha Askofu Mwijage katika makazi yake yaliyopo Ntungamo Bukoba.
Askofu Mwijage akikaribishwa katika makazi yake yaliyopo Ntungamo Bukoba.

Askofu Mwijage alizaliwa Bukoba, Desemba 2, 1966, baada ya masomo ya kipadre, Julai 20, 1997 alipewa daraja takatifu la la upadre.

Amefanya kazi katika parokia mbalimbali katika jimbo la Bukoba ikiwemo kuwa mwalimu na mlezi katika seminari ndogo ya Rubya.

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2011 alitumwa na jimbo la Bukoba kwa ajili ya kujiendeleza kwa masomo ya juu na hivyo kupata shahada ya uzamivu kwenye historia ya kanisa mwaka 2011.

Kati ya mwaka 2011-2012 alikuwa jaalimu wa historia ya Kanisa Seminari Kuu ya Segerea. Mwaka 2012 hadi 2023 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS, Tanzania.
Kuanzia mwaka 2012 hasi uteuzi wake Oktoba 19 mwaka jana,alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja waMapadre Wazalendo Tanzania (UMAWATA) na kuanzia mwaka 2020 ni Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Uchumi ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS.
-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 735 997 777 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI MWANZA

RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI MWANZA

January 30, 2024




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
Baadhi ya Machifu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana tarehe 30 Januari, 2024.
Baadhi ya Viongozi wa dini pamoja na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielekea kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi vya ngoma Chapakazi kutoka Ilemela na Buyegi kutoka Kisesa Magu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi na ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Msanii Dullah Makabila akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi na ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.