KOROGWE MABINGWA COPA COCA COCA TANGA.

August 14, 2013
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA TANGA(TRFA),SAID SOUD AKIZUNGUMZA NA TIMU YA WILAYA YA MUHEZA MARA BAADA YA KUMALIZIKA MCHEZO HUO.





KOROGWE WATAWADHWA KUWA MABINGWA WA COPA COCA COLA MKOA.

August 14, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU ya soka wilaya ya Korogwe leo imetawadhwa kuwa mabingwa wapya wa Mashindano ya Vijana ya Copa Coca Cola ngazi ya mkoa baada ya kufanikiwa kuichapa Muheza mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Mchezo huo ambao ulianza majira ya saa nane mchana ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia ambapo hadi timu zote zinakwenda mapumziko,Korogwe walikuwa wakiongoza bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani hapo zikiwa na hari ya mchezo baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake.

Mabao ya Korogwe yalifungwa na Erick Msagati ambaye alipachika mabao yote kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.

CHIZA ADAM KINDA WA MIAKA 12 ALIYEKUSUDIA KURITHI NAMBA YA SULEIMAN KASSIM SELEMBE KATIKA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR (ZANZIBAR HEROES) .

August 14, 2013
NA MASANJA MABULA,PEMBA.
Kwa wale ambao walikuwa wakifuatilia kwa karibu michuano ya vijana waliochini ya umri wa miaka 15 iliyomalizika hivi karibuni katika shehia za Tondooni na Makangale Wilaya ya Micheweni waliridhika na kiwango kilichooneshwa na kinda Chiza Adam wa timu ya Chuo Kids .
Kinda huyo anayemudu kucheza nafasi ya kiungo mshambauliaji (namba nane)aliiwezesha timu yake kuibuka bingwa wa michuano hiyo iliyoandaliwa na mwandishi wa makala haya na kupata ufadhili kutoka shirika la habari la Korea CTS ,  chini ya usimamizi  wa mchungaji Samwel  E. Maganga wa kanisa la TAG .
Katika michuano hiyo kinda huyo alionesha uwezo mkubwa na hivyo kuwa  ni gumzo kwa mashabiki waliokuwa wakifuatilia michuano hiyo ambayo ilizishirikisha timu tisa ambapo pia aliibuka kuwa mchezaji bora .
Uwezo mkubwa wa kupiga chenga ,kumiliki mpira ,  kutoa pasi za mwisho pamoja na kufunga mabao ulisababisha viongozi na wachezaji wa timu pinzani kuumiza vichwa kutafuta mbinu za kumzuia ili asisababishe madhara katika lango la timu zao .
Pia uwezo wake wa kupanda na kushuka , kukimbia na mpira na kupiga mpira akiwa katika mwendo ni moja ya vitu alinavyo navyo kinda huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Skuli ya Msingi ya Makangale,  vitu ambavyo ni adimu kwa wachezaji wengi hapa nchini .
“ Wakimkapa huyo anayeitwa  ‘Selembe’ katikati , Chuo Kids hawawezi kufunga bao , lakini hakabiki ni majanja ajabu kwani anatumia akili zaidi na hatabiriki atafanya nini na kwa wakati gani , huyu dogo ni hazina ya taifa kwa siku za baadaye ” alisikika mlezi wa Timu ya Maji Maji ya Tumbe Hamad Haji wakati wa fainali ya michuano hiyo .  
Akizungumza na makala haya Chiza amesema kuwa lengo lake ni kutaka kuichezea Timu ya Taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) huku akitamani kufuata nyayo za mshambuliaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga Suleiman Kassim Selembe .
Amesema kuwa amekuwa akifuatilia sana kila inapocheza timu ya Taifa ya Zanzibar na pia hufarajika kusikia au kuona kinsi mchezaji huyo anavyokimbia na mpira pamoja na staili ya uchezaji wake .
