WAZIRI UMMY MWALIMU KUZINDUA KAMPENI YA WAZEE KWANZA

April 06, 2016

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wandishi wa habari juu ya uzinduzi wa kampeni ya Wazee kwanza toa kipaumbele apate huduma, leo Mkoani Morogoro kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kibwe Stephen.


Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima y Afya (NHIF) Michael Mhando Akizungumaza na wazee wa Mkoa wa Morogoro leo`
Wazee wakimsikiliza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu .(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii-Morogoro ).

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI NA RAIS KAGAME WAKIWA NCHINI RWANDA

April 06, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bi Tonia Kandiero, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Rusumo linalounganisha nchi za Rwanda na Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiweka jiwe la ufunguzi la kituo cha pamoja cha huduma za mpakani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa daraja la Rusumo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Rusumo mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bi Tonia Kandiero, pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakipita kwenye Daraja la Rusumo mara baada ya ufunguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasili kwenye ardhi ya nchi ya Rwanda na kulakiwa na kikundi cha ngoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kutoa hotuba yake kwa upande wa Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Kagame katika mazungumzo rasmi baina ya nchi hizo mbili nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Rusumo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakielekea jukwaani mara baada ya kuwasili Rusumo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakizungumza jambo kabla ya ufunguzi wa daraja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika eneo la Rusumo Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya ukaguzi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani huku Rais wa Rwanda Paul Kagame akifurahia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia upande wa Rwanda katika eneo la Rusumo. Picha na IKULU

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM,

April 06, 2016

Kaimu Mhariri Mtendaji wa Uhuru ublications Limited, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Ramadhani Mkoma, akimweleza jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaa Kikwete alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Uhuru Publicatiions Ltd  alipotebelea kampuni hiyo leo. Pamoja naye ni Msemaji wa CCM, Cliristopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa Bodi ya Uhuru Media, Adam Kimbisa.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni alipoingia katika Ofisi za Uhuru FM leo. Wengini ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, Adam Kimbisa na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
Baadhi ya wayanyakazi wa UHURU FM wakiwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia studio wa Uhru FM. KWA PICHA KIBAO ZA UPL NA UHURU FM>BOFYA HAPA
WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KIKAZI IFAKARA, MOROGORO

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KIKAZI IFAKARA, MOROGORO

April 06, 2016

8560f637-78b3-467f-95ea-e2f591c0189a
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi katika hospitali ya Rufaa ya St. Francis pamoja na wajawazito wanaosubiri kujifungua na ambao wapo chini ya uangalizi wa madaktari.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya siku 1 mjini Ifakara kufuatilia utendaji wa shughuli mbalimbali za Afya Wilayani Kilombero, Morogoro.
Katika ziara hiyo, Mhe Ummy ambae alieambatana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe Florence Tonguely-Mattli alifungua kozi ya miezi mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kina mama wajawazito hususani katika eneo la upasuaji na utoaji wa dawa za usingizi.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH) chini ya Mradi wa “Upatikanaji wa Uzazi Salama Tanzania” yanawahusisha Washiriki 70 kutoka mikoa ya Morogoro, Njombe na Mbeya.
Mhe Ummy pia alikagua shughuli mbalimbali za taasisi za afya ikiwemo kutembelea Taasisi ya Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute), Hospitali Teule ya Rufaa ya St. Francis, Chuo cha Uunguzi cha Edgar Malanta na Chuo Kikuu cha Tiba cha St. Francis.
0f1f0d9a-ef44-4d26-bb82-c85e3a577fd9
2da305bb-0c4e-49f9-953c-105cabb0c669
69adfba7-e3c5-42fd-a407-ff0981d8fccd
449c9d9c-134c-4d45-b132-66e5ecab2fb1
Mhe Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH) Prof. Pemba, Balozi wa Uswisi nchini Mhe Florence Tonguely-Mattli.
3527b65c-f43a-4359-bc0b-9a25fefda589
Picha ya pamoja.
b85fa399-431e-4ade-84c1-c55a1076097e
d7d05480-8495-4f65-ae56-423c9a313630
eea390ef-f89d-458f-92b7-145abb5e19c8
Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na washiriki wakati wa kufungua mafunzo ya miezi mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kinamama wajawazito mjini katika taasisi ya TTCIF, Ifakara.
f92df671-ceb3-45a5-8093-a889995f1267
TFF KUWACHUKULIA HATUA KALI,VIONGOZI NA WATUMISHI WAKE

TFF KUWACHUKULIA HATUA KALI,VIONGOZI NA WATUMISHI WAKE

April 06, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa zilizosambaa katika mitandao kuanzia jana zikiwahusisha viongozi wa timu moja ya daraja la kwanza na baadhi ya watumishi wa TFF.
Pamoja na kwamba taarifa hizo zilizosambazwa hazihusiani na kesi ya kupanga matokeo iliyoamuliwa siku ya tarehe 03/04/2016, TFF inachunguza kubaini uhalisia (authenticity) wa taarifa hizo na itachukua hatua kali sana kwa watumishi wa shirikisho na viongozi wa timu husika watakaobainika kushiriki vitendo vilivyo kinyume na maadili ya mpira wa miguu.
TFF imekwishaweka bayana nia ya kupambana na yeyote atakayehusika katika upangaji matokeo na uhalifu mwingine unaoharibu ustaarabu wa mpira kwa njia yoyote ile.
Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa onyo kwa baadhi ya viongozi, watumishi wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla wanaotumia majina ya viongozi wa juu wa TFF katika kufanikisha mipango yao kwa manufaa binafsi.
TFF inawaomba wapenda mpira wa miguu kuwa watulivu na waangalifu wakati  suala hili linashughulikiwa.
Aidha, kuhusu hukumu ya Kamati ya Nidhamu ya TFF ni muhimu ikaeleweka wazi kwamba zipo taratibu za kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni ili upande usioridhika na maamuzi yanayotolewa uweze kuhoji maamuzi husika.
Ni vema tukaacha kamati huru zifanye kazi zake kwa mujibu wa taratibu. Kutoa hukumu  mtaani au kwenye vyombo vya habari kunaweza kuwanyima haki wanaostahili na kutengeneza kichaka cha kujificha watenda maovu.

STARTIMES YAPELEKA VIZIMBUZI BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANANCHI WAFURAHIA

April 06, 2016
 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, Salimu Juma Mavaga (kushoto), akizungumza wakati wa kupokea vizimbuzi 'ving'amuzi' vya Kampuni ya StarTimes vilivyo tolewa kwa gharama ya sh,50,000 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya  Yombo, Chasimba na Maimbwa wilayani humo jana.
 Bibi Maendeleo ya Ustawi wa Jamii wa Kata hiyo, Melitha Kiwanga akizungumza katika mkutano huo wakati akiishukuru kampuni ya StarTimes kuwapelekea vizimbuzi hivyo.
 Meneja Mauzo wa StarTimes, Tanzania, Tang Jing Yu akizungumza katika mkutano huo kuhusu ugawaji wa vizimbuzi hivyo na nia ya Rais wa China ya kusaidia nchi za Afrika katika mfumo wa mawasiliano wa Kidigitali.
 Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa wa Idara ya Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Mayala.
 Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba, akizungumza kwenye mkutano huo wakati akiishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo na kwenda kufungiwa.
 Wakina mama wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo.
  Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba (kushoto), akimshukuru Meneja Mauzo wa StarTimes, Tang Jing Yu kwa kuwapelekea huduma hiyo ya vizimbuzi katika karafa yao.
 Mwalimu Hilda Stambuli wa Shule ya Msingi ya Yombo akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Tang Jing Yu (wa tatu kushoto), akimkabidhi  Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah (wa pili kulia), Kizimbuzi na Dishi lake baada ya kulipia sh.50,000 katika hafla iliyofanyika Kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Juma Mavaga na Fundi Mkuu wa StarTimes Michael Mkufya.
 Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kata ya Yombo, Ramadhan Kibwana Shomari (wa pili kulia), baada ya kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa StarTimes, Michael Mkufya.
 Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kijiji cha Chasimba,Miraj Mukadase (wa pili kulia), baada ya kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa StarTimes, Michael Mkufya.
 Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah  akisaini fomu za malipo kabla ya kukabidhiwa kizimbuzi chake pamoja na Dish. Kulia ni Ofisa Idara ya Mauzo wa StarTimes, Joanna Nuhu.
 Wananchi wakisubiri kulipia vizambuzi kabla ya kwenda kufungiwa.
Walimu wa Shule ya Msingi ya Yombo wakiwa na madishi yao wakienda kufungiwa baada ya kulipia.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Vizimbuzi ya StarTimes Tanzania imetoa vizimbuzi 50 kwa bei ya sh.50,000 kwa vijiji vitatu vya Matimbwa, Chasimba na Yombo vilivyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vizimbuzi hivyo kwa wananchi wa vijiji hivyo, Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Tang Jing Yu alisema lengo lao kubwa ni kusogeza huduma ya kidigitali kwa wananchi.

"Kampuni yetu imejipanga kuhakikisha inasaidia watu wa vijijini kupata huduma nzuri na kuwanufaisha katika mfumo wa kidigitali" alisema Jing Yu.

Jing Yu alisema kwa awamu ya kwanza wameanza kwa kusambaza vizimbuzi 50 chini ya mradi huo katika vijiji hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wao wa China za kusaidia nchi za Afrika kidigitali hasa katika maeneo ya vijijini.

Alisema China inajisikia fahari kubwa kuona wananchi wa Afrika wananufaika na mradi huo na kwa hapa Tanzania wameanza katika eneo hilo la Bagamoyo lakini lengo likiwa ni kuvifikia vijiji vingi zaidi.

Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala alisema kabla ya kuanza mradi huo waliwatembea wananchi na kuzungumza nao na kujionea changamoto kubwa ya kukosa mawasiliano hayo ya kidigitali.

Alisema kampuni hiyo imetoa vizimbuzi hivyo kwa watu 50 wa vijiji hivyo ambapo watatumia kwa kipindi cha mwezi mmoja bila ya kulipia na amewataka wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo Rashid Kiwamba alisema kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu ni fursa kwao hasa katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia ambapo dunia imekuwa ni kijiji kimoja.

Kiwamba alisema kwamba mradi huo uliopelekwa na StarTimes ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.John Magufuli aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu za kuhahikisha huduma mbalimbali zinawafikia wananchi ikiwa ni pamoja na mawasiliano.

"Mradi huu tulioletewa na hawa ndugu zetu wa StarTimes ni mzuri na ni mwanzo mzuri na mambo mengi mazuri yanakuja hapa kwetu Yombo ni muhimu wananchi kuuchangamkia" alisema Kawamba.

Mkazi wa Kijiji cha Chasimba Miraj Mukadase aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea mradi huo ambao utawasaidia kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.

"Tulikuwa tukikosa taarifa mbalimbali kwa kuwa tulishindwa kupata vizimbuzi vya bei nafuu na vilivyobora ambapo vilikuwa vikuzwa hadi sh.120, 000 lakini leo hii StarTimes wametukomboa tunawapongeza sana" alisema Mukadase.





KID BWAY ATAMBULISHWA RASMI LAKE FM MWANZA

April 06, 2016
Baada ya Watu wengi kujiuliza maswali mengi juu ya alipo Sandu George, maarufu kwa jina la Kid Bway (Pichani), ambae kwa muda mrefu amejizolea sifa kubwa katika tasnia ya utangazaji na uandaaji wa muziki, ukweli ni kwamba amejiunga na kituo kipya cha redio Jijini Mwanza kiitwacho Lake Fm, Raha Ya Rock City.

Katika kurasa za Mitandao ya Kijamii za redio hiyo, kuna post ya kumtambulisha Kid Bway iliyokuwa ikisomeka "Wananzengo tunayo Furaha Kumtambulisha Mwananzengo Kid Bway @kidboytz ambae ni Mtangazaji na Mkuu wa Vipindi 102.5 Lake Fm Mwanza. 

Raha yake ya Rock City ni Kuona Vipaji vya Wasanii wa Mwanza vinakua na Kutambulika hadi ngazi ya Kimataifa.
JE WEWE RAHA YAKO YA ROCK CITY NI NINI?
Follow ‪#‎LakeFm Instagram, Twitter & Facebook @lakefmmwanza
‪#‎RahaYaRockCity #‎RadioYaWananzengo".
MARAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI WA TANZANIA NA PAUL KAGAME WA RWANDA WAZINDUA DARAJA LA LUSUMO

MARAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI WA TANZANIA NA PAUL KAGAME WA RWANDA WAZINDUA DARAJA LA LUSUMO

April 06, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Rwanda ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Mh. Paul Kagame wa Rwanda kwenye mpaka wa Rusumo ambapo viongozi hao wote kwa pamoja wamefanya tukio la Kuzindua daraja la Lusumo linalounganisha nchi za Rwanda na Tanzania na pia wamezindua kituo cha Forodha kilichopo upande wa Rwanda katika mpaka huo, kama wanavyoonekana wakikata Utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la Lusumo watatu kulia katika picha ni Mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia Kandiero,  kutoka kulia ni  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba na Waziri wa Ujenzi Tanzania Mh. Profesa Makame Mbarawa
lsm1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli  na mwenyeji wake Rais Mh. Paul Kagame wa Rwanda pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika uzinduzi huo wakipiga makofi mara baada ya kulizindua rasmi, watatu kulia katika picha ni mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia Kandiero,  kutoka kulia ni  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba na Waziri wa Ujenzi Tanzania Mh. Profesa Makame Mbarawa
lsm2
Daraja la Lusumo linalounganisha nchi za Tanzania na Rwanda linavyoonekana mara baada ya kuzinduliwa na marais hao leo.
lsm3
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli  na mwenyeji wake Rais Mh. Paul Kagame wa Rwanda pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiuo cha Forodha katika mpaka wa Rwanda na Tanzania uliopo Lusumo katika picha kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mh. Agustine Mahiga na Mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia Kandiero pamoja na balozi wa  Japan na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
kagm
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli  na mwenyeji wake  Rais Mh. Paul Kagame wa Rwanda pamoja na wake zao Mama Janet Magufuli na Mama Jeannette Kagame mabalozi, Mawaziri  wa nchi hizi mbili pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kituo cha Forodha kilichopo Lusumo  mpakani mwa Tanzania na Rwanda
lsm4 
Jiwe lenye kibao linaloelezea uzinduzi huo na lenye majina ya viongozi wa nchi hizo mbili za Rwanda na Tanzania.