“ Nimeanza kumfuatilia Selembe tangu akiwa na Timu ya Azam FC na kipindi hicho nikuwa naishabikia Azam , lakini mara baada ya Selembe kuhamia timu ya Coastal Union , mimi siku hizi naipenda Coastal ” alifahamisha .
Ameeleza kwamba siku zote amekuwa anajaribu kuiga uchezaji wa Seremba , jambo ambalo lilimfanya abadilishe namba kutoka kiungo mkabaji na kuwa kiungo mshambuliaji na wakati mwengine kucheza kuingo wa Pembeni ( namba saba ) .
Staili hiyo ya kumuiga mchezaji huyo  , Chiza amelezimika kubadili hata jina na kutaka aitwe  Selembe pindi awapo uwanjani ambapo baadhi ya wachezaji wenzake amegombana nao kwa kushindwa kumuita Seremba na badale yake kumuita Chiza .
Aidha Kinda huyo ambaye pia ni shabiki wa klabu ya Barcelona  alisema pamoja na kuishabikiana kuipenda klabu ya Coastal Union pia ndoto zake mbali na kuichezea timu ya Taifa ya Zanzibar , anatamani kucheza soka la kuliwa katika viwanja vya Nocamp .
“ Kwa Ulaya naipenda timu ya Barcelona , kwani inacheza mzuri ambapo wachezaji wote wanashambulia , wanacheza pasi fupi fupi naaimini juhudi zangu ndizo zitakazotimiza  ndoto yangu  hiyo  ”alieleza Chiza anayevaa jezi  namba kumi (10)  ambayo inavaliwa na Lionel Messi .
Chiza ambaye ni mtoto wa pili katika familia ya Adam Pesa Mbili Shija na mama Fortinata Majaliwa yenye watoto wawili alizaliwa mwaka 2001 katika Kijiji cha Mbuzini Unguja na alihamia Pemba baada ya akiwa na umri wa miaka wa nane baada ya wazazi wake kudai kwamba hafuatilii masomo ambapo anajishughulisha zaidi na mpira .
Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Chuo Kids Stanslausi Markus Stanslausi (Kibabu)  aliiambia makala haya kwamba Chiza ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu , anasikiliza na anafuata kile anachofundishwa pia ni mwepesi ya kushika mafundisho .
Amesema kuwa kutokana na sifa alizonazo kinda huyo kwa amemteuwa kuwa Kocha Msaidizi wa Timu hiyo akimsaidia Ali Makame Ali na wameweza kushirikiana na kuweza kuipa mafanikio timu yao .
“ Anaweza kufika mbali kisoka kwani anajituma , ana nidhamu ya hali ya juu awawapo ndani na nje ya uwanja  , msikivu na mwepesi wa kushika mafundisho , hizi ndiyo sifa alinajaaliwa kuwa nazo kijana huyo ”alifahamisha kibabu .
Amesema kuwa katika mshindano hayo Chiza alifunga mabao watano , huku akitengeneza  pasi za mwisho  kumi ambazo zilizaa magoli kwenye michezo yote kumi iliyocheza timu yake kuanzia kwenye makundi , nusu fainali na fainali  .
Kibabu aliongeza kwamba michuano hiyo imemsaidia katika kuibua vipaji kwani amebaini kuwepo kwa vijana ambao wanauwezo wa kucheza mpira na wanaweza kufika mbali ikiwa wataendelezwa zaidi .
“ Michuano hii imenisaidia kubaini vipaji vya wachezaji ambao walikuwa wamejifika , nawaombeni wapenda michezo kujitokeza kwa ajili ya kuzifadhili timu hizi ili tuweze kufanikisha azma ya kuinua vipaji na kuzalisha ajira kwa vijana ”alieleza .
Hata hivyo ametoa wito kwa makampuni na wadau mbali mbali wa michezo kujitokeza kwa ajili ya kumdhamini na kumuendeleza Kinda  huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa ili kutimiza ndoto yake ya kuitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar . 
Nazo taarifa ambazo zimepatikana na mwandishi wa makala haya zinesema kuwa wafanyakazi wa Shirika la CTS kutoka Korea wameahidi kumtafutia mawakala kinda huyo ili wamuendelezwe zaidi kisoka .